Ni mtu gani maarufu ulitamani ukutanae lakini kabla hujakutana nae alikufa. Je, unge mwambia nini...?

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,679
12,248
kipindi naifahamu Facebook, rafiki yangu mkubwa alikuwa Marehemu Steve Kanumba....na nina uhakika alikuwa ni yeye haswa maana kuna matukio ambayo alikuwa anaya post yalikua real kabisa ya muda huo huo.

Nilikuwa nikichat sana na Kanumba na kiujumla alikuwa social sana kwa hilo namsifu sana.
images (22).jpeg
hili hakuna ambae ange amini ila simu niliyo kuwa natumia enzi hizo ilikuwa ya button na haikuwa na uwezo wa ku screenshot kama ilivyo leo.

masaa machache kabla Kanumba hajafa tulichat nikawa nampa hongera ya ubunifu wake kwenye kazi yake ya Anko J.J ambayo ilikuwa hot sana enzi zile.

Muda kama wa saa 6 hivi kuelekea saa 7 usiku nikaona walaka mrefu ulio andikwa na Thesi {mdogo wake Kanumba ambae pia ni Marehemu R.I.P} andiko hilo la Thesi lilielezea tukio zima Lili lotokea hadi Kanumba akafikwa na Umauti.

lakini ni kama Thesi aliandika haraka haraka kisha akaifuta ile post kule Facebook. kwani baada tu ya kulisoma lile bandiko lilifutika siku liona tena hadi leo😭

kutokana na harakati zangu. nilikuwa mfuasi mkubwa sana wa Marehemu mzee Mtikila R.I.P kwa kweli mzee Mtikila alinijenga sana kiitikadi nikawa nina tamani sana kukutana nae. kwa bahati mbaya nikapata taarifa za ajali iliyo sababisha kifo chake...nilihudhunika sana.
images (21).jpeg
kwenye taaluma yangu uandishi kuna waandishi ambao walichangia kwa namna moja ama nyingine mimi kuipenda fani ya uandishi. muandishi Ben Mtobwa ni miongoni mwa waandishi ambao kwa kiasi fulani walichangia mimi kuipenda fani ya uandishi haswa ukizingatia jinsi walivyo kuwa na uandishi ambao hauchoshi kusomwa.

kipindi namfatilia muandishi huyu sikuwa najua kuwa amefariki mpaka siku nilipo nunua kitabu chake ambacho kwenye wasifu wa muandishi nilikuta wameandika Tanzia yake. nili hidhunika sana kwakweli. nilitamani sana nimuone.

je ni mtu gani maarufu ulitamani kumuona lakini hukuwahi kupata bahati ya kumuona kutokana na yeye kutangulia mbele ya Haki...!

ungebahatika kukutana nae je unge mwambia nini?​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom