incredible terminator
JF-Expert Member
- Aug 1, 2016
- 2,229
- 3,525
Habari wakuu, Naandika huu ujumbe kwa maumivu makali sana, kilio simanzi na maumivu yasiyoelezeka,
Nilishawahi kuleta mada hii hapa jukwaani bahati mbaya sana haikupata wadau wengi, haikupata wachangiaji na mwisho wa siku uzi wangu ulifunikwa na nyuzi za vichekesho, vibonzo na stori za kuchekesha hii inaonesha ni kiasi gani Watanzania tusivyochukulia sereous mambo mhimu.
Leo naandika hapa nikiamini hapa jukwaani wapo viongozi mbalimbali au watu mbalimbali ambao wanaweza kuucopy huu ujumbe wangu kisha kumtumia waziri mwenye dhamana ya kulitatua hili au kwa mkuu wa Polisi Tanzania, au hata kuniwekea hapa namba ambayo anapatikana whatsup au email ili nimtumie mimi mwenyewe kero hii pengine hapo anaweza kuitatua.
Ninaamini nchi yangu na viongozi wetu hawana lengo baya kwa vijana na wanainchi wake ila kuna baadhi ya watu wanafanya haya kwa masrahi yao binafsi na chuki zao binafsi kutufanya vijana tuichukie serikali na kuona kama tunaserikali kandamizi na isiyo na huruma kwa wanainchi wake.
Mara nyingi nilishaleta malalamiko ya Polisi Kituo kikuu Dodoma (Dodoma centro police) kuwatesa na kuwanyanyasa madereva bodaboda na hata kuwapiga vijana makofi kwa makosa yasiyokuwa na sababu, na ikiwa bodaboda anakamatwa kwa kosa la trafic case kuna haja gani ya kumpiga kumdhalilisha na hata kutumia lugha za kashfa na matusi kwa kijana ambae anatafta riziki?
Kumekuwa na tabia ya Polisi kukamata bodaboda na kumtaftia makosa mengi kisha kumtoza shilingi elfu kumi kwa kila kosa 10,000/=, hapa utakuta Bodaboda amejumlishiwa makosa 10 na anatakiwa kulipa laki moja,
Sasa hapo kijana wawatu anadaiwa rejesho na boss pikipiki ya mkataba kila siku rejesho, na ikikamatwa kama hana hela hapo pikipiki inaenda kupakiwa kituoni na hapo kijana wawatu haingizi chochote na pikipiki inasoma rejesho zikipita siku5 maboss wanachukua pikipiki yao hapo kijana wawatu kala hasara maana pikipiki za mikataba huwa kuna kiasi wanatanguliza ko ikichukulia hapo kijana kala hasara.
Maana kwa sasa Kituo cha police Dodoma wanategemea mapato kutoka kwa bodaboda, vijana ambao kwa changamoto za kazi zao hata shilingi elfu 10 kwa siku wanaingiza kwa mbinde.
Nizaidieni kusambaza huu ujumbe huu.