Mwigulu Nchemba: Wizara ya Fedha hainufaiki na mikopo ya 'Kausha Damu'

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Suala la mikopo ya chap chap yenye riba kubwa maarufu 'kausha damu' limejitokeza katika mkutano wa hadhara wa Katibu wa NEC, Itikadi, Mafunzo na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda ambapo wananchi wa Singida Mjini wamemuomba kiongozi huyo kuwasaidia.

Leo Alhamisi Januari 25, 2024 Makonda akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya zamani ya mabasi wilayani Singida amepokea kilio cha kausha damu kutoka kwa mmoja wa wakazi wa wilaya hiyo, Shaban Itambusa aliyesema mikopo ya aina hiyo inawatesa wananchi.

Baada ya maelezo hayo, Makonda alimuita Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba aliyekuwa katika meza kuu kwenda jukwaani kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.

Akijibu maswali hayo, Dk Mwigulu amesema ni kweli wakopesha wa kausha damu wamepewa leseni na riba wanayoipata ni kwao si Wizara ya Fedha au waziri anayenufaika.
 
Hao ndiyo wasomi.

Anachotaka ni asilimia kumi.

Je, hajui kuwa mzunguko wa hiyo hela unaongeza kodi ?

Je, hajui kuwa wanaonyonywa ni wananchi ambao yeye Nchemba anategemea kuwaomba kura anapowaza kugombea urais?

Au anaona upenyo kuzidi kuwa mgumu?
 
Leseni za masuala ya fedha zinatolewa na serikali kupitia Bot, bot ndiyo inayosimamia maswala ya riba za mikopo. Kusema serikali haihusiki na mikopo ya kausha damu Bali kutoa leseni kunaobyesha wazi PhD yake ni ya kufoji.

Lakini kwanini wananchi wanaenda kwenye mikopo ya kausha damu, ni kwa sababu taasisi zetu za fedha hazijatengeneza mazingira rafiki kwa wakopaji kitu ambacho serikali inabidi ikisimamie.
 
Back
Top Bottom