Mkuu kuna kitu umekisema hapo kuwa unapewa simu unaongea na ndugu zako ila unachoongea wanakuwa wanasikiliza sasa mfano kama mtu anaongea kilugha cha kwao labda kihaya kigogo kisukuma wakikusikia nn kinatokea
Kwanza unatakiwa uandike namba zako ambazo utahitaji kuzitumia,
Halafu unaziwakilisha hizo namba kwa chief wa prison.
Wanazisajili.
Baada ya mwezi utapata majibu ya kuanza kutumia hizo namba.
Unapewa na tahadhari kwamba simu zote ni recorded na zinasikilizwa..
Na kama itatokea watashindwa kuelewa unachoongea basi wanaweza kusitisha mawasiliano yako.,
Au wakablock namba unazozungumza kwa lugha tata.
Mfano ,
week moja baada ya kukamatwa kuna barua moja niliiandika kwa Kiswahili kuituma nyumbani Tanzania.
Lakini ilijaa maneno ya kiswahili cha mitaani,
Ile barua haikufika hadi leo ,
Means waliishindwa kutafsiri baadhi ya maneno na kuamua kuitupa.
Barua zinazomwa kabla ya kuzituma,au zinazomwa kabla ya kuzipokea.
Simu pia zinasikilizwa.