Nilipanga mwaka huu nijiunge na siasa lakini Nimeghairisha mpango

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,893
Kwema Wakuu!

Mpango wangu tangu mwaka jana kama nilivyoandika kwenye uzi hapa Panapo majaliwa mwakani nitajiunga rasmi na siasa za nchi hii. Je, ungependa nifanye siasa na chama kipi?

Nilitaka nijiunge na Siasa za nchi hii lakini kwa sababu za kiufundi nimeamua kughairisha mpango huo.

Wapo walionipongeza kwa kutangaza nia hiyo.
Wapo walionibeza na kunitukana huku wakijaribu kueleza kuwa nataka kujiunga na jopo au tuite bench la ufundi kula Keki ya taifa.
Wapo waliopuuza habari hizo iwe kwa kuwa haziwahusu au Kwa kunipuuza kama mtafuta Kiki.
Wapo waliofikiri kuwa huenda sasa nataka kuwa Chawa na kusema nimeishiwa maarifa na kichwani kumebaki makapu.

Nimeghairisha mpango kwa sababu bado sijamaliza kusoma vile vitabu nilivyoambiwa nisome.
Niliambiwa nisome vitabu vitatu ili niwe Mwanasiasa mahiri na mwenye mafanikio makubwa sana.
Vitabu hivyo ni kama ifuatavyo;

1. Bendera Yapepea
2. Dhahabu Kilimani
3. Peremende ya Mwanasesere

Hivi vitabu bhana mwanzoni wakati naenda kuvinunua, niliviona ni vitabu vidogo sana. Havina kurasa nyingi. Chenye kurasa nyingi kuliko vingine ni Peremende ya Mwanasesere ambacho kinakurasa 93, chenye kurasa ndogo kabisa ni Dhahabu Kilimani ambacho kinakurasa 57.

Muuzaji wa vitabu nilipomtajia majina ya vitabu hivyo alionyesha sura ya kunishuku kama sio kushtuka. Vipi kwani? Maelezo aliyonipa ni kuwa vitabu hivyo vipo kwenye maktaba moja tuu nchi nzima ambayo ndio hiyo(kwani nilishaelekezwa), pili, vitabu hivyo wanaojua vipo ni wachache mno. Sasa anashangaa mimi nimepatia wapi hiyo taarifa.

Tatu, vitabu hivyo ukinunua haupaswi kuvisoma mbele za watu. Unatakiwa kuvisoma kwa kificho.
Mmmh! Vitabu gani hivyo? Hiyo ikaongeza shauku ya kutaka kuvipata. Masharti ya vitabu ni kama masharti ya mganga wa Jadi anayetoa utajiri wa Majini. Vitabu unasoma kwa siri kama unaangalia video za ngono. Kutakuwa na nini humo?

Nne, vitabu hivyo nikimaliza kuvisoma nitatakiwa nivirudishe. Na havipaswi kuharibiwa wala kuandikwa ndani yake kwa namna yoyote.

Lakini Mkutubi si nimevinunua kwa pesa yangu? Iweje nivirudishe?
Ikabidi niulize. Akaniambia ni sehemu ya masharti ya hivyo vitabu.
Je nikirudisha vitabu narudishiwa pesa yangu? Akacheka alafu akajibu, utatakiwa utoe pesa nyingine ambayo ni mara mbili ya uliyonunulia kisha unaviacha.

Kwa nini?
Ndio masharti ya hivi vitabu.

Vikowapi?
Hapo akatoka akaenda kuvileta akiwa anapita katikati ya mashelfu ya makabati yaliyojaa vitabu vya kila namna. Macho yangu yakawa yanaikagua ile maktaba nikiwa nimepatwa na shambulio la kifikra. Nilikuwa ninahamukubwa ya kuviona hivyo vitabu vikoje.
Hamu ya kuviona vitabu hivyo iliipiku hamu ya kujiunga na siasa.

Punde lakini sio kwa sekunde zikiwa zimepita dakika kama tano bila mapatano Mkutubi alirejea akiwa amebeba bahasha ya kaki iliyofungwa vyema. Nikiwa namtazama mkononi kwenye mkono aliobeba ile bahasha akafika na kuibwaga ile bahasha mezani. Jambo ambalo liliifanya ile bahasha itoe kavumbi kepesi. Na kabla dakika haijaisha nikapiga chafya. Pyaa! Fyaaa! Chyaaa! Nafikiri ni kale kavumbi kaliichokoza pua yangu.

Akaniambia, sipaswi kufungua ile bahasha mpaka nifike nyumbani. Lakini pia alinitahadharisha kuwa nihakikishe vitabu hiyo vinakuwa salama. Hawatahitaji kisingizio chochote endapo nitaenda kinyume na maelezo niliyopewa.

Nikauliza, nani hao? Akanijibu nenda kavisome hivyo vitabu utajua ni kina nani hao?
"Na vipi nikiibiwa njiani kabla sijafika nyumbani?" Nikawaza kimoyomoyo.

Basi ilimradi nimeshavikamata vitabu nikaona sina haja ya kuuliza maswali mengine isijeikatokea dharura akaahirisha kuniuzia. Nikalipia kisha nikasema.

Kudadadeki! Yaani nilikuwa ninahofu njiani kama nimebeba Pembe za ndovu. Hakuna niliyemuamini. Kila niliyepishana naye njiani nilihisi angeweza kuniibia. Licha ya kujua kuwa Watanzania wengi hawapendi kusoma lakini kwa maelezo ya yule mkutubi kuhusu vitabu vile niliamini kuna kuna utajiri mkubwa umo ndani yake. Hapo utabaki na jibu mwenyewe kama kuna mtanzania asiyependa utajiri?

Nichukue Bolt,Uber au nipande zangu Daladala kama nilivyokuja? Nisije nikatumia pesa bure alafu nikakuta vitabu vyenyewe havina la maana. Lakini lazima viwe na la maana. Aliyeniambia nivitafute vitabu hivyo sio mtu Mdogo. Na maelezo ya Mkutubi kwa umri na wajihi wake haonyeshi kama ananidanganya.

Nikaamua nichukue Bolt. Sasa nielekee Mbezi Beach au Kimara. Wapi ni salama. Aaa! aam! Mbezi. Huyo ndani ya Gari.

Baada ya nusu saa hivi nilifika nyumbani. Kisha moja kwa moja sikutaka kupoteza muda nikaingia chumbani kwangu na kujifungia mlango kama mtu anayefanya sala za utakaso.

Kumbe juu ya bahasha kulikuwa na herufi na namba ambayo sikuyaona. Yakisomeka " TS108" alafu pembeni juu ya bahasha kulikuwa na Stampu yenye nembo na jina la ile Maktaba.

Nikaifungua mikono ikiwa inatetemeka sijui ni hofu au ilikuwa shauku. Sikujua Mimi! Nikatoa kitabu cha kwanza,
Juu ya jalada yalisomeka maandishi " PEREMENDE YA MWANASESERE" Kilikuwa kitabu kikuukuu alafu chini yake ulisomeka Mwaka 1711.
Picha ya kwenye jalada ambayo ilikuwa haionekani vizuri na imefutikafutika ilikuwa inaonyesha mchoro wa Mwanasesere, ambapo ukiitazama vizuri ndipo utagundua kuwa kumbe mkononi mwake amebeba peremende ambayo sijui ni pipi kijiti au niiteje lakini sina uhakika miaka ya 1711 kulikuwa na hiyo pipi kijiti.
Ilinichukua dakika tano kugundua kuwa kumbe meno ya Mwanasesere yanarangi ya kahawia labda tuseme yameoza.
Moja kwa moja nikajua ile ilikuwa ni athari mbaya ya kula peremende kupitiliza.

Upande wa nyuma ya kitabu kwenye jalada. Huku palizidi kwa kuharibika. Hapakuwa panaonekana vizuri. Sehemu kubwa ilikuwa imeharibiwa vibaya. Lakini macho yangu yalijitahidi kupata taswira ya kustaajabisha, ulikuwa mchoro wa Mwanasesere akiwa nje ya Uzio wa shamba la peremende akiwa analia..
Ilikuwa lazima nikaze macho na kutulia ili nitambue picha hiyo.

Sikutaka kukifungua kwanza. Nikatoa kitabu kingine. Hiki kilikuwa kimeandikwa DHAHABU KILIMANI. Hiki hakikuwa na jalada. Nafikiri jalada lake lilikuwa limefika. Hiki nacho kilikuwa kikuukuu, kulikuwa na maandishi ya wino yenye hati ya mkono wa mtu ambapo kuliandikwa " GoldRich Family" alafu chini yake ukaandikwa mwaka "1931" kisha chini ya huo mwaka ikawekwa sahihi.
Nyuma ya kitabu ambapo nilisema hakina jalada kulikuwa na maandishi ya wino ambayo yaliandika kwa lugha ya kingereza maneno ambayo muandishi wake aliyecharaza kikamilifu.

Kisha nikatoa kitabu cha mwisho ambacho hiki kilikuwa kipyakipya ingawaje kilikuwa cha mwaka 1965. Kiliandikwa BENDERA YAPEPEA"
Alafu jalada lilikuwa na picha yenye Mlingoti wa chuma ambao juu yake umeshikiliza bendera iliyokuwa inapepea. Kwenye ile benderakuliluwa na rangi tatu. Nyeusi, kijani na Nyeupe(kama sio maziwa). Katika hizo rangi za hiyo bendera kulikuwa na maandishi madogo mno ambayo kama isingekuwa taa ya kujiunga yangu kumwekuamwekua nisingeweza kuyaona. Maandishi yale yalikuwa kama yale yanayopatikana kwenye Noti ambayo ukibinua kitabu hivi huyaoni, ukibinua hivi unaona, ukibinua vile unaona yanaalama nyingine.

Vitabu vyote vinamaandishi lakini mtunzi na mwandishi wa vitabu hivyo hajatajwa mahali popote pale. Hii ilinishangaza mno.

Kwa uchu wa kujiunga na siasa, nikaanza kuvisoma. Siku moja nilimaliza vitabu viwili. Havikuwa na kurasa nyingi na mimi ni mzoefu wa kusoma vitu virefu.
Kesho yake nikamaliza.

Vile vitabu raha yake ni kuwa kila ukimaliza Sura mwisho wa sura Kun karatasi yenye maswali ambayo chini ya ile karatasi yenye maswali inaamrisha kuwa ninatakiwa kuchukua karatasi yangu ya majibu kisha nijibu yale maswali.

Maswali yale yanatokana na kile ulichosoma kwenye Sura husika. Hapo ndipo kizaazaa kilipoanza.
Nilisoma vile vitabu kwa siku mbili lakini kwenye upande wa kujibu zile karatasi za maswali kazi ilikuwa kazi. Mwaka sasa unaisha mpaka sasa nimejibu maswali ya kitabu kimoja ambacho namalizia mwezi huu kama sio mwezi wa kwanza.

Kuna mtu atataka mfano wa Maswali. Isijeonekana ni porojo.
Taikon sinaga hiyana. Ngoja nitoe mfano wa swali lililoko kwenye hicho kitabu ingawaje inaweza kuwa ni kinyume na taratibu za vitabu hivi.

1. Bendera Yapepea inarangi ngapi?
Kwenye jalada nilisema inarangi tatu. Lakini katika kujibu wakati najibu swali hilo nilirudi kwenye jalada kuthibitisha jibu kabla sijajaza. Kuziangalia zile rangi zipo tatu vilevile lakini kilichonishangaza sio tena Nyeusi, kijani, na Nyeupe(kama maziwa) ambazo zimelaliana. Nyeusi ikiwa chini, kijani ikiwa katikati na nyeupe(kama maziwa) ikiwa juu. Hazikuwa hivyo. Zimebadilika ya juu imeenda chini na ya chini imeenda juu. Lakini kijani ipo palepale.
Hapo nikapata wazo la kukipindua pindua n kukigeuzageuza kile kitabu. Hapo ndipo nilipo vurugwa. Rangi zilikuwa zinabadilika kulingana na ulivyokiweka kile kitabu. Haikuwa tena bendera inarangi tatu bali inarangi zaidi ya tisa kulingana na utakavyokipindua kitabu chenyewe.

Swali la pili lilikuwa linanitaka nieleze rangi hizo, sababu ya kutokea rangi hizo, kulingana na nilivyosoma kwenye sura?
Hapo ikanibidi nirudie tena kusoma ile sura huku ndani ya maelezo ya kitabu kile kukiwa na mafumbo mengi yaliyofichika na kila fumbo ukiweza kulifumbua unapata jibu la swali husika.

Maelezo ya kitabu yanaeleza kuwa siasa inategemea bendera na rangi yake na jinsi inavyopepea. Kitabu kinaeleza zaidi kuwa bendera yaweza kuwa na rangi fulani kwa sababu imegeukia upande fulani au inaweza kuwa ya rangi fulani kwa sababu inapigwa na upepo wa kiwango fulani. Bendera inayopepea ni tofauti na ile isiyopepea.

Taikon unaandika manini?
Mimi nipo kwenye kujibu haya maswali ya hivi vitabu ambavyo nimeambiwa nivisome. Na nikiweza kuvimaliza kuvisoma na kuvijibu angalau nikipata maksi 71% ninaweza kujiunga na siasa kubwa.

Taikon amechoka kuandika, nikirudi kama nitakuwa na hamu ya kuandika nitaendelea kueleza sababu za kuahirisha kujiunga na siasa.

Acha nipumzike sasa.
Nawatakia sikukuu njema na Kheri ya Mwaka Mpya.

Robert Heriel
Taikon WA Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Unafaa kuwa mwanasiasa, kama kuandika tu uko na maandishi mengi hivi, naamini ukipewa mic uhutubie ndio itakuwa mara tatu au nne ya hiki ulichoelezea hapa kuhusu hivyo vitabu vyako.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu yàani linapokuja suala la kuongea ninaweza kukuangusha.

Sema kwa mara ya kwanza nilianza kujifunza kuzungumza hasa mbele za Watu nilipokuwa Advance. Nikaamua kujiingiza kwenye uongozi kwa lengo la kuji-shape.
Nilikuwa na kasoro hizi;
1. Kigugumizi
2. Kuongea haraka haraka.
3. Kuachia sentensi hewani na kurukia nyingine.
4. Kuongea kwa kuuliza maswali na kujijibu papo kwa papo.
Mfano, unajua nini? Tunatakiwa tufanye nini?

Kasoro hizi baada ya miaka miwili ya uongozi ziliyeyuka.
 
Huwezi kuwa na kigugumizi na ukaongea haraka haraka lakini ndiyo hivyo tena paka mwenye malengo hamli panya mwenye mimba.Endelea kujipanga.
 
Moja ya sababu ya kigugumizi ni kuongea haraka. Acha ubishi.

Kuna kilichokolea(kikali)
Alafu kuna kigugumizi cha kawaida.
 
Mkuu yàani linapokuja suala la kuongea ninaweza kukuangusha.

Sema kwa mara ya kwanza nilianza kujifunza kuzungumza hasa mbele za Watu nilipokuwa Advance. Nikaamua kujiingiza kwenye uongozi kwa lengo la kuji-shape.
Nilikuwa na kasoro hizi;
1. Kigugumizi
2. Kuongea haraka haraka.
3. Kuachia sentensi hewani na kurukia nyingine.
4. Kuongea kwa kuuliza maswali na kujijibu papo kwa papo.
Mfano, unajua nini? Tunatakiwa tufanye nini?

Kasoro hizi baada ya miaka miwili ya uongozi ziliyeyuka.
Ok, nimesoma bandiko lako la kwanza kutaka kujiunga chama cha siasa kusudi lako likiwa ni ili uwepo kwenye mgao wa kula keki ya taifa, wala sio kuhangaika na wananchi, basi usijali, hata ukiwa bubu kule ukienda utagombea na kushinda.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hujui hata kigugumuzi ni nini?Yaani stuttering inasababishwa na kuongea haraka!!!

Kigugumizi kina sababu nyingi mojawapo ni pamoja na hiyo kuongea haraka kunaweza kupelekea kigugumizi.
Mtu anayehusika(kisicho kikali) mwambie aongee polepole uone kama hataongea taratibu.

Kigugumizi pia inatokana wakati mwingine na hofu, hasira kali, presha, kuchangañyikiwa, stress

Alafu kuna kigugumizi cha kurithi. Nje ya athari ya mifumo ya ubongo

Sasa wewe na mimi itaonekana hajui maana ya kigugumizi.
 
Rudi kasome hujajua bado kigugumizi ni nini.Na kinasababishwa na nini.Hizo ni sweeping statements tu lakini sio majibu ya kitaalamu ya kuelezea kigugumuzi (stuttering) ni nini.
 
Ndio shida ya elimu ya kukariri.

Wewe ndio ukawaulize hao watalaamu waliokufundisha kuwa Hasira au hofu haiwezi kusababisha kigugumizi. Au kuongea haraka hakuwezi kusababisha kigugumizi.

Tatizo la Watu ambao elimu ipo limited ndio hii kwa watanzania wengi.
 
Tatizo lako ni kuelewa.Baada ya hasira au hofu kwisha unaporudi kwenye hali ya kawaida kigugumizi kinakuwa kimekwisha?Kigugumizi ni speech disoder.Hata kuna watu wasiokuwa na kigugumizi wanakuwa na matatizo ya kuongea wanapokuwa na hasira au hofu.Je wanakuwa wamepata speech disorder ya muda mrefu ambayo inahitaji theraphy??Yaani kwa ufahamu wako ukiongea haraka haraka unapata kigugumizi!!!!
 
Back
Top Bottom