Hili linasikitisha sana na kufurahisha pia - Maisha Ya Harry Maguire

Lackson Tungaraza

New Member
Dec 3, 2015
3
1
🎯HILI LINASIKITISHA SANA NA KUFURAHISHA PIA.

By Lackson Tungaraza

FB_IMG_1698050141329.jpg
♦️Pichani ni mchezaji wa mpira wa miguu katika kilabu ya Manchester United iliyopo Uingereza.

Jina lake ni HARRY MAGUIRE na anacheza katika nafasi ya beki wa kati.

Harry Maguire alisajiliwa kwa pesa nyingi sana katika kilabu ya Machester United, na kwa wakati huo yeye ndiye aliyekuwa beki mwenye thamani kubwa zaidi.

.
♦️Lakini baada ya kufika Manchester United, kila kitu kilibadilika...

Zile sifa nyingi alizokuwa akizipata kutoka kwa mashabiki na wachambuzi wa soka juu ya uwezo wake mkubwa katika kuwazuia mashambuliaji kufikia lango Lao... ziliyeyuka.

Badala yake akaanza kupokea matusi na vitisho vya kila namna kutoka kwa watu wale wale waliokuwa wanamsifia alipokuwa anafanya vizuri.

♦️Kwanini walikuwa wanamzomea na kumtishia maisha?

Kwa sababu uwezo wake wa kuzuia mpira kama beki wa kisasa ulipungua sana. Akaanza kusababisha timu yake ifungwe kirahisi na wapinzani.

Na kibaya zaidi, na yeye alianza kujifunga (alianza kuwasaidia wapinzani kuifunga timu yake).

AKAWA ANACHUKIWA NA KILA SHABIKI WA TIMU YAKE.

Hata uwanjani walikuwa hawataki kumuona.
Wakimuona wanamzomea na kumtukana kwa bidii.

.
♦️LAKINI UNAJUA KILICHOTOKEA KWA HARRY MAGUIRE, nahonda wa Manchester United?

Harry Maguire hakukata tamaa.

Kila alipopewa nafasi ya kuingia uwanjani kucheza, alikuwa akifanya hivyo bila kuogopa matusi na kelele za mashabiki wa timu yao.

Ingawa alikuwa bado alikuwa anaendelea kufanya makosa yaleyale ya kukaba vibaya na kujifunga, bado aliendelea kuingia uwanjani kucheza.

Harry Maguire aliamua kwenda kinyume na Wahenga waliosema, ASIEKUBALI KUSHINDWA SIO MSHINDANI.

Hakukubali kushindwa, aliendelea kushindana.

♦️Na kwa vile MUNGU SIO ATHUMANI WALA TUNGARAZA... MAMBO YAKABADILIKA KWA HARRY MAGUIRE, Captain Fantastic!

Akaanza kucheza vizuri,
Kukaba vizuri,
Kuisaidia timu yake kupata ushindi (kwenye mashindano ya Ligi Kuu nchini Uingereza na UEFA CHAMPIONS LEAGUE)

Ubora Wake ukapelekea apate tuzo ya MCHEZAJI BORA WA MECHI (player of the match) katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliyoikutanisha timu yake dhidi ya timu ya SHEFFIELD UNITED F.C. Tarehe 21 Oktoba, 2023.

.
WALE WOTE WALIOKUWA WAKIMZOMEA NA KUMTUKANA, WAKAANZA KUMSHANGILIA TENA NA KUMUONGELEA VIZURI.

Na sasa captain fantastic, Harry Maguire, ameanza kuishi vizuri na kwa heshima katika mji wa Manchester.

♦️KUPITIA MAISHA YA HARRY MAGUIRE, UNAWEZA KUPATA MAFUNZO MATATU (3) YAFUATAYO;

👉1: Maisha yamefungwa katika majira tofauti tofauti. Kuna majira ya kulia na majira ya kucheka, kuna majira ya kushangiliwa na kuna majira ya kuzomewa, n.k. Hivyo, usitarajie kukutana na aina moja ya majira katika maisha yako yote. Kubali mabadiliko.

👉2: Watu wengi wanapenda vipawa, kipaji na huduma yako... sio wewe (hawakupendi wewe). Ndio maana wanapokosa kupata matunda ya vipawa, kipaji na huduma yako... wanaanza kujitenga mbali nawe.

Kwahiyo, kaa ukijua kwamba, zaidi ya 91% ya wanaokusangilia na kusema wanakupenda, HAWAKUPENDI wewe, ila wanapenda wanachopata kupitia vipawa, kipaji na huduma yako. Yawezakuwa ni vichekesho unavyowapatia, nyimbo nzuri unazoimba, mafundisho mazuri unayoposti, n.k.

Ukijidanganya kuwa ni wewe ndiye unaependwa, utakuja kufa kwa presha na msongo wa mawazo siku utakapokuja kukugundua hakuna aliyekuwa anakupenda.

👉3: Katika Changamoto zote unazokutana nazo katika kazi yako, biashara au utumishi... kamwe usikubali kukata tamaa.

Washindi huwa hawakati tamaa,
Na wanaokata tamaa huwa hawashindi.

Kama Harry Maguire alivyokataa kukata tamaa mpaka kiwango chake kilivyorudi na kuanza kupendwa tena... nawe uwe vivyo hivyo; usikate tamaa.

Endelea kupambana mpaka ufanikiwe (mpaka ufanikishe mipango yako).

.
Ni hayo tu kwa leo,
I hope umejifunza jambo fulani.
Tukutane wakati mwingine

#ShareThisPost

.
♦️Naitwa LACKSON TUNGARAZA

Nitafute ikiwa unataka...

👉1. Kujifunza Uandishi wa vitabu au Uuzaji wa vitabu

👉2. Unataka kupata huduma za Uchapishaji wa vitabu (book cover design, kupangiwa kitabu chako, n.k.)

👉3. Unataka kujifunza jinsi ya kuikuza biashara yako na kupata wateja kwenye mitandao Ya kijamii (digital marketing), pamoja na kupata account ya Stripe inayokusaidia kupokea pesa mtandaoni kutoka kwa mteja yeyote yule, duniani kote. Hivyo utakuwa na uhuru wa kufanya biashara na wateja waliopo Afrika nzima, Ulaya, America, Asia, n.k. bila wasiwasi.

👉4: Unataka kujifunza jinsi ya kufanya matangazo ya kulipia mtandaoni kwa usahihi (yaani, kuBoost post au kufanya Sponsored ads; Facebook Ads na Instagram Ads).

👉5: Unataka kupata vitabu vya bure (PDF za bure zinazofundisha uandishi wa vitabu, uuzaji wa vitabu, biashara, imani, n.k.)

👉6: Unataka nije nifundishe kwenye group lenu la WhatsApp au popote pale.

👉7: Unataka kupata vitabu vyangu vya kulipia. (Kitabu chochote kati ya vitabu zaidi ya 15 vilivyopo sokoni katika mifumo ya Softcopy na Hardcopy).

MAWASILIANO: 0764 793 105 (WhatsApp only)

ALL THE BEST!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom