EPISODE 6.
Nipo cellule ground floor,,hii ni cellule ambazo ni maalum kwa new arrival prisoners...
Hizi cellule zinakuwa na tv tu,,bila fridge.
Lakini inakuwa ni nzr na Safi Sana.
wakati nipo ndani natafakari,,
anafungua mlinzi wa gereza ananijulisha kwamba sasa ni muda wa kwenda promenade (matembezi nje)
Hii promenade ni hiyari kutoka na kutembea..(ni uwanjani ambapo watu hutembea na kufanya mazoezi )
Ila prominade ni hatari sn,,
Watu wale wasiopenda matatizo hukaa ndani mwa cellule zao bila kwenda promenade kuhofia vurugu.
Promenade inakuwa ni muda maalum uliowekwa kwa ajili ya wafungwa wote kupata nafasi ya kwenda promenade.
Promenade ni masaa 2 na ikifika nusu saa kabla ya masaa 2 kuisha huwa kuna tangazo mnatangaziwa kujiandaa kurudi kwenye cellule zetu.
"La promenade est terminee"
utasikia sauti za walinzi wakitujulisha kuisha kwa promenade kupitia speaker iliyopo pale uwanjani.
Hii promenade masaa 2 kila floor,
Watu wa floor Mfano 2nd,,au 1st ,3rd ,au 4th..
Kila baada ya masaa mawili floor moja wanaingia ndani,,wanatoka floor ingine.
Hawa ni wale ambao hawana kazi pale prison.
Ila kwa wale wanaofanya kazi mbali mbali hapa prison,,
wao wanakuwa na muda maalum wa saa nzima kukutana kwenye promenade.
Na muda wao ni Kati ya saa 7 mchana na saa 8 wanarudi cellule..
Hawa wanakuwa ni mchanganyiko wa wafungwa wote wa jengo lile(batman)
Bila kujali floor wanazotoka.
Wafungwa hupangiwa floor kulingana na aina za kazi wanazofanya..
Mfano 1st floor 99 percent wanafanyakazi na ndani ya cellule wapo double.2 prisoners.
ni wafanyakazi either la cuisine(jikoni) or atelier.(kiwanda kidogo cha kutengeneza vitu humu humu prison).
2 nd floor hawa nao ni wafanyakazi either la cuisine(jikoni) or kazi za kusafisha gereza.(hawa huishi double person Dan la cellule).
3 rd floor hawa huishi double persons kwa cellule).wengi hawafanyi kazi Ila wachache ambao wanafanya kazi la cuisine.(jikoni)
4 th floor hawa huishi peke yao .
Mara nyingi ni watu wasiopenda sn vurugu na kupenda kuishi peke yao gerezani ..
Ukiwa 4th floor maana yake utaishi peke yako cellule.
Kila mfungwa ana hiyari ya kuishi na amtakae gerezani.
Kama hamuendani kitabia na cellule partner,, unaruhusiwa kuandika barua na kubadilishiwa cellule na rafiki umtakae.
Kwa wastani kila cellule ni 1 person au 2 Tu kama ukipenda kuishi double.
Huko new arrival promenade tulikuwa kama prisoners 10 tu ,
Nilipata taabu Sana kwenye mawasiliano,,
maana sijawahi kuongea wala kukisikia kifaransa zaidi ya bonjour,,ca va?
Kila ninaekutana nae English hajuwi,,
ilikuwa shida sn kwangu,,
Baada ya week nikahamishwa 2nd floor.
Hapo ndipo nilipokutana na jamaa wengi sn kutoka Nigeria,, England,,na baadhi ya English countries wanazoongea kingereza.
Hapo ndipo nilipojuwa habari na mambo mengi ya gerezani..
Hapa ndipo nilipogunduwa kumbe promenade ni sehemu ya wafungwa kuonyesha ufahari wa nguo na viatu.
watu huvaa nguo mpya na za thamani kubwa.
Wafungwa wanapata nafasi ya kuonana na jamaa zao kutoka nje na kuwanunulia chochote wanachotaka huko nje..
Mfungwa anampelekea mkewe nguo bag zima,,
Zinakwenda kufuliwa home na kuletewa nguo mpya zingine kila week.
Hiyo siku ya kukutana na wapenzi wao kila mfungwa amependeza vizuri na kunukia vzr.
Wenyewe wanaita( Palwa).
Hapo promenade nilikutana na jamaa kibao kutoka Africa,,
nilishangaa sn kwa nn nusu ya gereza ni blacks?
Senegalese,, Malians, Cameroonians, Congolese,na wengi wanazoongea french.
Nilikuja kugunduwa vitu vingi sn baadae.,,
Sisi watu weusi na hawa waarabu(Moroccoans, Algerians, Egyptians,libyans, Tunisians tumekuwa ni tatizo Sana ulaya.
Nusu ya watu weusi na waarabu hapa gerezani wapo kwa uhalifu wa mitandao,,na drugs,,au kupigana nk.
Hapa promenade ndy watu huongea biashara za magendo,,
Mfano ukitaka simu ,
Kupigana hapa ni kawaida Sana,,na mkipigana walinzi watawaacha hapo,,Ila baada ya kuingia ndani mtazuiwa kupelekwa chumba cha adhabu for 2 weeks.
Lakini kabla ya kuadhibiwa mnapewa nafasi ya kujieleza chanzo cha ugomvi na atakae bainika ndy tatizo basi hupelekwa kwenye adhabu.
Hapa ,ukitaka mwanamke,,watu wanaongea na demu nje anakuja kukutembelea na kugegeda pia kwa malipo..
Connecting kibao za maisha utazipata pale prominade maana huna nafasi ya kumwona mwenzako popote zaidi ya prominade au mkutane tena shule,,
au msikitini,,au kanisani,,au library.
Hapa prominade ndy watu hupata nafasi ya kupiga simu kwa jamaa zao.
Na namba zote ni lazima ziwe approval by utawala wa gereza.
Promenade ndy kuna mawakili wa kesi mbali mbali za humu jela huzungumzwa.
Mfano kama kuna mfungwa snitch amewaambia walinzi habari za mfungwa mwenye simu.,,basi hapa ukigundulika utahukumiwa kwa kipigo na wenzio.
Kama mfungwa amekopa vitu vya watu na hajalipa hapa prominade ndy atapata kipigo hadi arudishe pesa za watu.
Hapa prominade watu hupata nafasi ya kuri fresh akili na kufanya mazoezi mbali mbali..
Hapa ndipo sigara na hashishi huuzwa .
Jela hakuna matumizi ya pesa lakini biashara hufanyika kupitia sigara.
Unaweza kununuwa chochote Mfano simu,,jiko kutoka kwa mfungwa mwenzio kupitia pakti za sigara kwa kiasi kile cha pesa.
Mfano simu ni euros 250,
Utahitajika utoe sigara pakti 25 kulipia simu.
Kama iPhone 6 ni euros 500 utalazimika kulipa packet 50 za sigara.
Ukinunuwa chochote kwa mfungwa mwenzio ujuwe malipo ni sigara.
Na mtu huziuza humo kwa mfumo wa bitcom..au kuna namba fulani kama system fulani ya kupata pesa nje.
Sasa wapo watu hutoa bitcoin fake,,ukigundulika ndy hapo utakapokula kichapo.
Hapo ndipo watu huuza sigara kwa ulanguzi.
Dukani sigara huuzwa 8 euros kwa packet na kuuzwa euros 20 hapo promenade.
Hapa kuna ma group ya watu mbali mbali ambayo wana connection tokea huko nje walipotoka.
Hupigana pamoja na hutembea pamoja,
Ukipambana na mmoja basi umepambana na kundi zima.
Na pia kama kuna mfungwa ni snitch na hataki kuja prominade
,,anaadalia mtu wa kuishi nae cellule moja bila muhusika kujuwa.
Lengo ni kufuatwa huko huko cellule kwako ili upigwe na huyo mbabe..
Na malipo ya huyo mbabe ni kupitia sigara.
adhabu ya kupigana jela ni kuwekwa chumba cha peke yako bila tv,au fridge..kwa week 2,
then unapokonywa kazi unayofanya na kurudishwa floor ambayo hutofanya kazi tena.
Ukiwa new arrival unapewa karatasi maalum ya kuandika number zako za simu za watu wako.(phone numbers)
Unaituma kupitia box maalum la kutumia barua.
Then baada ya mwezi mmoja ndy namba zako zinaidhinishwa na uongozi wa gereza tayari kwa kupiga simu.
Utaweka pesa kiasi unachotaka ktk acc yako ya phone call box.
Utatumia namba zako za jela kama code ya kupiga simu ili uweze kuunganishwa.
Utalazimika kurecharge pesa kila zinapikwisha kwenye salio lako la simu.
Kila mfungwa ana namba zake alizosajiliwa kupiga simu.
Hakuna namba ambayo haijasahiliwa na uongozi wa jela itaweza kuunganishwa.
Ni lazima iwe approved.
Na maongezi ya simu ni recorded na yanasikilizwa na utawala..
Hairuhusiwi kuwa na simu Ila prisoners karibu 90 percentage wanasimu gerezani..
Nilitumia mwezi mmoja kusubiri namba zng za simu ziwe approved na utawala ili nipige simu nyumbani.
Muda wote karibu mwezi mzima hakuna aliyekuwa nilipo...
Itaendelea..
View attachment 2075464