Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 8,184
- 11,607
Kausha damu ni mikopo ya yenye urahisi sana upatikanaji wake. Ina vigezo na masharti nafuu sana yanayowezekana kwa wakopaji wengi.
Kwa upande moja inasaidia sana watu wenye shida na malengo ya kujiunua kiuchumi, na wanafanikiwa bila wasiwasi.
Kwa upande mwingine ni mateso, vilio na kusaga meno kwa hiari yao na kwa kujitakia. Aibu, fedheha na dhahama zinawapata wahusika zinatukumba pia tusio husika.
Maana vilio vya shida zisizoisha, malalamiko, manung'uniko na majuto vinasikitisha sana.
Na kiubinadamu tunasaidia kadiri tunavyo jaaliwa na Mungu.
WALIMU wa shule za Msingi wanao elekea kustaafu wamekwama hapa kausha damu. Wanateseka sana.
Kadi za benki, vitambulisho na nyaraka zao muhimu za kazi zimehodhiwa na maofisa kausha damu, kama dhamana kutokana na malimbikizo ya marejesho na riba walizokosa kuzilipa huko nyuma na zinaongezeka kadiri mkopaji anavyochelewa kurejesha.
Muda wa kustaafu ukifika, afisa wa kausha damu na mwalimu mustaafu mguu kwa mguu kufanya clearance za mafao. Na baada ya hapo kausha damu anamkomba vizuri sana mstaafu huyu malimbikizo ya marejesho na riba, na akimuachia pumzi kidogo ya kupigia miyayo kwa muda mfupi tu ujao...
Watu hawa wasaidiwe, kustaafu sio tiketi ya kufa. Bado wanastahili kuishi kwa furaha na Amani ndugu zetu hawa.