Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Dah! nimeamini education can ruin your life, mfano ni huu, una masters lakini upo tayari kushauriwa na form IIB.
 
Mwanamme au sisi wanaume tukioa kitu cha kwanza tunataka mtoto,leah ulikua hijui? Kama hujui ndio nakufahamisha,hatuhitaji madoido,hata kama utaolewa tena,kitu cha kwanza kazae,watoto wanalinda ndoa,kama huamini basi,ungekua namtoto hata mdogo wako asingeshika mimba,huo ni uzembe wako,jamaa alitakamtoto fasta wewe unataka elimu? Ona sasa
 
Muachie dogo kwanza ana mimba yake, we kasome na PHD kabisa. Ki ufupi apo shule ilikuponza. Alaf elim haina mwisho sista, Kwa nini usingesema uzae ndo ukaendelee na shule!!?, na hakika hata mdogo ako angeona mna mtt ange chukulia uzito hiyo kitu, next time ujue ku prioritize mambo ya muhim
mkuu acha kupotosha UMMA. kutokuzaa kwake kwa sababu YOYOTE ile, hakuhalishi mume wake KUZAA na MDOGO WAKE WA DAMU. umeelewa? acha dhihake zisizokuwa na tija kwa mkuu Leah 2.
 
Chezea mtoto mbichi tena dot com wewe chuchu saa 6.
Dah! nimeamini education can ruin your life, mfano ni huu, una masters lakini upo tayari kushauriwa na form IIB.


Kakajambazi eh; kuna kitu hatujaelewa. Masomoni tunapataga ujuzi.Akili kama hujazaliwa nazo utapata kutokana na changamoto za dunia hii vinginevyo hadi unakufa hutapata
 
Kuna mzee mmoja aliniambiaga kitu lakini pamajo na hii scandar ya huyu dada ndo nimeona. Alisema kwamba levo za maisha zipo na zitaendelea kuwepo. Kwamba kama mtu anakuzidi tambua hilo. Akanambia hivi: "mwanangu sikujui hunijui; ila mwanamke anaekuzidi elimu; anaekuzidi kipato na hela; anaekuzidi urefu, sahau usidhani hiyo ndoa itadumu"! Sasa nayaona kwa wenzangu.
Af pili; kwenye tatizo kila mtu hujitetea. Dada sikujui hunijui lakini kama tungekuwa tunaweza ona ndani ya nafsi yako; kwa hela zako na elimu yako umechangia 70% ya haya mambo kutokea. Maana wewe ndoto zako ziko mbali saaaana. Ndo maana jama akaona bora huyo wanaenda sawa
Wakati nimeamua kuingia kwenye ndoa nilijua naolewa na mwanaume mwenye level gani kielimu na pia kiuchumi, nilifanya maamuzi nikiwa najua ntawajibika kwake kama mke bila kujali tofauti ya elimu na uchumi pia..na ndivyo nilivyofanya ktk kila jambo tulishauriana na kuamua pamoja wala hakuna jambo nililoamua peke yangu.. Isipokuwa hili la kumpa kutembea na kumpa mimba mdogo wangu ndo sikuhusika.
 
Tatizo lako wewe bado unaangalia nini jamii itakavyo kuchukulia, watu wamezaa kiivyo na bado waliamuwa kuolewa pamoja. ndio mume wako kafanya kosa kubwa sana na sii dogo. Kosa ni wewe kuliweka swala hilo hadharani. wewe ungemwambia mdogo wako ayamalize na mume wako, usitake kusikia upumbafu wake. then ungewapa time frame if watafanyaje.
 
Kifupi Leah2 huyo mme wako ni malaya...hata ungemzalia watoto 8 bado angefanya ufilauni wake..ukiona mtu anafanha ufuska nyumbani ujue kazini kashamaliza vibinti vyote vya field na wale wahudumu...Hapo bado wale anaokutana nao njiani...

Hao wanaosema Kisomo chako kimesababisha wanakupotosha..naamini yote uliofanya ni kwa ajili ya kuinua kipato cha familia..

We unangaika kutafuta maisha mwenzako anakusaliti nyumbani....Biblia inasema ndo haivunjiki isipokuwa kwa sababu ya uasherati...hapo ndoa katika ulimwengu wa roho haipo hata kama ungeilazimisha...lile agano mliloagana kanisani limeshavunjika

Endelea kusoma na kumsihi Muumba wako akuumbie wa kwako...akupe mme wako...huyo hakuwa wako..
 
Some men are selfish jamani khaaaa. Hivi ukiolewa ndo huruhusiwi kwenda shule, kwamba ndoa ndo mwisho wa ndoto zako? Mbona wanandoa wengine wanaamua kukaa kwa muda bila kupata mtoto? What if huyu mdada kwa mapenzi tu ya Mungu angechelewa kupata mtoto mumewe angeenda kuzaa nje? Angekuwa anamnyima mumewe haki yake ya ndoa at least tungesema mume alizidiwa (though hakuna justification ya cheating). Afu mbona huyo mume kama alikuwa na shida sana ya kuitwa baba, alimwambia huyo mdogo mtu atoe mimba, shida yake si mtoto au na alikosa wa kuzaa naye hadi mdogo wa mke wake? Shameless man.

Wamekubaliana wasizae kwanza dada amalize shule, kosa liko wapi? Mwanaume hatakiwi kusupport ndoto za mkewe? Kila familia ina maamuzi yake na jinsi wanavyoendesha maisha yao, tusilazimishe watu waishi kama sisi. No wonder wanawake wengi wenye mafanikio ni either
1. Hawajaolewa
2. Waliolewa wakaachika
3. Wamefanikiwa kabla ya kuolewa. (I'll get married though hihihi, Amen)

Bana wewe leah2, cheating is a deal breaker. Ukiweza kusamehe samehe tu kwa moyo mmoja. Ukishindwa pia no one is gonna blame you. Watu wanasema tu humu easy "eti huyo mtoto akikua arudi tu nyumbani umleee" eishhhhhh. Mtu unamkuta tu mwanaume ana mtoto before, but still kumlea kuna kaugumu fulani sembuse huyo wa kuletewa ndani ya Ndoa!!!! BTW are you a nanny or what kwamba mtu akaspread tu his seeds afu wewe unaletewa tu kulea mtcheew. Afu worse enough mumeo haonyeshi kuregret at all na wakati ana makosa kabisa. Haya wewe ndo ukamuombe msamaha umrudishe ndani ya nyumba au? Cha mwisho kama una dream za kusoma tena hapo baadaye kasome tu na PHD my dear na ndoa isiwe mwisho wa ndoto zake.

Hao wa kusema eti ukimuacha huyo unaweza kukosa mume mwingine, then let it be, God knows what's the best for you. Kama ndoa haikupi amani ya moyo just quit it kabla hujapata na depression kabisa au hujadondoka kwa presha. Huna haja ya kuishi na maumivu for the sake of a purposeless union. Kuna mtu kafa mapema kwa sababu hajaolewa/ kaachika ? Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu. It shall be well with you
Asante heaven sent umeugusa moyo wangu mpaka nimejikuta nalia, to be honest siwezi endelea na hii ndoa, sioni future serious na huyu mtu.
 
Inategemea wewe ni mwenyeji wa wapi. Kule kwetu ni ufahari. Wala hakuna issue hapo. Sanasana unachoweza kufanya ni kumwambia mdogo wako akupishe maana hapo ni kwako. Watakuwa wanakutana hukohuko anakoenda.
Sikushauri kabisa kuachika.
 
Dada Leah2 pole sana kwa mtihani mgumu. Pia nakupongeza kwa kuweza kuwa jasiri na kufuatilia mambo kwa upole. Nimejifunza jambo la maana sana kutoka kwako.

Kuhusu hii ndoa yako mi naona hauna haja ya kuwaza sana. Ni kweli jamaa hakuheshim na inawezekana alikubali kufunga ndoa nawe kwa sababu za kiuchumi. Kwa ninavyoona wewe unacareer nzuri na kipato cha uhakika na hivyo huyo shemeji mume aliamua kukuoa tu juu ya hilo ila hakupendi ki ukweli.

Fanya maamuzi ya haraka ya kuachana nae kabla mtoto hajazaliwa maana akishazaliwa stori inaweza ikabadilika. Hakikisha mnaachana kisheria kabisaaa ili asikusumbue baadae. Jipe muda kidogo baada ya hili tatizo kabla hujaanziasha uhusiano mwengine.

Halafu hao wanaosema eti ulikosea kwenda kusoma ni maselfish tu. Mimi nimezaa baada ya kupata masters na immediately nilipopata mtoto nimeanza PhD. Kwa mwanamke kusoma kunahitaji kujitoa sana hasa baada ya kuwa na watoto. Kuamua kumaliza masters yako sio kigezo cha mumeo kuzaa na mdogo wako.Tena usipoangalia anao watoto wengine huko nje sema Mungu ametaka kukuonyesha mapema kwamba huyo jamaa ni opportunistic tu na wala hana mapenzi kwako.
 
Pia Leah2 wasamehe kabisa ili Mungu atende muujiza kwako...fungua moyo wako samehe yote...kila kitu kinafanywa kwa kusudi...pengine hilo limefanyika ili Mungu akuepushe na kuletewa magonjwa ya zinaa na ukimwi nyumbani kama mngeendelea kuishi..Mungu anakupenda na anamakusudi na wewe na yeye huwa anaona mbele...So wasamehe na endelea na maisha yako.
 
Dada yangu leah2 ningependa ufwatwe ushauri wa mwisho wa Don Mangi na sifi leo... Wamesema na kuchambua vyema sana. Nami nasema USIVUNJE NDOA YAKO. No body is perfect under the sun. Unaweza kimbilia mume mwengine na huyo akaja kuzaa na Dada yako mkubwa (Kama yupo) ama akafanya kituko zaidi ya mumeo wasasa. Uvumilivu ndio ndoa. Hata sisi tupo kwenye hii taasisi. Ni ngumu sana. Mungu ndio hututangulia. Hakuna fundi wa ndoa leah2

Hongera kwa busara zako za kutafuta ukweli wa mambo. Heshimu mawazo na ushauri wa wazazi. Mwisho, hata Kama una mali kiasi gani, umekorofishana na mume kiasi gani, usiweke mipakano ya umiliki. Kwamba nyumba yangu hivyo toka! Gari langu usipande, bafuni peleka maji mwenyewe n.k. Hapana!

Busara ukiuongoze na uone kila kilichopo ndani ni chenu nyote, regardless. Usifukuze mume. Ni indication ya mwanamke jeuri na mwenye majivuno. Kwa maana ya kwamba siku ukimaliza PhD ukarudi home baba kachelewa basi kuna hatari ya yeye kulala nje au sitting room. Ni mbaya sana. Samehe. Piga moyo konde maisha yaendelee.

Goodluck Mshana
Goodluck Mshana nimekuelewa lkn to be honest hilo ni suala gumu sana, emu niambie nafuata nini kwake? Speak frankly hapa.
 
Uamuzi wako nami nimeukubali, sio heshima na sio busara jamaa alivyokufanyia. Kama ndoa ya kiislamu talaka inawezekana kama kanisani basi waambie wasirudi tena nyumbani, waendelee na maisha yao.
 
Leah 2 ningekuwa wewe hata nisingekuja hapa kuuliza ushauri, ndoa hakuna hapo tena. Jikusanye upya Mungu atakuletea mume mwingine. The bottom line is men are men, no comparison.

Mungu gani anataka wanawake wapange ratiba za lini anatka kuzaa na lini hataki?? tatizo la wanawake wengi huku kusoma kwenu kunawapotosha sana, yaani wewe uolewe alafu hapohapo upange ratiba ya kuzaa, na sio wewe tu ni wengi wanagongewa wadogo zao au beki tatu na humu pia wamo ila hizo mimba hazijaingia ndio maana wako vifua mbele kukutetea.

Hilo umelitaka mwenyewe kwa kupanga ratiba za mechi na lini uzae, ndoa changa kabisa na makalenda kibaoooooooooooo. ulitakiwa ukae na ndoa yako kwanza kisha upate kamtoto kakumliwaza mzee ndio sasa ukasome hayo madudu yako. sasa masters ukae 2 years bila kuzaa, then PhD ukae 5 years bila kugegedwa we utakuwa unawazimu sio bure.

Mliobaki sasa hili ni somo kwenu, ukiolewa angalia ndoa kwanza kiasi cha 5 years, sio leo kesho unaanza minyodo ya masters. Ukija kuona jamaa ameparamia muhudumu wa tigo pesa anaweza kuoa kabisa na wewe ukabaki na makabrasha yako ya masters.
 
Pole Leah dear..hz ndoa hizi..mi nimeshindwa hata kuwaza nimejikuta tu namwambia Mungu aseme na ww na akuongoze ktk maamuzi yako
 
Duuh!pole sana!hii dunia imearibika total.. Yesu arudi tuuh Hamna namna nyingine..!ndoa ya kanisani pia inavunja kienyeji hivyo?!

Sasa huyo yesu ndio atabeba mimba badala ya huyo dada?? yeye ameolewa usiku asubuhi anapanga ratiba za lini atazaa, unaweza ukapanga ratiba na mwanaume akakubali lakini anakulia timing tu. Kwanza kaeni mkijua katika swala la kugegeda mwanaume huwa hataki kupangiwa hata sekunde, na kama atakubali ujue ni shingo upande sana, sasa huyu hata mwaka hana tayari anaanza mambo ya kuweka ratiba za kuzaa. je alimwambia hayo kabla ya ndoa??
 
Mungu gani anataka wanawake wapange ratiba za lini anatka kuzaa na lini hataki?? tatizo la wanawake wengi huku kusoma kwenu kunawapotosha sana, yaani wewe uolewe alafu hapohapo upange ratiba ya kuzaa, na sio wewe tu ni wengi wanagongewa wadogo zao au beki tatu na humu pia wamo ila hizo mimba hazijaingia ndio maana wako vifua mbele kukutetea.

Hilo umelitaka mwenyewe kwa kupanga ratiba za mechi na lini uzae, ndoa changa kabisa na makalenda kibaoooooooooooo. ulitakiwa ukae na ndoa yako kwanza kisha upate kamtoto kakumliwaza mzee ndio sasa ukasome hayo madudu yako. sasa masters ukae 2 years bila kuzaa, then PhD ukae 5 years bila kugegedwa we utakuwa unawazimu sio bure.

Mliobaki sasa hili ni somo kwenu, ukiolewa angalia ndoa kwanza kiasi cha 5 years, sio leo kesho unaanza minyodo ya masters. Ukija kuona jamaa ameparamia muhudumu wa tigo pesa anaweza kuoa kabisa na wewe ukabaki na makabrasha yako ya masters.

Hili wazo inabidi ujeumshauri namtoto wako wa kike, maana watu kamanyie ni rahisi sana kushauri kwa watu baki ila si kwa familia zenu. Halafu unafikiri kutokuzaa kwakwe ndio kumemfanya huyo mume azae na sheji yake? Ukweli hata kama Leah angekuwa nawatoto huyu jamaa bado angelala na shemeji yake. N kama swala lilikuwa ni mtoto mbona jamaa alikuwa analazimisha wakatoe mimba. Hii inaonyesha hakufanya ngono kwa lengo la kuzaa bali ni tamaa zake za kimwili.
 
Back
Top Bottom