Nitajieni biashara nyingine inayotoa faida kama mikopo ya kausha damu!

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,022
144,380
Kausha damu: Unawekeza mtaji wa shilingi 1,000,000, unavuna faida ya shilingi 300,000 mpaka 400,000 kwa mwezi. Nitajieni biashara nyingine kama hii.

Tunaposema hii mikopo ni kausha damu na initia watu umasikini, basi hicho ndicho kinachofanyika.

Hivi leo hii ukipewa mtaji wa shilingi 1000,000 unaweza kufanya biashara gani halali ukapata faida kama hiyo ndani ya siku 30 tena ukiwa umetulia tu unahesabu siku? Hiyo ni riba ya asilimia 30 mpaka 40 kwa mwezi na Serikali ipo na Bunge lipo.

Hatumpendi Makonda, lakini saaa tumuombe amvae Waziri wa Fedha na Viongozi wa BOT maana hii biashara ni kama imewashinda kuidhibiti kwani Makonda kwa sasa ndio anasikilizwa na kujadiliwa kwa kila atachokisema.

Uzembe umezidi ndio maana Makonda anakuwa maarufu.
 
Hiyo mikopo ikizuiliwa maskini ndio watakuwa wa kwanza kupiga kelele.
Maskini wa Tanzania hana pa kujikwamua zaidi ya huko kausha damu.
Kodi , malipo ya natibabu ya afya na misiba ndivyo vinawapeleka huko.
Ni heri kausha damu iendelee.
Nchi bila pesa mfukoni unafia kwenye korido za hospital tena ni hospital za umma
Hii biashara idhibitiwe kama Bangi na Madawa ya kulevya. Sio kabisa hii biashara. Watu wanakimbia makazi yao kwassbabu ya hii mikopo.
 
Mkuu BOT waweke mipaka kwenye riba.kampuni au tasisi itakayo pita mpaka huo wa riba ishugulikiwe.
Kama wameferi hivyo kuna timu ya BOT ya mkoa ikagua hivi vikampuni vya uchochoroni kama vina vigezo vya kufanya kazi hizo.
Kama wameshindwa kabisa, basi kila mtu anaetamani kufugua kampuni ya kukopesha awe chini ya benk fulani, na hao wataalm wa benk watakua wanaisimamia hiyo kampuni ya mikopo, ikienda kinyume wataalam wa benk wamuonye, kama haelewi benk imkatae na taarifa zake ziandaliwe wapewe BOT makao makuu afungiwe na afirisiwe.
 
Pamoja na wizi kwenye hizo kampuni za mikopo lakini nadhani hapa Duniani sidhani kama kuna watu wajinga kama raia wa Tanzania.......

Bila shaka hao mabwana kabla ya kukupatia huo mkopo wanakufahamisha kupitia mkataba wao kwa maana mpaka unachukua mkopo maana yake ni khiyari yako......

Inakosa nguvu kwa kuwa ipo kwenye khiyari........
 
Kausha damu: Unawekeza mtaji wa shilingi 1,000,000, unavuna faida ya shilingi 300,000 mpaka 400,000 kwa mwezi. Nitajieni biashara nyingine kama hii.

Tunaposema hii mikopo ni kausha damu na initia watu umasikini, basi hicho ndicho kinachofanyika.

Hivi leo hii ukipewa mtaji wa shilingi 1000,000 unaweza kufanya biashara gani halali ukapata faida kama hiyo ndani ya siku 30 tena ukiwa umetulia tu unahesabu siku? Hiyo ni riba ya asilimia 30 mpaka 40 kwa mwezi na Serikali ipo na Bunge lipo.

Hatumpendi Makonda, lakini saaa tumuombe amvae Waziri wa Fedha na Viongozi wa BOT maana hii biashara ni kama imewashinda kuidhibiti kwani Makonda kwa sasa ndio anasikilizwa na kujadiliwa kwa kila atachokisema.

Uzembe umezidi ndio maana Makonda anakuwa maarufu.
Makonda? Achachana na Hilo tapeli, hakuna ambacho amefanikiaha kwa mikwara mbuzi yake.
 
Riba ya 30% - 40% kwa MWEZI ni hatari ! Nadhani, hao wanatakuwa wanafanya bila ya kuwa na usajili wa BOT.
Kama benki zimeamua kuhudumia matajiri pekee na kuwakataa wauza chai mnawezaje kuiondoa kausha damu ?

Hela za mikopo ya halmashauri mnawanyima mnapeana mnataka waende wapi ?

Kwa mfano Hela zote za mikopo ya wajasiriamali na walemavu Temeke alipewa Mwenyekiti wa Wilaya wa ccm , na hakurejesha .

Peke yake alilamba mil 300 , ushahidi wote upo lakini kesi imezimwa
 
Kausha damu: Unawekeza mtaji wa shilingi 1,000,000, unavuna faida ya shilingi 300,000 mpaka 400,000 kwa mwezi. Nitajieni biashara nyingine kama hii.

Tunaposema hii mikopo ni kausha damu na initia watu umasikini, basi hicho ndicho kinachofanyika.

Hivi leo hii ukipewa mtaji wa shilingi 1000,000 unaweza kufanya biashara gani halali ukapata faida kama hiyo ndani ya siku 30 tena ukiwa umetulia tu unahesabu siku? Hiyo ni riba ya asilimia 30 mpaka 40 kwa mwezi na Serikali ipo na Bunge lipo.

Hatumpendi Makonda, lakini saaa tumuombe amvae Waziri wa Fedha na Viongozi wa BOT maana hii biashara ni kama imewashinda kuidhibiti kwani Makonda kwa sasa ndio anasikilizwa na kujadiliwa kwa kila atachokisema.

Uzembe umezidi ndio maana Makonda anakuwa maarufu.

sema kuna huyu shoga [mention]Ritz [/mention] anajiuza atakua anazijua
 
Hii biashara idhibitiwe kama Bangi na Madawa ya kulevya. Sio kabisa hii biashara. Watu wanakimbia makazi yao kwassbabu ya hii mikopo.
Kumbuka hiyo biashara inatambulika kwenye mamlaka husika. Hivyo ni biashara halali. Na utambue pia hizo taasisi hazimlazimishi mtu kukopa!! Na uzuri wapo wakopaji ambao wanalipa hayo marejesho ya 30% kila mwezi na hawajawahi kukimbia nyumba zao. Kwa sababu wanaitumia kwa malengi ya kibiashara! Na siyo kwa malengo ya kununulia sofa set au kukipia ada za watoto. Ila kwa hao wenzangu na mimi wanaoshindwa kurejesha, ndiyo hao sasa wanaodhalilishwa.

Kumbuka pia watu wanakopa kwa sababu serikali imeshindwa kuwatengezea mazingira mazuri ya kukopa fedha kwa riba ndogo, kutokana na sababu mbalimbali.
Lakini kubwa zaidi ufahamu hao watu wanakopa hela benki kwa ajili ya kuanzishia hiyo biashara. Na riba za benki nazo ziko juu! Asilimia 16+ siyo riba ndogo!

Na wakati huo huo wanatakiwa kulipa kodi za serikali na Halmashauri/miji, nk. Wanatakiwa kuwalipa wafanyakazi, kulipia pango la ofisi zao, nk.
Kwa hiyo mimi nashauri uanzishe kampeni ya kutoa elimu kwa hao wakopaji, ili watambue madhara ya hiyo mikopo ya kausha damu. Kinyume na hapo, hakutakuwa na namna nyingine yoyote ile. By the way, huyo Makonda ni kilaza tu na mtafuta kiki. Wala hana uwezo wa kuzuia mambo ambayo yapo kisheria.
 
Tuongee ukweli ulio mitaani wakuu,, maisha magumu ndiyo yanayofanya watu wakope hela hovyo mfano mdogo ni mimi nina kikazi changu kidogo ila watu wananifata sana kukopa.

Mtu anaweza kuja anakupa simu yake umpe elfu 10 tu anasema kesho yake analeta elfu13 ni yeye mwenyewe anamejipangia sasa mimi naachaje,,

Na kuna jamaa sasa aliniachia simu yake toka mwezi wa9 alichukua elfu15 tu hadi leo itakua shingapi? Taasisi uchwara ziacheni zile hela kwasababu watu wenyewe wameenda na shida ndio zimewapeleka.
 
Back
Top Bottom