Mwaka mmoja ndani ya Merigos Fleury Prison

mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
10,518
19,883
EPISODE 1.
Nina mwezi mmoja tangu nifungwe gerezani miezi 18.
Bado natafakari jinsi gani nitaijulisha family yangu kwa yaliyonikuta.

Nilitokea Zurich Swiss kupitia France. Nilipanda Swiss Air to Charles degaulle airport Paris France.

Nilikamatwa kwa kosa la Money trafficking na kufungwa miezi 18 jela. Nilikuwa na euros 35000.

Ilikuwa j mosi tulivu, nilipotua airport Charles de gaulle ,,

sikuona shida yeyote wala usumbufu wowote kutoka kwa askari wale.

Kumbe bila kujua wana taarifa zangu ambazo walishatumiwa kutoka Zurich airport na askari wa uwanjani pale.
Nilikuja kugunduwa hilo baadae.

Nilikuwa na pesa kwenye bag langu ziliwekwa kwa ustadi mkubwa Sana,
Sio rahisi kugundulika kwa haraka,
nilishangaa niliposhikwa bega kwa kuitwa majina yangu yote kamili na huku wale customs wana picha ya passport yng .

Waliniweka kwenye chumba maalum,
Wakanihoji na kuanzia kunipekuwa mwilini hata kwnye mabag yangu.

Hawa jamaa wapo advance sn ktk kupekuwa, wakikutaka hawakukosi.

Walianza kunihoji nafata nini Paris, nikawaambiya mm napita njia nakwenda zangu nyumbani. Africa.

Still hawakukubaliana na Mimi.

Itaendelea..
 
Back
Top Bottom