Nani yupo nyuma ya Uhuni huu kwa Sabaya?

Haya ni matumizi mabaya ya madaraka na hii ni sababu tuna katiba ambayo inawapa wenye madaraka kunyanyasa raia kwa kutumia vibaya madaraka waliyopewa na katiba isiyofaa...
Machawa wa sabaya mmeanza kupiga miayo, hata akiachiwa huru karma haitomuacha salama, huwezi kuwakata binadamu wenzako maskio, ukawagongea misumari ya ugoko, ukaenda kwa mzee wa watu ambaye ni mstaafu unampora milioni mia moja, ndg Mungu si mwanadam
 
Na hapo ndio chadema mnapojifelisha mbele ya Jamii.
Kwa mara nyingine huyu jamaa atawapiga chini tena.
Ndugu voicer, unafikiri vizuri kweli kabla ya kusema/kuandika? You seem to be so desperate kiasi cha akili yako kushindwa kufikiri vyema kabisa..!

Hebu tuambie. Kwani hao CHADEMA ndiyo wanamshitaki huyo ndugu yenu Sabaya?

Si anashitakiwa na Jamhuri [serikali] aliyokuwa anaitumikia na CHADEMA wala hawamo huko..!

Sikiliza ndugu. Matendo ya mtu, mazuri au mabaya huambatana naye. Matendo mazuri/ya haki, humtetea mtu mbele za Mungu...

Matendo mabaya/yasiyo haki/ya uovu humhukumu mtu akiwa hapa hapa duniani kabla ya hukumu ile ya mwisho..

Huyu ndugu yenu, hakuna mtu anamtesa. Anateswa na uovu [wickedness] wake mwenyewe...

Dawa ya dhambi/uovu ni kutubu tu [kukiri makosa] na kamwe siyo kulaumu watu wengine...!

Jaribu tu kufikiri hili;.

Kwamba, kwanini asiwe mtu mwingine kushitakiwa...?

Kwani yeye ndiye DC wa kwanza kupita hapo Hai?..

Jibu ni hapana...

Wamepita wengi lakini hawakuwahi kufanya makosa ya uonevu kama yeye...

Wenzake wote wako salama. Yeye analipia adhabu ya matendo yake...!

Acha kulala mr voicer. Acha kutetea usichokielewa. Mshauri kaka yako Sabaya kufanya lililo sahihi...

TOBA NDIYO SULUHU ya makosa yake. TOBA kwa Mungu Yehova ndiyo mlango wake pekee wa kutokea na kisha kuokolewa...

Akichelewa, utashangaa mno maana jela siyo lazima iwe ni zile kuta nene za mawe/tofali zilizojengwa na wanadamu tu...

Jela ya nafsi kuugua na kusononeka na kukosa amani milele ni mbaya zaidi kuliko hiyo kufungiwa kwenye kuta za matofali ya wanadamu. Jela hii hakimu mtoa hukumu ni Mungu muumba mwenyewe..

Nduguyo, anaweza kufa na makosa yake kabla ya wakati wake na kupotea milele...

Nanyi rafiki zake, mshauririni kutenda lililo sahihi badala ya kumpotosha. Mwambieni aache kiburi...
 
Jana tuliambiwa hukumu ya kesi iliahirishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi, Arusha.

kwa kile kilichodaiwa kuwa hakimu alikuwa anatimiza majukumu mengine ya kiofisi,mahali ambapo hatukutajiwa.

Leo asubuhi tunasikia taarifa ya Sabaya kuhamishiwa alfajiri,kutoka Gerezani Kisongo,na kupelekwa Mkoa mwingine kwenda kufunguliwa mashitaka mengine.

Anapelekwa Gereza lingine na Mkoa mwingine bila hata taarifa za Removal Order ya mahakama kutolewa.

Pia mshitakiwa huyu alieko chini ya ulinzi kama Mahabusu,huko Kisongo,anahamishiwa mkoa mwingine bila hata wakili wake kupewa taarifa.

Huyu mtu sio mfungwa kwa sasa bali Mahabusu.
Tena ambaye hukumu yake ni mwezi wa sita huu siku ya tarehe 10.

Halafu amehamishwa kwenda mkoa mwingine,na kusomewa mashitaka ambayo hata hajawaji kuhojiwa au kutakiwa kutoa maelezo yake na vyombo husika hapo awali.

Je!
Anachokihubiri Rais Samia na yale yanayoendelea kwa watendaji wake vinafanana?

Je!
Ni nani yuko nyuma ya hii Project Sabaya?

Katika kesi aliyoachiwa huru tulisikia tuhuma za kaimu DPP Kweka.
Ambaye alihusishwa na Familia ya Mbowe kama mkwe wake.
Akihamishia makazi kwa muda pale Arusha kwa kuisimamia kesi ile.

Sasa tunalazimika kuamini kwamba haya mambo yamerudi na yanashamiri kwa kasi.

Time will Tell!

Mnyonge Mnyongeni Lakini Haki Yake Mpeni.

View attachment 2247466
Tulieni dawa iwaingie wapuuzi nyie, mlishangilia sana issue ya Mbowe.
 
Jana tuliambiwa hukumu ya kesi iliahirishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi, Arusha.

kwa kile kilichodaiwa kuwa hakimu alikuwa anatimiza majukumu mengine ya kiofisi,mahali ambapo hatukutajiwa...
Sabaya ni jambazi, mwivi, mnyang'anyi, miaka 91 jela itapendeza
 
Najaribu kuwaza nje ya box. Hizi drama haziwezi kuwa ni mazingira yanaandaliwa kumwezesha kutokea Mahakama ya rufaa?
Kama Kweka asingekuwa ndie Mtengeneza mashitaka,hata mimi ningewaza hivyo.
 
Acha kupotosha wasomaji kwa mahaba Niue uliyonayo juu ya sabaya. Kuhusisha makosa yake anayotumiwa kuyatenda na uwepo wa naibu dci na Mbowe ni kuonyesha jinsi Gani ulivyo biased na obsessive na sabaya.

Kama kweli huna maslahi na sabaya ni kwanini uwataje watu wengine Tena wasiohusika na kesi za sabaya?

Acha kumchafua image za watu Kwa mahaba Yako binafsi!
Hata Sabaya binafsi leo ameitamkia mahakamani kwamba hana imani na Kweka.
Sasa wewe ndie unaendekeza unyumbu bila facts.
 
Imechukua kutikiswa kwa mtu muovu kumfanya mataga adai katiba mpya!
Maajabu hayataisha nchi hii.
Ni jambo zuri kwa sababu katiba imara isingeruhusu Sabaya kufanya udhalimu wake kwa kuanzia.
Hatimaye umetambua umuhimu wa katiba mpya.
Yoda
 
Tulishasema tunaachana yaliyopita tunaanza ukurasa mpya kama ilivyofanyika kwa mbowe,Lisu na wengineo sasa kwa upande wa Sabaya mbona mambo ni tofauti kama ilivyokuwa kwa hao wengine ambao hawaishi vihoja kila kukicha.Tusameheane jamani.
Jinai haifi
 
Acha kupotosha wasomaji kwa mahaba Niue uliyonayo juu ya sabaya. Kuhusisha makosa yake anayotumiwa kuyatenda na uwepo wa naibu dci na Mbowe ni kuonyesha jinsi Gani ulivyo biased na obsessive na sabaya.

Kama kweli huna maslahi na sabaya ni kwanini uwataje watu wengine Tena wasiohusika na kesi za sabaya?

Acha kumchafua image za watu Kwa mahaba Yako binafsi!
Huyo atakuwa mmoja wa mademu zake jambazi sugu Sabaya,naona ametokwa mishipa shingoni kumtetea
 
Hata Sabaya binafsi leo ameitamkia mahakamani kwamba hana imani na Kweka.
Sasa wewe ndie unaendekeza unyumbu bila facts.
Hakuna kitu kama hicho kumkataa mwendesha mashitaka,kama analeta weak case ni mwanya mzuri Kwa upande wa defence kuipangua,na mwisho wa siku hakimu au jaji atatoa hukumu Kwa ushahidi ulioletwa mbele yake. Unaweza kumkataa jaji au hakimu Kwa kutokuwa na Imani naye lakini siyo mwendesha mashitaka
 
Back
Top Bottom