Mwanaumme ni nini?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,463
911,172
Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?

Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?

Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?
 
Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?

Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?

Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?

Mwanamke ni nini haswa?
 
[MENTION]Mwanamke ni nini haswa?[/MENTION]

CHUAKACHARA

Tujibu mwanaumme ni nini kwanza khalafu ya bibie tutayaangalia baadaye.......
 
Last edited by a moderator:
[h=2][/h]
hili shairi ni zuri sana hususani kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.. well done kaka mkubwa Ruta

ndetichia...............thanks
 
Last edited by a moderator:
ulipotelea wapi? Nilikumissije

BADILI TABIA........................nimebadili tabia siku hizi mwonekano wangu jamvini ni wa kimanati sana..................ingawaje sinati........
 
Last edited by a moderator:
Mhhh!
kadiri siku zinavyoenda swali linazidi kuwa zito
Kwangu mie wa zamani,
mwanaume (sio kijana)
- awe ana ambition - maono, au matamanio, au muelekeo unaoonekana na sie tunaomuangalia
- awe realistic na hali ailonayo kwa wakati ule yani ajijue, na mipango yake ianzie hapo,
- mimi nilisoma na nikaamini kuwa mwanaume anatakiwa awe ana mtazamo wa kutafuta solutions kwa vitendo, awe anasukumwa na kutafuta mambo boda zaidi kwa matendo sio kwa maneno, yani akiongea kuwa ni kwa kuelekea kwenye solutions sio kuzunguka zunguka tu kwenye stori then kuacha hewani, (mfano stori za mpira kwa wasiocheza wala kujiunga na vyama vya mpira)
- anakuwa mwanaume pale anapokuwa amepata ile sense ya kuwa mwangalizi, kuwa responsible kwa watu wengine, watoto, wazee, mke jamii. anapokuwa anajisikia kuwatunza na kujipa jukumu la kutimiza mahitaji yao, anapoacha kujifikiria mwenyewe kwa aslimia kubwa

Hii ya mwisho ndio inapungua sana siku hizi
mtoto wa kiume (over 25) haoni shida wala aibu kuomba, tena kuomba kwa wazee au wasichana. Mimi inanitatiza sana.
wavulana wanatilia mkazo nguo, viatu, perfume, saluni kuliko wanavyofikiria jinsi ya kuikwamua jamii yao,
unakuta kijana bajeti yake yote inaishia huko, akijua au akidhani kuwa kwa kuwa wazazi au wadogo zake hawamuombi hela, hawamuhitaji,
Basi japo kuwa na tabia ya kujipa jukumu la kulipa umeme, au la kununua uniform, jpo hukaombwa!!!
jamani mnakera!
 
Rutashubanyuma hoja hii ni tatizi,
Ni hoja tata vizazi hata vizazi,
Siyo hoja ya wajenzi wala wapagazi,
chanzo chake ni nyumbani, aina ya malezi,
Umelelewaje?

Kwani kwenu mko vipi, ni kipi cha thamani,
kwenu shujaa ni yupi, yule mnaye thamini
Nani kwenu ni kapi, asiyetakiwa nyumbani,
Kipi mnachothamini?

Kama nguo ndiyo mali, Elimu ni vuvuzela,
Basi hata wanawali, wamachinga watawala,
Watapenda suruali, elimu kwao jalala
Mnakuzwaje?

Uanaume ni sifa, si maumbile ya jalali
Uanaume si shufaa, au uwe jabali
Uanaume ni kufaa, jamii ikukubali,
Ni sifa ya uongozi.

Siyo kuvunja vitanda, au hodari kufanya,
Uanaume sawa sanda,hutunza si kutapanya,
Uanaume si kupinda, au tabia za panya
Uanaume utu wema

Mwanaume huwa kinga, kiongozi familia,
Hana sifa za kijinga, masuala hufuatilia,
Kama likizuka janga, hawezi kulia lia
Ni sifa ya Utume.
 
Last edited by a moderator:
Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?

Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?

Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?

mwanamume siyo kuvaa suruwali
 
Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?

Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?

Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?

Ushujaa na uzuri wa Mwanaume ni nguvu za kiuchumi.
 
Kwa hali ya sasa Mwanaume ni Vitu Mbili... URIJALI(AFYA) na PESA......
 
rutashubanyuma hoja hii ni tatizi,
ni hoja tata vizazi hata vizazi,
siyo hoja ya wajenzi wala wapagazi,
chanzo chake ni nyumbani, aina ya malezi,
umelelewaje?

Kwani kwenu mko vipi, ni kipi cha thamani,
kwenu shujaa ni yupi, yule mnaye thamini
nani kwenu ni kapi, asiyetakiwa nyumbani,
kipi mnachothamini?

Kama nguo ndiyo mali, elimu ni vuvuzela,
basi hata wanawali, wamachinga watawala,
watapenda suruali, elimu kwao jalala
mnakuzwaje?

uanaume ni sifa, si maumbile ya jalali
uanaume si shufaa, au uwe jabali
uanaume ni kufaa, jamii ikukubali,
ni sifa ya uongozi
.

siyo kuvunja vitanda, au hodari kufanya,
uanaume sawa sanda,hutunza si kutapanya,
uanaume si kupinda, au tabia za panya
uanaume utu wema

mwanaume huwa kinga, kiongozi familia,
hana sifa za kijinga, masuala hufuatilia,
kama likizuka janga, hawezi kulia lia
ni sifa ya utume.
asante mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom