Kibiashara, huu ulikuwa mwaka wangu…

masai dada

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
15,679
12,364
Nimeona tusifunge mwaka na Mimi niweke japo tips kadhaa.

Nafanya biashara ya aina moja lakini na source sehemu mbalimbali. Kwa sasa ni China, Uturuki na Nairobi.

Hii biashara nilianza kama 5yrs ago ila kidogo kidogo sana na haikuwa ya kwanza nishafanya nyingi.

Hii niliamua kuifanya Kwa moyo wangu wote na kwa kila ncha ya mwili wangu. Pamoja na kwamba nimebustiwa pesa na Mr lakini nimejitoa Mimi mwenyewe.

Napambana sana godown, nasimama dukani mwanzo mwisho, nabeba mizigo ya wateja yaani kifupi ni mwili na roho. Ukweli katika maisha yangu sijawahi kuwa na mzunguko mkubwa hivi wa pesa.

Ninataka kufungua na k.koo ila nilichogundua ni kwamba kuna vitu flani flani ukiwa navyo wateja wanakuja hata kama upo Kyela Mbeya.

Nitatoa tips chache mpaka kesho nitakuwa nimemaliza.

1. MUNGU
Amini nakwambia jiunganishe na Mungu. Nimepata marafiki wachache lakini wanavyoviamini tena Kwa bidii sana kuliko uzanivu, huwezi kukaa mtupu tu, huna Mungu na huna kingine yaani biashara lazima uwe na unapohemea huwezi kaa hivi hivi. Mimi huyu MUNGU siwez muelezea. Sala yangu kwake Kila siku ni Ile Ile yaani sifichi kabisa.
"Mungu kama unavyonijua, nataka pesa nyingi sana, nitakutumikia kwa pesa hizi, kwa sadaka za kila hali"

Pia maombi ya ulinzi ni muhimu.

2. USITANGE TANGE
Amua kitu kimoja hata kama sio common ila kina uhitaji. Kwa mfano unaweza uza packages uza packages za aina zote kuanzia kontena, chupa, vindoo, mifuko migumu yaani kifupi ni package.

Halafu ndo humo ndani unatoa udwambwi udwambwi. Rejea k.koo kama somo, huwezi kuta duka lilikuwa linauza nguo za watoto halafu next year anauza vitenge yaani kuwa na consistency usitange. Mwaka wa kwanza utapata wateja 10, wale kumi wanaweza kukuzalishia wengine 50, 100 n.k.

Pia usichanganye changanye vitu, ila weka vya aina moja moja ila mbalimbali. Tuliza kichwa, usitapetape kila unapoona wenzako wana biashara za aina nyingine

3. MTAJI
Mimi nilianza kidogogo kidogo, lakini nimekuja kugundua ukiwa na mtaji mkubwa una faida mbili kubwa. Ya kwanza utauza kwa jumla hata kuanzia pisi chache; hicho kitu wateja wanapenda hata wewe mwenyewe ukienda duka wanauza jumla akikwambia kuhusu idadi akasema labda kuanzia pisi tano wewe ukamwambia nataka mbili ni rahisi kukuvunjia vunjia Ile jumla hata kama itaongezeka kidogo.

Ya pili ni utauza reja reja lakini bei yako bado itakuwa nafuu kuliko wale wenye mitaji midogo. Kama unaleta mzigo wa jumla hata ukiuza kwa pisi moja moja hutafanana na wale wanaosource k.koo
(Kusuhu mtaji kweli nimebustiwa na Baba mtu, ila nilianza kidogo na ndivyo inavyotakiwa ili ucheki upepo)
Kama una biashara unaielewa weka mtaji mkubwa na uza jumla. Faida ya 1000 Kwa pisi 300 na faida ya 5000 kwa pisi 20 kwa siku/wiki ni tofauti kubwa. Kama utapata mtaji popote na biashara ushaielewa, weka mzigo usiwe muoga.

4. KAA GOLINI
Amua mwenyewe nini unataka ni biashara au kazi. Huwezi mfungulia mtu kitu cha ndoto yako. Unaweka 30M hapo halafu wewe unaendelea na ishu nyingine. Hawezi kurun kama unavyotaka wewe.

Amua kimoja, hakunaga kazi na biashara unapita juu kwa juu kukagua jioni unless hiyo biashara ipo very sophisticated. Cheki wakinga, asipokuwa yeye mama yupo mume wake au watoto.

Utapiga marktime sana. Mimi niliacha kazi nikaamua hili moja. Aisee asilimia 90 nipo GOLINI na camera nimefunga ikinilazimu kufatilia mizigo yangu. Nimesafiri mara chache sana na nimeshaweka mifumo.

So nikiwa najua Leo naenda kulipia mizigo adhana inanikuta bafuni saa mbili nipo kwenye kordo za waarabu wa Tanga namalizia malipo mapema nimerudi dukani.

Ofcoz kwa nature ya biashara nyingine itakulazimu kutokatoka ila tengeza utaratibu mwepesi wa kusolve hizo movement. Kwa kuwa Sasa hivi nauza jumla ila nina vijana wa store wawil(Nina store mbili) so karibu na maokoto nipo front. Ila katika hapa nataka nikwambie punguza watu katika mzunguko wako (katika kuendesha biashara).

Unakuta wafanyakazi kibao na most of the time kwanza haupo na pia watu kati wanakuwa wengi. Kwa kifupi biashara yako ndo itengeneze uhitaji wa watu. Sio unapigiwa simu na shangazi ana mtoto wake hana cha kufanya umuweke hapo wakati ukicheki tayari may be una wawili na bado mzunguko sio mkubwa. Punguza gharama za uendeshaji wa biashara..

Katika hili usionr aibu hata kama ni kiepe yai kaa wewe. Yaani kaa golini, hili nimejifunza kwa mama mmoja wa kihindi hapo K.koo. Saa moja na madakika kashafungua mpaka 11 daily. Nyie hakuna pesa rahisi, kaa zitafute.

Cheki mfano wa hawa mastaa wanaofungua maduka ya nguo
mfano Wema, Hamisa na wengine wengi. Maduka makubwa, gharama kubwa za uendeshaji ila mwenye duka haonekani anaweka ustaa wajuba wanajilia tu

5. NENEA BIASHARA YAKO MAMBO CHANYA
Yaani unaleta mzigo tu unasema hapa lazima niuze tena sana. Akija mteja anataka let's say kitana cha nywele kwenye display kaona kimoja mtolee vyote, visifie. Yaani kifupi bidhaa zako zihadithie hadithi nzuri kwa wateja na hii ndo faida ya kukaa mwenyewe. Haya mambo mfanyakazi hawezi.

Mtu anakuja kuulizia let's say jiko la umeme, mteja anaulizia hivi hili jiko liko vizuri? Yeye anaweza akamwambia mimi hata sijawahi tumia.

Wewe sasa: Muelezee mteja hilo jiko kana kwamba unafanya kazi katika hicho kiwanda, tengeneza positive aura. Yaani hata kama umelala inenee biashara yako kuchanua. Kama wewe huamini kwamba utauza hata ukienda Kwa nabiii akuombee huwezi kuuza. Sasa utauza vipi wakati Imani huna? Wewe mwenyewe hujiamini unataka kuaminishwa na mtu mwingine!

6. MATANGAZO
Mambo yako mengi ila hili naomba liwe la mwisho kabisa. POST LIKE THERE IS NO TOMORROW. Usiweke ustaa kwenye biashara yako, ingiza mzigo. Usiweke tamaa ya faida kubwa. Post sponsored ads, anzisha group za WhatsApp.Watu wanakaa kwenye simu zao zaidi.

Usijali location weka mzigo mzuri, raia watakuja tu. Mimi sipo location mbaya nipo nzuri lakini ni katikati ya watu wanaouza vitu vingine ila simu hii ndo imenipa wateja
NB: MPE SABABU MTEJA YA KUKUFATA ULIPO.
Mteja 500 au 1000 inamfanya azunguke maduka saba K.koo Kwa kitu kile kile
Usiweke tamaa

LAST ONE
Usiwasahau wazazi. Mimi mama yangu yupo kwenye payroll yangu na sadaka nashukuru huyu mwaka nimetoa na Mungu kanipa za kutosha.

MUNGU AWABARIKI NYINYI NYOTE MNAOTUMIA MIKONO YENU KUHANGAIKA. Awaangazie nuru za uso wake.

AMINA
 
Hongera sana mleta mada, unaweza kuona kawaida tu unavyoandika hapa lakini huwezi jua ni kwa kiasi gani unatoa hamasa kwa wengi nami nikiwa moja wapo.
Miaka mitano yangu nyuma na hata kumi na kumi na tano nipo kwenye utafutaji ila sioni hatua ya maani ninayo weza kujivunia ila kwa kuna mawili matatu nimeyapata hapa na natarajia kuyapata maana naona mada inaendelea, binafsi nashuku, lakini pia nakutakia iwe hivyo mwakani kama ilivyokuwa mwaka huu kwako.
 
Hongera sana mleta mada, unaweza kuona kawaida tu unavyoandika hapa lakini huwezi jua ni kwa kiasi gani unatoa hamasa kwa wengi nami nikiwa moja wapo.
Miaka mitano yangu nyuma na hata kumi na kumi na tano nipo kwenye utafutaji ila sioni hatua ya maani ninayo weza kujivunia ila kwa kuna mawili matatu nimeyapata hapa na natarajia kuyapata maana naona mada inaendelea, binafsi nashuku, lakini pia nakutakia iwe hivyo mwakani kama ilivyokuwa mwaka huu kwako.
Mungu na akasikie maombi yako,jibiidishw na umuombe,amini katika Mungu na weka Imani yako kwamba unauza na utauza....
 
Back
Top Bottom