Endeleza uliposhuka pale Airport Bongo nini kiliendelea
Ilikuwa ni vurugu tupu mkuu..
Kama nisingekuwa smart basi ningesumbuliwa Sana.
Baada ya watu wa usalama kukabidhiwa passport yangu kutoka kwa pilot wa ndege iliyonileta,
Jamaa wakasema tufate,, nikawafata walipo,,baadae wakaniuliza,
-kwann umerudishwa?
-Na unatokea wp?
Nikawajibu France.
Wakasema umekaa muda gn kizuizini?
Nikawaambiya mwaka mzima.
Wakauliza kwa mm umekaa muda mrefu?
Nikawajibu niligoma kusign karatasi ya kurudi nyumbani,,
Ndy wakaniweka sn kizuizini.
Wakauliza hukufungwa?
Nikawambiya mm sijawahi kufungwa,,Bali niliwekwa kizuizini kwa passport case.
Niliamua kudanganya ili yasiwe makubwa..
Nawajuwa wabongo hatuna dogo.
Jamaa wakasema wewe una kesi kesi ya kujibu.
Nikawaambiya kesi gani tena?
Jamaa wakasema ulipokuwa gerezani unalishwa na kulala kwa gharama za France .
Baadae bili za gharama ulizotumia gerezani zinarudi kwa serikali ya Tanzania..
Gharama zinapelekwa ubalozi wa Tanzania France hivyo unapaswa ujiandae kulipa gharama.
Dah!!!!
Nilichoka kabisa.
Wakasema ticket umegharamiwa na Nani?
Nikawambiya ni serikali ya France imenigharamia.
Jamaa wakasema lazima nilipe gharama zote nilizotumia gherezani.
Jamaa walinishangaza sn..
Mm nilipinga yote hayo,,nikasema France wamesema sina cha chochote cha kulipa wala Mambo yangu na wao serikali ya Tanzania hayawahusu.
Nilishamalizana nao that time when the plane take off.
Na mm sio muhalifu Bali nili over stay muda wa kuishi ulaya nikawa kizuizini kurudishwa home
Nimekaa zaidi ya mwaka baada ya kukataa kusign karatasi ya kurudi nyumbani..
Over stay not a crime ni passport case.
Wakati huo sina karatasi hata moja inayonieleza natoka jela.
Nishatupa kila kitu nilipokuwa transit adis Ababa.
Jamaa wa usalama nikawazidi points wakanikabidhi kwa migration.
Hapo napo niliwekwa kizuizini kwa masaa kwa mahojiano.
Also there was a story to tell...