Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,101
- 128,716
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Nipashe la Jumapili ya leo.
Mwezi huu wa March, mwaka 2026, Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari nchini Tanzania, JAB, imetimiza mwaka mmoja tangu kuzinduliwa kwake, ambapo Bodi ilizinduliwa rasmi tarehe 3 March, mwaka 2025, hivyo kufikia tarehe 3 March, Bodi hii, imetimiza mwaka mmoja, ambao ni mwaka mmoja wa mafanikio lukuki, ila kama ada, kila kwenye mafanikio, hapakosi changamoto.
Declaration of Interest
Kwa vile, hapa juzi kati nilifinywa na JAB, makala hii isichukuliwe, kama ni pongezi za kichawa baada ya kufinywa!. Niliisha andika makala mbili kuipongeza JAB kabla hata sijafinywa, Pongezi Bodi ya Ithibati kwa Waandishi wa Habari kwa Mwanzo Mzuri, Cheti Kisitumike kama Fimbo Kuwachapia Wenye Vipaji, Uwezo na Uzoefu wasio na Cheti
na kwa vile JAB imefanya makubwa ya mafanikio, kufinywa kwangu na JAB, hakuniondolei objectivity yangu kuelezea mazuri ya JAB yakiwemo mafanikio ya JAB.
Makala hii, inaangazia mafanikio ya bodi hii katika kipindi cha Mwaka Mmoja tangu kuzinduliwa mwaka jana, fanikio kubwa la kwanza, la bodi hii baada tuu ya kuanzishwa, ni kujenga mfumo wa usajili wa waandishi wa habari unaoitwa Tai Habari na tovuti rasmi ya Bodi, hivyo mwandishi, huwajibiki kufunga safari hadi ilipo Idara ya Habari Maelezo na kujisajili, ambapo usajili ulikuwa unafanyika munualy, ki analogia kwa kujaza makaratasi, kupiga picha ya passipoti, picha hiyo isafishwe, inabandikwa na gundi kwenye kitambulisho, na process ya usajili ilichukua siku kadhaa,
Lakini sasa kupitia mfumo wa TAI Habari, mwandishi anaweza kujisajili akiwa mahali popote pale nchini Tanzania, bila kuhitajika kufika JAB, na akiwa amekamilisha viambatisho vyote, anaweza kusajiliwa ndani ya nusu saa, na kupatiwa kitambulisho chake, ila kwenye kupokea kitambulisho, hapo sasa ndipo lazima akipokee, ki analogia, ama kwa kukifuata, ama kutuma mtu amchukulie. Hii imeondoa usumbumbufu mkubwa kwa waandishi, hata hivyo wafaidika wakuu wa mfumo huu ni waandishi wa kisasa wa hizi zama za dot com, sisi waandishi wa mwaka 47, ambao sio wa zama za kidigiti, tunapata changamoto ya kujisajili kidigitali, hata hivyo Afisa wa JAB, kwa jina la Kibamba, amekuwa msaada mkubwa kwa sisi waandishi wa mwaka 47, kuna siku nimemshuhudia, afisi nzima wameondoka baada ya kuisha mud awa kazi, yeye akinihudumia, mimi niliondoka pale saa 12:30 jioni, kigiza giza kinaanza, na bado nilimuacha mzee mwenzangu mmoja wa gazeti la Chama Uhuru, sijui, alitoka saa ngapi?!.
Mafanikio mengine makubwa ya bodi hii ni kutoa ithibati na Vitambulisho vya Uandishi (Press Cards) ambapo tangu mfumo uanze kufanya kazi Mei 21, 2025 tayari Bodi imefanya usajili kama inavyoonekana katika takwimu za kwenye jedwali hili la Machi 10, 2026 ambapo sasa tunakwenye kwenye Data Journalism
Muhtasari wa Maombi
Na sasa, nazichakata data hizi.
· Takribani asilimia 81 ya maombi yote yameidhinishwa.
· Karibu asilimia 10 ya maombi hayajakamilika.
· Asilimia 5.8 bado yanasubiri uchakataji.
· Asilimia 3.3 yamekataliwa.
“Katika maombi 4,110 yaliyopokelewa, asilimia 81.19 yameidhinishwa, asilimia 5.84 bado yanasubiri uchakataji, asilimia 3.31 yamekataliwa, na asilimia 9.66 hayajakamilika.”
Maombi ambayo hayajakamilika yanatokana na baadhi ya waandishi kujisajili zaidi ya mara moja, na wengine wamejisajili lakini bado hawajalipia.
Haya ni Mafanikio makukubwa kwani Malengo ya awali ilikuwa kusajili waandishi wa habari kati ya 1,000 hadi 1,200 kwa kuzingatia rekodi ya Waandishi waliokuwa wakipewa Press Card na Idara ya Habari Maelezo kila mwaka kutovuka 900.
Baada ya kuvuka lengo, lengo la pili ilikuwa kusajili waandishi 3,000 ifikapo Desemba 31 hata hivyo, hadi kufikia tarehe hiyo Bodi ilikuwa imesajili waandishi 3,839. Hivyo, Bodi ilivuka lengo kwa takribani asilimia 27.97 (karibu 28%).
“Lengo la pili lilikuwa kusajili waandishi 3,000. Hata hivyo, hadi tarehe 31 Desemba jumla ya waandishi 3,839 walikuwa wamesajiliwa, ikiwa ni waandishi 839 zaidi ya lengo lililowekwa, sawa na ongezeko la takribani asilimia 28 juu ya lengo.”
“Katika waandishi 3,337 waliopata ithibati, waandishi 3,158 sawa na asilimia 94.63 tayari wamechukua vitambulisho vyao, huku waandishi 179 sawa na asilimia 5.37 bado hawajavichukua.” - Hii ya waandishi 179 walioomba vitambulisho, wakapata lakini hawajavichukua vitambulisho vyao, inamaana hawa ni waandishi wenye shughuli nyingine za kuendesha maisha yao, hivyo kwa vile ni waandishi, wameomba tuu wawe navyo ila hawavitegemei sana, kumaanisha hawajishughulishi na uandishi wa habari.
Makundi yaliyosajiliwa ni Waandishi wa Habari, Wahariri, Watangazaji wa Redio na Televisheni, Wawakilishi (Correspondents), Waandishi wa kujitegemea (Freelencers), Waandaaji wa Maudhui, Wapiga picha, Maafisa Habari na Wanafunzi waliopo mafunzo kwa vitendo (Field).
Jitihada mbalimbali zimefanyika kufikia lengo hilo, zikiwemo kampeni za uhamasishaji, utoaji wa elimu kuhusu Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, pamoja na ziara za kutembelea vyombo vya habari kwa ajili ya kutoa ufafanuzi na kuhamasisha waandishi kujisajili na kupata ithibati.
Miongoni mwa mafanikio yaliyojitokeza ni kupungua kwa kiwango cha uvunjifu wa maadili ya uandishi wa habari. Hali hii inaonekana kupitia kupungua kwa idadi ya malalamiko ya ukiukwaji wa maadili yaliyokuwa yakipelekwa kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na Bodi, hasa katika miezi ya awali baada ya uzinduzi wa mfumo wa ithibati.
Kupungua kwa malalamiko hayo kunahusishwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa idadi ya waandishi wa habari na watangazaji waliopata ithibati katika vyombo vya habari, jambo lililochangia kuimarika kwa uelewa na uzingatiaji wa maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Mafanikio mengine ni kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Bodi na umuhimu wa ithibati, kusimamia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari, kuandaa mipango mkakati ya Bodi, kutoa mafunzo kwa waandishi wenye ithibati, hususan katika kipindi cha mchakato wa uchaguzi pamoja na uandaaji wa nyaraka zote muhimu za usajili wa Bodi kwa Msajili wa Hazina.
Tukutane tena wiki Ijayo katika muendelezo wa Makala hii, ambayo hiyo itaangazia changamoto za JAB.
Paskali

| Aina ya Maombi | Idadi | Asilimia |
| Maombi yote yaliyopokelewa | 4110 | 100% |
| Maombi yaliyoidhinishwa | 3337 | 81.19% |
| Maombi yanayosubiriwa | 240 | 5.84% |
| Maombi yaliyokataliwa | 136 | 3.31% |
| Maombi yasiyokamilika | 397 | 9.66% |