Mkakati wa kuelekea Ikulu

kapingili

Senior Member
Jul 4, 2012
155
192
MKAKATI WA KUELEKEA IKULU - 1
.
IMEANDIKWA NA : HUSSEIN WAMAYYA
*********************************************************************************
Simulizi : Mkakati Wa Kuelekea Ikulu
Sehemu Ya Kwanza (1)

Utangulizi
Wakati Baba wa Taifa anamlea Masurufu Hussein Masurufu hakuwa anajua kuwa analea mtu ambaye alikuwa amechoshwa na udhalili wanaoishi wapigania uhuru.

Hakujua pia kuwa mzazi mwingine wa Masurufu alikuwa mstaafu wa uliokuwa Muungano wa Afrika Mashariki na ambaye licha ya kuutumikia Muungano huo kwa nguvu na uwezo wake wote, bado ameishia kudhalilika wakati akidai mafao yake kiasi cha kufikia kuvua nguo hadharani.

Hakujua pia kuwa hizo ni sababu chache miongoni mwa nyingi zilizomfanya Masurufu huyu aanze kuhubiri utakatifu huku akifanya uhalifu baada ya kupata nafasi na kuzitumia vyema fursa za Vita vya Kagera, Uhujumu uchumi, Ubunge, Uwaziri na baadae ubalozi wa Tanzania nje ya nchi.

Na sasa akishirikiana na Christopher MacDonald Beberu wa G-8 Original, Masurufu anajiandaa vyema kwenda Ikulu kwa lengo moja tu, kuzinyonya rasilimali za Tanzania mpaka tone la mwisho…!
Ikoje hiyo safari yake?

SURA YA KWANZA
UHOLANZI - JANUARI 2005
Zilishapita siku za kutosha toka Dr. Masurufu na watumushi wenzie katika Ubalozi wao kule Uholanzi wafanye mkutano. Na ilishapita miaka tisa toka Dr. Masurufu alipoteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi hiyo. Asubuhi hii akiwa ndiyo kwanza ametoka kuoga, mkewe akaingia ndani na kumuuliza.

“Habari za Asubuhi Baba Rose!”
“Nzuri tu, sijui za kwako” Anajibu hali akijifuta maji kwa taulo. Mkewe anafungua kabati na kumtolea suti safi.
“Zangu pia njema!”
“Ulikuwa wapi?”
“Nilikuwa namuhimiza Rose awahi shule. Mwenzie Dan keshaondoka saa nyingi!”
“Oh!Vizuri!” Masurufu akaanza kuvaa nguo.
“Una habari mume wangu?”
“Habari gani?”
“Rais wa nchi yetu ya Tanzania anamaliza muda wake mwaka huu. Nasikia chama tawala kitaanza kugawa fomu mwezi ujao!”
“Sema haki ya Mungu!”
“Haki ya nani tena!”
“We habari hizi umezipata wapi?” Sasa Dr. Masurufu alikuwa akivaa viatu.
“Redioni. Idhaa ya kiswahili ya BBC. Zimetangazwa asubuhi wakati ulipokwenda kuoga!”
“Enhe!” Dr. Masurufu akaacha kufunga kamba za viatu na kumtazama mkewe kwa mshangao. “Wamesemaje?”

“Katibu Mkuu amesema fomu zitaanza kutolewa mwezi ujao kwa watanzania wenye sifa. Gharama yake itakuwa shilingi milioni mbili kwa kila fomu. Kutoka hapo itakubidi uzunguke nchi nzima kutafuta wadhamini kabla ya kurudisha fomu mwezi unaofuata ambapo chama kitayapitia majina ya wagombea safi na kuyapeleka kwa wajumbe wa Kamati kuu kwa uamuzi wa mwisho!”

Masurufu akamaliza kuvaa viatu, mkewe akamuongoza mpaka eneo la kupatia chakula ambako kulikuwa na chai ya nguvu. Akasema.

“Kikao kilichopita nilitoa onyo kali kwa wale watumishi wenzangu ambao walidhani wanaweza kuniendesha kama yule Balozi aliyepelekwa Singapore. Hiki ni chuma cha pua bwana hawataniweza katu ha…ha….haaah!” Akacheka. Mkewe akatabasamu tu. Dakika chache baadae tabasamu lilizimika akarudi ndani ya tafakuri tena.

“Mpenzi mke wangu!” Dr. Masurufu akamwita “Kwa nini una majonzi mpenzi? Huonekani kuwa mke wangu niliyekuzoea. Kulikoni?”
“Huu Uchaguzi laaziz!”
“Ndiyo!”
“Una nini ?”
“Huujali kabisa!”
“Siujali ndiyo!”
“Kwa nini huujali?”
“Unatuhusu nini? Ingawa sisi ni watanzania, tuko maili nyingi nje ya Tanzania. Sidhani kama una athari kwetu!”
Kicheko cha uchungu kikamponyoka Glady mkewe! Akamwambia “Kwa taarifa yako, uchaguzi huu unatuhusu sisi zaidi, kuliko unavyowahusu watanzania wengine!”

“Kwa namna gani dia?”
“Swali zuri, sisi tunaitegemea Serikali iliyopo madarakani kutuweka huku Ubalozini. Ikimaliza muda wake na kuondoka hatutaipata tena fursa ya kuishi kivulini hapa Uholanzi. Hatutaipata nafasi ya kuishi katika kasri hili wala hatutapata wasaa wa kutembelea magari haya ya kifahari. Hii ni pamoja na watoto wetu kuacha kusoma shule za kimataifa na kwenda kubanana na akina kajamba nani huko uswahilini. Bado tu hujali?”

Yakamuingia Dr. Masurufu. Akavua miwani na kuisafisha “Unajua kwa nini sijali?” Akairudisha miwani usoni.
“Sijui!”
“Yupo mtu anayenifanya nisijali. Mtu ambaye amechangia kwa asilimia kubwa mimi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi. Mtu huyu ni Profesa Zonga!”
“We’ ndiyo uko nyuma kweli kweli. Huyo Profesa Zonga ndio atasababisha uteuliwe tena?”
“Ndiyo! Hata akiingia nani pale Ikulu, sisi tutaendelea kuula tu. Watake tutaula, wasitake tutaula!”
“Yaelekea unajiamini kupita kiasi baba Rose?!”
“Kwa nini nisijiamini mama watoto?! Dawa zake ninatumia vizuri, masharti yake ninatimiza. Gari nimemuachia. Nyumba nimemjengea. Kwa nini nisijiamini?! Kwa nini?”

Mkewe akashusha pumzi za kukata tamaa.

“Lakini mume wangu, utakuwa Balozi mpaka lini? Lini na sisi tutakuwa viongozi wa juu kabisa wa Taifa letu la Tanzania, tukiandikwa na vyombo vya habari kila tunapokohoa, tukilindwa kama miungu wadogo, tukimiliki uchumi wote wa nchi?
Saini yako ikiamua juu ya kuishi au kufa kwa mtu yeyote. Ukiwa Amiri Jeshi Mkuu unayeheshimika, zulia jekundu likikulaki kila unapokuwa ziarani! Kwa nini hutaki neema hii mume wangu?”

Dr. Masurufu akavuta tafakuri kwa muda. Akasema, “Tatizo ni watu laaziz, watanikubali kweli? Watu watanipa nafasi?!”
“Watu ndio kitu gani?”
“Una maana gani?”
“Labda ungezungumzia fedha. Kama huna fedha kabisa, labda hicho kinaweza kuwa kikwazo. Lakini watu?! Mbona ukiwa na fedha ni rahisi kupata chochote unachotaka. Seuze watu! Na wewe fedha unazo!”

“Lakini hazitoshi kufanya kampeni katika chama na nchi nzima.”
“Zinatosha mume wangu. Zinatosha kabisa Dr. Masurufu! Jiulize una rasilimali kiasi gani, una marafiki wangapi wanaokuunga mkono ndani na nje ya nchi. Hapa hapa Uholanzi wapo zaidi ya kumi. Hao ni wale uliopata kunitambulisha na kuwaleta nyumbani ambao kwa kinywa chako umekiri kwamba ni wafanyabiashara wakubwa ambao hawazungumzii milioni bali bilioni!”

“Hilo ni kweli!” Masurufu akaafiki.
“Bado hujanitambulisha wa nje ya hapo. Ambao sina shaka unao wa kutosha!”
“Ni kweli ninao wa kutosha!”
“Unataka kuniambia wote hawa ukiwaendea kuwaomba msaada na sio msaada hasa bali wakuazime na ukishaukwaa urais tu utawarudishia. Unataka kuniambia watakataa wote?”
“Glady, unafahamu vizuri sana kama kitu hicho hakiwezekani!”
“Kumbe kinachokufanya uhofie ni nini?”
“Hofu yangu iko kwenye kuanguka. Watu wanaweza kula fedha zako halafu wakakunyima kura!”

“Mawazo kama hayo mtafutaji hatakiwi kuwa nayo, lakini pia huwajui watanzania vizuri. Watanzania wana ukarimu uliopatiliza. Wanakumbuka hisani kama sio fadhila hata katika hali inayokatisha tamaa kabisa. Wakishakula fedha zako hawatakuwa na zaidi ila kukupigia kura wakifika katika sanduku la kura.

Kwa sasa ukiwazungukia marafiki zako wa ndani na nje wakatupa walau bilioni mbili tu, hesabu utakuwa umeshinda tayari. Niulize kwa nini!”

“Kwa nini?”
“Ukiwa na fedha hizo, ukaongezea na zako haidhuru hata zikafikia bilioni nne au tano. Unaweza kuanzisha gazeti lako ambalo si tu litakuwa likikupigia debe kama mgombea safi, mgombea chaguo, mgombea unayefaa na kupendwa na wengi, usiye na kashfa na kadhalika na kadhalika. Lakini pia, gazeti lako hilo litashiriki kwa siri kuwachafua na kuwapaka matope wagombea wengine kwa hila , wagombea ambao watakuwa tishio kwako!”

“Enhe, nikingali nakusikiliza!” Dr. Masurufu alianza kusisimkwa.
“Huo hautakuwa mwisho, utawanunua wahariri na wamiliki wa vyombo vingine vya habari pamwe na waandishi wao, ambao kazi yao itakuwa ni kukufagilia mpaka chama kitakapokupitisha ambapo hutalazimika kutumia nguvu katika Uchaguzi Mkuu kwa vile chama na Serikali yake vitakusaidia kwa nguvu zote, mpaka unaingia Ikulu!” Masurufu akakenua
“Je,” Mkewe akahitimisha kwa swali akitabasamu “Bado tu una hofu?”

“Hapana, sina hofu kabisa!” Alijibu Masurufu kwa moyo mweupe kabisa.
“Kwa hiyo tunakwenda kupigana siyo? Kupigana kwa ajili ya maslahi yetu, kupigana kwa ajili ya urais wetu, kwa ajili ya kuiweka Tanzania ya sasa na ijayo mikononi mwetu siyo!”

“Ndiyo mke wangu!”
“Ahadi?!”
“Ahadi!”
“Good!” Glady akafurahi akitabasamu. Alikuwa amefaulu kumfanya mumewe arudi katika reli. Arudi kuyatazama maisha katka mwanga bora. Mwanga ambao kama utawamulika vizuri utawafanya waingie katika historia ya nchi na kuishi kama sio kukumbukwa milele. Heshima iliyo


SURA YA PILI
KIGOMA - 1952

Wakati Tanganyika inapata uhuru mwaka 1961, Masurufu Hussein Masurufu alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili akiwa darasa la pili katika shule ya Mkoloni. Alikuwa kijana shababi na umbile lake liliashiria kuwa atakuja kuwa jitu la miraba mine baadae. Alijaaliwa sura jamali iliyowavutia wengi ingawa mwenyewe hakulijua hilo kwa wakati huo.

Baba yake Kepteni Hussein Masurufu alikuwa katibu Mkuu wa TANU kanda ya magharibi kanda iliyojumuisha mikoa ya Kigoma, Tabora na Rukwa. Yeye akiishi Kigoma Mjini.

Akiwa miongoni mwa wazee wa awali wa Tanganyika walioianzisha TAA na baadae kumkaribisha Nyerere kabla hawajamchagua kuwa Mwenyekiti wake, Hussein alikuwa ameshiriki kwa kina katika harakati za kuisambaza TAA na baadae TANU, na kupigania Uhuru mpaka hapo ulipopatikana

Kuipenda kwake TAA hakukuja bure, alijikuta akiipenda TAA kupita kiasi baada ya kuchoshwa na utawala wa kibabe na wa kidhalimu wa wakoloni wa Ujerumani na baadae Waingereza.

Awali alikuwa chini ya wajerumani Kapteni wa meli, akiendesha meli za MV Lyemba na MV Mwongozo zilizokuwa zikitoa huduma katika ziwa Tanganyika kwenda katika nchi za Zambia, Burundi na Zaire (sasa Congo), kupitia katika vijiji vilivyopo katika mwambao wa Ziwa hilo lenye kina kirefu kuliko yote Afrika. Katika Dunia likishika nafasi ya pili baada ya lile la Bekari lililopo Urusi. Alikuwa akilipwa mshahara mzuri wa wastani uliomfanya awe na maisha mazuri tofauti na wananchi wengi ambao walikuwa hawaishi kuwatupia lawama wakoloni kuwa hawafai hawafai.

Yeye akiwa na kisomo cha darasa la nane, kilichomuwezesha kuzijua lugha za kingereza, kijerumani, kigiriki na kiitaliano sawasawa, mke mzuri, nyumba bora, mshahara wa kutakata na mengine mengi, kamwe hakuona ubaya wa wakoloni mpaka ilipofika siku ile.

Siku ambayo alikuwa anakabiliwa na safari ya kwenda Zambia na baadae Zaire. Kama kawaida alijilawa asubuhi na mapema na kuelekea bafuni. Aliporudi mswaki ukingali mdomoni na taulo likiwa mkononi ndipo mambo yalipoanza kuwa mambo.
Mkewe ambaye alikuwa mjamzito mwenye mimba ya miezi nane na ushei alikuwa akigaa gaa huku na huko kitandani mdomoni akiachia mayowe yaliyoashiria kuwa alikuwa ndani ya Uchungu uliopatiliza

Taulo likatupwa kushoto mswaki ukindondoka mdomoni bila yeye kuwa na habari akakimbia kimbia hovyo mle ndani akishika hiki na kile bila uelekeo maalumu baadae akili zikamrejea, akamjongelea mkewe na kumuuliza

“Fatuma…. Fatuma, vipi mpenzi?!”
“Na… na…. nahisi siku zimefika!” Akasema kwa taabu akishusha pumzi kwa nguvu. Maumivu yakamzidi katika nyonga.
“Kwani hujaenda kliniki tena?”
“Nilienda! Niitie gari Hussein”
“Madaktari walisemaje?”
“Gari Pliz, gari tafadhali”
“Bila kujua tatizo ita…!
“Hussein!” Fatuma akabweka kwa nguvu machozi yakimtoka kwa wingi. Hussein Masurufu akashtuka, “Naam!” Akaitika kwa woga!
“Unataka nife?”
“Oooh! No hapana…. Hapana mahabuba wangu nakupenda sana!”
“Basi ita gari Upesi!”
Wakati anainuka akayaona majimaji mazito yakichuruzika katika miguu ya mkewe. Akaogopa zaidi umakini ukimpotea akaondoka upesi akielekea sebuleni akajigonga katika mlango na kuanguka chini.

“Shit!” Akaguta akiinuka na kuingia sebuleni.
Akaifikia simu ya mezani na kupiga hospitali kuomba aletewe gari la wagonjwa. Baada ya kuelekeza vya kutosha, alirudi tena sebuleni kwa mkewe, akawa akiugulia pamoja nae. Ingawa huu ulikuwa uzazi wake wa kwanza, na uchungu ulikuwa ukimsumbua bado, lakini mafundisho aliyoyapata kabla hajaolewa na Hussein Masurufu yalikuwa yakingali mabichi kichwani mwa Fatuma.

Alimuagiza mumewe amuandalie kanga na pamba za kutosha katika mkoba. Alimwambia pia amchukulie kadi ya kliniki chupa la chai na vingine vingi.

Kutahamaki gari lilishafika
Fatuma alichukuliwa mpaka katika hospitali ya Maweni akapokelewa na kupewa kitanda. Manesi wakimuakikishia Hussein kwamba mgonjwa wake angejifungua baada ya muda mfupi.

Dakika kumi baadae akawa ndani ya Teksi no. 7 Peugeot 404 mali ya mzee Shaka wakieleka Kasingirima Ujiji aliko mama mzazi wa Fatuma Malilo. Ambako alifika anamzoa na kuja nae hospitali.

Kichwa chake kikiwa hakitulii, Hussein Masurufu alirandaranda hospitali nzima bila uelekeo maalumu mpaka zilipokuja zile taarifa za faraja masaa sita baadae, kwamba mkewe alikuwa amejifungua mtoto wa kiume kwa operesheni ndogo.

Furaha zilizomvaa hazikuwa na mfano, “Nami nitaitwa baba! Nimemzaa baba yangu! Mzee Masurufu Laiti angelikuwepo!” Aliendelea kufurahi nusunusu mpaka waliporuhusiwa kuingia wodini na yeye kukabidhiwa mtoto ambebe! Akambeba kwa furaha na bashasha, tabasamu likiupamba uso wake. Walifanana kama reale kwa ya pili

Waliporuhusiwa na kurejea nyumbani, ndipo akili zilipomrejea Hussein kwamba alitakuwa kuwa ndani ya meli ya Liemba muda huu akiwapeleka abiria Zambia, Zaire na baadae Burundi. Ukweli huu ukafanya akiliye iingiwe na ganzi.

Aliwafamu waajiri wake vizuri sana kosa dogo tu la kutosafisha sakafu vizuri lingeweza kukugharimu kibarua. Au wizi wa mali ya shirika wakati chombo kikiwa safarini, hukumu yake ilikuwa kutoswa baharini na kupoteza maisha yako.

Akajifikiria yeye!
Meli ilitakiwa kuondoa saa mbili kamili asubuhi. Inapeleka abiria. Abiria waliolipa pesa zao, pesa ambazo zinampa yeye mshahara. Mpaka muda huu saa nane mchana yeye alikuwa hajatokea bandarini
Masaa sita mbele!

Akajipeleka ofisini kama ambavyo mbwa hujipeleka mbele ya chatu tayari kuliwa! Yeye akiamini kwamba alikuwa na sababu ya msingi. Sababu ya kuokoa maisha ya mkewe na maisha ya mwanae.

* * *
waajiri wake vizuri sana kosa dogo tu la kutosafisha sakafu vizuri lingeweza kukugharimu kibarua. Au wizi wa mali ya shirika wakati chombo kikiwa safarini, hukumu yake ilikuwa kutoswa baharini na kupoteza maisha yako.
Akajifikiria yeye!

Meli ilitakiwa kuondoa saa mbili kamili asubuhi. Inapeleka abiria. Abiria waliolipa pesa zao, pesa ambazo zinampa yeye mshahara. Mpaka muda huu saa nane mchana yeye alikuwa hajatokea bandarini

Masaa sita mbele!
Akajipeleka ofisini kama ambavyo mbwa hujipeleka mbele ya chatu tayari kuliwa! Yeye akiamini kwamba alikuwa na sababu ya msingi. Sababu ya kuokoa maisha ya mkewe na maisha ya mwanae.

* * *
Hussein hatakaa aisahau siku ile. Maana alimkuta mwenyeji wake Meneja uajiri akiwa mwekundu amefura kwa hasira. Hakupewa hata nafasi ya kusikilizwa, alitupiwa barua ya kufukuzwa kazi akingali mbali wa hatua tano hivi toka ilipo ofisi ya Meneja.

Maneno ya kashfa kejeli na dharau yakimfuta huku akimtimua na kumfukuza ki-mbwa kinguruwe!
Katika mambo yote hili Hussein hakulitarajia. Kufukuzwa kazi?! Kwa staili hii? Hata kama alikuwa na makosa bado alikuwa na haki ya kusikilizwa, haki ya kuachishwa kistaarabu na mengine mengi. Ni hili lililomfanya asiondoke licha ya matusi na kashfa alizopewa.

“Tokah!” Von Duzy Meneja uajiri akaunguruma “Toka unasuburi nini? Sitaki uingie ofisini kwangu wala sitaki kukuona hapa teena. Tokah!”
“Ungenisikiliza kwanza lakini!”
“Eti nini?” Kicheko cha Uchungu kikamtoka Von. “Sikiliza wewe Sokwe mweusi usiye na mkia. Baada ya hasara yote uliyotutia bado unataka tukusikilize? Umefanya tuingie gharama ya kumkodia mtu ndege kutoka Zambia aje apeleke meli? Tumekupigia simu hupatikani tumekuja nyumbani kwako haupo, la hapana wako wengine wa kuvumilia sio sisi. Tokaah!”
“Ndio, ungenisikiliza sasa!”
“Sitaki, tokaah!”
“Nilikuwa na matatizo…!”
“Tokaah!”
“Mke wangu ame…!”
“Tokaah!”
“Lakini…!”
“Tokaah!” Hasira zikaanza kumpanda Hussein. Mikono ikanza kumchezacheza hali akili yake akishindwa kuidhibiti sawaswa. Naye akabweka!
“Sitoki! Sitoki sasa!”
Von akageuka na kumtazama vizuri, zaidi akimshangaa. Hussein akaendelea
“Kama mnadhani kunifukuza ndio tumemalizana mnakosea. Nimekuwa mfanyakazi wenu kwa karibuni miaka 10 sasa. Bado nina wadai haki zangu nyingi tu, tena za msingi kabisa.”

“ Haki?” Von akauliza kama ambaye hakulisikia vizuri neno lile.
“Ndiyo haki!” Hussein akaunguruma tena.
“Haki gani?”
“Kwanza mafao, nataka nipewe pesa zangu za kiinua mgongo!”

“Oooh!” Alikuwa Von kwa dharau, kumbe unataka haki; ngoja nikuletee. Von akavuta hatua ndefu ndefu mpaka pale aliposimama Hussein. Alimpofikia tu bila kuchelewa akaupeleka mkono wake kushoto na kuurudisha kwa nguvu, ukatua vizuri sana katika shavu la kulia la Hussein na kulia Paah! “Ukiambiwa uwe unaelewa kenge we!” Ikawa kauli iliyosindikiza kofi.

Kofi kali la Kelbu.
Hussein akayumba mara mbili kwa nguvu na kwenda chini sikio lake la kulia likipiga mbinja ya kukata na shoka. Alikuwa amepigwa na kitu kama ubao vile. Shavu lote lilikuwa linawaka moto vibaya sana.

Kupigwa?! Hussein akashangaa zaidi ya alivoumia. Hakuwa na kumbukumbu kama aliwahi kupigwa toka kule shule ya msingi ambapo alichapwa fimbo mbili tu kutokana na mwenendo wake mzuri.

Hasira sasa zikauvaa mwili katika namna ambayo hakuweza kuihimili. Akaimuka kama zombie, akamkamata Von na kumkunja kunja huku akimsuka suka kwa nguvu kabla hajampigiza chini mara mbili.

Pamoja na Von kujitahidi kupambana na Hussein bado alijikuta chini mara kadhaa mpaka nguvu zilipomuishia ambapo aliamua kupiga filimbi ya hatari iliyofika inatuama kunako masikio ya walinzi wake vibaraka.Wakaja mbio na kumdhibiti Hussein.

Hapo ndipo Von aliposimama akaanza kumtandika Hussein makonde mazito mazito katika katika tumbo, mbavuni, usoni na pengine popote alipoweza kupiga. Alimtandika hasa, alimtandika kweli kweli. Kutoka hapo mashataka yakaandaliwa ombi likapelekwa kwa DC na baadae mahakamani. Kesi ikapelekwa haraka haraka, hatimaye Hussein akafungwa jela miezi tisa na kazi ngumu.

Hakuna cha mafao, hakuna haki, hakuna kusikilizwa, hakuna kila kitu na kifungo juu.

Alipotoka kifungoni, kila kitu kilikuwa kimebadilika! Kila kitu. Alikuwa amepoteza kazi, wamefukuzwa katika nyumba ya Shirika mwanae alikuwa na afya mbaya huku akiwa hana uhakikia wa chakula; Hali wajerumani wakiwa wameondoka tayari na nafasi yao kuchukuliwa na Waingereza. Ni hili lililomfanya awachukie wakoloni.
Akaapa kupambana nao.

Kupambana kwa hali na mali. “Ni aibu kutawaliwa!” Aliropoka mara kwa mara akiwahamasisha wenzake kuungana pamoja ili kumtia adabu Mjerumani, “Umoja ndiyo nguvu yetu. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu!” Aliendelea kuhamasisha. Watu wakaendelea kumuunga mkono.

Halafu akasikia kitu
Kwamba akina Abdulwahid Sykes, Dossa Aziz Dossa na Tewa Said Tewa walikuwa wameanzisha chama, Tanganyika African Association TAA. Chama cha kudai na kupigania uhuru. Zilikuwa zaidi ya habari njema. Haraka akaruka hadi Pwani akaeleza dhamira yake na kupokelewa kwa mikono miwili akapewa kanda nzima ya magharibi ahangaike nayo.
Akarejea nyumbani na kuhangaika nayo.

Hata Nyerere alipojiunga na TAA baada ya juhudi zake na wenzake za kuanzisha chama cha kupigania Uhuru wa Tanganyika yeye na wenzake kule Makerere kukwama, alikuta wakina Hussein wameshafanya kazi kubwa hasa. Kazi ya kutosha kama sio kujivunia.

Kwa sababu ya usomi na uwezo wake wa kujenga hoja, kushawishi wachilia mbali Busara na hekima alizokuwa nazo, Nyerere akapewa Uongozi mara moja katika mkutano uliofanyika Tarehe 17 April 1953 katika ukumbi wa Arnatouglo; huku waanzilishi wakikaa pembeni kwa hiyari yao. Wakibakia kuwa washauri. Na hatimaye ikaundwa TANU badala ya TAA chini ya Nyerere.

Na matunda yakaonekana. Ghafla TANU ilivuma na kupaa kama dege la kivita. Kila mmoja aliisikia. Kila mmoja akaipenda kuitamani, kuikubali na kuihubiri. Nchi ikawa haitawaliki kwa raha. Kila mara, kila mahali ikawa ni kelele za Tunataka Uhuru! Tumechoka kutawaliwa!

Wakati huu akiwa anatawala Muingereza hali ilikuwa mbaya zaidi, watu walipigwa na wengine kuuawa wakidai na kuulilia Uhuru, wakiupigania ujamaa na kujitegemea wakiuhami umoja na mshikamano hadi ilipofika ile siku.

Siku ambayo Nyerere alisimamama katika baraza la Udhamini la la Umoja wa Mataifa pale New York Marekani na kuuhutubia Ulimwengu. Akawaambia Waingereza sasa inatosha! Mmeshatutawala kiasi cha kutosha, Tunataka nchi yetu, Tunataka Uhuru!

Kama mnadhani kwamba hatuna uwezo wa kujitawala mmekosea sana. Tupeni nchi yetu kisha mje kuitazama tena baada ya miaka kumi tu. Mtaona jinsi tutakavyokuwa tumeboresha huduma, mtaona tutakavyokuwa tunaishi kwa upendo, amani na mshikamano, mtayaona matunda matunda ya uhuru wetu, mtaona… mtaona!

Nyerere akasema mengi na vingi. Hotuba yake ikamvutia na kumsisimua kila mmoja. Mmoja wapo akiwa Malkia wa Uingereza. Huyu aliamua kumtembelea Nyerere jioni yake Akamsaili hili na kumuuliza lile. Akapokea maelezo timilifu yaliyomtosheleza. Mpaka anaondoka, moyo wake ulikuwa safi na usio na chembe cha shaka juu ya Tanganyika.

Hatima ya mkutano huo ikawa ni Nyerere kurejea tena Uingereza kwa mara kadhaa na aliporudi kwa mara mwisho, Uhuru wa Tanganyika ukawa umepatikana.

Kila mmoja hakuamini. Kila mmoja alifurahi kupita kiasi. “Hatimaye!” watu walinong’ona baada ya kuona bendera ya Mwingereza ikishushwa na kupandishwa ya Tanganyika “Mwingereza amesalimu amri! Shenzi taip!” walihitimisha.
Miongoni mwa watu ambao hawakujiweza kwa furaha alikuwa Kepteni Hussein Masurufu. Yeye alicheka mpaka nguvu zikamuishia. Akacheka mpaka machozi yakamtoka.

Aliitamani alie, apae juu hadi juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro akaitangazie dunia kuwa wamefaulu kuirudisha nchi mikononi mwa watanganyika, akatamani laiti angeweza kufyatuka atoke mbio aende mpaka kule bandarini ili akampashe yule bwege, gabachori wa kijerumani Von. Kwamba nchi imerudi mikononi mwa wenye nayo, wananchi! Na kwamba afungashe kila kilicho chake arudi kwako.

Hakuweza kufanya lolote kati ya hayo, na hii ilikuwa ni baada ya kujikumbusha kuwa Wajerumani walishaondoka kitambo. Akaishia kucheka tu. Alicheka na kucheka na kucheka. Watu walipomuulizia jibu lake lilikuwa moja tu “Yako wapi?
Wangemuulizia zaidi angeanza kuimba ule wimbo maarufu wa uhamasishaji “Wako wapi waliowakijigamba sasa twawataka! Tumekwisha kuwakanyagaa..!”

“Huu Uhuru unatufanya tuwehuke sasa!” Mmoja alihitimisha wakiondoka.

* * *
Akiwa amekwishakuwa mwanasiasa mzoefu, Kepteni Hussein Masurufu alikataa tena kurudi kuendesha meli, kazi aliyokuwa akiifanya awali. Hili lilijiri wakati kamati kuu ya TANU, ilipoketi chini ya Uenyekiti wa Rais Nyerere na kuamua kipi kiende wapi baada ya Uhuru.

Kwa kuzingatia historia yake na mchango wake katika chama, Hussein alikuwa amepewa kuisimamia Bandari ya ziwa Tanganyika. Akawashangaza watu pale alipokataa jukumu hilo. Alipotakiwa kutoa sababu zilikuwa tele, kwamba ameshazoea harakati, kwamba umri ulikuwa unaanza kumtupa mkono na hadhani kama angeweza kuhimili mikikimikiki ya Bandari. Akataka aendelee kuwa Mwanasiasa.

Ni hapo alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa TANU kanda ya magharibi ili aendelee na siasa. Aendelee kufanya ile kitu roho yake inapenda. Aliifanya kazi hiyo kwa miaka michache kabla hajateuliwa kuwa Katibu Tawala wa kanda ya magharibi, wadhifa aliondelea nao hadi alipostaafu miaka mingi baadae. Masurufu angali anakumbuka vizuri sana.

Kwamba kitendo cha baba yake kustaafu kilikuwa kama kukata mzizi wa mwisho wa mawasiliano baina yake na TANU na viongozi wa Serikali.

Vile alikuwa kiongozi bora na siyo mtawala, vile alikuwa mkweli wa maneno na vitendo, vile ambavyo alichukia ubepari na kukataa kujilimbikizia mali kama walivyo Nyerere, Kawawa na wengineo, Kapteni Hussein Masurufu alijikuta hana pa kushika.

Hakuwa amejilimbikizia mali, rasilimali pekee aliyokuwa nayo lilikuwa shamba la michikichi la ekari tano ambalo ndani yake kulikuwa na kibanda cha kuishi kilichokandikwa tope na kuezekwa Bati huko katika mashamba ya Ruwanda kando kando ya mto Luiche.

Baada ya kustaafu na kutoka katika nyumba za shirika la nyumba la Taifa pale Mwembetogwaalikokuwa amepangiwa, Hussein Masurufu alikwenda kuishi katika kibanda hicho yeye na familia yake. Wakati huu mwanae Masurufu alishakuwa mkubwa akielekea kunako balehe, sasa akiwa anasoma middle school.

Maisha mapya baada ya kustaafu katika viunga hivi vya mto Luiche yalikuwa mabaya na yaliyoumiza sana waliishi kwa kutegemea kilimo ambacho nacho hakikuwa msaada wa kujivunia.

Hali ikiwa hivi kwa upande mmoja upande, upande wa pili mafuriko hayakuwaonea huruma hata kidogo, yaliwajia mara kwa mara na kusomba mazao kama sio mifugo yao. Yalisomba hata akiba ya chakula walikuwa wamehifadhi ghalani kwa ajili ya baadae.

Nguvu zikiwa zimeanza kumtupa mkono, Hussein kwa msaada wa mwanae Masurufu alifanya kila alichoweza kutaka kuonana na viongozi wa TANU ili wafikishe kilio chake makao makuu ambako wangeweza kumsaidia.

Jibu alilopewa mara zote lilimtia matumaini
“Suala lako linajulikana na linashughulikiwa njoo mwezi ujao, kila kitu kitakuwa sawa!” Sekretari angemjibu lakini angekuja tena huo mwezi ujao jibu hili hili lingekuwa linamsubiri tena. Mara hii alipojibiwa tena hivi mwanae Masurufu hakukubali “Lakini mwezi uliopita ulituambia hivyo hivyo” akakumbusha kwa hasira.

“Mimi nakueleza nilichoambiwa!” Alikuwa Sekretari wa Mwenyekiti kijeuri kabisa.
“Ndio maana nimekwambia leo tunahitaji kumuona. Vyovyote iwavyo lazima tumuone. Hatutaondoka hapa hadi tumemuona!”
“We bwana ni kiziwi, hayawani au kitu gani?” Sekretari akauliza kwa karaha akiacha kujipodoa kwa muda na kumtazama Masurufu kwa jicho kali. Akaendelea, “Nimekwambia Mwenyekiti hayupo mwezi wa pili huu. Anahudhuria semina za Utawala bora kule Ngurdolo! Semina zitachukua mwezi mzima!”

“Basi tumuone Katibu mkuu!”
“Hayupo pia! Wameondoka pamoja!”
Kitu fulani kikamfanya Masurufu ashindwe kuondoka hapo, akimtazama baba yake, akifikiria shida walizonazo kule shamba na yale mafuriko ya wiki iliyopita ambayo yaliwachukulia akiba yote na kuwaachia roho zao katika tundu la sindano baada ya wao kuparamia paa la nyumba, akaona leo hawezi kuondoka mpaka kimeeleweka.

“Kwa hiyo?” Akauliza tena. “Shughuli za hapa kwa wakati huu anazifanya nani? Au wameondoka na ofisi yao?”
Jicho alilotazamwa lilitosha kuwa jibu.
“Si nimekuuliza dada yangu!”Akakazania.
“Anakaimu Mapunda! Program 0fficer!”
“Tunaomba tumuone huyo huyo, pengine hujui tu. Lakini wenzio tuna tatizo na kuendelea kwenu kutupiga kalenda kunatuumiza zaidi.”
“Naye hayupo! Msubiri pale katika benchi la ofisi yake.”
Alipomaliza kuwaambia hivyo akageukia kioo chake na kuendelea kujipodoa! Hussein na mwanae wakaenda na kuketi.
Mapunda aliingia ofisini saa tisa mchana. Alikuwa na haraka mno. Akawasikiliza kidogo na kuwaambia, “Suala lenu linashughulikiwa! Njooni wiki ijayo!”

Hussein ambaye wakati huu hakuwa muongeaji sana alimtuliza mwanae na wakaondoka na kurejea shambani kwao. Njiani alisononeka sana kutosikilizwa, thamani yake kutoonekana na vibinti vidogo vidogo kutomtambua na kumdharau kana kwamba alikuwa si lolote si chochote.

Masononeko hayo na hali halisi ya maisha waliyoishi vilimchosha, kumuudhi na kumuumiza sana mwanae Masurufu. Akajikuta anaanza kukichukia chama, Serikali na viongozi wake.

Binafsi hakuona ni vipi chama kilishindwa kutengeneza mifumo ya kuwasaidia watu waliojitolea jasho na damu katika kupigania kufikisha chama hapo kilipofika. Hakuona ni vipi walishindwa kumjengea mzee wake nyumba ya kisasa, kumpa gari ya kutembelea na nyenzo zingine za kuboreshea maisha katika wakati huu ambapo nguvu zilikuwa zimemtupa ukweli wa kumtupa.

“Bahati yake!” Hussein alimsikia mwanae akiropoka kwa bahati mbaya, mara tu walipomaliza kujenga zizi jingine. Akamsaili kwa macho na kugundua kwamba ingawa Masurufu alikuwa jirani yake pale alipoketi juu ya mtumbwi; lakini alikuwa maili nyingi nje ya pale kifikra.

Ilikuwa ni katika wakati huu Hussein alipopata fursa nyingine ya kumwangalia mwanae vizuri. Alikuwa kijana barobaro hasa, videvu vikianza kuchomoza kidevuni misuli iliyokaidi kukaa vizuri katika mikono yake ilikuwa imevimba na kutokeza hapa na pale katika mikono yake na kuashiria kitu kimoja tu, kuwa itakuwa mikono yenye nguvu.

Ile sura ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa imeanza kuachana na ujamali, sasa ilikuwa imerandana na ya kwake ikiashiria upole na utulivu siku zote. Kifua kipana na mwili wa wastani, upole, utaratibu, busara na hekima vilimfanya Hussein atabasamu tena. Alikuwa amejizaa “Bila shaka litakuwa jitu la miraba minne”

ni katika wakati huu Hussein alipopata fursa nyingine ya kumwangalia mwanae vizuri. Alikuwa kijana barobaro hasa, videvu vikianza kuchomoza kidevuni misuli iliyokaidi kukaa vizuri katika mikono yake ilikuwa imevimba na kutokeza hapa na pale katika mikono yake na kuashiria kitu kimoja tu, kuwa itakuwa mikono yenye nguvu.

Ile sura ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa imeanza kuachana na ujamali, sasa ilikuwa imerandana na ya kwake ikiashiria upole na utulivu siku zote. Kifua kipana na mwili wa wastani, upole, utaratibu, busara na hekima vilimfanya Hussein atabasamu tena. Alikuwa amejizaa “Bila shaka litakuwa jitu la miraba minne”

Akanong’ona, akiendelea kumuangalia mithili ya msanii anayeangaliwa kazi bora kabisa aliyoifanya kwa mikono yake.
Halafu wazo likampata. Itakuwaje mwanae akiwa mwanasiasa, kama yeye? “Bila shaka na yeye ataishia katika maisha haya!” Akawaza kwa uoga akijitahidi kuyafukuza mawazo haya.

Lakini ikamshangaza mawazo haya yalipoonyesha ukaidi, yakarudi kumtembelea tena tena. Katika mawazo haya alimuona mwanae katika picha na vyeo vya kisiasa. Ubunge, Uwaziri na kadhalika, akipitia huku na huko akifanya mambo makubwa kama akina Nyeree, Kawawa, Sokoine, Karume na wengine.

Vyombo vya habari vikimsimulia kama kiongozi wa mfano, mtu wa watu kama baba yake, akialikwa huku na huko kufanya shughuli za kijamii zenye tija. Akiwa havumilii uozo wa aina yoyote, hana tamaa ya utajiri, muadilifu, mwenye kukubali matakwa ya jamii, mtu wa watu n.k.

Huku yeye Kapteni Masurufu wakati huo licha pengine ya umri wake kuwa umeenda sana akisimama kidete kumshauri kufanya haya na yale, historia yake ikiendelea kudumu masikioni mwa watu kupitia kwa mwanae Neema iliyoje! Fahari iliyoje? Akawaza tena tabasamu lake likikomaa zaidi.

Bila shaka, akaendelea kuwaza kwa furaha hali tabasamu likiwa bado limeupamba uso wake. Nchi itakimbia vibaya sana. Utendaji wake utawaambukiza vijana wengi kama sisi tulivyoambukizwa uadilifu na Nyerere, na hapo Tanzania itaelekea moja kwa moja katika nchi ya maziwa na asali bila wasiwasi wowote tena… “Bahati yake!” Sauti ya mwanae ikatoka tena kwa ukali ikayakata mawazo yake. Akaacha kuwaza na kumtazama Masurufu kwa mara nyingine tena. Bado Masurufu alikuwa mbali kifikra. Akamsogelea taratibu na kuketi jirani yake. Akamtikisa mwanae taratibu, akimuuliza.
“Bahati yake nani?”

Mwanae akashtuka na kutaharuki “Hapana!” Akasema kwa hofu na kuongeza “Hakuna kitu!”. Hussein akamkazia macho na kumsaili tena
“Kwani nani amesema kuna kitu?”
Masurufu akababaika asijue mzee wake amekusudia nini hasa Akajikusuru “Si wewe umeniuliza?”
“Ndiyo nimekuuliza, Bahati yake nani? Sijakuuliza kama kuna kitu!”
Masurufu akashindwa kujibu. Mzee Hussein akaendelea “Mara mbili nimekusikia ukitamka kwa dhati bahati yake! Tena ukiwa hatua nyingi nje ya hapa kifikra. Ndio maana nikaona nikurudishe tusadiane kufikiri usiumize kichwa peka yako mwanangu!”
Masurufu akatahayari.
Akashangaa jinsi alivyokosa umakini hata akaruhusu maneno kutoka nje ya kinywa pasipo ridhaa yake. Hakujua ametamka mangapi akiwa katika hali hiyo. Hata hivyo akajikakamua na kusema “Leave it baba, yaache tu. Hayawezi kukusaidia!”
“Kwa nini?”
Akashusha pumzi. “Nahisi kama ni ya kijinga. No! yaache kama yalivyo baba!”
“Masurufu!” Hussein akaita kwa upendo. Mwanae akaitika “Naam!”
“Umeanza lini tabia hii?”
Masurufu akatatanishwa, akainua uso na kumtazama baba yake. Akajikuta akitazamwa mfano wa fundi aingaliavyo saa ya thamani kutafuta tatizo liisumbuavyo. Akashindwa kuyakabili macho ya baba yake na kuangalia chini haraka.
“Tabia gani?” Akauliza kwa sauti isiyo yake!
“Ya kunificha mambo yako?”
“Kukuficha mambo yangu? Mambo gani baba?”

“Mambo yako ndiyo!! Mara hii umesahau kwamba mimi ndimi baba yako, rafiki yako mpendwa na mwandani wako pekee. Ambaye daima nimeondokea kuwa mshauri, kiongozi na msiri wako mkuu. Ulidiriki kuniambia hata habari za Glady msichana ambaye ungependa awe mkeo baadae! Mbona hayo hukutaka niyaache yalivyo?! Halafu ujinga unaoweza kukutoa mbele yangu na kukupeleka maili nyingi nje ya hapa, ni ujinga ambao kila mzazi mwenye mwanae angependa kuusikiliza. Au ndio umekuwa sana siku hizi?”

Masurufu akajiona mwenye hatia.
“Mimi najua!”Aliendela kushutumu mzee Hussein “Najua lipo jambo. Tena jambo kubwa, jambo linaloitafuna akili yako kiasi hata cha kuondoa kama sio kuathiri umakini wako. Na kwa taarifa yako mimi ninamjua sana Mwanangu Masurufu. Huwa hapotezi umakini kizembe.

Toka ulivyomaliza kazi niliyokutuma na wewe kuketi juu ya mtumbwi huo, nimekuwa jirani yako nikikuangalia na kufuatisha kila akitendo chako, ambapo nimegundua mengi tu! Ndio maana nakuuliza umeanza lini tabia hiyo?” Akahitimisha Hussein.
Hatia zikamuelemea Masurufu, machozi yakamtoka. Akainuka na kwenda kupiga magoti mbele ya baba yake. Huku machozi yakiendelea kumtoka akamwambia kwa majuto.
“Samahani baba, nimekosa!”

Baba yake akamuinua pale chini na kumketisha jirani yake kwa upendo uliotukuka. akamfuta machozi huku akinong’ona “Haina haja ya kulia! Usilie kijana wangu. Kulia ni tukio la mwisho unaloweza kufanya baada ya kutokea kitu ambacho hukipendi na jitihada zako zote zimeshindwa kukizuia.

Mimi na wewe hatujafika huko bado tukingali tuna nguvu nyingi uwezo mzuri wa kufikiri na njia nyingine mbadala. Tafadhali yahifadhi machozi yako leo, ili siku utakapoyahitaji uweze kuyatumia kikamilifu sawa?” Akatua na kumeza mate
Masurufu akaafiki kwa kutikisa kichwa
“Good!” Baba yake akasema kwa furaha “Sasa niambie huyo unayemwambia bahati yake ni nani?”
“Nyerere!” Masurufu akajibu pasipo kutafuna maneno
Ilikuwa sawa na nyundo iliyogongwa katika kichwa cha Kapteni kwa nguvu, Akahisi akipepesuka mithili ya bondia aliyepigwa konde la maana jukwaani. Akauliza kwa mshtuko.
“Umesema nani?”

“Nyerere! Julius Kambarage. Baba wa Taifa la Tanzania!” Masurufu alirejea jibule kwa sauti thabiti. Safari hii akimtazama baba yake usoni, kuashiria kwamba alikuwa na uhakika na anachokinena.
“Kwa nini?” Mzee Hussein akasaili kwa macho.

Jibu la Masurufu kwa baba yake likawa kuyasaili mazingira wanayoishi kwa macho. Ile nyumba ya tope ya vyumba vinne na sebule mbili ambayo iliezekwa bati ndiyo kilikuwa kitu pekee cha thamani.

Vingine viivyofuatia vilichusha na kuudhi. Zizi bovu la ngo’mbe na mbuzi ambalo halikuwa na mifugo ya kujivunia, mabanda ya kuku ambayo nayo yalikuwa matupu baada ya mafuriko kuwachukua. Ghala lisilo na kitu, Mashine ya kukamulia mafuta, michikichi michache isiyo na afya na pengine siha ya kuridhisha pamoja na kutokuwa na uhakika vilikwisha baadhi ya vitu vilivyoyafanya mazingira yao kuwa duni hasa, duni kwa maana halisi.

Kamwe maisha haya hayakumstahili mtu aliyepigania uhuru kwa jasho na damu yake. Hayakumfaa hata kidogo mtu aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama na katibu Tawala wa Kanda ya magharibi katika Serikali ya wamu ya kwanza. Hayakumstahili hata kidogo.

Ilikuwa ni baadae sana Masurufu alipoanza kueleza
“Chama kimekutelekeza baba, Serikali hali kadhalika. Jinsi ulivyokitumikia na kukitendea sivyo kinavyokutendea wewe. Nimefikiria sana baba, halafu nikajaribu kubashiri mwisho wa maisha yetu nikagundua utakuwa mbaya na unaodhalilisha kama sio wa kuabisha.

Ni haya yanayoyonifanya nikione chama na Serikali katika jicho hasi, ambalo daima dawamu huwa halivutii hata kidogo. Na bahati yake alivyoufuta upinzani na vyama vyake. La sivyo mimi ningejiunga na upinzani, nikashirikiana na akina Kasangatumbo, Kasela Bantu, Kambona na wenzao kuwaeleza wanachi ukweli hata wakauona ubaya wa chama na Serikali yake. Ningekuwa na mifano hai Mingi wewe ukiwa mmoja wao!”

Hussein akatabasamu
Mwanae alikuwa anaanza kuiva kisiasa. Uwezo wa kuunganisha mambo na mazingira, na kisha kuufanyia uchambuzi mzito, ulikuwa unalithibitisha hilo vizuri kabisa. Kwa upande mmoja akauhusudu upande huu, lakini kwa upande mwingine hakuvutiwa na njia aliyotaka kupita mwanae. Njia ya chuki dhidi ya Nyerere na Serikali yake. Chuki dhidi ya chama tawala.
Hapana ninahitaji kufanya kitu. Akajiambia akimwambia mwanae.

“Penginse uko sahihi mwanangu, pengine hauko sahihi. Ninachotaka kukwambia ni hiki, humjui Nyerere mwanangu. Humjui baba wa Taifa na katika hili kumlaumu au kumchukia ni kumuonea bure.

Mimi nimefanya kazi na Yule mtu. Ni mtu muadilifu mfano hakuna, msikivu, mtulivu na mwaminifu hujapata kuona. Mtu anayewatazama wenzake kwanza. Anayeitazama nchi yake kwanza! Sisi ametulea hivyo na ndio maana unaona hatukujilimbikizia mali japo uwezo huo tulikuwa nao.

Mali hizo tuliwawekea ninyi, nanyi mnatakiwa kuzitunza kwa manufaa ya vizazi vyenu. Unachosahau ni kwamba, Nyerere sasa ni kiongozi wa juu kabisa nchini. Ana watu na matatizo mengine mengi ya msingi. Na tena usisahau kuwa mimi ni mwakilishi wa kanda moja tu ya magharibi.

Wapo wa kanda ya mashariki, kanda ya kati, kanda ya Nyanda za juu kusini, kanda ya Kaskazini na kanda ya pwani. Na kote kuna watu zaidi ya mmoja, ukisema aboreshe mazingira ataboresha mazingira ya wangapi? Na rasilimali za kufanya hivyo ziko wapi hali unajua kuwa nchi yetu ni miongoni mwa nchi masikini kabisa duniani?

Mbona mie tayari nimepewa kiinua mgongo? Nimejenga na kufuga ingawa Mungu hakupenda. Nadhani kutokuwa na uhakika wa maisha ya kesho kunatokana na sisi kutokuwa na kazi. Unaonaje nikikutafutia kazi mwanangu?” Akahitimsha. “Hakuna taabu!” Masurufu akakubali akitafakari maelezo ya baba yake. Alikuwa na hoja, ingawa haikuwa na nguvu kiasi kile. Kama Serikali inaweza kuwahudumia makatibu Kata, Tarafa, Wakuu wa wilaya, Mikoa, Wabunge, Mawaziri, Waalimu, Wanajeshi na wengineo, inashindwaje kuwaangalia hawa wapigania Uhuru? Ambao idadi yao haifiki hata mia mbili?

Eti kiinua mgongo! Akawaza kwa hasira. Kiinua mgongo gani ambacho kimeshindwa hata kuigharamia elimu yangu hapa hapa nchini? Hivi wabunge na mawaziri nao wanalipwa kiinua mgongo kama hiki. Kama sio ugawaji wa rasilimali za taifa usiozingatia jinsia ni nini? Katika hali hii unawezaje kukiita kiinua mgongo?! Hapana hiki ni kiua mgongo kabisa.

Na je, hivi yeye Nyerere anaishi maisha kama haya ya Hussein Masurufu kule Ikulu? Mjadala ulikuwa mkali sana kichwani mwake. Na aliufanyika kichwani mwake kwa vile alimjua vizuri baba yake, kwamba Demokrasia ilikuwa imemuingia hadi katika mishipa ya damu yake na kuweka hifadhi ya kudumu ndani ya mifupa na chini kabisa ya moyo wake.

Kubishana na huyu ni kujisumbua. Akaamua kukubaliana nae kwa nje huku ndani akimpinga vibaya sana. Bahati yake hakuna upinzani! Masurufu akarudia kuwaza tena, baada ya kukubaliana na mzee wake, na mzee huyo kuondoka. Kungekuwa na upinzani imara ningejiunga na kumuondolea mbali! Akahitimisha.

* * *
Wiki iliyofuata walirudi tena ofisi za chama pale mkoani Mapunda akawapokea na kuipeleka shida yao kwa Mwenyekiti. Mwenyekiti naye akuwazungusha kwa siku kadhaa mpaka Masurufu alipomlilia machozi ofisini. Ambapo alisutwa na dhamira akajikuta akimshughlikia kikamilifu, wakapata fedha za kutosha kiasi.

Pesa ambazo, Hussein alizitumia pia kama nauli kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kwenda kuonana na Nyerere!
Walipokelewa vizuri sana, na kupelekwa nyumbani ambako waliandaliwa chakula cha maana. Chakula maalumu wakala na kusaza kama vile haitoshi wakaletewa hiki na kile na mradi tu wajisikie wako nyumbani.

Jioni Nyerere alirudi, akaketi na kuzungumza pamoja nao. Kapteni Hussein alimueleza maisha anayoishi sasa na jinsi alivyo na taabu. Machozi ya uchungu yakamtoka Nyerere.

“Pole sana!” Akamwambia kwa upendo “Kwanini hukwenda pale makao Makuu na ukawaeleza yako?”
“Nilikwenda lakini sikupolewa vizuri. Nimezungushwa karibuni miezi sita!”
“Kitu gani?” Nyerere akaghadhibika

Hussein Masurufu akamueleza kila kitu tokea walivyoanza kufuatilia, dharau walizoonyeshwa, ahadi za njoo kesho na mengine kadha wa kadha hadi pale walipompigia magoti na kumlilia Mwenyekiti ofisini kwake ambapo aliidhinisha pesa kidogo walizopewa.
Kilichofuatia hakuna aliyekitarajia.

Kwa kutumia simu,Nyerere alimuauru Katibu Mkuu wa TANU Taifa kuushughulikia Uongozi wa mkoa Kigoma kwa vitendo walivyomfanyika Kapteni Hussein na familia yake, akaomba kupewa taarifa zake ndani ya wiki moja
“Mie sitapenda uwafukuze kazi?” Hussein alimwambia baadae Hasira zilipotulia. Nyerere akamtazama kwa mshangano, kabla hajamuuliza baadae.
“Kwa nini?”

“Ningependa waonywe tu, ili kama watarudia tena, ndippo hatua hizo zichukuliwe maana wana familia zinazowategemea! Kuwaondoa pale itawafanya wao na hasa familia zao kuishi katika wakati mgumu na m’baya zaidi!”
Nyerere akatafakari tena akishangazwa na moyo wa mtu huyu.

Hata hivyo alitabasamu alipoona kuwa falsafa yake ya Ujamaa na lile azimio la Arusha vilikuwa vimewakaa watu wake katika namna iliyomfanya hata wakati mwingine awaogope. Walikuwa na huruma mno! Wakawa na upendo uliopitiliza huku wakiiweka nchi na raia wao mbele.

Pamoja na ukweli kwamba wao walikuwa washika wadau wakuu, walihakikisha washikiwa dau wengine hasa jamii wamenufaika vya kutosha ndipo na wao walipofikiria kunufaika. Bahati mbaya washikiwa dau hao walikuwa wengi mno, wengi hasa! Kuwanufaisha wote ingekuwa shughuli pevu kweli kweli, pevu haswa! Kwa maana hiyo wao waliendelea kusubiri mpaka mdau wa mwisho afikiwe…, ndipo wajifikirie na wao!

“Any way!” Akasema baadae. “Tuache hayo, tuzungumze yetu, nimemleta kijana! Nataka umsaidie kupata kazi ili naye anisaidie kuishi. Pamoja na kazi nataka pia umfundishe siasa!”

Nyerere akamtazama Masurufu kwa muda na kutikisa kichwa. Alikuwa kama anayemuangualia Kapteni Hussein enzi za ujana wake. Akaulizia elimu yake na kuambia darasa la sita.

Nyerere akamtazama Masurufu kwa muda na kutikisa kichwa. Alikuwa kama anayemuangualia Kapteni Hussein enzi za ujana wake. Akaulizia elimu yake na kuambia darasa la sita.

Alipouliza sababu ya kutohitimu, jibu lilikuwa lile lile, umaskini ulioikumba ghafla baada ya yale mafuriko. Nyerere akasikitika tena.
“Itabidi asome kwanza!”
“Hilo silikatai, lakini kwa sasa huyu ndio mboni yangu. Namtegemea kwa kila kitu. Nilitegema mshahara atakaopewa…!”
“Usijali!” Akamkata kalima na kuendelea “Tutafanya utaratibu uwe unapata senti za kujikimu, huyu mwache asome. Akifanya siasa huku ana kisomo atakuwa msaada mkubwa kwa taifa sawa?

“Sawa” Alikuwa Kapteni kwa shingo upande. Hakutaka kuendelea kuwa tegemezi kwa chama na Serikali lakini alipojitahidi alisemee hili, akawa anazidiwa hoja.
Ndivyo ilivyokuwa.

Masurufu akarudi shule, akawa pia miongozi mwa watoto kadhaa waliokuwa wakilelewa na mwalimu. Kapteni Hussein alikaa pale kwa wiki chache kabla hajaomba ruhusa na kurejea nyumbani kwa mkewe. Juhudi za kumtaka abakie hapo ikibidi ailete familia yake zikashindikana.
Kitu kimoja kilikuwa dhahiri kwa Masurufu.

Kwamba mafahali wa uadilifu walikuwa wamekutana! Mazungumzo yao na mapendekezo yao kuhusu maisha na familia zao yakawa yamemfanya ajifunze kitu kikubwa maishani. Kwamba ni muhimu kuishi kwa ajili ya watu, kwa ajili ya makundi yaliyo pembezoni. Ili utakapoondoka duniani uwe umetimiza wajibu wako wa kuletwa hapa duniani. Jamii ikukumbuke na uendelee kuishi milele.

Pia akagungua kuwa kumbe Nyerere hakuwa mtu mbaya. Alikuwa mtu mzuri kwa maneno na vitendo, akifurahia kuona mabadiliko na maendelo ya kweli ya watu wake. Lakin ah! Laiti angeliweka utaratibu wa kuonana na watu wake mara kwa mara na kusikiliza shida zao…
Akaendelea kusoma akiongeza bidii na juhudi katika masomo.

* * *
Ki’ uhakika kabisa, Masurufu aliacha kabisa kumchukia Nyerere na CCM. Badala yake akampenda na kumthamini. Akawa jirani nae akimuomba ushauri huu na ule pamoja na kumsaidia kazi hizi na zile. Ni katika wakati huu Nyerere alipogundua akili na Busara za kijana huyu. Naye akajikuta akimpenda na kumuamini.

Shule alihitimu vizuri akajiunga jeshi la kujenga Taifa baadae akaenda Chuo kikuu kuchukua Digrii ya Sayansi na utawala wa jamii miaka mitatu baadae akarudi na kuwekwa Makao Makuu ya chama ofisi ndogo pale Lumumba, akisaidia hiki na kile pamoja na kuisaidia ofisi ya umoja wa vijana.

Hakudumu sana, akapelekwa Kigamboni kuongeza ujuzi wa kisiasa na kupelekwa nje ya nchi mara kadhaa. Aliporejea akapewa kazi ya kuwaandaa vijana kuwa wanasiasa bora, kupenda siasa ya nchi yao na kupenda kujitolea kwa ajili ya nchi yao.

Kazi alizozifanya kwa moyo mmoja. Matokeo yake yalishangaza kama sio kustaajabisha. Vijana wakatokea kuwa wazalendo wa kweli , wakiijenga nchi yao kwa kasi ya aina yake.

Hali ikiwa hivi, akili ya Masurufu ilikuwa haitulii kila kukicha yeye alikuwa akitafuta mwanya wa kujilimbikizia mali, kuchuma zaidi. Hakutaka kuja kuishi kama babaye yake.

Katika Upenzi huo baina yake na Nyerere, alikuwa amefaulu kutembelea mikoa mingi na akawa amejionea kwa macho yake namna wastaafu wengi wakiwemo mawaziri jinsi wanavyoishi maisha duni kwa kutegemea kilimo na mifugo, huku jamii ikiwacheka na kuwaona mabwege. Wakitolewa mfano usiofaa na kususuikwa hata na watoto wadogo.

Hapana! Haya siyo maisha!! Masurufu akaamua kwa dhati. Leo Nyerere yupo, kesho atakuwa hayupo. Nisipogangamala na kuuanika katika kijua hiki, ntautwanga mbichi.
Kweli akagangamala

Alihubiri na kufundisha uadilifu huku yeye akifanya uhalifu. Kila ulipotokea mwanya aliutumia kikamilifu kwa maslahi yake binafsi kwa manufaa ya baadae. Kila alipotumwa mahala, hakusita kujipa majukumu ya ziada.

Majukumu ambayo yalimkutanisha na wafanyabiashara wa magendo, wakwepa kodi, majambazi wa kalamu na wengineo. Ambapo aliwatisha na kuwaambia ametumwa na Nyerere awashughulikie. Kitambulisho chake halisi na kile cha bandia vikimtisha yeyote aliyeonyesha ukaidi.

Naam! Alifanikiwa, akaunti na miradi yake ambavyo alivifungua kwa majina bandia na mikoa tofauti zikinenepa taratibu. Alipohisi uwepo wa msako wa wahujumu uchumi waliopenya kwenye chujio la azimio la Arusha, Upesi akazihamisha pesa zake nchini na kuzifungulia akaunti nje ya nchi.

Bahati ikawa yake, yeye akapewa ukuu wa kuendesha msako huo. Ilikuwa neema nyingine. Waliokamatwa na kufikishwa mbele ya sheria ni wale tu ambao yeye hakuafikiana nao, au walileta ujuaji na kujifanya wajuzi.

Nduli alipotuchokoza na mwalimu kutangaza vita, baada ya TANU kuungana na Afro-Shiraz Party na kuzaa CCM; Masurufu naye hakuwa nyuma. Alishirikiana vilivyo kumchapa nduli Amin ambaye alikimbia na kuacha vitu vingi vya thamani katika Ikulu yake.

Yeye akiwa miongoni mwa askari wachache waliongia katika Ikulu ya Uganda na kukuta amana hizo madini yakiwemo, akajikuta akipagawa huku akiomba kimoyomoyo wagawane. Hawakugawana! Badala yake vito hivyo walimpa Masurufu avifikishe kwa Nyerere kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.
Hakufikisha.

Waliporejea kutoka Uganda na yeye kuzifanyia utaratibu wa kuzificha na kuziingiza mali alizochuma katika mkondo halali; akawa amemkabili Nyerere na kumuomba ruhusa aende kwao akagombee Ubunge. Nyerere akamshangaa kwa uamuzi huu, akamuuliza.
“Kwanini umefikiria uamuzi huu Dokta?”

Aseme nini? Akawaza kwa haraka. Ndiyo kwanza akagundua kuwa hakuwa amejipanga kama angeulizwa hivi. Sababu ya kutaka kupata mshahara mnono, saluti, gari la mamilioni, posho hata ukisinzia, lita elfu moja za mafuta kila mwezi, na marupurupu mengine, hazikuwa sababu ambazo zingemvutia Nyerere.

“Nataka kuwa karibu na baba yangu!” Akatamka baada ya kufikiri kwa muda “Nataka kuwa jirani nae. Nataka kuwapigania watu wa jimbo langu, kusaidiana nao kuboresha maisha na miundombinu yetu! Nataka… Nataka..”

Alisema vingi na mengi! Nyerere alimsaili zaidi na zaidi kabla ya kuridhika na kumpa ridhaa. Akamuuliza tena, “Vipi vijana wako pale Umoja wa vijana?”

“Hakutaribika kitu!” Akamjibu kwa unyenyekevu. “Nimeacha kila kitu katika mstari. Boniface ataendelea pale nilipoishia. Ni mmoja kati vijana wangu ninaowaamini. Na Kigoma sio kuzimu mwalimu nitakuwa nikirudi mara kwa mara kuangalia maendelo ya pale nilipoishia. Isitoshe kuna simu, naweza kupigiwa na kuambiwa hivi au vile nami nikatoa ushirikiano wangu!” Akamalizia.
Ilitosha.

Mwalimu akainama kutafakari. Masurufu ambaye sasa alikuwa Daktari wa filosofia alikuwa na sababu za msingi. Vile alikuwa kijana mwenye busara na hekima huku akifanya kazi kwa nguvu zake zote, Nyerere akajaribu kuuhisi upweke ambao ungemtawala baada ya Masurufu kuondoka.

Hata hivyo akajirudi pale alipogundua kuwa Dokta Masurufu sasa sio mtoto tena ingawa angali alikuwa akihitaji ushauri wa hapa na pale. Ushauri utakaomfanya aendelee kuwa Masurufu halisi liwazo na chaguo la watu.

“Dokta” Nyerere akasema akingali ameinama kwa tafakari “Sio uamuzi mbaya! Sio uamuzi mbaya hata kidogo. Bahati mbaya na mimi nang’atuka, Uchaguzi ujao sitagombea Urais wa nchi hii tena, miaka ishirini na mitano niliyokaa Ikulu ni mingi sana, inatosha. Nastaafu! Nawapa nafasi wengine.

“Kitu gani?” Dokta akashtuka. Zilikuwa habari mpya kwake.

“Umesikia vizuri. Ukigombea Ubunge na kushinda kisha Rais atakayeteuliwa akakuwekea katika Baraza la mawaziri, nchini itakimbia vibaya sana.

Ni hili linalonifanya nikuruhusu kwa moyo mkunjufu. Maana hata nikiendelea kukuzuia bado unatakiwa uwatumikie watanzania wote ambao ni muhimu kuliko mimi mmoja, watanzania ambao kwa hakika wanahitaji mchango wako ili kufanikiwa. Nenda baba, nenda ukatimize wajibu wako wa kuletwa hapa duniani! Nenda!”

Nyerere alisema mengi kumuasa Masurufu. Haikuhitaji digirii kujua kuwa Nyerere alikuwa anaumizwa na kutengana na kijana huyo. Lakini angefanya nini? Akamruhusu.

Labda ambacho hakukijua na ambacho kilikuwa chini kabisa ya moyo wa Dokta Masurufu ni ule ukweli uliotisha. Kwamba Masurufu huyu, hakuwa yule Masurufu anayeonekana mitaani kila siku akihubiri na kutenda upendo, midomo yake imejaa maadili na macho kubeba utakatifu.

Huyu alikuwa Masurufu mwingine chui katika ngozi ya kondoo. Masurufu mwenye pipi mdomoni hali mikono yake ikichuruzika damu. Masurufu mwenye hofu ya umaskini unaochusha na kuudhi baada ya kustaafu.

Ilikuwa vigumu kwa Nyerere kujua. Kwani Masurufu aliyafanya haya kwa hila sana, wakati mwingine katikakati ya usiku mnene huku akiwa kilometa nyingi nje ya macho na upeo wa Nyerere. Wakati huo huo akimpeleka kuzimu yeyote aliyeonyesha kumjua na kutaka kutia mchanga kitumbua chake.

Akaruhusiwa. Akijua anakwenda kuingia katika siasa rasmi, sasa Masurufu aliweza kuandaa washenga waliopeleka posa kwa mpenzi wake Glady. Majibu yalipokuja mazuri na taratibu zingine kufanyika, ndipo Masurufu Hussein Masurufu alipofunga pingu za maisha na Glady Stevenson Ombwe. Ndoa yao ilifanyikia bomani kwa Mkuu wa wilaya.

Akijua anakwenda kuingia katika siasa rasmi, sasa Masurufu aliweza kuandaa washenga waliopeleka posa kwa mpenzi wake Glady. Majibu yalipokuja mazuri na taratibu zingine kufanyika, ndipo Masurufu Hussein Masurufu alipofunga pingu za maisha na Glady Stevenson Ombwe. Ndoa yao ilifanyikia bomani kwa Mkuu wa wilaya.
* * *
ITAENDELEA

Kupata muendelezo Bofya Hapa MKANDA WA SIRI 💣🧨⚰
 
MKAKATI WA KUELEKEA IKULU - 2

Simulizi : Mkakati Wa Kuelekea Ikulu
Sehemu Ya Pili (2)

Kigoma alipokelewa kwa mbwembwe kama shujaa. Dhamira yake ikajulikana mitandao ikaundwa naye akagombea Ubunge wa Kigoma mjini. Ushindani ulikuwa mkali, alitumia mbinu huku akipewa ushauri huu na ule na wazee wa chama Nyerere akiwemo.
Lakini wananchi wakamkataa, kura zikagoma kutosha.
Pengine walimwona mdogo kiumri, pengine walikuwa hawajamzoea na mengine mengi. Sanduku lilipofunguliwa mpinzani wake alikuwa amemshinda kwa kura chache. Akiwa hakutegemea, Masurufu alitaharuki. Akawachukia wananchi vibaya sana. Akapanga kuwafanyika mambo ya ajabu ajabu. Lakin mzee wake Kapten Hussein alikuwa jirani yake siku zote akimfariji kwa maneno mazuri, maneno yatiayo faraja na nguvu.
“Huna haja ya kukata tamaa kiasi hicho. Umri wako bado unaruhusu, damu inachemka. Ni wakati wako sasa wa kufanya maandalizi ili awamu ijayo usifeli tena. Mwenzio imemchukua miaka kumi kujiandaa wewe usingweza kumshinda kwa maandalizi ya miezi sita. Kuchukulie kuondoka kwake kama fursa ya wewe kujijenga zaidi sawa?”
“Sawa!”
Kweli alijijenga. Akaingia mzima katika shughuli za uhamasishaji wa chama akipita hapa na kusema hiki kabla hajashauri kile kule. Upande wa pili akajizatiti na kupanua wigo wa biashara zake alizozifungua kwa majina bandia katika maeneo mbalimbali.
Miaka mitano ilipokatika, Masurufu alikuwa sawa na mti wa mbuyu kwa ukubwa, Kisiasa alifahamika na kukubalika sana. Kijamii alikuwa kipenzi cha watu, katika chama alikuwa kipenzi cha kila mmoja, hali kitajiri akiwa na uchumi imara kabisa! Naam, mtu anayejiweza kwa maana halisi!
Safari hii akaongeza na kitu kimoja zaidi. Akamtafuta Profesa Zonga aliyemsaidia katika ushirikina. Uchaguzi ulipofika aliingia Bungeni kama anamsukuma mlevi vile vile. Nyerere alikuwa angali mshauri mkuu wa Serikali, na kiongozi anayekubalika sana kwa watu. Dokta Masurufu hakushangaa pale alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa viwanda na Biashara, Akapelekwa Nishati na Madini kabla hajateuliwa kuwa Waziri wa Fedha.
Mambo yalikimbia haraka sana, huku mtalamu wake Profesa Zonga akimpa ushauri huu na ule, na kumtaka atimize masharti haya na yale. Vitu ambavyo Dokta Masurufu alivifanya kwa umakini wa hali ya juu.
Huu ulikuwa wakati mwingie ambao kila alichogusa kiligeuka dhahabu na kila alichokanyaga kikawa petroli. Jina lake likaimbwa kila mahala, wazazi wakawapa watoto jina lake. Akawa kiogozi wa kutolewa mfano.
Ambacho wananchi hawakukijua ni kwamba wadhifa huu mpya ulimfanya akutane na watu wenye kiu kali ya utajiri. Kiu ya kupora na kumiliki mali ya umma. Watu hawa wakageuka kuwa marafiki zake na kwa pamoja wakajitengenezea mtandao wao wa kufisadi mali za umma uliokuwa na maafisa wa jeshi, mapolisi, wabunge, mawaziri n.k. kwa lengo la kujinufaisha kwanza wao, mengine baadae.
* * *
Halafu ikaja ile ishu ambayo ilimgharimu hasa. Dokta Masurufu angali anakumbuka vizuri jinsi ilivyotukia kwa bahati mbaya kama mtoto mwenye jnsia mbili. Ilikuwa ishu ya msamaha wa kodi kwa wafanyabiashara wa vifaa vya pikipiki za kichina, wenye asili ya kiasia. Likiwa dili ambalo ameunganishwa na rafikie mpendwa Akimu Yusuph ambaye alimuamini.
Dokta Masurufu akawa amesahau kuchukua tahadhari zake za kawaida, akafanya majadiliano na wafanyabiashara hao katika hoteli ya kawaida ambayo pia kulikuwa na waandishi wa habari. Waasia hao wakamuahidi kumpa mshiko wa kutakata kama angeweza kuwaondolea kodi hiyo.
Akiwa Waziri wa fedha, hii ilikuwa shughuli ndogo sana kwake. Barua moja kwa Mkuu wa Bandari na TRA, vimemo kadhaa kwa watumishi wa bandari na kadhalika na kadhalika vingeweza kumfanya aifanye kazi hiyo kwa wepesi tu. Akaahidi kuwasaidia
Waandishi wakazinasa habari hizo na kuanza uchunguzi siku chache baadae shehena ya mzigo wa spea za pikipiki ukaingia nchini.
Siku hiyo hiyo, Waziri Masurufu akapokea waandishi ofisini kwake ambao walimuuliza maswali kadhaa kuhusu spea hizo na tetesi walizonazo za Spea hizo kutolipiwa kodi. Akawajibu waandishi wale kijeuri na kuwatimua. Waandishi wakaondoka na kwenda kuandika hali halisi.
Habari zilipotoka, Dokta Masurufu alijikuta akiujutia uamuzi wake. Jamii ilizipokea katika namna ambayo hakuitarajia. Vyama vya upinzani vikailaki kama mpira wa kona na kuigeuza ajenda ambapo viliipigia debe huko na huko, hali mashirika yasiyo ya kiserikali yakiandaa matamko, makongamano na maandamano kuipinga na kumtaka Rais amuwajibishe Masurufu
Katika hali hii masurufu alifanya kila alivyoweza kukutana tena na wale waandishi, safari hii na wahariri wake ili kuibalansi habari iliyotoka, jibu alilopewa lilimkatisha tama
“Tungeweza kuibalansi vizuri kabla haijatoka” Alijibu mwandishi mmoja na kuongeza “Lakini sasa haitawezekana, na hili limetokana na wewe kujibu jeuri na kuwafukuza waandishi. Isitoshe walioipokea habari hii tayari wamefanya mengi, tayari wana ushahidi wa kutosha hata sie tukikana haitasaidia!”
“Je” Dokta Masurufu akauliza kwa sauti iliyokata tamaa “…Huwezi kufanya namna yote nikaokoka na hii adha? Kila mahala sasa ni msamaha wa kodi… Msamaha wa kodi!”
“Tunaweza kufanya namna mkuu!” Akasema Mhariri mmoja na kuongeza “Zipo njia za kuifanya habari hii isiendelee”
“Njia zipi na kwa nini zisitumike?”
“Zipo njia mbili ya kwanza ni kuzusha jambo lingine kubwa kuliko hili, na wakati huo huo kuanza kuandika makala za kukupamba na kuwasahaulisha watu kilichotokea! Ila itachukua muda kidogo na itahitaji pesa! Mbinu ya pili ni…”
“Subiri kwanza!” Masurufu akamkata kauli akiwa na wahka. Akaendelea “Niambie!
Itahitaji pesa gani?”
“Kitu kama million tano hivi!”
“Basi andaeni. Pitieni kwa Sekretari wangu atawaandalia cheki hiyo. Nisaidieni leo nitawasaidia kesho!” Aliomboleza Masurufu, hakuiona hata haja ya kusikiliza njia ya pili. Waandishi wakakubali na kuanza juhudi za kumsaidia. Juhudi ambazo zilikuwa sawa na kubwa mithili ya mbegu ya haradali. Hazikusaidia kitu.
Kuona hivi, Dokta Masurufu akakimbilia kwa mtaalamu wake Profesa Zonga wa Zonga. Huyu alikuwa Mtabiri na Mnajimu maarufu wa ndoto. Kiuhalisia hakuwa mganga hasa ila mtundu fulani ambaye aliweza kucheza vizuri na namba pamoja na akili za watu Masurufu akiwemo, kiasi cha kuwafanya watu hao wafanye mambo ambayo wao wenyewe wasingeweza kuyafanya kama Profesa Zonga asingekuwa nyuma yao.
Zonga alimpokea vizuri, akamsaili na kumsikiliza. Akajua Masurufu ana hofu, wasiwasi na ameshakata tamaa. Na dawa ya kukata tamaa aliijua, si zaidi ya matumaini. Akampa moyo, dawa na masharti. Mpaka Dokta Masurufu anaondoka kwa Profesa Zonga, alikuwa na uhakika wa kutosha wa kuendelea kutesa.
Kesho yake akiwa katika kufuata ushauri wa Zonga na kutekeleza masharti yake, Dokta Masurufu alikwenda kumuona Rais kumueleza kilichotokea.
“Masurufu!” Rais alisema akizipanga karatasi zake vizuri pale mezani baada ya kunakili mambo muhimu kutoka katika maelezo ya Dokta Masufuru. Akaendelea “Umefanya vizuri sana kuja na kunieleza yaliyotokea. Ungechelewa zaidi ungekutana na rungu langu kwani nisingevumilia upuuzi wa Serikali yangu kuchafuliwa. Niliunda Tume na imenipa ukweli wote, toka ulivyofanya mpaka mtazamo wa jamii juu ya Serikali yangu. Kwa sasa hali ni mbaya sana, una njia moja tu ya kujinusuru na kadhia na kuendeleza heshima yako ambayo ulikuwa umeanza kujikusanyia! Nayo ni kujiuzulu!”
Moyo wa Dokta Masurufu ukafanya Puuh!
“Kujiuzulu!!” Akashangaa zaidi ya kuelewa Heshima yote, fedha zote, kiinua mgongo chake! Vyote viende na maji? Impossible. Akawaza kwa hasira
“Mheshimiwa…” Masurufu akaita kwa sauti iliyopwaya. Ni dhahiri alikuwa amevunjika moyo vibaya sana “Nitaishi vipi baada ya hapa?! Ndio kwanza nina miaka miwili katika Ubunge na mmoja katika Uwaziri? Ina maana huu ndio mwisho wangu?”
Moyo wa Dokta Masurufu ukafanya Puuh!
“Kujiuzulu!!” Akashangaa zaidi ya kuelewa Heshima yote, fedha zote, kiinua mgongo chake! Vyote viende na maji? Impossible. Akawaza kwa hasira
“Mheshimiwa…” Masurufu akaita kwa sauti iliyopwaya. Ni dhahiri alikuwa amevunjika moyo vibaya sana “Nitaishi vipi baada ya hapa?! Ndio kwanza nina miaka miwili katika Ubunge na mmoja katika Uwaziri? Ina maana huu ndio mwisho wangu?”
“Sikiliza Masurufu! Kujiuzulu siyo mwisho wa maisha, wakati mwingine tunalazimika kutoana kafara ili tuweze kutimiza lengo. Jiuzulu, tusafishe hali ya hewa halafu tutakutana kuona tunafanyaje!” Rais akahitimisha na kuinuka.
Masurufu naye akainuka akiwa na moyo mzito. Safari yake iliishia kwa Profesa Zongo ambaye alimuhakikishia ajiuzulu hakuna shida. Kwamba kila kitu kitakuwa sawa sawa. Nyumbani mkewe naye pia alimshauri kufuata ushauri wa Rais.
Siku iliyofuata akawaita waandishi akawasomea hotuba nzuri aliyoandaliwana mtaalamu wake wa siasa na mwisho hotuba atakangaza kujiuzulu.
Kilichofuata kilikuwa ajabu na kweli.
Mara moja aligeuka shujaa. Mtu wa mfano, kiongozi bora na muwajibikaji. Ikatolewa orodha ya viongozi wenzie ambao wanatuhuma na kashfa nyingi ambao wamegoma kujiuzulu, yeye akatofautishwa nao.
Hakuna aliyekumbuka kuulizia hatima ya zile spea ambazo wakati huu zilikuwa madukani zikiuzwa. Hakuna aliyetoa walau ushauri wa kuchukua kitu kidogo alichopewa ili kitumike katika shughuli za maendeleo ya jamii. Kila moja aliimba Masurufu Shujaa, Masurufu Shujaa.
Aliporudi kwa Profesa Zonga safari hii hakurudi mikono mitupu alikuwa na Bonge la gari, jipya kabisa la kifahari aina ya Landcruiser Wizard. Akamwambia mara aliposhuka.
“Nashukuru mzee, nimeona nguvu zako! Kila mmoja anaimba jina langu! Hii ni zawadi yako” Akahitimisha akimpa fungo na kadi ya gari.
“Tawire” Profesa Zonga akashtuka akimtengea kapu la madawa aweke vitu hivyo. Nusu haamini kama kweli ameletewa gari hilo la kifahari. “Nilikwambia, we jiuzulu tu. Si umeona sasa? Na bado itakuwa zaidi ya hapo we subiri tu!”
“Nashukuru!” Alikuwa Masurufu. “Na je kuhusu wadhifa, ntapata mwingine kweli?”
“Kwa nini usipate? Nyota yako sio chafu tena. Nilishaitengeneza kitambo na sasa inang’ara kweli kweli. Inang’ara mithili ya maua katika jua la asubuhi! Kamwe usiwe na shaka. Midhali Profesa Zonga yungalipo Dokta Masurufu yuko salama siku zote!”
“Nitashukuru Profesa. Nikirejea tena kazini nitakujengea jumba la maana ili iwe kumbukumbu yangu kwako. Najua maadui ni wengi lakini nikiwa na wewe hawatoniweza!”
Dokta aliendelea kushukuru, kabla hajapewa dawa zingine tena na masharti. Waliaagana kila mmoja akichekelea tumboni Zonga akichekelea gari jipya la thamani la chee alilolipata bila jasho, Masurufu akichekelea namna alivyowapatia watanzania na matarajio yake ya kushika wadhifa mkubwa nchini.
Ndiyo ilivyokuwa.
Alipokutana na Rais, Rais alimwambia asiwe na papara. Atulie ayasome mazingira na kufanya kazi yake ya ubunge vizuri. Akatulia na kusoma mazingira akiendelea kuutumikia ubunge na kufanya biashara zake kwa siri.
Muda wa Ubunge ulipokwisha, Rais akamshauri asigombee na uchaguzi ulipokwisha akawa ameteuliwa na Rais kuwa Balozi wa Tanzania kule Uholanzi. Uteuzi huu ulikaribia kumfanya awe chizi kwa furaha. Ukweli huu ulijidhihitisha pale alipojua kuwa atakuwa mbali na vyombo vya habari na macho ya wanoko wengine na hivyo kupata fursa ya kutusua mali za wabongo bila woga.
Ni hapo alipokwenda tena kwa Dokta Masurufu na kuitimiza ahadi yake ya kumjengea nyumba. Akamjengea Bangaluu hasa, kabla hajamleta Uholanzi aizindike nyumba na kumuombea dua njema.
Kuondoka kwa Profesa Zonga, kulimfanya afanye kazi kwa moyo wote akiiendeleza mipango yake kwa nguvu zake zote. Haikuchukua muda sana lile alilolihofia likatimia. Mlezi wake Mwalimu alifariki dunia. Dunia nzima ilatikisika na kuomboleza. Masurufu akalia na kulia na kulia. Akaruka yeye na familia yake mpaka Dar es salaam,Tanzania na baadae Butiama ambako alishiriki kikamilifu katika Msiba wa Baba wa Taifa.
Msiba uliisha, siku za majonzi na maombolezo zikaisha pia hatimaye akarejea Uholanzi.
Kutoka hapo ameishi vizuri katika nchi hiyo ya maziwa na asali hadi ilipofika ile siku ambayo alikuwa ametoka bafuni ambapo alikutana na mkewe Glady aliyempa habari za kusisimua. Habari za Tanzania kuingia katika awamu nyingine ya kinyang’anyiro cha Urais.
Awamu ambayo nae aliamua kwa dhati kuiingia baada ya majadiliano ya kina na mke wake mpendwa. Naam! Dokta Masurufu aliwaza kwa furaha wakati akitoka nyumbani kwake. Naitaka nchi yangu, naitaka Tanzania! Lazima nikae Ikulu na hakuna wa kunizuia!
Akahitimisha akiitekenya stata ya gari yake na kuondoka hali tabasamu lingali limeupamba uso wake. CHRISTOPHER MACDONALD
Safari yake iliishia ofisini kwake ambapo alijikuta akiwa na mambo mengi ya kufanya hali muda ukimfanyia hiyana alipiga simu nyumbani Tanzania kuulizia hili na lile ukiwemo upepo wa kisiasa n.k. majibu aliyopata yakampa moyo na kumfurahisha. Akatengeneza orodha ya mahitaji kabla hajaanza kujipangia mkakati wake wa kuelekea Ikulu. Ulikuwa mkakati mzuri ambao ulimchukulia muda kiasi.
Alipomuonyesha mkewe ambaye alikuwa hodari wa kusoma, akauafiki hadi akatikisa kichwa kwa namna ya kushangaza. Mkakati ulikuwa umemridhirisha katika namna iliyomfurahisha.
“Mkakati safi sana huu. Unahitaji maboresho machache sana kuwa mpango mkakati imara utakaofanikisha kuitwaa Tanzania. Nani amekuandalia?”
“Sionekani kuuandaa mimi?” Alijibu kwa swali masurufu na kuongeza. “Mara hii umesahau kuwa mimi ni bingwa wa kuandaa michanganuo ya miradi ya kijamii na ile ya kibiashara? Kwa kujibu swali lako nimeuandaa mwenyewe. Umenigharimu siku mbili tu kuutengeneza!
“Hongera!’
“Asante!”
Ukimya mfupi ukapita, Glady mkewe akiurejea mkakati kutafuta maeneo ambako alikuwa ameweka alama.
“Glady mpenzi!” Dokta Masurufu akasema akivunja ukimya. Mkewe akaitika “Beeh laaziz!”
“Je” Akauliza “Utafaa?”
“Kwanini usifae! Nimekwambia mkakati safi sana huu. Ungali unahitaji marekebisho machache kuwa mpango bora kabisa. Utafaa mume wangu. Ila lazima ufanye kitu kimoja!”
“kitu gani?”
“Utalazimika kuupeleka kwa watu wengine kadhaa unaowaamini ili na wao wakupe maoni na mawazo yao! Naamini ukipita mikononi mwa watu kadhaa utakuwa mkakati usio na shaka ndani yake!”
“Hilo nalifahamu fika mke wangu. Katu sitaweza kuuacha kama ulivyo! Lazima upite kwa wajuzi kwanza!”
Naam mkakati ulipitishwa kwa watu kadhaa baada ya mkewe nae kuongeza mawazo yake. Mpaka unatoka kwa mtu wa mwisho ulikuwa safi na tayari kwa utekelezaji. Kukamilika kwa hatua hii kulifuatiwa na ile hatua muhimu ya kuongeza nguvu za kiuchumi. Alianza kuangalia katika marafiki zake ni nani na nani wanaoweza kumpa kama sio kumkopesha au kumfadhili ili aingie katika kinyang’anyiro cha urais kama mshindani aliyepania kushinda na kwenda Ikulu na sio mshindani anayetarajia kuwa msindikizaji.
Masurufu hakuwa mjinga. Alifahamu fika kuwa wako wengi ambao wangependa kushiriki katika mbio hizi za Ikulu, ambao wangetamani kujimwaga katika hekaheka za uchaguzi, hekaheka ambazo zingewasafishia njia katika safari ya kuelekea Ikulu!
Aliamini wote wana nia na mbinu. Baadhi wanakubalika na baadhi hawakubaliki. Lakini yeye mbali ya kujivunia sifa zake, sifa ya na kiongozi anayeheshimika zaidi nchini. Wachilia kuwa kwake kiongozi wa mfano kwa kujiuzulu alipotuhumiwa kusamehe kodi, alijua lazima atahitaji fedha. Fedha za kutosha.
Fedha ambazo zitamtangulia mbele na kutatua vikwazo vyote ambavyo vitakuwa vimeshindwa kutatuliwa na sifa zake. Ni kwa mantiki hii ndiyo maana leo asubuhi alikuwa amefika ofisini mapema na kuwatambua marafiki zake muhimu akawapata wa kuridhisha.
Hatua iliyofuata ilikuwa kuwapigia simu na kuomba miadi nao, baadae akawatembelea na kufanya nao mazungumzo ya kina mmoja baada ya mwingine. Baadhi walimwelewa kwa urahisi, wengine walimwona kama mwendawazimu na wengine walimsikiliza kwa makini zaidi na kuupitia mkakati wake na kumpa ushauri huu na Yule, huku wakimpa matumaini na kumtia moyo.
Waliomwelewa wakaanza kumpa michango, dola laki moja, dola elfu hamsini, thelathini mpaka kumi zikaingizwa katika akaunti yake, akaunti aliyoifungua maalum kwa ajili ya kurahisisha safari yake ya Ikulu.
Fedha hizi zilipochanganyika na zile za kwake ambazo alikuwa amezificha huku na huko, matumaini yake ya kushiriki vyema katika kinyang’anyiro cha kuteuliwa na chama, kupitishwa na mwishowe kutwaa urais; yakaongezeka!.
* * *
Miongoni mwa waliomsikiliza vizuri na kumpa moyo Masurufu alikuwa Dr Christopher McDonald! Huyu alikuwa amesisimkwa na kuvutiwa sana na mpango wa Dk Masurufu Hussein Masurufu hata akawa amemtembelea tena siku hii ofisini kwake kwa siri.
“Umesema unataka kuwa rais wa Tanzania siyo?”
“Ndiyo!”
“Good idea!” MacDonald akashindwa kuizuia furaha yake “Nimekuhusudu kwa hili!” Akaongeza. Masurufu akatabasamu tu, halafu akajibu.
“Nami nakushukuru sana kwa mchango wako. Dola laki moja sio fedha ndogo hata kidogo hasa ukizingatia thamani ya fedha ya kwenu ilivyo juu!”
“Usijali!” McDonald akasema kama asiyejali sifa hizo, “Kilichonileta hapa ni kufanya mazungumzo mengine ya kina na wewe, mazungumzo ambayo sina shaka yataweka lami katika safari yako ya Ikulu!” Akatua na kujiwashia sigara. Akavuta na kupuliza moshi mwingi hewani. Akasema
“Ninachokitaka kujua ni kama umedhamiria kweli kweli kuwa rais wa nchi yako. Rais wa Tanzania?”
Dokta Masurufu akamtazama vizuri mgeni huyu hali hasira zikianza kumpanda. Hakujua ni dhamira gani izungumzwayo, wakati tayari alikuwa ameandaa mkakati wake maridhawa na tayari alikuwa ameanza kuchangisha na kukopa na akingali anaendelea na zoezi hilo hadi leo. Hata hivyo akazimeza hasira zake na kumuuliza mgeni wake taratibu.
“Nadhani sijakuelewa McDonald.”
“Nataka kujua msimamo wako katika hili. Je uko thabiti au unatingisha kiberiti?”
“Kutingisha kiberiti?” Masurufu akafoka. “Wakati nimeandaa mkakati wangu, wakati hata wewe umeuafiki na kuchangia? Wakati kila mmoja amenipa moyo! Wakati...!”
“Sikuja kwa shari Masurufu!” McDonald akamkata kaIima. “Nimekuja kukusaidia, nimekuja kuongeza nguvu katika mipango yako. Nichukulie kama rafiki na mtu niliye upande wako ili tuweze kwenda vizuri!”
“Kumradhi Chris!” Masurufu akapoa. “Nilidhani umekuja kunidhihaki. Ni kweli nimedhamiria kwa dhati na ninahitaji msaada wako wa hali na mali katika kutimiza hili. Na ninaapa lazima nikumbuke fadhila. Sisaidiwi bure, nakopa na nitarejesha!”
“Kumradhi Chris!” Masurufu akapoa. “Nilidhani umekuja kunidhihaki. Ni kweli nimedhamiria kwa dhati na ninahitaji msaada wako wa hali na mali katika kutimiza hili. Na ninaapa lazima nikumbuke fadhila. Sisaidiwi bure, nakopa na nitarejesha!”
Akatua kumeza mate. McDonald akatabasamu. Lilikuwa tabasamu la dhati kwa kuwa Masurufu alikuwa amegusa pale alipotakiwa aguse ...lazima nikumbuke fadhila! mvumo wa sauti ya masurufu ukavuma tena akilini mwake na kubakia ukirejea kama mwangwi ...sisaidiwi bure, nakopa, nitarejesha!

Ni hili alilotaka kulisikia. Ni hili ambalo alikuwa amepanga kutumia hila kulipenyeza, hadi hapo Masurufu atakapolikubali ili aweze kumsaidia kinaganaga, kumsaidia kichwa na miguu. Hata hivyo alijirudi pale alipogundua amefurahi kiasi cha kujisahau na kukaribia kuweka siri yake peupe. Akasema “Sikiza masurufu! Tanzania ni nchi yenye kila kitu, amani, upendo , demokrasia na zaidi utajiri wa mali asili. Ni moja kati ya nchi kubwa zenye heshima ya aina yake ulimwenguni, ambazo zingali masikini hadi leo hii. Bila kupatikana kiongozi makini kama wewe, aliye na dhamira na nia ya dhati ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi, haitajikwamua maisha.
Ukiacha hilo, kwa upande mwingine Urais ni taasisi kubwa ambayo kila aliyetimamu anatamani kuimiliki walau kwa miaka mitano tu. Ili awe na kauli ya mwisho kuhusu matumizi ya mali na rasilimali za nchi.
Kwa maana hii kuingia kwenye kinyang’anyiro kikubwa kama hiki na kushinda sio shughuli ndogo. Ni lazima nguvu nyingi zitumike na jasho jingi limwagike ili dhamira yako iweze kufanikiwa! Tuko pamoja?”
Masurufu akakubali kwa kutikisa kichwa. Wakati huo mlango ukafunguliwa na mhudumu wa Dk Masurufu, akaingia na kuwatengea chai.
“Ndiyo maana!”Akaanza tena McDonald huku akijiwekea sukari katika kikombe cha maziwa “Nikakuuliza. Ni kweli umedhamiria? Maana dhamira ni kitu kingine na ukipanga ni lazima utimize. Liwake jua, inyeshe mvua lazima mkakati ufanikiwe.
Maana mwenye dhamira ya kweli huwa haoni taabu kuipinda na kuipindua mikakati yake ili tu lengo lake kuu, lengo lake la mwisho litimie. Nikirejea kwako sina shaka lengo lako kuu ni kwenda Ikulu siyo! Na uko tayari kufanya lolote kutimiza dhamira hiyo siyo?”
“Ndiyo!” Masurufu akajibu kwa moyo mzito. Sasa akiwa ameanza kukerwa na mtu huyu ambae alimuona kama anazunguka zunguka tu pasipo kusema wazi anataka nini. McDonald akaendelea
“Na sina shaka kuwa dhamira yako ni ya ukweli na ya dhati, si ndivyo?”
“Kabisa Chris!”
“Good! Very good!” McDonald akasema akisimama bila hata kumalizia kikombe cha maziwa ambacho alikuwa amekionja tu. Akaongeza akingali amesimama.
“Nimefurahi kusikia hivyo Dokta! Ni hilo lililonileta kwako, nadhani utafanikiwa katika mkakati wako. Kwa heri ya kuonana na kila la kheri ndugu yangu!”
“Mara hii!” Masurufu aliwaza nae akisimama kwa lengo la kumzuia McDonald, ambaye wakati huu alikuwa anafungua mlango wa ofisi tayari kwa kuondoka.
“Hapana!” Hatimaye Masurufu alisema kwa taabu akianza kuvuta hatua kumfuata mgeni wake huyu. “Hauwezi kuondoka kwa haraka hivi. Bado nina kiu ya kuongea na wewe!”
Akatua akihema. Sasa walikuwa mlangoni,
“Bado hujanieleza kwa nini umeamua kuja ofisini kwangu kwa siri namna hii, kwa nini umekazania kujua nia yangu na kama nina dhamiri ya dhati! Lazima kuna jambo na huwezi kuondoka bila kuniambia, tafadhali Chris!”
Christopher McDonald akasimama mlangoni na kumtazama Dokta Masurufu. Ni kweli alikuwa na kiu ya kujua. Akaachia tabasamu la haja kumpoza. Akamwambia
“Usijali Dokta, usijali! Tuliloliongea leo ni la muhimu kuliko yote unayotaka kuyajua. Na muda bado upo. Ingawa uchaguzi ni mwaka huu, lakini ndio kwanza huu ni mwezi wa kwanza. Bado kuna miezi tisa mbele.
Usiwe na haraka. Naenda kuwaona marafiki zangu ambao niliwataka wakuongezee fedha za kutosha ili uweze kutimiza dhamira yako . Na nisingeweza kuwaona bila kujua kama una nia ya dhati au lah!”
“Hao marafiki zako ni akina nani?” Ushawishi ukamzidi Masurufu. Tabasamu la McDonald likakomaa, akacheka!
“Haraka ya nini Dokta?” Akasema katikati ya kicheko. “Ndio kwanza nawapelekea wazo baada ya mimi kuuona mkakati wako na kuukubali. Baada ya kukukabili na kugundua ukweli wa dhamira ya dhati uliyonayo na sio ubabaishaji.
Nipe muda. Ikibidi kuwajua utawajua. Wacha niwape wazo lako. Pengine watakubali, pengine wasikubali. Ila kama watakubali na kukupa fedha lazima uwe tayari kufanya kitu kimoja muhimu!”
“Kitu gani!”
“ Kuupitia upya mkakati wako pamoja nao, ili kuona kama utakidhi vigezo. Na katika hili inabidi uwe tayari kuubadili na kuupanga kisomi zaidi pasipo kuathiri lengo lako kuu. Lengo la wewe kuwa rais wa Tanzania!”
Zilikuwa habari njema kwa Dokta Masurufu. Akauliza,
“Kwanini tuufumue mkakati wangu uliogharimu muda, fedha na akili kuutengeneza”
“Swali zuri” Alikuwa McDonald akirudi na kuketi katika sofa.
“Swali zuri sana!” Akaingiza mkono katika koti, akatoa pakiti ya sigara na kujiwashia sigara nyingine kama kawaida akaivuta na kupuliza moshi mwingi.
Akasema “Rafiki zangu ni wafanyabiashara Dokta. Ni watu Smart na makini wakati wote. Wanapoweka mkono wao mahala ni lazima waone mafanikio ya uwepo wao huko. Umeelewa?”
“Nimeelewa!” Masurufu akasema kwa mshangao. “Je”, akauliza “Wao wanatarajia kunufaika katika hili?”
“Mara hii umesahau umeniambia unataka kukopa? Kwamba ukishakuwa rais pale Ikulu utarejesha kufumba na kufumbua?!”
Dokta Masurufu akatahayari. “Kumradhi Chriss!” Akaomba.
“Samahani ya nini Dokta?! Huhitaji kuomba samahani hata kidogo, pengine ninayestahili kuomba samahani ni mimi!” Akatua na kupiga mkupuo mwingine mrefu wa sigara. Akaacha moshi wa sigara uingie mapafuni kwa wingi na huku akiruhusu kutoka nje kidogo kidogo. Bado Masurufu alikuwa amemtumbulia macho. MacDonard akaendelea.
“Mimi ambaye nimekuja na kuingia ofisini kwako bila ruhusa yako, bila miadi na zaidi bila mwaliko. Na kama hiyo haitoshi nikaanza kukuuliza maswali yasio na kichwa wala miguu. La! kumradhi bwana Masurufu!”
“Usijali Criss,” Akasema Masurufu kwa bashasha
“Nitapenda kusikia kutoka kwa marafiki zako!” Akaongeza.
“Tuombe Mungu!”
“Inshallah!”
MacDonald akainuka, Akaagana na Masurufu akafungua mlango na kutoka. Kabla hajafika mbali akaitwa tena, akageuka na kumtazama Masurufu kwa Mshangao.
“Samahani, nakutegemea!”
“Unanitegemea?”
“Yeah! Hakikisha umewashawishi rafiki zako, mpaka wakubaliane na matakwa yangu. Wakikubali hata wewe utakuwa na fungu nikifanikiwa!”
“Kweli?!”
“Haki ya Mungu tena!”
“Nitajitahidi!” Likawa jibu la mwisho. MacDonald akaondoka zake. Waliachana kila mmoja roho yake ikiwa kwaatu kabisa, kila mmoja akiona amempatia mwenzake.

* * *

Christopher MacDonald alikuwa mmoja kati ya wageni wengi walioihusudu Tanzania kupita kiasi hata wakijikuta akiomba uraia wa nchi hiyo kwa siri. Kuihusudu huku kulikuwa kumekuja kama nasibu tu, wakati ule Benjamini Mkapa alipolihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa na kupaza sauti kuwa tayari amefungua milango kwa wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania.
Kwamba tayari ametengeneza mazingira mazuri ambayo siyo tu yatavutia wawekezaji pekee, bali yatawafanya wajisikie wako nyumbani hasa.
Akiwa mfanyabiashara wa kimataifa, aliyewekeza vitega uchumi vya haja katika nchi za Angola, Botswana, Zambia, Congo na Afrika ya kati; Christopher hakuona kama kuna ubaya wa kwenda Tanzania kujionea ukweli wa hali halisi na kile alichokisema Mkapa kule UNO.


Akaja! Alianza kuyakubali maneno haya mara tu aliposhuka katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere pale Kipawa Dar es salaam, akitumia ndege ya kukodi akitokea Congo ambako pia alikuwa mwekezaji katika sekta ya madini.
Hali ya hewa ilikuwa nzuri na ya kuvutia sana, jua likiwaka mchana na giza kuingia usiku tofauti na kwao. Ardhi ikiwa ya kijani iliyobeba majani na mimea ya kijani haswaa. Kabla hili halijamkifu akashangazwa na ukarimu na upendo waliokuwa nao watu wake. Wachilia mbali umoja na mshikamano. Ikamshangaza zaidi kuona mtu anaingia dukani kununua bidhaa akiwa na hela mkononi na kuomba auziwe! Badala ya kuamuru apewe.
Na hata baada ya kuhudumiwa na kulipia bado alisema ahsante kabla ya kuondoka. Ukarimu huu! Christopher alishangaa kwa dhati Ustaarabu ulioje?
“Naam!” Akakubali “Nyerere alifanya kazi kweli kweli!”
Siku kadhaa zikakatika akisoma hiki na kujifunza kile. Kutoka hapo akaenda kupanda mlima Kilimanjaro. Mlima mrefu kuliko yote Afrika, akajionea vilele viwili maridhawa vya Kibo na Mawenzi.
Akajionea pia chemchem ya maji safi ambayo kwa macho yake aliona kuwa yalikuwa bora kabisa. Safari yake haikuishia hapo alikwenda Selui, Mikumi, Tarangire, Manyara, Mahale na kwingineko ambako alijionea utajiri wa wanyama wakiwemo sokwe mtu ambao kwa Afrika walipatikana Tanzania na Congo pekee.
Yale Maziwa yenye maji baridi yaliyoizunguka Tanzania nzima, samaki wa migebuka wakubwa, watamu na watamu waliomo katika ziwa Tanganyika na lile la Viktoria vilikuwa vitu vingine vilivyomfanya ailaani bahati yake kwa nini hakuzaliwa Tanzania.
Alipokuja kuyatembelea machimbo ya Dhahabu yaliotapaa karibu mikoa yote, Machimbo ya Almasi kule Mwadui na Tanzanite pale Arusha, Christopher alijikuta akiachama kwa mshangao na kusema. “Masalaleeh! Kweli kwenye miti hakuna wajenzi!”
Wiki moja baadae alikuwa ofisini kwa Mkuu mmoja wa Serikali kuulizia taratibu za uwekezaji, ambako mshangao mwingine ulikuwa ukimsubiri.
Alipokuja kuyatembelea machimbo ya Dhahabu yaliotapaa karibu mikoa yote, Machimbo ya Almasi kule Mwadui na Tanzanite pale Arusha, Christopher alijikuta akiachama kwa mshangao na kusema. “Masalaleeh! Kweli kwenye miti hakuna wajenzi!”
Wiki moja baadae alikuwa ofisini kwa Mkuu mmoja wa Serikali kuulizia taratibu za uwekezaji, ambako mshangao mwingine ulikuwa ukimsubiri.
Ahadi ya kupewa msamaha wa kodi kwa miaka mitano endapo angewekeza nchini, pamoja na kuipa serikali mrabaha sijui mrahaba wa asilimia tatu tu za faida kati ya silimia mia moja kwenye sekta ya madini na yenyewe pia ilikuwa ni ahadi iliyomfanya asahau hata kumuaga mwenyeji wake na kurudi kwao Uingereza na Marekani.
Huko alikutana na wenzake watatu ambao walikuwa na mtandao wao. Mtandao ambao kazi yake ilikuwa moja tu. Kupora utajiri wa Afrika na kuurudisha Ulaya, huku wakiziachia nchi za Afrika uhuru wa bendera chini ya sera yao ya ukoloni mamboleo.
Mtandao huu ulikuwa umeanza kama utani tu baada ya wahusika wake ambao walikuwa wanachama katika Mashirika ya CIA, BOSS, MOUSAD. IMF na Benki ya Dunia; kuamua kujitoa na kutengeneza chombo kingine ambacho kingeweza kuyatekekeleza malengo yao kwa ufanisi na haraka zaidi ukilinganisha na huko walikotoka.
Ni katika hili walipojibatiza uwekezaji ambapo kazi yao kubwa ilikuwa kuandaa mipango ya kiutendaji (Business Plan) yenye majina ya kuvutia kama NEPAD, Structure Adjustment Programme, Utandawazi, Mkakati wa kupunguza Umasikini, Malengo ya Milenia, Maono 2015 n.k na kuwauzia marais wa nchi za Afrika ambao walilazimishwa kuwasikiliza na G8 ambayo ilikuwa moja kati ya mitandao yao.
Na matokeo ya Business Plan hizo, yakawa ni marais wa kiafrika kuwakaribisha nchini mwao na kuwapa makampuni ambayo yalikuwa yakiendeshwa na wazawa ili wao wayainue yawe na tija na kuongeza ushindani.
Wakapewa kila kitu! Heshima, makazi, mikopo ya mitaji na uhuru wa kutosha. Matokeo yake badala ya kuyafufua mashirika hayo, wao wakayaua huku wakipora kila rasilimali waliyopewa na wenyeji wao na kwenda kuujenga Mtanadao wao.
Kutahamaki mashirika yakafa. Mtandao wao ukakaua. Wakayaacha mashirika hayo yakiwa hoi mikononi mwa Serikali yakihangaika japo kurudisha utendaji wao wa zamani.
Wakati nchi nyingi za kiafrika zikianza kulalamikia hali hii katika Umoja wa Mataifa kama ilivyo kawaida, Mtandao wa akina Christopher ulikuwa umekua tayari na kuanza kuwekeza katika nchi za kiafrika na kuuchuma utajiri wa nchi hizo taratibu na kuurudisha kwao.
Kama vile haitoshi, Mtandao ulijihusisha na kwa siri sana kufanya ujangili katika maeneo yenye malighafi nono, yakapenyeza silaha kwa waasi mbalimbali na kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi za ukanda wa Maziwa makuu, huku wao wakijichotea rasilimali zao kiulaini kabisa.
Agenda yao ilikuwa ile ile, kunyakua kila kilichowezekana madini, malighafi na vinginevyo na kukimbiza Ulaya na Amerika. Naam, hawakuwa na rafiki wala adui wa kudumu. Wao walikuwa na maslahi ya kudumu tu.
Hatimaye walichokitaka kilitimia. Utajiri waliokuwa nao ulizidi kuwatetetemesha vigogo wengine wote katika Bara la Amerika na Ulaya. Wengi walihitaji kujiunga na kushirikiana nao katika hujuma mbalimbali.
Kutahamaki wakawa wameziweka chini ya himaya yao Taasisi kubwa kubwa kama zile za Shirika la Biashara Ulimwenguni WTO, Shirika la fedha ulimwenguni IMF, Benki ya Dunia WB na jamaa zao wa nchi tajiri kabisa ulimwenguni G8. Na kwa makusudi kabisa wakawa wameamua kujiita G-8 Original. Naam, kila mmoja aliwanyenyekea!
* * *
Wenzake walizipokea taarifa za uwepo wa neema katika Tanzania mithili ya wachezaji wa mpira wa miguu wanavyoupokea mpira wa kona tayari kwa kufunga goli na pengine kuokoa. Wiki ya kwanza wakawa Tanzania ambapo walizunguka tena na MacDonald na kuangalia hiki na kile kwa pamoja.
Wiki ya pili wakawa Uingereza tena, wakajipanga na kuchukua kila kilichohitajika. Waliporejea tena Tanzania na kuomba kuonana na Waziri wa nchi pale Ofisi ya Rais Mipango na ubinafsishaji, walipokelewa kama wafalme na kunyenyekewa zaidi ya malkia Elizabeth.
Wakapewa maeneo waliyohitaji, ulinzi na msamaha wa kodi wa miaka mitano! Wakachuma na kuchuma. Miaka mitano ilipoisha walibadili majina ya kampuni kwa hila ya kuleta jamaa zao wengine ambao nao walipata msamaha wa kodi wa miaka mitano tena.
Wakaendelea kuchuma, rasilimali zilipopungua sehemu moja, walihamia sehemu nyingine bora yenye rasilimali nzuri zaidi. Ni katika kipindi hiki Christopher alipoomba uraia wa nchi hii ambayo ukweli alitokea kuipenda sana.
Ndio! Nchi gani kila mmea unaoupanda unaota na kustawi kana kwamba ardhi hiyo imetengenezwa kwa ajili yake?
Halafu malalamiko ya wananchi yakaanza. Nchi ikabadili muundo wa kuingia katika mfumo wa vyama vingi. Wapinzani nao wakazaliwa na kuanza kubweka huku na huko.
Laiti wasingaliuogopa Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi na kusitisha mikataba yao kabla ya kuondoka nchini kabisa kwa hofu kwamba uchaguzi ungeambatana na umwagaji damu; Pengine wangekuwa wanatawala hadi leo hii. Uchaguzi ule uliopita salama na Benjamini Mkapa akawa Rais na kuingia Ikilu huku akifuatisha falsafa ya ukweli na uwazi kwa kutumia miiko ya uongozi. Kidogo mambo yalibadilika, hivyo Christopher MacDonald na wenzie akina Bob Roberts Marshal, Alfred Winer na Anton Baker Senior wakashindwa kuingia kwa urahisi.
Hili likawashangaza sana.
Hata walipofuatilia kwa Rais bado hawakukubaliwa, sababu zilikuwa nyingi, lakini kubwa ikawa ni kwenda kinyume na makubaliano na kupora rasilimali za Taifa. Wakaghadhabika na kuondoka kwa hasira.
Siku chache baadae wakawa wakiongea na viongozi wa kisiasa.
Walianza na Augustine Lyatonga Mrema wa Tanzania Labour Party, wakafuata na Dokta Ibrahimu Haruna Lipumba wa chama cha Civic United Front na baadae na John Momose Cheyo wa United Democratic Party. Kama vile haitoshi walionana tena na Bob Makani na Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kuhitimisha na Chrisopher Mtikila wa Democratic Party.
Mazungumzo na viongozi hao wa upinzani yalianza na kwisha vibaya kwani viongozi wote walikataa kuiingiza nchi katika machafuko kwa kuipindua serikali ya CCM.
Pamoja na kwamba akina Christopher MacDonald walikuwa tayari kutoa pesa za kutosha kwa vyama, pesa za maandalizi, silaha na utaalamu na kusaidia uratibu hadi pale Rais atakapoondoka madarakani; bado viongozi hao hawakuwa tayari asilani.
Wakaishia kuwalaani kuwa walikuwa na uoga wa kipumbavu na kwamba kamwe asilani hawataweza kufanikiwa kuitia nchi mikononi mwao kama wataendelea kuwa waoga kiasi hicho. Kila mahala pakaondokea kuwa pagumu. Wakawa hawana jinsi ila kurudi kwao kutafuta namna mpya. Namna ya kumuweka mtu wao pale Ikulu! Mtu ambaye ataiongoza nchi kama kivuli huku akitamka na kutenda kila watakalomwambia!
Wote walikuwa wamekubaliana kuionyesha serikali ya CCM kile kilichomnyoa kanga manyoya. Na hili lilitakiwa kutimia kwa kila hali. Bahati haikuwa yao kwa vile kila waliyejaribu kumuuzia wazo hilo, aliwaona kama wendawazimu. Miaka mitano ya Mkapa ikaisha, akaongezewa mitano mingine.
Christopher na wenzie wakaendelea kutafuta namna, muda ukiendelea kupita.
Wote walikuwa wamekubaliana kuionyesha serikali ya CCM kile kilichomnyoa kanga manyoya. Na hili lilitakiwa kutimia kwa kila hali. Bahati haikuwa yao kwa vile kila waliyejaribu kumuuzia wazo hilo, aliwaona kama wendawazimu. Miaka mitano ya Mkapa ikaisha, akaongezewa mitano mingine.
Christopher na wenzie wakaendelea kutafuta namna, muda ukiendelea kupita.
* * *
Katika hali hii, Christopher alikujikuta akikaribia kuruka kwa furaha pale Glady Steveson Ombwe, mmoja kati ya Hawara zake aliyekuwa amempata kwa kisingizio cha kufanya nae biashara ya maua, alipomfuata ofisini na kumuomba amsaidie mumewe Dokta Masurufu kumchangia ili akagombee Urais!
Masikio yakamsimama.
Dakika zilizofuata zilimkuta Christopher na Glady wakiwa katika hoteli moja ya nyota tano pembeni ya uwanja wa ndege wa Heathrow, wakiwa kitandani uchi kama walivyozaliwa baada ya kufanya mapenzi ya kina.
“Umesema mumeo anataka kugombea Urais wa Tanzania?” Alimuuliza tena kupata uhakika. Glady akakubali kwa kutikisa kichwa.
“Kweli?”
“Kabisa Cris!”
“Mbona mapema hivi, mara hii ameshachoshwa na Ubalozi?!”
“Sidhani kama ni busara kusema amechoshwa. Ila ni sahihi kusema nae anataka kuteua mabalozi badala ya kuteuliwa! Anataka kuwa Amiri Jeshi mkuu nami nikiwa First Lady wake! Hutajisikia fahari kuwa na hawara ambaye ni first lady wa nchi tajiri na masikini kama Tanzania?”
“Glady mpenzi!” Criss akasema akijiwashia sigara. “Unajua vizuri sana kuwa ninapenda!”
“Basi ndo utuchangie!”
“Kiasi gani?”
“Chochote ulicho nacho, chochote kiasi cha uwezo wako. Euro laki moja, elfu hamsini, milioni moja na kadhalika na kadhalika!”
“Lakini nikitoa fedha nyingi jamaa hatashtukia kweli?”
“Ashtukie nini?”
“Kwamba namchukulia mali zake?”
“Mara ngapi nilikwambia muda huo hana? Kwamba ananiamini kupita kiasi, kwamba mimi ni kila kitu kwake?!”
Glady akakereka.
“Basi my love. Nitawachangia! “Nitawapa dola laki moja!”
“Wow!” Glady akashangilia akimgeukia Criss na kumkumbatia kwa nguvu huku akimbusu hapa na pale kwa fujo! Akasema
“Ahsante my love! Ahsante sana. Ninakupenda sana Chris! Ninakupenda kwa kuwa unaniunga mkono na kuchangia harakati za maendeleo yangu. Ahsante tena na tena!”
“Usijali!” Criss akapuliza moshi hewani. “Hebu nisimulie tena mlivyolipata wazo hili. Kwa kweli ni wazo zuri sana. Naam. Good idea!”
Akitumia sauti nzuri, Glady alianza kumsimulia tena toka mwanzo hadi mwisho.
Ndivyo ilivyokuwa, saa chache baadae, Criss alikuwa na mkakati wa Dokta Masurufu wa kuelekea Ikulu. Kama vile haitoshi wakati wa kutoa mchango huo, Criss alihakikisha anautoa mbele ya Dokta Masurufu na mkewe Glady.
Mchango huu ulifuatiwa na urafiki wa awali baina ya Criss na Masurufu. Urafiki huu ulimfanya Dokta Christopher MacDonald amjue vizuri Dokta Masurufu. Alipata pia kujua yale ambayo hakuyajua kwa Glady.
Hata alipolifikisha wazo hili kwa wenzake watatu, nao walimshukuru Mungu kuona amewaletea windo lao hadi miguuni. Hata hivyo kabla hawajaridhia kuunga mkono kichwa na miguu, MacDonald na wenzake, walimtuma mlinzi wao Ben Tapeli kwenda Tanzania kuchimbua yale ambayo Masurufu hakuweza kuyabainisha kwao.
Ben aliporejea taarifa yake ilikuwa nzuri isivyo kawaida.
Kilichowavutia sio ule ukweli ulio dhahiri kuwa Masurufu alikuwa mtoto wa mpigania uhuru aliyelelewa na Mwalimu Nyerere, mwenye shahada ya uchumi na ambaye amepitia mafunzo ya Jeshi pale monduli; bali ni ule ukweli uliokuwa nyuma ya pazia wa namna alivyokuwa na miradi anuai yenye majina bandia na akaunti nje ya nchi. Namna alivyoweza kujipenyeza kila palipo na ulaji akiwa fisadi mdogo akituhumiwa pia kuwa mmoja wa watu waliofanikiwa kuchota pesa za EPA kule hazina, kuhujumu kampuni ya umeme pamoja na ule mradi wa mkaa wa mawe, wachilia mbali gesi ya Taifa. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni haya waliyotaka kusikia. Kwamba wanashughulika na mjasiriamali wa siasa. Mtu anayeijua fika ladha ya fedha. Wakamchambua kwa muda na kuamua kufanya nae kazi.
Ingawa katika macho ya kawaida Masurufu alikuwa na hela, lakini hela zake katika mtandao huo zilikuwa sawa na tone la mvua katika maji ya bahari! Kutangaza fedha zake mbele ya mtandao huo unaoiogopesha hata benki ya Dunia ingekuwa sawa na kutangaza umasikini wake.
Wakaitazama bajeti yake na kuangua kicheko.
Kwao ilikuwa bajeti ndogo mithili ya mbegu ya haradali na katu isingeweza kufanya lolote la haja. Hili likawa miongoni mwa mambo mengi yaliyowafanya wamwite baadae na kujadiliana nae kwa tuo. Kikao cha majadiliano kilikuwa kimefanyikia nchini Uingereza katika hoteli ya Sheraton katika mazingira ya usiri uliopindukia na chini ya ulinzi usio wa kawaida.
Wajumbe wa kikao hicho walikuwa wanne kama ilivyo kawaida na Mwenyekiti alikuwa Christopher MacDonald. Mjumbe ambaye alikuwa ameongezwa kwa makusudi na ambaye ilijulikana kuwa hatakuwa wa kudumu labda mpaka pale atakaposhinda kinyang`anyiro cha Urais alikuwa Dokta Masurufu.
Ilikuwa ni baada ya Masurufu kuelezea mkakati wake vizuri ndipo maswali yalipoanza kumiminikia moja baada ya jingine.
“Kwanini unataka kuwa Rais wa Tanzania?” Mmoja aliuliza.
“Sababu ziko nyingi, kuna kuboresha maisha ya jamii, kuboresha miundo mbinu ya nchi, kuondoa umasikini, kuinua pato la Taifa na kadha wa kadha.
“Sio kwamba unataka kujineemesha?” Mwingine akadhihaki.
Masurufu akatabasamu.
“Kuneemeka kwa kweli ni lazima! Naam, lazima uneemeke. Na ninadhani kuneemeka ndio hasa kumetufanya tukutane hapa. Kwa ujumla sio tu nataka kuneemeka pekee, bali tunataka kuneemeka au ninyi wenzangu hamtaki neema?”
Wakacheka!
“Unajua kabisa kuwa jibu ni sio!” Roberts akasema katikati ya kicheko. Walikuwa wameanza kuvutiwa na Masurufu toka alivyoanza kujieleza, akiuelezea mkakati wake. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kujielezea na maelezo yake yalishawishi masikio ya kila mmoja kumsikiliza na akili kumuunga mkono hali moyo ukimpenda.
“Ila!” Aliendelea Marshal “Sababu za kwanza zieleze kwa jamii, zile za pili zifiche chini kabisa wa moyo wako!”
“Najua, daima dhamira yangu haitajulikana kwa watu baki. Sitathubutu kuwaambia Tanzania ni kama Tembo mkubwa ambaye tunamuwinda. Tukimpata huyu, hakika tutagawana tushibe na kusaza!”
“Na kwa nini usipitie chama cha upinzani? Wenzako tayari wameanzisha CCJ, ingawa pia kuna fununu kuwa hawatopata usajili karibuni. Huoni ukipitia upinzani itakupa uhuru wa kufanya na kujiamulia mambo yako bila taabu? Unadhani akina Kawawa, Kingunge, Mkapa na Mwinyi watakuunga mkono?!”
“Kwanini wasiniunge mkono?” Masurufu akawahi kwa pupa. “Mimi nitakuwa pendekezo lao. Kwao mie ni zao la mwalimu Nyerere. Kuniacha mie nitawale ni sawa na kumrejesha tena Nyerere madarakani. Sitaweza kupitia nje ya CCM, Na nina sababu mbili muhimu za kufanya hivyo!”
Akatua na kupiga funda la maji.
“Kwanza, CCM ndio chama mama Tanzania. Ni chama kilichoshika dola na kuitawala Tanzania kwa takribani miaka arobaini sasa. Ni rahisi kuwarubuni viongozi wachache walioishika hatamu ndani ya CCM kwa majina ya Kamati Kuu, Halmashauri na kadhalika ili wakupe ridhaa kuliko kuurubuni umma ukupe ridhaa ya kuiongoza nchi nje ya CCM, wakati huohuo CCM yenye kila kitu, polisi, Usalama wa taifa, Jeshi na zidi dola ikikupiga vita. Hutapata zaidi ya hasara.
Pili, CCM ndio chama chenye mizizi kila pembe ya nchi. Kipyenga kikipulizwa pale Dodoma, kinakuwa kimepulizwa Tanzania nzima ambako maelfu kwa maelfu ya makada wake wataanza mbio za kukusafishia njia na utaingia Ikulu kiulaini kabisa. Kazi yako itakuwa ndogo tu, kupitia katika pembe hizo na kuwaambia mimi ndio fulani. Nikopeni kura zenu niwalipe maendeleo baas! Simple like that.
Wajumbe wakacheka tena.
“Huhofii tuhuma za ufisadi ambazo zimeshika hatamu?” Mjumbe mwingine akakumbusha.
“Sihofii! Sihofii kabisa. Najua mambo sio shwari kabisa kabisa ndani ya CCM hasa ukizingatia ukali wa hoja zinazotoka midomoni mwa watu kama akina Mwakyembe, Selelii, Ole Sendeka, Alfred Mpendazoe, Anne Killango, Sofia Simba na Wengineo.
Lakini malumbano haya yapo mjini. Kule kajificheni kwenye asilimia kubwa ya watu, kwenye watu wanaoishi chini haswaa ya dola moja kwa siku, watu ambao wanasaka tonge kama sio nyoka, habari hizi hazijafika na pengine hazipo. Kule hakuna umeme, hakuna internet, hakuna gazeti, hakuna TV na hata hizo redio zilizopo bado hazisikilizwi kutokana na ughali wa betri! La hapana sihofii kabisa!”
“Lakini unasahau kwamba huko wewe unakokuita kwa wachache ndio jikoni. Ndiko kwenye kila kitu. Ndiko ambako ukishatolewa kama mgombea, huko vijijini kazi yao ni kufuata tu mithili ya kundi kuubwa la Ng’ombe linaoongozwa na mtu mmoja mwenye fimbo tu!”
“Ni kweli!” Masurufu akakubali, “Lakini umesikia wapi mpishi asiyependa fedha. Nikiwa na fedha za kutosha, sidhani kama kuna kitakachoshindikana. Nchi ya demokrasia ile, kila kitu kinakwenda kidemokrasia na kwa sasa demokrasia ni pesa.
“Je” akawauliza “Kuna lililobakia!”
“Bado yakingali mengi, ila…” MacDonald akasita kidogo. Kusita kwake kulikuwa na sababu. Hata hivyo ni wakati ametaka kuitamka ndipo alipojiwa na wazo haraka kuwa haikuwa busara kuiweka shaka yake mbele ya Masurufu. Akaendelea
“La muhimu kama nilivyokwambia awali, mkakati wako unahitaji kupangwa upya bila kuathiri lengo lako. Tuachie mkakati huo na wiki ijayo tukutane na kuuperuzi pamoja kabla hatujafanya makubaliano ya mwisho unaonaje?”
Masurufu akaafiki. Angeona nini? Alichohitaji yeye ni fedha, fedha ambazo alitaka kuzipata haraka kabla ule Muswada wa kuthibiti fedha haramu katika uchaguzi haujapitishwa na kuwa sheria. Sheria ambayo pengine inaweza kuyafanya malengo yake yasitimie.
Awali alikuwa ameyawekea shaka mazungumzo yake na MacDonald, lakini akajikuta akiyapa nguvu pale alipokwenda kuongea na mkewe Glady na Glady kumthibitishia kuwa MacDonald na wenzie hawakuwa tu malodi pekee, bali mabilionea hasa.
Hili lilipata nguvu pale alipofanya mikutano michache na MacDonald ambayo ilikuwa ikimaliza kwa Masurufu kupewa ‘posho’ ya maelfu kwa maelfu ya dola. Hatua hii ikamfanya Masurufu amgeuze Christopher MacDonald kuwa baba na mama akimtaka ushauri wa hili na lile.
Hali hii iliendelea mpaka pale alipomuita katika kikao cha mwisho ambacho alimwambia kile ambacho Masurfu alikuwa akihangaika kukijua. Kwa nini akina MacDonald wamsaidie? Maana hata kama angekuwa Rais, madeni yale yangeweza kuchukua miaka kuyalipa. Ndiyo! yalikaribia kufanana na yale ya Tanzania inayodaiwa na IMF, WTO, World Bank n.k
MacDonald alimueleza kwamba wameamua kumsaidia kwa kuwa wanatarajia kulipwa fadhila kutoka kwake yeye ambaye uchunguzi wao ulithibitisha kuwa ana nafasi kubwa ya kuwa Rais katika uchaguzi huu. Fadhila walizotarajia ni kuwa washauri wakuu wa Rais katika sekta ya uchumi. Kwamba akiwa Rais asingeruhusu watu kuwekeza Tanzania pasipo ushauri wao, lakini pia kampuni kutoka nchi zao zipewe kipaumbele katika uendeshaji wa sekta za madini, utalii, misitu na uvuvi.
Ambapo wao watahakikisha kampuni hizo zinaajiri wazawa na baadae kulipa kodi baada ya mitaji yao kukomaa na wao kujijenga. Tena walimwambia hawatokula peke yao, Rais pia atakuwa na hisa kwa kila kitakachofanyika. Na fungu la Rais linaeleweka. Sio dogo hata kidogo.
Na kama atauafiki mpango wao huo, msaada wa fedha zote za kampeni na mwingine wa ziada ataupata bila masharti ukiwa na ziada ya ulinzi, mipango na hata utekelezaji wa baadhi ya mambo akihitaji.
Akiwa na akili timamu na uwezo mzuri wa kufikiri, mahitaji haya yaliingia na kutuama chini kabisa za fahamu zake. Akachukua muda kuyatafakari kabla hajamuuliza MacDonald maswali haya na yale.
Maswali ambayo yalikuwa na majibu muafaka.
Kwamba hawatamuingilia katika maamuzi ya kuongoza nchi. Atapewa kila anachohitaji na kwamba ubia huu utamfanya nae awe miongoni mwa wale mabilionea wanne wanaounda G8 Original.
Jioni alichukua muda wa kutosha kujadiliana na mkewe ambaye alimtaka kuondoa hofu na kuchangamkia tenda.
“Kwa sasa wewe ni sawa na mtaka cha uvunguni!” Glady alimwambia akimkumbatia. “Huna budi kuinama!” Akambusu.
“Lakini kuinama huku…!” Glady aliendelea, “Kutakuwa kwa muda mfupi tu. Itachukua pigo moja tu la Almasi pale Mwadui au mawili ya Tanzanite pale Mererani kurejesha deni lao lote! Kubali mume wangu, kubali baba Rose. Woga wako ndio umasikini wako!” Akambembeleza.
Ilitosha kuulegeza moyo wake. Penzi la haja alilopewa usiku likawa limemmaliza kabisa. Masikini laiti angejua kwamba mkewe nae alipewa donge nono ili amshawishi?!
Alipokutana na MacDonald na kumwambia kuwa amekubali, hapo ndipo aliposhuhudia tabasamu la furaha ya dhati likichanua katika uso wa Criss na kung`ara mithili ya maua katika jua la asubuhi.
Tabasamu hili lilifuatiwa na Masurufu kukatazwa kuombaomba tena michango hovyo, na kufuatiwa na ile safari ya Uingereza ambapo alikutana kwa mara nyingine na ile timu ya wafanyabiashara wa kimataifa wanne wanaojiita G8 Original na kufanya mazungumzo yale yenye mafanikio.
Masurufu aliporejea nyumbani kwake, bado tabasamu lilikuwa limeupamba moyo wake.

* * *

Nchini Tanzania vuguvugu la uchaguzi lilikuwa limeanza mapema kuliko ilivyofikiriwa. Mheshimiwa Frederik Tluway Sumaye Waziri Mkuu wa Tanzania alikuwa wa kwanza kutangaza azma yake ya kugombea uraisi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi akitumia mahojianao maalum aliyoyafanya na gazeti la Tanzania Daima.
Tangazo hili lilifuatiwa na lile lililotolewa na Mheshimiwa John Samweli Malechela. Kabla hawajafuata wakina Salim Ahmed Salim, Balozi Patrick Chokala, Balozi Ali Karume na Profesa Mark Mwandosya.
Kama vile haitoshi siku kadhaa mbele walijitokeza akina John Magale Shibuda, Abdalah Kigoda na Dokta Wiliam Shija. Wakati siku zikielekea ukingoni wakawa wamejitokeza tena akina Iddi Simba, Jakaya Mrisho Kikwete na John Charles Tengeneza, huku wengine wengi zaidi wakitarajiwa wajitokeze katika siku za baadae.
Huu ukiwa upande wa CCM, kambi ya upinzani nako mambo yalikuwa yamepamba moto. Mbali ya Mrema na Lipumba ambao waliwaambia wapenzi wao kuwa wao wataendeleza libeneke la kugombea urais;
Walijitokeza vijana wengine machachari kama akina Freeman Mbowe aliyetangaza kuing’oa CCM kupitia Chadema, akiahidi kutumia Helkopta. Mgombea pekee wa kike Mama Anna Senkoro aliyepitia PPT – Maendeleo, Christopher Mtikila na chama chake cha DP na wengine wengi.
Tofauti na matarajio ya wengi, safari hii mgombea kipenzi cha wasukuma na ambaye ni nadra umsikilize bila kucheka kutokana na utani anaoiingiza katika hotuba zake, Bwana John Momose Cheyo wa UDP yeye kwa makusudi kabisa alitangaza kuachana na Urais na kwenda kugombea Ubunge nyumbani kwao Bariadi Shinyanga.
Hekaheka hizi, kufumka na kuibuka kwa utitiri wa vyombo vya habari hasa magazeti ambayo sio siri mengi yalidaiwa kumilikiwa na wagombea Urais na ubunge kwa ajili ya kupata urahisi wa kupeleka habari zao na kujinadi kwa wananchi; pamoja na kule kutazamwa na macho yote ya ulimwengu, kwa pamoja vilimfanya Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi Inspekta Kimaro kuwa hoi kimawazo na taabani kifikra.
Tayari alikuwa amechukua kila tahadhari aliyoiona inafaa ili kuhakikisha imani inaendelea kuwepo ili kulinda heshima ya Tanzania usoni mwa ulimwengu.
Kila kitu kilikuwa sawa, kila hatari ilikuwa imeondoshwa hata kabla haijatukia. Na machoni pa wengi hali iliendelea kuwa shwari, lakini kwa Inspekta Kimaro bado alikuwa na wasiwasi, bado alikuwa na hofu.
Hakujua ni vipi anaweza kuimaliza hofu hii. Vijana wake makini aliowapachika kila kona, kila mahala ambako aliamini kungeweza kutokea lolote hasa katika vyama vya siasa, walikuwa wakichpa kazi barabara chini ya maelekezo yake na kumpa taarifa zote. Yeye Akiwapa amri hii na ile.
Pengine ni hili lililomfanya leo amwite Samson Kidude, yule mpelelezi wa kujitegemea ambaye awali alikuwa mwajiriwa wa jeshi la polisi, lakini akawa ameacha kazi katika mazingira ya kutatanisha, na akaanza kujadiliana nae.
Majadiliano ambayo yaliisha bila tija kwani Samson nae hakuwa na lolote la maana zaidi ya kuendelea kumsisitizia kuwa hali ilikuwa shwari.
“Kwanini unaamini hivyo?” Kimaro akauliza kwa karaha.
“Nina sababu za Msingi Kamishna!” Akajisogeza vizuri kitini na kuendelea “Nimechunguza kila mahala, kila nilipopatilia shaka. Bahati mbaya nimekutana na madai ya kipumbavu tu! Madai ambayo yeyote aliyeyazusha ama alikuwa na ajenda zake, ama hakuwa timamu kichwani!”
“Madai gani?” “Kuna vile visu vya rangi ya Bluu, Nyeupe na kijani. Ambavyo ilizushwa vimeletwa na chama cha wananchi CUF ili wakishindwa waanzishe vita na kumwaga damu!”
“Kweli hilo ni dai la kipumbavu sie pia lilifika kwetu. Mwenzetu mmoja akalikurupukia, lakini uchunguzi tulioufanya ulidhihirisha kuwa CUF hawakuwa wanahusika. Enhe dai lingine?”
“Ilisemwa pia CCM imemnunua Bi Naila Jidawi ili apambane na Maalimu Seif ili kupunguza kura zake za urais na kumpa ushindi mgombea wa CCM madai haya yalifanya Maalim aje juu, kitu ambacho kilipofuatiliwa kikaonekana hakina ukweli na suala hilo likamalizwa kwa njia za kidiplomasia.
Kamishna akatikisa kichwa kuafiki. Mengi ya madai yaliyotolewa na Samson yeye pia alikuwa na habari nayo kwa kuwa vijana wake walimpa mengi na vingi. Kumwita kwake Samsoni ilikuwa ni kutaka kujua kama Samson ambaye ni hodari wa kunusa kama bado hajaambua lolote. Ikamshangaza kuona Samson aking’ang’ania tu kuwa hali ni shwari!
“Lakini hii haimaanishi hali ni shwari Samson!”
“Kwa nini Kamishna?”
“Ule uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, hali ilikuwa shwari hivi hivi, lakini kilichokuja kutokea kwa King Halfan King na yule beberu Adrian sote tunakifanamu. Laiti Adrian asingegongwa na gari, bila shaka muda huu tungekuwa tunaongea mengine!”
“Ni kweli lakini uchaguzi huu ni toauti na ule?” “Ki vipi?”
“Huu hauna mdahalo!”
“Lakini muda bado, lolote linaweza kutokea!”
“Ndio lolote linaweza kutokea lakini sio la mdahalo. Tayari Augustine Mrema ambaye wakati huu atagombea tena kwa tiketi ya Tanzania Labour Party amesema hatoshiriki. Yeye anaamini alihujumiwa kwenye midahalo alipogombea mara ya kwanza kwa tiketi ya chama cha NCCR Mageuzi, na kwamba mdahalo ule alichangia kumpora kura zake za urais.
Wakati Mrema ametangaza na kusema hatoshiriki katika midahalo, ipo minong’ono kuwa wagombea wanaotajwa kugombea kupitia upinzani na hata chama tawala nao watakataa kata kata kushiriki katika mdahalo!”
“Kwanini wakatae?” Inspekta Kimaro akasaili.
“Sasa mi’ nitajuaje mkuu hali mimi sio mwanasiasa? Sio mgombea urais? Waulize wenyewe wanasiasa waliotangaza kugombea. Pengine wana udhaifu wa kujenga hoja, pengine sio mahiri wa kujieleza mbele ya wagombea wenzao, waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla. Pengine wanaogopa maswali ya moja kwa moja toka kwa jamii na pengine wanaogopa kulogwa!” Akatua. Hili la mwisho likamfanya Inspekta Kimaro acheke. Akacheka sana. Samson pia akacheka na kumwambia bosi wake
“Huonekani kuamini uchawi Inspekta!”
“Nitaamini vipi vitu visivyo na uthibitisho. Pengine upo, pengine haupo!” Akajibu akiendelea kucheka.
“Uchawi upo mkuu!” Samson akasisitiza.
“Kama upi?”
“Kuna kesi ya Rama yule aliyekutwa akila kichwa cha mtoto kule muhimbili, kuna yule aliyeua mtu chumbani kwake kule Kibaha na kisha kulichukua fuvu lake kuliweka chini ya uvungu ndani ya ndoo ya plastiki iliyojaa mafuta, kuna mauaji ya vikongwe wenye macho mekundu kule Shinyanga. Kuna mauaji na uchunaji wa ngozi ulioshamiri miaka ya nyuma kule Mbeya. Vyote hivi ni Baadhi tu ya uthibitisho wa kuamini kwa watu juu ya uwepo wa nguvu za giza!”
Inspekta akachoka.
Aliyoambiwa na Samson yalikuwa ya ukweli na baadhi ya operesheni kesi hizo ameziongoza yeye na kuwatia ndani watuhumiwa. “Hata hivyo!” akasema baadae na kuendelea
“Hatupaswi kupuuza kitu! Hali bado ni tete na tuna wajibu wa kuwa macho zaidi!”
“Haina neno Kamishna. Samson Kidude unamjua fika, akipata lolote atakujuza tu!” Baadae waliagana. Samson akaondoka akimuacha Kimaro akiendelea kutaabika kama sio kukonda kwa mawazo.
* * *
“Haina neno Kamishna. Samson Kidude unamjua fika, akipata lolote atakujuza tu!” Baadae waliagana. Samson akaondoka akimuacha Kimaro akiendelea kutaabika kama sio kukonda kwa mawazo.
* * * Mkutano wa pili baina yake na akina MacDonald ulikuwa mfupi na mzuri kuliko mingine mingi iliyotanguliwa. Safari hii ulifanyikia Born Ujerumani katika mazingira yale yale ya usiri. Mkakati wake ulikuja ukiwa umepangwa kisomi na vizuri zaidi. Ulimvutia kupita kiasi. Maeneo kadhaa yaliokuwa na utata yalikuwa na maelezo ya kina yaliyoiondoa shaka yake yote.
Labda kilichomfurahisha ni kule kukuta maelezo yalioandikwa kwa wino mzito mweusi na kupigwa mstari. Kwamba lazima mkakati huu ufanikiwe kwa bei yoyote ile, hata kama ni kwa mtutu wa bunduki baada ya njia ya kidiplomasia kushindikana. Ni hili alilotaka kusikia, ni hiki alichotaka kukiona.
Baada ya kumaliza kusoma mkakati wa kuelekea Ikulu, mkataba wa makubaliano yao nao ulikuwa mezani ukimsubiri. Aliusoma neno kwa neno. Baadhi ya mambo yalimsisimua na mengine kumugofya. Kilichomfurahisha ni kule kukuta kipengele kinachomuingiza katika lile kundi la mabilionea wanne baada ya yeye kusaini.
Kuingia huku kutamfanya apewe mtaji wa dola bilioni 40 ili anunue hisa na kuwa mmoja wao, Mwanachama wa G-8 Original! Ilikuwa ajabu na kweli! Machozi ya furaha yakamlengalenga huku moyoni akifoka taratibu. “Nimeukata… nimeukata… nimeukata!”
Aliendelea kuusoma kwa makini mpaka alipofika mwisho ambapo alikuwa akitetema. Akautua ule mkataba chini na kumtazama MacDonald. Akamuuliza.
“Kwenda kinyume na makubaliano haya, adhabu yake ni kifo?!!!”
“Ndiyo!”Akasisitiza akimtazama usoni moja kwa moja.
Masurufu akaogopa. Kwa mikono inayotetemeka akauinua tena ule mkataba na kuisoma tena sehemu ile. Maandishi yaliendelea kuwa vile vile kama yanayomdhihaki. Akauliza kwa pupa
“Kwa nini kifo? Mnataka kuniua?!”
“Hatutazamii kuuana katika hili, ni endapo tu makubaliano yataenda kinyume kwa makusudi!”
“Ikitokea ninyi ndio mmekwenda kinyume?”
Ikawa zamu ya MacDonald kumtazama Masurufu vizuri. Halafu akaangua kicheko cha haja huku akitikisa kichwa kushoto na kulia. “Kitu kama hicho kwetu, kamwe hakitawezekana. Ujue sie ni watu ambao daima damu huwa hatuyakani maamuzi yetu.
Mwenyewe umeliona hilo, nilipokuahidi mchango nilikupa bila usumbufu na ningali ninakupa fedha zingine hadi leo, fedha ambazo zipo nje ya makubaliano. Na kabla ya kukaa na wewe, tulikaa na wenzangu na tukakubaliana kufanya tulichokifanya. Sioni kwa nini tugeuke! Naam hatutageuka!” MacDonald akatua, akavuta sigara na kutoa moshi mwingi hewani, akaongeza. “Halafu makubaliano kama haya mkigeukana na kupelekana mahakamani ninyi ndio mtakaofungwa. Ni ya kihaini!”
Maswali mawili matatu yaliyofuata kutoka kwa Masurufu yanajibiwa vizuri na washirika wa MacDonald. Hofu inamuondoka Masurufu. Anavuta peni na kuweka saini yake katika mkataba ule. Nakala moja ngumu ya mkataba akapewa Masurufu na kuiweka katika mkoba wake na ile laini akaiweka katika Laptop na flash yake. Nakala nyingine akazichukua MacDonald.
“Hizi ni fedha za awali!” MacDonald akampatia Masurufu mfano wa kadi ya ATM ya rangi ya hudhurungi. Masurufu akaipokea. “Nenda katika ATM yeyote, ila ya benki yako ni zuri zaidi!” Akaendelea MacDonald. “Ita nambari za akaunti yako na uingize kadi hii. Baada ya muda utapokea ujumbe wa salio la akaunti yako na unaweza kuanza kazi!”
“Ahsante!” Akashukuru Masurufu.
“Kumbuka kuanzia sasa sisi ndio washauri wako wakuu. Hupaswi kufanya chochote bila kutuambia. Na ukifanya tutajua mara moja ingawa sisi hatutokuja Tanzania! Na tukijua itakuwa hasara kwako!”
“Msijali! Tuko pamoja”
“Unaweza kwenda!”
Masurufu akasimama na kuondoka.
“Masurufu!” MacDonald akamwita tena alipofika mlangoni. Dokta Masurufu akageuka.
“Nakuonya tena, huwa hatugeukwi ndugu yangu pesa hizo!”
Kiasi Masurufu alianza kukereka. Ananitisha? akajiuliza. Nusura arudi na kumrushia ile kadi yake alipojirudi …Kumbuka wewe ni mtaka cha uvunguni… Mvumo wa sauti ya mkewe ukamrejea na kumpa nguvu. Akaachia tabasamu la haja, halafu akasema.
“Huna haja ya kuwa na hofu Chris, Ninajua ninachokifanya. Usihofu kabisa!”
“Kweli?”
“Kweli tupu!”
“Poa kila kheri!”
“Kwako pia!” Masurufu akatoka.
Safari yake iliishia benki alikofika anafanya aliyoelekezwa na MacDonald. Alipouliza salio alikaribia kuzimia kwa mshtuko. Dola Milioni Mia mbili na hamsini zilikuwa zimetulia tuli katika akaunti yake! Ikiwa ni kinyume na dola milioni hamsini alizoomba katika mchango wake!
Hakuamini akaingia ndani kwa keshia na kuuliza salio tena.
Jibu lililokuja lilikuwa lilelile. Kwamba ana dola hizo. Kwamba ameingia miongoni mwa mabilionea wachache waliopo. Furaha asiyomithilika ikamvaa na kumchukua hata kumtoa machozi.
Alipomueleza mkewe kuhusu hili, Glady alishindwa kujizuia na kuangua kilio cha furaha. Walikuwa wameukata kwa kila hali. Sasa safari ilikuwa yao. Njia ilikuwa nyeupe kuelekea Ikulu. Kikwazo pekee ambacho waliamini kingekuwa kikwazo, tayari kilikuwa kimeondolewa na G-8 Original.
Siku chache baadae kwa kuitumia familia na marafiki zake walio Tanzania. Masurufu alipokuwa amepata timu ya watu kadhaa ambao walikubaliana kushikamana kwa namna na kwa kadiri ya uwezo wao hadi pale Masurufu atakapoingia Ikulu. Mmoja wa watu hawa alikuwa Frank John Mariki.
* * *
ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom