Mwigulu Nchemba: "Napendekeza kupunguza adhabu kwa makosa ya pikipiki na bajaji lengo ni kuweka adhabu kwa kuzingatia uwezo wa kulipa"

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Good evening jamiiforums

gfghbnhg.jpg

Soma hapa>>> Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika?

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA LEO BUNGENI
=====
"Mh. Spika napendekeza kupunguza adhabu kwa makosa ya pikipiki na Bajaji kutoka elfu thelathini za sasa hadi elfu kumi kwa kosa moja, lengo ni kuweka adhabu kwa kuzingatia uwezo wa kulipa"

ghbghghnj.jpg

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hahahahaaa mkuu, hao jamaa niliowa-tag sijafanya hivyo kuwa kupenda ila nimelazimika kwa maana walinikejeli sana siku nilipoandika humu kuwa tozo zinapaswa kuendana na uzito wa kosa.

Kosa la bajaj sio sawa na la mwenye lorry.
Uzito wa kosa...mfano bajaj kapita taa nyekundu na mimi na Vitz nimepita taa nyekundu, kosa si lile lile? Inakuwaje huyu alipe 10,000 na yule 30,000?! Bodaboda na bajaj pamoja na faini 30,000 ndio wavunja sheria wakuu sasa kuwapunguzia hadi 10,000 si ndio watatumaliza?!!
 
Tena tuwe makini sana juu ya hawa watu
 
Uzi naukumbuka vyema huo ila naendelea na mawazo yale yale.

Hapo kutaongeza ajali hakika.

Fatilia vyema takwimu za ajali za barabarani zilizosababishwa na bodaboda utaelewa nini kitakachotokea.

Hadi sasa pamoja ni 30k ila ndio wanaongoza kwa uvunjifu wa sheria.

Bodaboda wengi ni vijana wadogo ambao akili zao hazijakomaa kwahiyo mambo mengi wanachukulia poa sana.

Naona ajali nyingi sana baada ya mabadiliko hayo ya faini.

Mungu tusaidie kwa vijana wetu hawa.
 
Good evening jamiiforums

View attachment 1814583

Soma hapa>>> Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika?

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA LEO BUNGENI
=====
"Mh. Spika napendekeza kupunguza adhabu kwa makosa ya pikipiki na Bajaji kutoka elfu thelathini za sasa hadi elfu kumi kwa kosa moja, lengo ni kuweka adhabu kwa kuzingatia uwezo wa kulipa, vilevile adhabu kwa makosa mengine ya vyombo vya moto zitaendelea kuwa kama zilivyosasa"

View attachment 1814598

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Hii ingekua mpaka kwa magari ingepunguza sana rushwa ..kuliko Utoe 5K as Rushwa Bora upigwe fain ulipe na kosa urekebishe
 
Hata makosa wapunguziwe vifungo akigonga mtu akaua asishitakiwebatoe noti nyekundu asepe ndiyo maana yake.
 
Ngoja wataalamu wa falsafa ya adhabu jinai waje kutujuza, kuongeza au kupunguza adhabu ni kipi kinapunguza matokeo ya uhalifu? Hapa serikali imeangalia hoja ya kiuchumi (uhimili wa fine) affordability peke yake.
 
Back
Top Bottom