Wana JF
Ninavyoona mimi Hoja za mwakyembe hazina mashiko hata kidogo, kama sikumnukuu vibaya amesema kuwa ilikuwa shamhuna afikirie dhana ya collective responsibility na asipinge kauli ya PM Mizengo Pinda ,OKAY. Sasa hapa ninapata kigugumizi..... collective responsibility ipi aliyoikusudia Harison Mwakyembe kwa sababu kama ni utendaji wa Baraza la Mawaziri Shamhuna hahusiki na baraza la mawaziri la T/bara au pengine kuna mantiki mengine yaliyiojificha. ......... Sijui, lakini nafikiri kama Mwakyembe hataki kuelewa mipaka ya kiutendaji kati ya SMZ/ SMT/bunge/ baraza la wawakilishi hio ni kasoro kubwa akiwa yeye ni mwanasherisa wa kuheshimika.
La pili, Kwa mtazamo wa haraka hoja hii ya znz ninchi, wilaya au handeni, biharamulo, haipewi nguvu si tu ndani ya bunge au kwenye vyombo vya habari. Inaonekena wazi wazi kuwa Spika anamlinda PM pinda asijibu hoja yoyote ile inayohusiana na sakata hii. Kwa nini? Hapana jawabu ya mkato lakini ni mkakati tu wa SMT(Serikali ya Muungano) kukandamiza uhuru wa mawazo kwa wabunge wetu kule bungeni. Je hili Mwanasheria Mwakiyembe ameliona na kulikemea ?????
Ukifuatilia ktk media za bara, utaona kuwa vyombo vyote vya habari haviko objective and neutral katika kuielezea sakata hii ya znz ikielekea kuwa ni wilaya ya handeni / babati. Wahariri wanaendeleza ajenda ya kutulaumu sisi wazanzibari eti hatutaki muungano na hawataki kuandika makala za kiuchambuzi ambazo zingeeleza mambo mengine ambayo yako nje ya boksi na hayapewi nafasi.
Lililobaki, ni sisi wananchi kuja na activism ya hali ya juu na tuoneshe wazi kuwa hatutaki muungano kabisa na sio tu ufanyiwe marekebishao. Wanasiasa wamejitahidi na wanaendelea kujitahidi kuunda jukwaa la kueleza maoni yao na inapasa tuwaunge mkono kwa juhudi zao.
Unatakiwa ujibu hoja Ila fahamu katika hili Mwakiembe na Shamhuna ndio wahusika wakuu ,otherwise u may skip.Wewe kila kitu "Shamhuna hiki" "Shamhuna hivi" "Shamhuna vile". Au wewe ndiyo Shamhuna mwenyewe?? Unaboa sana aisee!
Wewe unaonekana umefukuka maana unaposema Zanzibar wakipata maji bure na umeme bure ,hayo hayakutoka Tanganyika ,tokea zama Zanzibar maji ni bure ,umeme ukilipwa ,mashule bure madaftari kabakaba,balaa la kulipia mashule na kuadimika vifaa anavyohitaji mwanafunzi limezuka kwa utawala wa Tanganyika kujivalisha ndani ya Tanzania na kuikaba koo Zanzibar kupitia udhibiti wa njia za uchumi na serikali ya Zanzibar kushindwa kutimiza malengo yake nakuhakikishia hata umeme ungelifikia kuwa bure ,lakini leo maji yanaanza kulipiwa ,mashule ndio hivyo usiseme umeme bwanamkubwa mara kazima switch,Zanzibar imegandamizwa na haiwezi hata kufurukuta kwa jamaa waTanganyika roho zilivyowabadilika ,kuna jamaa huko bara wanafikiri Zanzibar ni sawa na Ulaya, this is too macha.
Fedha ikiletwa Tanzania inabidi igawiwe 50 / 50 ,,zimeungana nchi mbili na hapo pia napo pana kero ,vipi utaipa Zanzibar fedha kama unaigawia Wilaya ,hapo ndipo Mawaziri wa Tanzania wanaposhindwa kuwajibika ndani ya Serikali ya Muungano uzalendo unawajaa na kumega sehemu kubwa ya msaada kwa ajili ya kwa Tanganyika ,hivyo sivyo kabisa angalau msaada ungewekwa 2/3 tukafahamiana ,na ndio Muungano lakini mnabinya na mwisho au misaada mingine hata Zanzibar haioni ndani inagawiwa juu kwa juu.
Naona busara inakushinda,na ukienda huko tutapoteza muelekeo ,kusema wanategemea ankal kuwaletea mitumba kutoka maskati,sio baya ila sasa naamini kuna watu huko Tanganyika wanaona Zanzibar kuna waarabu watupu, watu wa dizaini zenu inaonyesha hata wabunge wanaowakilisha Zanzibar hamuwajui, nilikwisha sema hapa kuwa Tanganyika kuna waarabu wengi kuliko Zanzibar ya leo. Weka kando hilo inaonyesha ni mfinyu wa historia. Itafute Zanzibar Empire katika vitabu vya tarehe za zamani.Zao la karafuu wameliua watanganyika? Utalii wameua watanganyika? Yaani mlitegemea biashara ya kuingiza chupi bure na kuzipeleka Tanganyika ndiyo kungewanasua katika dhiki!
Kama alivyouliza mwenye busara kuliko mimi, tugawane fedha 50/50 na tugharamie matumizi 50/50! Mbona mnaangalia mapato tu? Tena misaada! Mawazo tegemezi kama hayo ndiyo yatakayowabakiza hapo mlipo. kila wakati mnasubiri ankal wa Muscat awatumie makombo.Jiangalieni kwanza kabla ya kukimbilia kumlaumu jirani.
Unapozungumza kuwa mkweli mwanzo mpaka mwisho. Ivo umesahau yule Mnyamwezi wa Tabora ndie alikuwa Deputy Chief Minister wa mwanzo?
)Yaani mkuki kwa nguluwe au sio ,pale Shamhuna alisema hakuna selikali ya Mseto wala choloko ,akina Mwakiyembe walipiga makofi,sasa inakuwaje leo aombe lazi.tamko rasmi kutoka serikalini SMZ mmelisikia ni majibu kutoka CCM kisiwa ndui Zanzibar(Wahafidhina wakiitaka timu ya Butiama iombe razi
UDINI NA UELEWA MDOGO UNAWASUMBUA MWIBA, NGEKEWA NA MIZIZI
Ukifuatilia kwa karibu hoja za akina Mwiba, Ngekewa na Mizizi unagundua bangi inayowasumbua - UDINI na uelewa mdogo. Mizizi ndo kashindwa kabisa kuficha kiini cha hasira zake dhidi ya Dk. Mwakyembe-UDINI! Kakasirika kwa nini Dk. Mwakyembe alilimwagia maji Bungeni suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ambayo itaendeshwa kwa kodi yetu wote, Waislamu na wasio Waislamu. Wote watatu wanafanana kwa uelewa usioridhisha wa hoja yenyewe; wametoka nje ya mjadala!
Hivyo nawaomba wasome hansard ya Bunge katika mtandao, wajue alisema nini Dk. Mwakyembe!
Sisi wengine tumemwelewa! Dk. Mwakyembe anasema hakuna mgogoro wa kikatiba ila utovu wa nidhamu wa Mawaziri wa Zanzibar, kitu ambacho ni kweli. Toka lini Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar akawa level moja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Kiprotokali ni mtu wa sita katika mlolongo wa itifaki: Rais wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar, Waziri Kiongozi, halafu ndo unamkuta Shamhuna na U-naibu Waziri Kiongozi! Hata kama tuna Serikali mbili, haziko ngazi moja, ndo sababu ya hiyo itifaki! Ki-CCM, Shamhuna hayuko hata kwenye orodha! Pinda ni mjumbe wa NEC na Kamati Kuu ya CCM! Waziri Mkuu anasema jambo, halafu Shamhuna anamjibu, tena kwa fujo na kusema "enzi za kutishana zimepita!" Halafu Mwiba, Ngekewa na bwana udini Mizizi, mnashindwa kuona hoja ya msomi Mwakyembe! Hana adabu huyu ati!
Jana nilimsikia msomi mwingine Dk. Mvungi akisema Mwakyembe ana hoja ya msingi. Vipo vyombo chungu nzima vya kushughulikia mambo ya Muungano k.m. ofisi ya Makamu wa Rais, hivi Shamhuna hakuviona mpaka aropoke kumshambulia kiongozi wake wa CCM na wa Serikali? Ipo hoja aliyoiongelea Dk. Mwakyembe ya kuwa mawaziri wanafungwa na kanuni ya katiba ya kuwajibika kwa pamoja kama serikali. Hili ni suala la kitaalamu ambalo sisi wengine akina Mwiba, Ngekewa na bwana udini Mizizi, tunyamaze tu!
Bora umewatolea uvivu mjomba. Hawa Waislamu wa Visiwani bwana vichwa ngumu kweli. Haya ndiyo matatizo ya elimu za madrasah na jadi ya kuhusudu Wamanga.
Naona busara inakushinda,na ukienda huko tutapoteza muelekeo ,kusema wanategemea ankal kuwaletea mitumba kutoka maskati,sio baya ila sasa naamini kuna watu huko Tanganyika wanaona Zanzibar kuna waarabu watupu, watu wa dizaini zenu inaonyesha hata wabunge wanaowakilisha Zanzibar hamuwajui, nilikwisha sema hapa kuwa Tanganyika kuna waarabu wengi kuliko Zanzibar ya leo. Weka kando hilo inaonyesha ni mfinyu wa historia. Itafute Zanzibar Empire katika vitabu vya tarehe za zamani.
UDINI NA UELEWA MDOGO UNAWASUMBUA MWIBA, NGEKEWA NA MIZIZI
Ukifuatilia kwa karibu hoja za akina Mwiba, Ngekewa na Mizizi unagundua bangi inayowasumbua - UDINI na uelewa mdogo. Mizizi ndo kashindwa kabisa kuficha kiini cha hasira zake dhidi ya Dk. Mwakyembe-UDINI! Kakasirika kwa nini Dk. Mwakyembe alilimwagia maji Bungeni suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ambayo itaendeshwa kwa kodi yetu wote, Waislamu na wasio Waislamu. Wote watatu wanafanana kwa uelewa usioridhisha wa hoja yenyewe; wametoka nje ya mjadala!
Hivyo nawaomba wasome hansard ya Bunge katika mtandao, wajue alisema nini Dk. Mwakyembe!
Sisi wengine tumemwelewa! Dk. Mwakyembe anasema hakuna mgogoro wa kikatiba ila utovu wa nidhamu wa Mawaziri wa Zanzibar, kitu ambacho ni kweli. Toka lini Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar akawa level moja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Kiprotokali ni mtu wa sita katika mlolongo wa itifaki: Rais wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar, Waziri Kiongozi, halafu ndo unamkuta Shamhuna na U-naibu Waziri Kiongozi! Hata kama tuna Serikali mbili, haziko ngazi moja, ndo sababu ya hiyo itifaki! Ki-CCM, Shamhuna hayuko hata kwenye orodha! Pinda ni mjumbe wa NEC na Kamati Kuu ya CCM! Waziri Mkuu anasema jambo, halafu Shamhuna anamjibu, tena kwa fujo na kusema "enzi za kutishana zimepita!" Halafu Mwiba, Ngekewa na bwana udini Mizizi, mnashindwa kuona hoja ya msomi Mwakyembe! Hana adabu huyu ati!
Jana nilimsikia msomi mwingine Dk. Mvungi akisema Mwakyembe ana hoja ya msingi. Vipo vyombo chungu nzima vya kushughulikia mambo ya Muungano k.m. ofisi ya Makamu wa Rais, hivi Shamhuna hakuviona mpaka aropoke kumshambulia kiongozi wake wa CCM na wa Serikali? Ipo hoja aliyoiongelea Dk. Mwakyembe ya kuwa mawaziri wanafungwa na kanuni ya katiba ya kuwajibika kwa pamoja kama serikali. Hili ni suala la kitaalamu ambalo sisi wengine akina Mwiba, Ngekewa na bwana udini Mizizi, tunyamaze tu!
Mnaona haya kitu gani kuitaja Tanganyika yaani mnashindwa kumpa sapoti hata Mtikila mnashindwa kuwaunga mkono wale G55 ni aibu kwa wazalendo waTanganyika kama Wazenji waTauwana ni wao kwa wao nyie hayawahusu nde wala sikio ,lakini ilivyo sasa kama mauaji ya 2001 yalioendeshwa na benyamin Serikali ya Tanganyika ilijiyovisha koti la Muungano inahusika moja kwa moja ,mauaji ya kina Hanga na wenziwe Serikali ya Tanganyika ilijiyovisha koti la Muungano inahusika moja kwa moja.