Ushauri kwa Wizara ya Fedha kuhusu kuongeza mapato kupitia usajili wa namba za magari

Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,402
7,310
Waziri wa Fedha pamoja na wasaidizi wako nataka niwashauri kuhusu kodi ya plate number binafsi [Majina kwenye plate Namba] za vyombo vya moto (Magari) kama tunataka kuongeza mapato huduma hiyo iwe na watumiaji wengi

Ishuke iwe kwa mwezi, serikali iweke Tsh laki moja kwa mwezi [100,000] itapata Watanzania wengi sana kuliko hizo gharama za milion 5 inabaki kwa watu wachache.

Ikishuka ikawa laki moja kwa mwezi hata IST watu wataweka namba binafsi(Majina) ,wenye namba A ,B,C,D wataweka namba binafsi.

mwigulu Nchemba
 
SIO SAWA.
UKISHUSHA BEI KILA MMOJA ATAMUDU TUTAKUWA NA MAJINA MENGI BARABARANI HUTAJUA YUPI NI YUPI KIRAHISI ALAFU WABONGO WENGI MAJINA YANAFANANA. JUMA, JOHN, PETER, RAMADHANI, HAMISI, ETC.
 
Kweli kabisa,wabongo wengi wanaopenda sifa na kutaka kuonekana wataweka

Ova
 
Kodi zikiongezeka itasaidia kuongeza v8 za kutosha kunogesha misafara ya viongozi wetu
 
Back
Top Bottom