President Mobutu Sese Seko of Zaire

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,792
Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga alikuwa kiongozi wa kijeshi dikteta huko Zaire. Mke wake wa kwanza Marie-Antoinette Mobutu, alifariki kwa ugonjwa wa moyo mwaka 22 October 1977 Genolier, Switzerland akiwa na umri wa miaka 36.

mobutu-sese-seko-14101997politiker-demokratische-republik-kongo-mit-picture-id545959047

1 May 1980 alimuoa Bobi Ladawa pamoja na pacha mwenzake Kosia, Bobi na Kosia ni identical twins na mzee aliamua kuoa wote wawili.

Capture-d%E2%80%99e%CC%81cran-2015-09-14-a%CC%80-12.05.46.png


012092012122701000000JA2696p029.jpg

Bobi Ladawa was Mobutu Sese Seko’s wife. She shared her marriage with her twin sister Kosia. Bobi gave birth to two sons and two daughters while Kosia had three daughters.

Mobutu alitoka kabila la Ngbandi na alizaliwa Lisala Congo, mama yake Mobutu Marie Madeleine Yemo, alikua mhudumu wa hoteli aliekimbia kijijini kwao Lisala kwa vitisho vya chifu wa kijiji. Alikutana na baba yake Mobutu Alberic Gvemani ambae alikua mpishi wa jaji wa Kibelgiji. Jina la Mobutu alipewa na mjomba wake, baba yake Mobutu alifariki akimwacha na umri wa miaka nane. Mke wa jaji alihuzunishwa sana na kifo hicho na alijenga mapenzi makubwa kwa kijana Mobutu, alianza kumfundisha kuongea, kusoma na kuandika Kifaransa hatimae Mobutu alikuwa na uwezo mzuri sana wa lugha hiyo.

Yemo aliishi kwa kutegemea msaada wa ndugu na jamaa hali iliyomlazimu kuhama kila mara ili kukidhi mahitaji ya watoto wanne alioachiwa.

Elimu ya kwanza ya Mobutu ilikua Leopoldville, lakini mama yake alimhamishia kwa mjomba Coguilhaville, ambako alijiunga na shule ya Christian Brothers School, hii ilikua shule ya boda chini ya kanisa katoliki. Kutokana na umbo lake alikua maarufu katika michezo, alikua na uwezo mzuri kimasomo pia. Pamoja na haya alikua mhariri wa gazeti la darasa.

Mobutu pia alijulikana kwa kuiga kwa kubeza, wanafunzi wenzake wanakumbuka alivyokua anambeza padre wa Kibelgiji ambae lugha yake ya kwanza ilikuwa Kiholanzi alipoongea Kifaransa kwa makosa. 1949 Mobutu alitoroka shule kwenda Leopoldville kukutana na girlfriend. Mapadre waligundua hilo, walimkamata wiki chache baadae. Mwaka wa shule ulipokwisha Mobutu alipewa adhabu ya kutumikia jeshi kwa kosa la kutoroka shule hii ilikuwa adhabu wa wanafunzi watukutu.

Maisha ya Jeshini

Mobutu alikutana na nidhamu katika maisha ya jeshini, pamoja na mfano wa baba alivyokuwa Sagent Joseph Bobozo kwake. Mobutu alifanya yote aliyotakiwa kufanya kwa nidhamu pia alianza kuazima magezeti kutoka kwa maofisa wa Kibelgiji na vitabu kila alikoweza na alipenda kusoma kila alipopata nafasi. Katika vitu alivyopenda kusoma ni mada za raisi wa Ufaransa waka huo Raisi Charles de Gaulle, Wazieri Mkuu wa Uingereza Winston Churchil na mwana philosopha Muitaliano Niccolo Machiavelli.

Baada ya kumaliza na kufaulu masomo yake ya uhasibu, alianza kufanya kazi kama mwandishi wa habari. Bado alikuwa na hasira na mapadre wa shule waliompa adhabu ya kwenda jeshini, alimaua hataoa kanisani. Mchango wake katika harusi ulikua sanduku la bia, hii ndio mshahara wake ulichomudu.

Akiwa askari, Mobutu aliandika kwa kutumia jina bandia (kama ID za JF) mambo yanayoendelea katika siasa katika gazeti jipya lilianzishwa na wakoloni wa Kibelgiji Actulites Africaines. Mnamo mwaka 1965, aliacha jeshi na kuwa mwandishi wa habari, akiliandikia gazeti la Leopoldiville daily L'Avenier. Miaka miwili baadae alikwenda Ubelgiji kuchukua habari juu ya 1958 World Exposition, alibakia huko kupata mafunzo ya uandishi wa habari.

Muda huu Mobutu alishakutana na vijana wengi wa Kikongo wasomi ambao walipinga utawala wa kikoloni. Alianza urafiki na Patrice Lumumba na alijiunga na chama cha Lumumba cha Mouvement National Congolais (MNC). Mobutu hatimae alikua msaidizi maalum wa Lumumba ingawa watu walishaanza minong'no kuwa Mobutu anafanya kazi na shirika la ujasusi la Ubelgiji.

Kipindi cha mwaka 1960 mazungumzo mjini Brussels juu ya uhuru wa Congo yaliendelea, ubalozi wa Marekani ulihodhi mazungumzo ambayo yaliazimia kupata picha kamili ya uwakilishi wa Congo. Wafanyakazi kila mmoja walikabidhiwa majina ya wageni wa kuwapokea na kuongea nao, balozi aligundua jina moja lina jirudia, lakini hakuwa kwenye list kwakua hakua mmoja wa wageni, alikuwa katibu wa Lumumba. Lakini kila mtu alikubali kuwa mtu huyu alikuwa na akili sana, bado kijana lakini atafika mbali.

Mvutano wa Congo

Kufuatia ahadi ya uhuru hapo tarehe 30 June, 1960, serikali ya mseto iliundwa, iliongozwa na Waziri Mkuu Patrice Lumumba na Raisi Joseph Kasa-Vubu. Taifa jipya haraka lilianza kuona matatizo wakati jeshi lilipoanza kukaidi maofisa wa jeshi wa Kibelgiji. Lumumba alimpa cheo Mobutu kama Katibu Mkuu Kiongozi wa Jeshi la Wananchi wa Congo na Victor Lundula alikua Mkuu wa Majeshi. Katika nafasi hiyo Mobutu alitembea nchi nzima kuhimiza wanajeshi warudi kambini. Jitihada zilifanywa na serikali ya Ubelgiji kulinda mashimo ya madini ya kusini mwa Congo walileta jeshi la Umoja wa Mataifa.

Akiwa na wasiwasi kuhusu uwepo wa majeshi ya Umoja wa Mataifa si kwa kutuliza amani bali ni kwa lengo la kuligawa taifa, Lumumba aliwaendea Umoja wa Soviet kwa msaada, alipewa msaada mkubwa wa silaha na askari wa Kisoviet kama 1,000 kwa msaada wa kiufundi kwa wiki sita. Serikali ya Marekani iliona jitihada za Umoja wa Soviet ni njia ya kueneza ujamaa Afrika ya kati. Kasa-Vubu alihamasishwa na Wamarekani na Wabelgiji kuanzisha mpango wa kuchukua madaraka kijeshi na kumuondoa Lumumba.

Lumumba alipogundua hilo haraka alimtoa Kasa-Vumba madarakani. Wote wawili Lumumba na Kasa-Vubu walimpa maelekezo Mobutu ya kumweka ndani mwenzake. Akiwa Katibu Mkuu wa Majeshi Mobutu alikuwa katikati ya msukumo kutoka sehemu mbali mbali. Balozi za Magharibi ambazo zililipa mishahara ya askari, pia Kasa-Vuba na wanajeshi wa chini hawakupenda uwepo wa majeshi ya Umoja wa Soviet.

Mobutu alimlaumu Lumumba kwa kutafuta huruma ya Umoja wa Soviet sasa wamejenga mgongano na Wamarekani, Lumumba aliamua kwenda Staneyville, ambako alipanga serikali yake. Umoja wa Soviet tena walimpatika msaada wa silaha na aliweza kupigania nafasi yake. Baadae mwaka 1960, Lumumba alikamatwa na kupelekwa Katanga. Motubu bado alimuona Lumumba ni tishio kwahiyo aliamrisha akamatwe na apigwe hadharani hiyo ilikua 17 January, 1961. Baada ya hapo alitoweka kwenye macho ya watu na hakusikika tena. Baadae ilifahamika aliuwawa siku ile ile na majeshi maalum ya Moise Tshombe baada ya kuigeuka serikali ya Mobutu na mabishano na Wabelgiji. Wamarekani walimuona Lumumba ni kiongozi hatari na masilahi yao yangekuwa hatarini kama angebaki madarakani.

23 January 1961 Kasa-Vubu alimpandisha cheo Mobutu kuwa Mkuu wa Majeshi, De Witte anasema hii ilikua ni kwa sababu za kisiasa zaidi kwa nia ya kulipa jeshi nguvu kubwa zaidi, alikua mtu ambae raisi alimwamini zaidi pia umuhimu wake katika jeshi. 1964 Pierre Mulele aliongoza wafuasi wa vyama vingine katika mapinduzi. Kwa haraka walishikilia 2/3 ya eneo la Congo lakini jeshi la Congo likiongozwa na Mobutu waliweza kuchukua eneo lililotekwa lote ilipofika 1965.

Jaribio la pili la kupindua serikali

Waziri Mkuu Moise Tshombe ambae ndiye aliyekuwa kiongozi wa Congolese National convetnion alishinda uchaguzi kwa kura nyingi katika uchaguzi wa March 1965, lakini Kasa-Vubu alimtunuku kiongozi wa upinzani Evariste Kimba kuwa waziri mkuu, hata hivyo Bunge lilipinga uteuzi huo. Kufikia hapo serikali ilikua inayumba na Mobutu alichukua nafasi hiyo kufanya mapinduzi ya kijeshi 25 November 1965. Hii ni mara tu yakufikisha umri wa miaka 35.

Chini ya utawala wa dharura Mobutu alifikiri atapata nguvu kamili ya uongozi ndani ya miaka mitano. Hotuba yake ya kwanza baada ya kuchukua madaraka, Mobutu aliuambia umati wa watu mjini Leopoldville katika uwanja wa mkuu kuwa tangu wanasiasa waharibu nchi basi kwa miaka mitano hatutakuwa na chama cha siasa wala shughuli za kisiasa. Nguvu za bunge zilibaki kuwa ni mhuri tu kabla ya kufutwa kabisa lakini baadae zilirudishwa. Idadi ya majimbo ilipunguzwa na ushawishi wa majimbo ulidhoofishwa. Hii ilileta utawala wa amri kutoka kwa rais.

Kwakifupi serikali ya Mobutu ilikua madhubuti na pia siasa haikutakiwa kabisa. Neno siasa lilikua ni sawa na uhaini na mwanasiasa alimaanishwa ni mtu mpenda rushwa, tapeli na mhaini. Hata hivyo mnamo 1966 kulianza msukumo wa vikundi vya vijana vya kujitolea vilianza mikakati ya kumuondoa Mobutu ambae alijiita "Shujaa wa Pili wa Nchi"baada ya Lumumba. Kwa nguvu zote alijipa cheo cha mtu aliefuata nyayo za Lumumba na moja ya mambo aliyoazimia ni kuwa na serikali halali ndani ya Congo.

800px-Mobutu.jpg

Mwaka 1967 kilizaliwa chama cha Popular Movement of the Revolution (MPR) ambacho mpaka 1990 kilikua chama pekee cha kisiasa kilichoruhusiwa. Kwa lugha nyingine kilikua chama kilichoruhusiwa kisheria kuendesha shughuli za kisiasa nchi nzima katika imani moja. Serikali ilikuwa ni njia ya kuenzeza chama. Kila raia alikua mwanachma wa MPR tangia kuzaliwa. Agenda kubwa ya chama iliyojulikana kama N'Sele, ilikua na lengo la kuleta mapinduzi, uongozi wa vitendo ndani ya chama, hali hii ilionekana kama ni mchanganyiko wa siasa za ujamaa na ubepari.

Usemi mashuhuri wa MPR ulikua "Hatuko mwengo wa Kulia wala wa Kushoto". na wenyewe waliongezea "Hatuko hata katikati" miaka ya baadae. Chama cha MPR kilifanya uchaguzi kila baada ya miaka saba na mshindi kuwa raisi wa Jamhuri. Kila mwaka Mobutu alikua anapendekezwa kama mgombea pekee na jina lilipitishwa na uongozi mkuu wa chama ambao walikua na orodha ya wagombea nafasi za uongozi ndani ya chama.

Bunge lilirudi kila baada ya miaka mitano kama chombo cha kutunga sheria na kilimpa rais wa chama nguvu zote za kuendesha serikali. Mwaka huo huo vyama vyote vya kutetea haki za wafanyakazi viliunganishwa na kua chama kimoja National Union of Zairian Workers, chama hiki kiliendeshwa moja kwa moja kwa amri kutoka serikalini. Kwa matakwa ya Mobutu mwenyewe chama hiki kilikua chombo cha kuhakikisha agenda za serikali zinatekelezwa makazini iwe kwa sheria, nguvu au kwa ubishi. Vyama vingine vya kutetea haki za wafanyakazi havikuruhusiwa mpaka 1991.

Akikabiliwa na upinzani mwanzoni mwa utawala, Mobutu aliweza kuwanyamazisha aliweza kuwafanya wapinzani wake wengi wamkubali kwa kutumia mbinu mbalimbali na mbinu hizo zikishindwa, nguvu ilitumika. Mwaka 1966 mawaziri wanne waliwekwa ndani kwa kilichoaminika kuwa jaribio la kupindua serikali. Walishiatakiwa katika mahakama ya jeshi na walinyongwa hadharani, watu 50,000 wakishuhudia. Jeshi la Katanga liliteketezwa na mipango mingine iliyopangwa na jeshi la wazungu mwaka 1967 haikufanikiwa. Mwaka 1970 karibia kila aliekua tishio katika utawala wake alimalizwa and sheria za chama na serikali zilifikishwa karibu katika kila kona ya nchi.

Mwaka huu unaweza kuelezewa kuwa mwaka uliofikisha kileleni utawala wa Mobutu wa kisheria na nguvu. Mfalme Baudouin wa Ubelgiji alifanya ziara ya kiserikali iliyokuwa na mafanikio makubwa na mwaka huo huo uchaguzi wa bunge na rais ulifanyika. Chama cha MPR pekee ndio kilishiriki uchaguzi ingawa kwa kisheria ilitakiwa vyama viwili vya kisiasa vishiriki uchaguziKulingana na matokeo ya uchaguzi huo kwa mashaka MPR kilipata ushindi wa asilimia 98.33% ya wapiga kura wote. Katika uchaguzi wa raisi Mobutu alikua mgombea pekee, wapiga kura walipewa karatasi mbili wachague kati ya kijani kukubali au nyekundu kukataa. Mobutu alishinda kwa kuta 10.131.699 mpaka 157.

COLLECTIE_TROPENMUSEUM_Katoenen_overhemd_met_portret_van_Mobutu_TMnr_5829-1.jpg

Jinsi Mobutu alivyozidi kupata nguvu ndiyo alivyoimarisha jeshi kwa nia moja kubwa ya kumlinda yeye. Kulikuwa na Kikosi Maalum cha Raisi, Jeshi la Usalama, Jeshi Maalum la Upelelezi na Vitendo.

Mwendelezo wa Kampeni

Kulianza kwa kile kilichoaminiwa mwendelezo wa jadi ya Mwafrika au uasilia. Mobutu alianza kubadilisha majina ya miji ya Congo kuanzia 1 June, 1966; Leopoldville kuwa Kinshasa, Elisabethville kuwa Lubumbashi na Stanleyville kuwa Kisangani. October 1971 alibadili jina la nchi kuwa Jamhuri ya Zaire. Watu waliamrishwa kuacha majina yao ya ki Kristu na majina yaliyotambuliwa yalikuwa ni ya jadi tu. Viongozi wa dini walipewa onyo kali kuwa atakaembatiza mtoto ki Zaire kwa jina la Kikristu atafungwa jela miaka mitano. Suti za Magharibi na nguo nyingine zilipigwa marufuku na wanaume walilazimishwa kuvaa style ya Mao iliyokuwa koti fupi mpaka juu kidogo ya magoti lenye mikono mifupi lilojulikana kama abacost kifupi cha (a bas le costume down with suit).

1972 Mobutu alibadilisha majina yake wenyewe na kujiita Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu Wa Za Banga ("Shujaa wa mashujaa mshindi ambae kwa ujasiri na kutokukubali kushindwa atashinda na kushinda na kuacha moto nyuma yake"). Huu ndio wakati Mobutu alikuwa na style yake ya mavazi ambayo ni abacost, miwani yenye frame nzito, fimbo ya kutembelea na kofia yenye ngozi ya chui.

Utawala wa mtu mmoja

Mapema katika utawala wake Mobutu alijipatia nguvu kwa kupindua serikali, kunyonga wapinzani wake hadharani, kutesa na kuua wapinzani na utawala wa vitisho. Kwa mfano wengi walinyongwa mbele ya umati wa watu akiwemo aliekuwa Waziri Mkuu Evariste Kimba, ambae pamoja na mawaziri wengine watatu Jerome Anany (Waziri wa Ulinzi), Emmanuel Bamba (Waziri wa Fedha) na Alexandre Mahamba (Waziri wa Nishati na Madini) walihukumiwa May, 1966 na walipelekwa kunyongwa 30, May mbele ya watu 50,000. Wanaume hao waliuliwa kwa kuwa na mawasiliano na Colonel Alphonse Bangala na Meja Pierre Efomi, kwa mipango ya kupindua serikali. Mobutu alielezea kitendo hicho kama "Mmoja inabidi mmoja atoe adhabu ili iwe mfano kuweka utawala wenye nidhamu. Kamanda akichukua hatua ni mwisho wa maamuzi".

1968 Pierre Mulele, aliekuwa Waziri wa Elimu wa Lumumba na kiongozi wa upinzani waka wa Upinzani wa Simba 1964, alishawishiwa kurudi kutoka ukimbizini Brazzaville kwa mategemeo kuwa atakua na kinga, lakini aliteswa na kuuwawa na askari wa Mobutu. Wakati Mulele alikua hai, macho yake yalitolewa na sehemu za siri kukatwa na miguu ilikatwa mmoja mmoja. Mobutu baadae alihama kutoka kutesa na kuuwa na akabadili mbinu, na kuanza kununua maadui wake wa siasa. Alitumia usemi "Weka marafiki zako karibu lakini maadui waweke karibu zaidi, akimaanisha mbinu ya kubadili mioyo ya maadui zake kwa kutumia hongo.

Mnamo 1972 Mobutu alijitahidi bila mafanikio kujiweka yeye mwenyewe kuwa rais wa maisha. Katika amri iliyosainiwa na General Likulia Bolongo iliyompandisa Mobutu kufikia cheo cha Marshal, Victor Nendak Bika, kwa uwezo wake maka Makamu wa Rais wa Halmashauri Kuu, iliyokuwa ya pili ki madaraka katika nchi, alitoa hotuba iliyomsifu Rais Mobutu.

Alitaifisha mashirika ya nje na aliwalazimisha wawekezaji wa nje watoke nchini mara moja. Mara nyingi alikabidhi madaraka ya uendeshaji wa mashirika haya kwa ndugu zake ambao waliiba. Hali hii ilipelekea uchumi kuyumba kiasi ambacho mwaka 1977 Mobutu ilibidi ayashawishi mashirika ya nje yarudi.

Kikundi cha waasi cha Katanga kilichojiimarisha nchini Angola kilivamia serikali mwaka 1977 kikundi hiki kilipinga misaada ya Mobutu kwa MPLA. Ufaransa iliwaleta askari wa parachuti kutoka Morocco na kutuliza ghasia, hii ilimaliza vita ya kwanza ya Shaba ambayo ilidumu kutoka March mpaka May 1977. Waasi hawa waliishambulia Zaire tena katika jaribio la Shaba II, safari hii Ubelgiji ilileta majeshi ikisaidiwa na Marekani na kufanikiwa kuwatoa waasi.

Mbinu Mobutu aliyoipendelea sana ni kucheza "mziki wa viti", kubadilisha mawaziri wake katika serikali na kuhakikisha kwamba hakuna atakae kuwa hatari kwa serikali yake. Mbinu nyingine ilikuwa kuwaweka ndani na kuwatesa wakaidi wa serikali, baadae aliwatoa kwa msamaha na kuwapandisha cheo. Mfano mzuri wa hili ni tukio ni Jean Nguza Karl-u-Bond, ambae alifukuzwa kama waziri wa mambo ya nchi za nje mwaka 1977, alihukumiwa kufa, na aliteswa. Baadae Mobutu alibadilsha hukumu yake kuwa kifungo cha maisha, alitolewa mwaka mmoja baadae na baadae alipewa uwaziri mkuu. Nguza alikimbia nchi mwaka 1981 na alirudi 1985, kwanza alipewa cheo cha balozi wa Zaire nchini Marekani na waziri wa mambo ya nje.

Alichaguliwa tena kama mgombea pekee kwenye uchaguzi wa 1977 na 1984. Alitumia muda mwingi kujiongezea utajiri wake mwenyewe. Inakadiriwa US$ billioni, nyingi ya hizo zipo katika Swiss bank (hata hivyo sehemu ndogo ya pesa hiyo imepatikana alipotolewa madarakani karibu US$ 3.4 millioni). Pesa alizoiba Mobutu zilikuwa sawa na deni la nchi wakati anaondoka madarakani, na ilipofika 1989 ilibidi nchi ilibidi kutangaza kuwa haina uwezo wa kulipa madeni ya nje hasa ya Ubelgiji.

Alimiliki msururu wa magari ya Marcedes-Benz aliyoyatumia kusafiri kutoka nyumba yake moja kwenda nyingine wakati wananchi wake hawana chakula. Miundo mbinu ilikufa kabisa na wafanyakazi wa serikali walikaa kwa miezi bila kulipwa mishahara. Pesa nyingi ilichotwa na family ya Mobutu, wanasiasa wa vyeo vya juu na viongozi wa jeshi. Wafanyakazi wa karibu na rais tu, ambao walimlinda ndio walilipwa kila mwezi. Kuna usemi ulisema "wafanya kazi wa serikali waliigiza kama wanafanya kazi wakati serikali iliigiza kama inawalipa".

Jambo lingingine katika kushindwa kwa utawala wa Mobutu katika uendeshaji wa uchumi wa nchi, kulipelekea marafiki zake kuchota mali ya serikali, nchi ilifilisika, kulikua na tofauti kubwa kati ya mshahara unaolipwa na vitu unavyomudu kununua kwa mshahara huo. Serikali nzima kila mtu alikuwa mwizi kwa uwezo wake.

Mobutu alijulikana kwa maisha yake ya kifahari. Alitembea mto Congo katika meli yake nadhifu Kamanyola. Katika mji wa Gbadolite alijenga palace aliyoipa jina "Versailles of the jungle". Kwa safari zake za madukani Paris alikodi Concorde kutoka shirika la ndege la Air France na ilitua Gbadolite Airport, njia zake za ndege zilijengwa ili zimudu ukubwa wa Concorde na utuaji na upaaji wake. 1989, Mobutu alikodi Concorde F-BTSD kwa 26 June - 05 July kwa safari ya kwenda kuhutubia Umoja wa Mataifa New York City,na tena July 16 kwenda Paris alikokuwa wamealikwa na rais Francois Mitterrand na tarehe 19 July kwa safari ya Paris mpaka Gbadolite na tena safari nyingine kutoka Gbadolite mpaka Marseille.

Utawala wa Mobutu ulijulikana kama wa kwanza duniani kwa nafasi kutolewa kwa kujuana. Marafiki wa karibu na watu watu wa kabila lake la Ngbandi walipewa vyeo vya juu katika jeshi na serikali, alimtaarisha mtoto wake wa kwanza Nyiwa aje kuwa rais baada ya yeye, bahati mbaya alikufa kwa UKIMWI mwaka 1994. Aliendesha utawala wa usiovumilika wa kidiktekta barani Afrika. Alijitengenezea utajiri wake mwenyewe wa US$ 5 billion kwa kuuza mali asili za nchi, wakati watu wake ni masikini na wanakufa na njaa. Katika historia Mobutu ni rais aliyeweka rekodi kwa ubadhirifu wa mali ya umma na utawala wa kujuana.

Faida alizojipatia binafsi katika utawala wake

Mobutu alijichukulia fedha za nchi kwa mabillioni ya dola za ki Marekani. Inasemekana aliiba kati ya US$ billioni 4-5 lakini wengine wanasema inafika US$ billioni 15. Mkwe wa Mobutu Pierre Janssen aliemuoa binti yake Yaki Mobutu anasema, Mobutu hakujali gharama ya zawadi aliyotoa kwa marafiki na watu wake wa karibu. Wakati wa ndoa yao Janssen anasema bendi tatu zilitumbuiza na keki ya harusi pamoja na mapambo viligharimu US$ 65,000. Bibi harusi Yaki alivaa gauni la US70,000 na mapambo mengine kama mkufu na hereni yaligharimu US$ 3 million. Janssen anasema siku ya kawaida ya Mobutu iliambatana na vyakula na mivivyo ya gharama iliyoletwa kutoka Ufaransa na nchi nyingine.

Moja ya majumba ya Mobutu linavyoonekana kutoka angani. Ujenzi wake uligharimu US$ million 100

51e4e0e5-811d-4c86-ab65-b4ce049bfccc-1020x612.jpeg

Moja ya sherehe za kuapishwa kwa rais Mobutu ndani ya palace

23f7906d50f3c6c3bad6918126bd0aaf.jpg

Mke wa kwanza wa Mobutu ambae alimpenda sana Marie Antoinette Mobutu. Chanzo cha uhakika kimenieleza mauti ya huyu mama yalisababishwa na kipigo alichokipata kutoka wa mume wake akiwa mja mzito. Pamoja na kuwa aliwahishwa hospitali nchini Switzerland lakini aliaga dunia, hiyo ilikuwa mwaka 1977.

Serikali ya mseto

May 1990, kutokana na kumalizika kwa vita baridi kati ya Mataifa ya Magharibi na Mashariki barani ulaya, kulikuwa na vugu vugu jipya la kisiasa pamoja na ki uchumi, matatizo ya ndani katika Seriklai ya Mobutu yaliongezeka na kulikuwa na mivutano mikubwa. Mobutu ilibidi akubali mfumo wa vyama vingi. Alichagua serikali ya muda itakayosimamia uchaguzi wa vyama vingi lakini alijiachia madaraka yote muhimu. Kufuatia vurugu za Kinshasa kutoka kwa askari ambao hawajalipwa mishahara, Mobutu alileta vyama vya upinzani katika serikali ya mseto lakini bado alikuwa na madaraka makubwa na wizara zote za muhimu.

Mgongano huo uliletea kuundwa kwa serikali mbili mwaka 1993, serikali moja ilimuunga mkono na nyingine ilimpinga Mobutu. Serikali iliyompinga Mobutu iliongozwa na Laurent Monsengwo na Etienne Tshsekedi kutoka Union for Democracy and Social Progress. Hali bado haikuwa nzuri na kufikia mwaka 1994, magroup haya mawili yaliungana na kuunda bunge la pamoja. Mobutu alimchagua Kengo Wa Dondo kuwa mwanasheria wa kuangalia mipango na matumizi ya serikali na soko huria. Wakati huu hali ya afya ya Mobutu ilikuwa mbaya na alikuwa ulaya mara nyingi kwa matibabu. Tatutsi walivamia sehemu kubwa ya mashariki ya Zaire.

Kutolewa madarakani

Mobutu alitolewa madarakani katika vita ya kwanza ya Congo na Laurent -Desire Kabila, ambae alisaidiwa na serikali ya Rwanda, Burundi na Uganda.

Wakati serikali ya Mobutu ilipotoa amri November 1996 kuwafukuza Watutsi Zaire na kuwa wakibaki wanauwaw, Watutsi wa Zaire wanaojulikana kama Banyamulenge, walikuwa chanzo cha fujo. Kutoka mashariki mwa Zaire, waasai na majeshi ya nje kwa kuongozwa na rais Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Rwanda kwa amri ya Paul Kagame walifanya mashambulizi makubwa ya kumtoa Mobutu, walishirikiana na majeshi ya ndani yaliyompinga wakati wanatembea Magharibi wa nchi kuelekea Kinshasa.

Akiwa anasumbuliwa na cancer, Mobutu alikuwa Switzerland kwa matibabu, alishindwa kujipanga kujibu mashambulizi yaliyomaliza nguvu zake.

Katikati ya mwaka 1997, majeshi ya Kabila yalikuwa yamefanikiwa kuchukua karibia nchi nzima. Mnamo May 16, 1997, kufuatia kuanguka kwa mazungumzo ya amani yaliyofanyika Pointe-Noire katika meli ya kijeshi ya Afria Kusini chini ya uenyekiti wa Nelson Mandela akiwepi Laurent Kabila, Mobutu alikimbia nchi.

Majeshi ya Kabila yaliyojulikana kama alliance of Democratic Forces for the Liberation of Congo-Zaire (ADFL), yalitangaza ushindi siku ya pili yake. Hata hivyo Mobutu alikuwa na bahati ya kushika madaraka kwa kipindi kirefu hivyo, jeshi lake lililobakia halikuwa na nguvu ya kukabiliana na shambulizi lolote, kitu kilichozuia mapigano ya miguu ya AFDL ilikuwa miundo mbinu mibovu ya nchi. Kwa miaka mingi hakukuwa na barabara za uhakika; njia pekee za usafiri zilitumia barabara za vumbi na za kubahatisha. Nchi ilipewa jina jipya la Democratic Republic of the Congo.

Mazishi ya Juvenal Habyarimana

Mobutu alikuwa na mabaki ya mwili wa aliyekuwa rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana, aliyahifadhi kwenye kwenye jeneza huko Gbadolite. Tarehe 12 May 1997, jeshi la Kabila liilipokaribia, Mobutu aliamrisha mabaki ya mwili ule yasafiirishwe ndani ya jeneza lake kama mzigo kuelekea Kinshasa ambapo alisubiri katika kiwanja cha ndege cha N'dijili kwa siku tatu. Tarehe 16 May, siku moja kabla Mobutu hajakimbia, mabaki yale ya Habryrimana yalichimwa moto chini ya usimamizi wa kiongozi wa Hindu.

Mobutu ukimbizini mpaka mauti yalimpomfika.
Mobutu alikimbilia Togo mara baada ya kutoka Zaire lakini aliishi Morocco kwa muda mrefu zaidi. Alifariki tarehe 07 September, 1997, Rabat Morocco, kutokana na cancer ya tezi dume. Alizikwa Rabat, katika makaburi ya Wakritu kama Mkritu. Mwezi December 2007, Bunge la Democratic Republic of the Congo lilitoa mwongozo wa kurudishwa kwa mabaki ya mwili wa Mobutu na jeneza lake.

Siku ile Mobutu anakimbia, Larent-Desire Kabila alikuwa rais mpya wa Congo. Kabila aliuwawa na aliyerithi madaraka yake ni mtoto wake Joseph Kabila.

Mambo yaliyofanywa na Mobutu

Mobutu aliamrisha ngumi za Rumble in the Jungle ambazo zilimhusisha Mohamed Ali na George Foreman zipiganiwe Zaire tarehe 30 October 1974. Kwenye mahojiano ya luninga Don King aliyekuwa promoter wa Mohamed Ali, aliahidi US$ 5million kwa shindano hilo. Mobutu alikuwa mtu pekee aliyejitolea kutoa kiwango hicho cha pesa, lengo lake ilikuwa kuionyesha dunia kuwa serikali yake inauwezo huo. Mohammad ali alinukuliwa akisema " Nchi nyingine zinakwenda vitani ili kuonyesha uwezo wao wakati vita inagharimu zaidi ya $ 10 millioni".

The_Rumble_in_the_Jungle_poster.jpg

muhammad-ali-zaire.jpg

Mohammad Ali akiwa Zaire 1974.


Shwari Ameongeza:

Katika picha hiyo hapo juu, picha ya kwanza, nyuma ya Mobutu, kwenye ngazi ya ndege (ambaye sura yake inafanana na sura ya Moise Tshombe), ni Justin Bomboko, waziri wa mambo ya nchi za nje katika serikali ya Mobutu. Ndiyo huyo aliyekwenda Congo-Brazzaville, 8 October 1968, katika yatch ya Mobutu, kumshawishi Pierre Mulele arudi Congo-Kinshasa kusaidia kujenga taifa.

Alimwambia Mulele amesamehewa pamoja na wengine walioanzisha vurugu nchini. Sasa ni wakati wa kujenga taifa lenye amani na umoja. Miongoni mwaa walikuwa ni wafuasi wa Lumumba aliyekamatwa na Mobutu 17 January 1961 na kupelekwa Elisabethville, Katanga, ambako aliuawa na Tshombe siku hiyo hiyo usiku. Mulele alikuwa ni mmoja wa viongozi wa wafuasi wa Lumumba na ndiye aliyesemakana kuwa ni mrithi wa Lumumba.

Bomboko alitumwa na Mobutu kumshawishi Mulele arudi Kinshasa. Wakati ule, Mobutu alikuwa katika ziara rasmi Morocco. Alitumia ziara hiyo kujaribu kujiepusha na lawama itakayofuata baada ya Mulele kuuawa wakati yeye hayupo Kinshasa. Lakini, ingawa Mobutu alikuwa Morocco wakati ule, bila shaka ni yeye aliyetoa amri ya kumuua Mulele atakaporudi Kinshasa ingawa kuna taarifa iliyosema Mobutu alimaaanisha aliposema Mulele amesamehewa na kwamba askari waliomuua Mulele walikwenda kinyume cha matakwa yake. Askari na viongozi wengine waliomuua Mulele walijua Mobutu alikuwa ni kiongozi wa aina gani, mkono wa damu, na wasingethubutu hata kidogo kumpinga na kwenda kinyume cha matakwa yake. Ni vigumu kuamini Mobutu alitaka Mulele aendelee kuishi.

Pia Mobutu alimtuma Bomboko kumshawishi Mulele arudi nyumbani kwa sababu Bomboko na Mulele walikuwa wamefahamiana kwa muda mrefu. Walikuwa mawaziri pamoja katika serikali ya Lumumba. Mulele alikuwa waziri wa elimu; Bomboko, waziri wa mambo ya nchi za nje. Mobutu alimteua Bomboko kuwa waziri katika serikali yake kujaribu kuwatuliza wafuasi wa Lumumba na kuwahakikishia kwamba alikuwa na nia ya kuwaunganisha wananchi, wafuasi wa Lumumba na wafuasi wake pamoja na wengine, ili wajenge taifa lenye amani na umoja kwa manufaa ya wananchi wote.

Bomboko alipokwenda Brazzaville, ng'ambo ya Mto wa Kongo kutoka Kinshasa, alikutana na raisi wa Congo-Brazzaville, Marien Ngouabi. Ngouabi alikuwa na mashaka sana na ahadi aliyopewa na Bomboko kwamba Mulele akirudi nyumbani, Congo-Kinshasa, atakuwa salama. Hawatamdhuru. Mulele pia alikuwa na mashaka ingawa alifahamiana na Bomboko tangu walipokuwa mawaziri pamoja katika serikali ya Lumumba. Ngouabi alisisitiza Bomboko aweke ahadi hiyo katika maandishi na kuweka sahihi yake kuthibitisha aliyosema ni ukweli mtupu.

Bomboko aliongopa. Lakini alijua Mulele atamwamini, na labda atakubali kurudi Congo-Kinshasa, kwa sababu walifahamiana wakiwa mawaziri pamoja katika serikali ya Lumumba. Mulele aliporudi Kinshasa, aliteswa sana na kuuawa kinyama siku ifwatayo, 9 October 1968. Walinyofoa macho yake na kukata sehemu zake za siri, miguu na mikono na sehemu zingine vipande vipande, bado akiwa hai, na kutupa mwili wake (vipande mbalimbali) katika Mto wa Kongo kuliwa na mamba. According to Africa Contemporary Record: Annual Survey and Documents 1968 – 1969:
 
Alitafunwa na Kansa iliyotafuna Uume na kuishia kufia Morocco alipozikwa na watu wasiozidi 6 kama Balali japo alikuwa miongoni mwa Watu weusi Tajiri zaidi kuwahi kutokea katika Uso wa Dunia.
Alistahili hicho kifo mkuu,...unafiki waliomfanyia Lumumba ulikuwa wa kipuuzi sana,.....hell him.
 
Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga alikuwa kiongozi wa kijeshi dikteta huko Zaire. Mke wake wa kwanza Marie-Antoinette Mobutu, alifariki kwa ugonjwa wa moyo mwaka 22 October 1977 Genolier, Switzerland akiwa na umri wa miaka 36.
mobutu-sese-seko-14101997politiker-demokratische-republik-kongo-mit-picture-id545959047



1 May 1980, alimuoa Bobi Ladawa pamoja na pacha mwenzake Kosia, Bobi na Kosia ni identical twins na mzee aliamua kuoa wote wawili.

Capture-d%E2%80%99e%CC%81cran-2015-09-14-a%CC%80-12.05.46.png


Bobi Ladawa was Mobutu Sese Seko’s wife. She shared her marriage with her twin sister Kosia. Bobi gave birth to two sons and two daughters while Kosia had three daughters.
Samahani nikusahihishe sehemu chache za bandiko lako, Mobutu amekufa akiwa na umri wa miaka 66, 7 September 1997 (aged 66) huko Rabat, Morocco.
Tembelea hapa kwa taarifa zaidi:

Mobutu Sese Seko - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Wakati anamuoa Bobi (wa kushoto) Kosia alikua ameshaolewa, mzee alipomuona alimpenda na mume wa Kosia aliambiwa aachie wenye pesa wachukue mke.
Ilikua ngumu kumkatalia mzee mwenye nchi kwanza mwanamke tu mwenyewe atakua alianza kuleta shobo kwa mumewe. Hata mugabe alimpora bibie grace mugabe kutoka kwa rubani wa jeshi halafu jamaa akapewa post ulaya kimya. Trend imetoka mbali sana kama unakumbuka hata kwenye biblia mfalme daudi na mama yake suleiman kweli mwenye mamlaka na pesa sio mwenzio.
 
Back
Top Bottom