Mwanaumme ni nini?

owaishe, nkotalikuzoka si.., okabulila kanyigo? shairi zuli sana.

zimwimtu Waitu shumalamu..............okozile naiwe................lakini mwanaume ni nini?
 
Last edited by a moderator:
Mbona kiungo muhimu hakiongelewi hapa! kumbukeni hayo yote mwanamke pia anaweza kuyafanya...
[MENTION]
s.fm[/MENTION] usisahau hata dildo yaweza hayo yote................
 
Kigarama amesema, Haika kamalizia
mwanaume si lelemama, kila siku kulialia,
uanaume gharama, si mambo ya kuletewa,
mwanaume kusimama, heshima kuitetea.

Mambo yamebadilika, ni kweli siwezi pinga,
hatuutaki ukaka, jukumu tunalipinga,
unyumba tunautaka, ila nyumba twazipinga,
mwanaume kusimama, heshima kuitetea.

huyu anagawa tigo, yule nywele kalikiti,
hataki kupiga mzigo, kutwa shinda kwenye kiti,
jioni ye kama gogo, na bado ataka titi,
mwanaume kusimama, heshima kujiletea.

mwingine hataki kazi, japo elimu ye hana,
hata kusafisha zizi, kutwa kutongoza Anna,
mwishowe aomba hirizi, eti bahati ye hana,
mwanaume kusimama, heshima kujiletea.

kazi ndo hulka kiumeni, tena sifanye kitoto,
kitandani na juani, fanya bado damu moto,
uje lie kivulini,lisema jomba Mpoto,
mwanaume kusimama, heshima kujiletea.

mwanaume kusimama, miguu yote mitatu,
mmoja wa kwake mamaa, miwili ni ya viatu,
kwake usikae hama, mpende kwa wote utu,
mwanaume kusimama, heshima kujiletea.

hata nikisema sana, najua sitomaliza,
sitaki kunena sana, tamu nikaumaliza,
yuwapi babukijana, ama shemeji Kaizer,
mwanaume kusimama, heshima kujiletea.
 
Last edited by a moderator:
Mhhh!
kadiri siku zinavyoenda swali linazidi kuwa zito
Kwangu mie wa zamani,
mwanaume (sio kijana)
- awe ana ambition - maono, au matamanio, au muelekeo unaoonekana na sie tunaomuangalia
- awe realistic na hali ailonayo kwa wakati ule yani ajijue, na mipango yake ianzie hapo,
- mimi nilisoma na nikaamini kuwa mwanaume anatakiwa awe ana mtazamo wa kutafuta solutions kwa vitendo, awe anasukumwa na kutafuta mambo boda zaidi kwa matendo sio kwa maneno, yani akiongea kuwa ni kwa kuelekea kwenye solutions sio kuzunguka zunguka tu kwenye stori then kuacha hewani, (mfano stori za mpira kwa wasiocheza wala kujiunga na vyama vya mpira)
- anakuwa mwanaume pale anapokuwa amepata ile sense ya kuwa mwangalizi, kuwa responsible kwa watu wengine, watoto, wazee, mke jamii. anapokuwa anajisikia kuwatunza na kujipa jukumu la kutimiza mahitaji yao, anapoacha kujifikiria mwenyewe kwa aslimia kubwa

Hii ya mwisho ndio inapungua sana siku hizi
mtoto wa kiume (over 25) haoni shida wala aibu kuomba, tena kuomba kwa wazee au wasichana. Mimi inanitatiza sana.
wavulana wanatilia mkazo nguo, viatu, perfume, saluni kuliko wanavyofikiria jinsi ya kuikwamua jamii yao,
unakuta kijana bajeti yake yote inaishia huko, akijua au akidhani kuwa kwa kuwa wazazi au wadogo zake hawamuombi hela, hawamuhitaji,
Basi japo kuwa na tabia ya kujipa jukumu la kulipa umeme, au la kununua uniform, jpo hukaombwa!!!
jamani mnakera!
Sio tu kwenye nyekundu, bali pointi zako zinasimamia mfumo dume zaidi!.
 
Sio tu kwenye nyekundu, bali pointi zako zinasimamia mfumo dume zaidi!.

Unaposema mfumo dume una maana gani?
kama una maana mwanamke kuwa 100% responsible kwa mambo ya kike na mengine ambayo itabidi apambane nayo kwenye mazingira yake, na mwanaume kuwa 100% responsible kwa majukumu ya kiume na mengine ambayo life itamtupia then naomba niku 'like'

lakini kama una maana mwanamke kuacha majukumu yake kukimbilia mengine na kutaka watu wengine ndio watake cover ya alioacha, au mwanaume kukumbia majukumu yake na kukimbilia mengine ili akiacha watu wahangaikie na majukumu asilia ya kwake then HAPANA.
hivi mfumo dume hasa uwa ni upi? mimi hua nasikia wanautaja wakati wanazungumzia kupiwga kina mama, kuachiwa kazi ngumu etc kwa upande huu siwezi kuongea sana ila sipendi familia ya hivi.

Nilimaanisha kuwa, mwanaume kwa maumbile, ni lazima atumike na awe mwangalizi. kama atanunua mikuki na kulinda sungusungu, au ataweka walinzi, au atasimamia uwepo wa security alarms, inabidi imkae kichwani, ukiona mama ndio anahangaika na kama alarms, walinzi kama wamekuja, kama mbwa ni wakali, wamekula au kucheki milango imefungwa usiku, inabidi ujue significance yako inapotea

pia ukiona familia watoto wanakula usichojua, wanafunga na kufungua shule bila kuulizwa, wanaugua nakupona bila wewe kujuuliza, mama na watoto wanavaa mwaka mzima h ujihusishi lazima tukushangae
 
Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?

Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?

Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?

Welcome back Chief. Kwa mashairi sikuwezi. Mwanaume ni kiumbe wa ajabu sana..anajikana mwenyewe kisa kuogopa majukumu..baadaye yeye huyo huyo arudi na kuomba msamaha..
 
Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?

Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?

Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?

mmmmmmmmmmh ! nimetafuta vina sivioni, sijui hii ni barua ?:A S-coffee:
 
Nshomile Ruta nimekubali shairi lako. Imebidi niandike kwani nilihisi kitufe cha "like" kisingeyatendea haki mawazo yangu. Ila unaonaje ukijikita kwenye umalenga ikiwezekana uandike vitabu kwa ajili ya hiki kizazi kipya cha SMS.
 
ruta ,kidume kwangu mm ni yule anaejua wajibu wake ,mtendaji wa kazi anashughulia familia yake ,sio kuvaa shirt na suruali tu apa
 
[h=2][/h]
Kuku ni kuku,jogoo jina.Hujui ki baolojia tuko nusu wanaume,nusu wanawake.So,mwanaume ni UUME.Hata kama hana pesa,nyumba wala gari.
[MENTION]
Godwishes[/MENTION] waswahili hulonga.........................ukimchunguza sana kijogoo huwezi kumla kwani hula visivyoliwa........
 
ruta ,kidume kwangu mm ni yule anaejua wajibu wake ,mtendaji wa kazi anashughulia familia yake ,sio kuvaa shirt na suruali tu apa

wahida unaye au bado waangazaangaza?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom