Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 26,133
- 68,444
Habari wakuu, nmeona kipindi cha ripoti maalum ITV kuhusu mikopo kausha damu.
Malalamiko ni mengi sana licha ya kuwepo kwa uhitaji wa mikopo na wengine kufikia hatua ya kuomba hii mikopo isitishwe.
Dhamana zinazowekwa na kiasi cha mkopo haviendani kabisa.
Kwa maelezo ya wanawake wengi wanaochukua mikopo wanadai ina madhara makubwa kuliko faida, na wengi wanachukua bila kuwashirikisha waume zao, hii ni hatari zaidi.
Serikali inajinadi kutoa mikopo kwa makundi mengi ya kijamii hasa kwa wanawake lakini ina mlolongo mrefu na ndio chanzo cha wengi kukimbilia kausha damu kupata mkopo kwa haraka.
Kipi kifanyike kuboresha hii mikopo inayoonekana inawaumiza wengi na uhitaji wake bado ni mkubwa?
Taasisi za fedha kama mabenki hamuoni hii fursa kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwafikia watu wa matabaka ya chini kupitia vikundi? (tatizo hapa ni mlolongo mrefu mpaka kupata mkopo)
Wanawake wanadhalilika sana na hii mikopo ya kausha damu. Mtu una mikopo zaidi ya minne kausha damu lazima utadhalilika tu, huwezi kutoka shimoni kwa kuendelea kuchimba shimo.
NB: DAWA YA DENI NI KULIPA.