Mwaka mmoja ndani ya Merigos Fleury Prison

Hii ni true story na sasa sipo jela nipo uraiani nafanya kazi za meli.

Hilo ni tukio limetokea 3 years ago.
Sababu ujuwaji ni mwingi basi story naishia hapa..
Usikasirike, ungetupa utangulizi kuwa tukio hilo limetokea zamani. Nimeanza kusoma nikiamini unaandika ukiwa gerezani, na hii ni kwa vile umeandika hata familia hujaitaarifu
 
Usikasirike, ungetupa utangulizi kuwa tukio hilo limetokea zamani. Nimeanza kusoma nikiamini unaandika ukiwa gerezani, na hii ni kwa vile umeandika hata familia hujaitaarifu
Nimeandika kama story,,lakini ukisoma uzi wote utakuja kuelewa story yngu ilipoanzia.
Kila mwandishi na uandishi wake ktk story ya simulizi.
Hii ni aina ya uandishi wangu.
Fuatilia post zng
_ sitosahau siku niliyonusurika kuuawa na police south Africa.
- chenai upo wapi my love?
Lakini vyote ni matukio yangu ya kweli.
This is how I make my moves mkuu.
 
Kuna vitu vingi sana nimekubali kuwa mwanafunzi iwe ni kwa anayenizidi umri, tunalingana au nimemzidi. Nimechagua kuwa mwanafunzi zaidi katika kujifunza kuhusu dunia na walimwengu kwa ujumla. Huyu jamaa mwandende nimekuwa nikisoma post zake tele tu, kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwake na kizuri zaidi huwa anatanabaisha kama ni chafu ni chafu au kama ni safi imenyooka.


Watanielewa tu wale wayatafutayo maisha kwa namna zote bila kujali safi au chafu. Nyie wa formal system endeleeni kuishi maisha yenu clean, sio kitu ambacho hujawahi kukifanya basi hakiwezekaniki au hakipo!
 
EPISODE 5.
Nimeshahukumiwa miezi 18 jela for money smuggling.
Nipo cellule nasubiri kupelekwa gerezani.

Sheria za France sio ngumu Sana kwa wafungwa.
--Ukihukumiwa unaruhusiwa kukata rufaa ndani ya miezi 3.
Na procecutor ana nafasi ya kukata rufaa ya hukumu ndani ya muda huo kama hajaridhishwa na hukumu yako.
-- Ukihukumiwa unapata punguzo la miezi 5 kutoka kwa judge.
Hilo ni lazima.
-- kila mwezi wanapunguza siku 7 ktk kifungo chako.
-- kila mwaka mmoja wanapunguza miezi 3 ktk hukumu yako.
Ikifika 1/2 ya sentence yako yote unajadiliwa na judge kama Una sifa za kuachiwa huru na kupunguziwa tena miezi 3 ktk kifungo chako..

Mfano nimehukumiwa miezi 18 jela.
Nimepata miezi 5 ya punguzo la judge.
Itabaki miezi 13 .
Still napata punguzo la siku 7 kila mwezi wa hukumu yangu...
utapata miezi 3 mingine kwa mwaka.
nimepunguziwa,,itabaki miezi 9 ndy napaswa kukaa gerezani.

Katka miezi 9 hapo ndy nitajadiliwa na kupewa tarehe maalum ya kutoka gerezani.
Na kama ni raia wa inchi za kigeni kuna utaratibu wa kuwaachia kwa njia ya explusion.inakuwa kabla ya Ile miezi 9 kufika,,labda ningekaa miezi 6 Tu,, nikarudishwa home.(deportation)
Na uzuri wa France ukimaliza kesi yako hawana Mambo ya Pingu .
Ukiwa free basi wanakuacha free kuenda zako .
Kama ni kwenye ndege wanakata ticket unawekwa kwenye ndege, passport anapewa rubani na documents zako unapewa mwenyewe,, wanahakikisha ndege inaruka zako na wao wanaishia zao,

Hayo yote nilikuja kuyajuwa baadae nilipokuwa gerezani..

saa 0800 usiku,,walikuja walinzi wa gerezani,,tukabebwa wafungwa kama. 20 hivi kuelekea gerezani ambapo sikulijuwa hata jina lake kwa kipindi hicho.

Gari lilitembea kama umbali wa masaa 2 kutoka cello za mahakamani,, gari lilifungwa kila mahali lakini niliweza kuona kupitia sehem Nyembamba sn ya uwazi wa gari lile liliotubeba.

Mwisho tulijikuta tukiingia ndani ya majengo marefu yaliyokuwa yamezungukwa na waya wa senyenge pamoja na wire za umeme na cameras kila mahali..

Baada ya kushushwa nikagunduwa sasa nipo Merigos Fleury.
Baada ya kuona bango kubwa lililopo mbele ya uso wa jengo lile

Merigos Fleury prison,,ipo eneo linaitwa Fleury ambalo lipo ndani ya Paris.
Fleury ni jela kubwa kuliko zote ndani ya France.
Fleury ina majengo matano ambayo yote ni ya ghorofa 4 kila moja.
D 1
D2
D3
D4
D5
Na kila jengo linauwezo wa kubeba wafungwa 5000 kwa wakati mmoja.
Kila batman (jengo) Lina flour 1--4.
Na kila flour imegaiwa kwa maeneo 3.
Gauche(left)
Drote (right)
Milleu (middle)
Wafungwa watakaa humo,,ikitokea kuna chochote basi utatangaziwa taarifa kupitia radio ambayo ipo kwenye kila celo.
Kila celo ina TV 32 inches,, fully paid.
Fridge.kitanda double decker.
Na jiko kama ukihitaji kujipikia.
Choo self.
Dirisha kubwa lenye hewa nzr..
Jela ina maduka mle ndani,,na vitu vinauzwa Mfano lotions,,nguo,,vyakula,,radio,, home theatre ,,sigara,,majuice,,kuku,,nk.
Vyote hivyo ukivitaka wanakata ktkt pesa zako na wanakupa details kila mwezi.
Hii haikuwa jela bali ni 5 star hotel.

Nilipofika nikafanyiwa utaratibu wa kuchukuliwa alama za vidole.
Picha za upande zote tatu ya Sura yangu..
Uso upande wa mbele.
Uso kulia.
Uso kushoto.

Nikafunguliwa account ya jela,,kwamba ni utaratibu ili hata Kama ndugu na jamaa wakitaka kunitumia pesa popote walipo pesa zinaingia kwenye account yangu.
Kila mfungwa ana account ya jela hata Kama anafanya kazi basi pesa zake zinaingia kwnye account na wanakuletea bank detail kila mwezi kwamba Una umount kiasi gn,
Na kama haufanyikazi basi wanakuwekea euros 20 ktkt acc yako.

Baada ya kufunguliwa account,
,wale watu wa account ambao ni sehemu ya walinzi wa pale gerezani,, wakanambiya kwamba tumeweka euros 100 tu,,,ktk account yako.
Dah,,nilinyong'onyea sn,,

Yaani ktkt pesa zng zote zile 36700 euro wameweka 100 eurosTu?
Jamaa wakasema pesa zile zote ni chafu..zimetaifishwa,,
Nikasema hata zile zilizokuwa kwenye walett 1700 euros pia wametaifisha?
Nilihuzunika sn.

Baada ya kumaliza kuandikshwa kila kitu,,
tukachukuliwa na vitu vyetu tukapelekwa sehem ingine kwa ukaguzi zaidi tayari kwa kupelekwa cello..

Tuliitwa mmoja mmoja kulingana na tulivyoandikishwa,
Nilipoitwa jina langu,,nikakuta na mabag yangu yote yapo pale,,simu yng na kila kitu.

Wakanambiya nivue nguo zote,,moja baada ya ingine,,mwisho nikabali kama nilivyozaliwa..

Wakaanza kukaguwa nguo moja moja.
Mwishowe wakanambiya Unaweza kuvaa nguo zako.
Nilikuwa na kiatu changu fulani cha ngozi,,
Nikajaribu kukivaa,,Yule mlinzi akanikataza,,
This type of shoes is forbidden in prison..
Jamaa akanambiya..hairuhusiwi viatu vya ngozi hapa jela.
Shati au fulana ya blue pia marufuku,,
Maana zinafanana na Sare za walinzi wa jela.
Pia sweater la kuziba kichwa pia marufuku jela.

Nikapewa Raba mpya kabisa,,ambayo Africa unakwenda nayo disco.
Nikapewa na jeans 2,, track suits 2 pamoja na boxers kadhaa..
Nikapewa blanket moja ,,shuka nyeupe 2 ,taulo,na sandles za kuogea..
Jamaa wakanambiya ukihitaji nguo zingine kuna utaratibu wa kuomba nguo utapewa.

Nikakusanya nguo zote nilizoona ambazo naweza kuingia nazo celo,nikapelekwa cellule kwangu.

Sasa naanza maisha mapya ya jela Merigos Fleury.

Itaendelea.
 
Ana mwaka mmoja so bado miezi6 so anaandika akiwa ndani ila familia hajaijulisha tunaanza sisi JF
Mkuu naandika uzi huu nikiwa nipo huru,,nimeshamaliza kifungo,,
Ukikusanya simulizi yangu utajiona ulipo.
Nimendika Nina mwezi mmoja ktkt miezi 18 niliyofungwa.
Hapo nimeanza simulizi nipo jela,,nikakupeleka jinsi nilivyokamatwa..

Na sasa nakurudisha nimeshafungwa nipo celo,,
Hapo utakuja kujuwa kwann sikuweza kupata nafasi ya kupiga simu kwa muda wote?
 
Back
Top Bottom