Mwanaumme ni nini?

Namchukia mwanaume asiyejua majukumu yake!!!huwa ananikera wa hvyo kila k2 mpaka aambiwe naomba hiki!nataka hiki vikorokoro kibao akumbushwe,mwanaume ni mwanaume tu hakuna cha haki sawa wanawake wanacheza mchezo ambao hawatakuja kushinda kamwe.
 
kwangu mimi mwanaume ni yule anayejiamini,anayejipenda na kupenda wengine,msafi wa mwili na roho(kiroho inaweza isiwe 100% as no 1 is perfect before God),aniheshimu na kunijali,nimdekee na yeye adeke kwangu,asiyeboa ,pia awe ni mtu ambaye hata ukiwa nae unajiamini kwenda nae popote yaani asichague maeneo flan afu mengine aweke mipaka!
 
Rutashubanyuma hoja hii ni tatizi,
Ni hoja tata vizazi hata vizazi,
Siyo hoja ya wajenzi wala wapagazi,
chanzo chake ni nyumbani, aina ya malezi,
Umelelewaje?

Kwani kwenu mko vipi, ni kipi cha thamani,
kwenu shujaa ni yupi, yule mnaye thamini
Nani kwenu ni kapi, asiyetakiwa nyumbani,
Kipi mnachothamini?

Kama nguo ndiyo mali, Elimu ni vuvuzela,
Basi hata wanawali, wamachinga watawala,
Watapenda suruali, elimu kwao jalala
Mnakuzwaje?

Uanaume ni sifa, si maumbile ya jalali
Uanaume si shufaa, au uwe jabali
Uanaume ni kufaa, jamii ikukubali,
Ni sifa ya uongozi.

Siyo kuvunja vitanda, au hodari kufanya,
Uanaume sawa sanda,hutunza si kutapanya,
Uanaume si kupinda, au tabia za panya
Uanaume utu wema

Mwanaume huwa kinga, kiongozi familia,
Hana sifa za kijinga, masuala hufuatilia,
Kama likizuka janga, hawezi kulia lia
Ni sifa ya Utume.
Mkuu umetisha!
 
Uanaume ni sifa,yafaa kila jinsia,
Julikane kitaifa,ili ipate tulia,
sije kuwa kama "fifa",na mpira kufifia,
Uanaume juhudi...

Usije dhani ni rika,Siku moja tafikia,
wala sio ushirika,ndani yake kuchangia,
Uanaume pirika,ngaikia masulia,
Uanaume ni dhima....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom