Makinika na mijusi wa ndani ya nyumba!

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,125
22,616
Salaam, Shalom!!

UTANGULIZI.

Ndani ya nyumba zetu, Pana mijusi yenye RANGI nyeupe tofauti na mijusi wa nje. Na KAZI ya mijusi KIMWILI Huwa ni kutafuta na kula WADUDU watambaao na warukao nk nk.

MADA: MAKINIKA NA MIJUSI/ UPANDE WA PILI WA MIJUSI YA NDANI YA NYUMBA.

Kuna mjusi alikuwa akiishi ndani ya nyumba yetu, na tulimchukulia kawaida tu kama mijusi wengine. Tukiwa sebuleni utamuona juu katulia tulii anatuangalia,

Tukiingia chumbani, yupo, Kuna time tulitilia mashaka ,lakini sababu hatukuwa na HAKIKA kuwa Si mjusi wa kawaida, tulipuuza.

Siku moja tumelala, usiku, nikajikuta kwenye vita kubwa sana katika Roho, nilikuwa napambana na mijusi wakubwa sana, mijusi giant ambao nilikuwa napambana nao Hadi JASHO linanitoka.

Nilikuwa nakemea, Kwa Jina la YESU, Damu ya Yesu, vita ilikuwa Kali sana, nilijiuliza kwanini Leo vita imekuwa Kali sana tofauti na vita za siku zingine, niliemdelea kukemea.

Nikiwa katika vita nikashtuka na kuamka, kumbe, mke wangu pia alikuwa akipambana vita kama yangu nae aliposhtuka tukaanza kuulizana nini kilikuwa kinatokea.

Tulijiuliza labda ni wachawi walikuwa wametuvamia, tulipowasha taa, tulishangaa sana kumkuta mjusi ambaye alikuwa akikaa juu ya dari, ameingia ndani ya neti yetu ametulia pembeni mwa Kuta ya Net. Baada ya kumvizia tumuue, alituponyoka na kukimbia.

Tangu siku hiyo, Niko makini sana na mijusi wa aina hiyo ndani ya nyumba na WADUDU wenye kutilia mashaka sababu mijusi wanaweza kutumiwa kama Antenna za kichawi. Yaani unarushiwa makombora Toka kuzimu kupitia mjusi au paka au mbwa au mdoli uliyenunua au kumfuga mwenyewe.

Pia mijusi ndani ya nyumba wanaweza kukaribisha mapepo ambayo yanaweza kushambulia kupitia mwili wa mjusi.

Pepo halina mwili, hivyo likipata mdoli au kinyago ndani ya nyumba Yako, hupata Mahali pa kukaa na kukushambulia Kwa karibu na nguvu zaidi. Vita ya Wana wa Mungu ni katika Ulimwengu wa Roho, Vita zetu huanzia Rohoni kabla ya kuja mwilini.

SOLUTION.

1. Hakikisha huweki vinyago, midoli ndani ya nyumba. Mapepo yanaweza kuingia ndani ya vinyago na ukapata vita direct Kutokea vitu hivyo.

2. Acha mara Moja kufuga paka na kuishi naye ndani ya nyumba, paka au mbwa, Pepo anaweza kuwaingia na akawatumia kukuattack.

3. Puliza dawa ya kuua mijusi na WADUDU ndani ya nyumba, maana nyumba ya kuishi haipasi kuwa makazi ya chawa, mende, kunguni, viroboto, mijusi ,panya nk nk.

NB: Si mijusi wote ni kama niliyepambana nae Mimi, ni kukupa tu tahadhari kutokupuuzia mambo!!

ANGALIZO: Usilale bila kufanya maombi, funga milango Yako Kwa Damu ya Yesu, zungusha ulinzi katika anga lako na ardhi unayomiliki.

Ikiwa hujaokoka fuatisha Sala hii:

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA. NINAOMBA UWEZO WA KUSHINDA DHAMBI, NIWEZESHE NIISHI MAISHA MATAKATIFU. Amen

Mungu akubariki.

Amen
 
Huyo mjusi alikuwa special sana, kwa wenye machale kama mimi asingechukua round...

Ninapoishi kuna vile vimijusi vidogo, huwa vinakuwa ndani na nje, ila sijaona kama kuna "red ⏰" kwao.

Mfano saivi nimetoka kuchungulia nje, nimemuona mmoja anakomaa na kula wadudu, kama ujuavyo msimu wa mvua huu usiku kuna vi midudu virukavyo vingi....
 
Asingechukua round Kwa njia Gani, fafanua😀
Yani mjusi nikae sebuleni au niwe chumbani kisha awe ametulia kwenye dari ananiangalia?😂 Mjusi au mbwa au type ya vimnyama visivyoeleweka heshima namba 1 ni lazima wakimbie kila mkutanapo, kitendo cha kukuangalia ni dharau hizo, ni kosa la jinai..

Kwa haya haya maisha niliyoishi bush ama yapii, maana bush ukiona mjusi tu unatafuta jiwe lililo karibu ujifunze shabaha...

Hivi vya hapa vyenyewe kuna muda huwa navipa makonzi vikakaa vibaya😂😂😂
 
Ulokole ni ugojwa wa akili yaani mungu kamuumba paka na mbwa kwa ajili ya kuishi na binadamu alafu ww unasema watu wasifuge wanyama hao ww kama nani?

Suala la mchawi kutaka kukudhuru sidhani kama ana hitaji mzunguko mkubwa namna hiyo.
 
Urokole ni ugojwa wa akili yaani mungu kamuumba paka na mbwa kwa ajili ya kuishi na binadamu alafu ww unasema watu wasifuge wanyama hao ww kama nani?

Suala la mchawi kutaka kukudhuru sidhani kama ana hitaji mzunguko mkubwa namna hiyo.
Kufuga paka au mbwa ni tofauti na kuishi nao ndani ya nyumba.

Wengine wanalala na vijibwa vidogo chumbani.

Mbwa lake Banda nje Afanye KAZI ya ulinzi nje.

Afu wafuga paka wengi ni wachawi, fuga kuku utamla supu!!
 
Ndio maana nasema nyinyi warokole mna mambo ya ajabu na wengi hamna akili.

Mungu kaumba wanyama mbali mbali na kila mnyama ameubwa kwa kazi maalumu , mbwa wapo wa aina nyingi wapo mbwa kwa ajili ya ulinzi hao ndo wanao kaa bandani ,na tupo tumbwa tudogo twenye manyoya mengi ya kuvutia tunatakiwa kukaa ndani kama pambo la nyumba.

Paka kaubwa kwa ajili ya kukabiliana na wanyama wadogo waaribifu kama panya, nyoka na popo ambao wote wanapenda kukaa ndani sasa paka asipo kaa ndani hao wanyama waaribifu atawadhibitije?

Ulipo jionesha ya kuwa huna akili ni pale ulipo sema eti paka ni wachawi , paka sio wachawi bali wana weza kutumiwa na wachawi kutimiza matakwa yao kitu ambacho wanaweza kufanya hata kwa huyo kuku uliye sema nimfuge.

Mchawi kama amedhamilia kukudhuru ahitaji paka wala mbwa bali ana uwezo wa kumutumia hata huyo mkeo au watoto wako ulio wazaa mwenyewe kukudhuru sasa sijui hapo na penyewe uwashauri watu waache kuowa na kuzaa watoto maana wanaweza kutumiwa na mapepo kukudhuru.
 
Hv kwa kumuangalia ulikua unaona nini mpaka ukahis anapambana vita ya kiroho
Tangu nilipokuwa vitani katika Ulimwengu wa Roho nilipambana na mapepo katika mwonekano wa MIJUSI, na ndicho nilichokuja kukiona ndani ya net.

Mjusi yule alifanyika kitu Cha kuunganisha room na kule mashambulizi yalikotoka.

Najua nikisemacho.

Amen
 
Ndio maana nasema nyinyi warokole mna mambo ya ajabu na wengi hamna akili.

Mungu kaumba wanyama mbali mbali na kila mnyama ameubwa kwa kazi maalumu , mbwa wapo wa aina nyingi wapo mbwa kwa ajili ya ulinzi hao ndo wanao kaa bandani ,na tupo tumbwa tudogo twenye manyoya mengi ya kuvutia tunatakiwa kukaa ndani kama pambo la nyumba.

Paka kaubwa kwa ajili ya kukabiliana na wanyama wadogo waaribifu kama panya, nyoka na popo ambao wote wanapenda kukaa ndani sasa paka asipo kaa ndani hao wanyama waaribifu atawadhibitije?

Ulipo jionesha ya kuwa huna akili ni pale ulipo sema eti paka ni wachawi , paka sio wachawi bali wana weza kutumiwa na wachawi kutimiza matakwa yao kitu ambacho wanaweza kufanya hata kwa huyo kuku uliye sema nimfuge.

Mchawi kama amedhamilia kukudhuru ahitaji paka wala mbwa bali ana uwezo wa kumutumia hata huyo mkeo au watoto wako ulio wazaa mwenyewe kukudhuru sasa sijui hapo na penyewe uwashauri watu waache kuowa na kuzaa watoto maana wanaweza kutumiwa na mapepo kukudhuru.
Sasa kama unakiri paka anaweza kutumiwa na wachawi kukushambulia,

Kwann ukae na paka ndani ya nyumba?

Narudia kusema, wengi wafuga paka, hukosi mchawi katika familia hiyo.
 
Back
Top Bottom