Mwanaumme ni nini?

Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?

Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?

Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?
owaishe, nkotalikuzoka si.., okabulila kanyigo? shairi zuli sana.
 
Hello Ruta nilikumiss juzi nimemuuliza mtu umepotelea wapi akaniambia hajui, nice ur back, haswa wanaume wa sasa hivi tatizo ni haya mashule ya boarding toka baby class sasa atajuaje majukumu ya uanaume badala yake anafikiri umwanaume ni kuwa tu na uwezo wa kukatumia kakifaa kake, mwanaume hadi aitwe kichwa cha nyumba ni zaidi ya tujuavyo, kikubwa mi naona ni kujua majukumu na kujua maana ya kuchaguliwa na Mungu kuongoza familia, kwa hekima na maarifa.
 
Mwanamme ni kuingia bank kudeposit au kuchukua mzigo,Pili mwanamme kazi lzm mtarimbo uwe unafua nazi au dafu!!
 
Mhhh!
kadiri siku zinavyoenda swali linazidi kuwa zito
Kwangu mie wa zamani,
mwanaume (sio kijana)
- awe ana ambition - maono, au matamanio, au muelekeo unaoonekana na sie tunaomuangalia
- awe realistic na hali ailonayo kwa wakati ule yani ajijue, na mipango yake ianzie hapo,
- mimi nilisoma na nikaamini kuwa mwanaume anatakiwa awe ana mtazamo wa kutafuta solutions kwa vitendo, awe anasukumwa na kutafuta mambo boda zaidi kwa matendo sio kwa maneno, yani akiongea kuwa ni kwa kuelekea kwenye solutions sio kuzunguka zunguka tu kwenye stori then kuacha hewani, (mfano stori za mpira kwa wasiocheza wala kujiunga na vyama vya mpira)
- anakuwa mwanaume pale anapokuwa amepata ile sense ya kuwa mwangalizi, kuwa responsible kwa watu wengine, watoto, wazee, mke jamii. anapokuwa anajisikia kuwatunza na kujipa jukumu la kutimiza mahitaji yao, anapoacha kujifikiria mwenyewe kwa aslimia kubwa

Hii ya mwisho ndio inapungua sana siku hizi
mtoto wa kiume (over 25) haoni shida wala aibu kuomba, tena kuomba kwa wazee au wasichana. Mimi inanitatiza sana.
wavulana wanatilia mkazo nguo, viatu, perfume, saluni kuliko wanavyofikiria jinsi ya kuikwamua jamii yao,
unakuta kijana bajeti yake yote inaishia huko, akijua au akidhani kuwa kwa kuwa wazazi au wadogo zake hawamuombi hela, hawamuhitaji,
Basi japo kuwa na tabia ya kujipa jukumu la kulipa umeme, au la kununua uniform, jpo hukaombwa!!!
jamani mnakera!

Haika kwa kifupi mwanaumme ni kuyajua na kuyakubali majukumu yake........
 
Last edited by a moderator:
Rutashubanyuma hoja hii ni tatizi,
Ni hoja tata vizazi hata vizazi,
Siyo hoja ya wajenzi wala wapagazi,
chanzo chake ni nyumbani, aina ya malezi,
Umelelewaje?

Kwani kwenu mko vipi, ni kipi cha thamani,
kwenu shujaa ni yupi, yule mnaye thamini
Nani kwenu ni kapi, asiyetakiwa nyumbani,
Kipi mnachothamini?

Kama nguo ndiyo mali, Elimu ni vuvuzela,
Basi hata wanawali, wamachinga watawala,
Watapenda suruali, elimu kwao jalala
Mnakuzwaje?

Uanaume ni sifa, si maumbile ya jalali
Uanaume si shufaa, au uwe jabali
Uanaume ni kufaa, jamii ikukubali,
Ni sifa ya uongozi.

Siyo kuvunja vitanda, au hodari kufanya,
Uanaume sawa sanda,hutunza si kutapanya,
Uanaume si kupinda, au tabia za panya
Uanaume utu wema

Mwanaume huwa kinga, kiongozi familia,
Hana sifa za kijinga, masuala hufuatilia,
Kama likizuka janga, hawezi kulia lia
Ni sifa ya Utume.

Kigarama.....tupo pamoja......................naona nawe umo kwenye huu ulimwengu wa tenzi
 
Last edited by a moderator:
Hello Ruta nilikumiss juzi nimemuuliza mtu umepotelea wapi akaniambia hajui, nice ur back, haswa wanaume wa sasa hivi tatizo ni haya mashule ya boarding toka baby class sasa atajuaje majukumu ya uanaume badala yake anafikiri umwanaume ni kuwa tu na uwezo wa kukatumia kakifaa kake, mwanaume hadi aitwe kichwa cha nyumba ni zaidi ya tujuavyo, kikubwa mi naona ni kujua majukumu na kujua maana ya kuchaguliwa na Mungu kuongoza familia, kwa hekima na maarifa.
[MENTION]
Mamzalendo[/MENTION] hapo kwenye red umeniacha mbavu zinaniuma mno.........................nimecheka mno
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom