Unaposema mfumo dume una maana gani?
kama una maana mwanamke kuwa 100% responsible kwa mambo ya kike na mengine ambayo itabidi apambane nayo kwenye mazingira yake, na mwanaume kuwa 100% responsible kwa majukumu ya kiume na mengine ambayo life itamtupia then naomba niku 'like'
lakini kama una maana mwanamke kuacha majukumu yake kukimbilia mengine na kutaka watu wengine ndio watake cover ya alioacha, au mwanaume kukumbia majukumu yake na kukimbilia mengine ili akiacha watu wahangaikie na majukumu asilia ya kwake then HAPANA.
hivi mfumo dume hasa uwa ni upi? mimi hua nasikia wanautaja wakati wanazungumzia kupiwga kina mama, kuachiwa kazi ngumu etc kwa upande huu siwezi kuongea sana ila sipendi familia ya hivi.
Nilimaanisha kuwa, mwanaume kwa maumbile, ni lazima atumike na awe mwangalizi. kama atanunua mikuki na kulinda sungusungu, au ataweka walinzi, au atasimamia uwepo wa security alarms, inabidi imkae kichwani, ukiona mama ndio anahangaika na kama alarms, walinzi kama wamekuja, kama mbwa ni wakali, wamekula au kucheki milango imefungwa usiku, inabidi ujue significance yako inapotea
pia ukiona familia watoto wanakula usichojua, wanafunga na kufungua shule bila kuulizwa, wanaugua nakupona bila wewe kujuuliza, mama na watoto wanavaa mwaka mzima h ujihusishi lazima tukushangae