Mwaka Jana nilikuwa na mpango wa kutoa kitabu cha Facebook Ads Manager, lakini sikufanikiwa kwa sababu hii

Lackson Tungaraza

New Member
Dec 3, 2015
3
1
Kwenye laptop niliyokuwa ninatumia kukiandaa, nilikuwa nimetengeneza Folder maalumu kwa ajili ya kazi hiyo.

Ndani yake nilijaza screenshot ya hatua zote (muhimu) ambazo mtu yeyote (beginner) anaweza akazifuata na kuishia kutengeneza matangazo ya Sponsored ads yenye matokeo mazuri.

Ila kila wakati nilikuwa ninaghairi kuzipangilia hizo screenshot ndani ya kitabu nilichokuwa ninampango wa kukitoa... kwa kuamini kuna siku nitapata muda wa kutosha wa kufanya hiyo kazi.

Bwana weeeh! Waswahili hawakukosea waliposema, "Majuto ni mjukuu" na "Usilolijua ni sawa usiku wa kiza kinene"

"Eh! Screenshot zangu ziko wapi?

Ndilo swali nililokuwa najiuliza kwa saa 2 mfululizo huku nikiendelea kuzunguka kwenye laptop yangu kama kichaa.

Lakini sikuziona screenshot zangu.

Nilipoongeza umakini zaidi, nikazipata, ila zilikuwa tofauti na matarajio yangu.

Zote zilikuwa zimeandikwa "0 KB"

Nikajiuliza, "Ndio kitu gani hiki?"

"Aiseeh! Wadudu wameshakula kazi yangu." Nikajisemea baada ya kujua 0KB ni aina ya virusi vinavyokula kazi za watu kwenye vifaa vya kielektroniki kama vile kompyuta, smartphone, flash disk, n.k.

Nikawa nimepoteza kazi yangu niliyoteseka kuiandaa kwa zaidi ya siku 14 kwa sababu ya kughairi-ghairi kuifanyia kazi

Ndio maana huwa nawapatia huu ushauri waandishi wa vitabu...

"Jitahidi kutunza vitabu vyako kwenye email au Google drive ili viwe salama zaidi...

"WhatsApp inaweza ikapata shida ukapoteza kazi zako...

"Na vivyo hivyo kwa simu yako na laptop; vinaweza kuharibika, kuibiwa, au kuvamiwa na wadudu (virusi) ukapoteza kazi zako."

Ni hayo tu kwa leo
Yafanyie kazi
Ili usije ukajilaumu kama mimi nilivyojilaumu baada ya kupoteza kazi zangu (zilizoliwa na virusi kwenye laptop yangu).

BY THE WAY,

Karibu @lamaxdesigns
KWA HUDUMA ZIFUATAZO...

1. Typesetting
2. Layout Design (kupangiwa kitabu chako vizuri)
3. Cover Design (sanifu ya jalada la kitabu chako)
4. Editing (uhariri wa vitabu)
5. Printing

MAWASILIANO: Bonyeza hii link kuja WhatsApp Lackson Tungaraza

Angalia hapa Shuhuda (Zaidi Ya 57) za Waandishi wa Vitabu Waliofanya Kazi Nasi

Angalia hapa Sample (Zaidi Ya 97) za Book Cover Design Tulizofanya:

BY LACKSON TUNGARAZA
Mwandishi wa Vitabu zaidi ya 15, Tanzania, Muasisi wa @lamaxdesigns na Mkufunzi wa Waandishi wa Vitabu.
 
Back
Top Bottom