Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

pole sana mdau uamuzi uliochukua naona huko sahihi kabisa kwasababu mume wako ameshindwa kukuheshimu mpaka akatembea na mdogo wako ila Mungu akusaidie ktk kipindi hiki aise


Yuko sahihi wapi! Wakati haya wanayatakaga wenyewe! Kuna sehwmu ameandika mdogo wake kabakwa! Hapa kuna badhi ya mambo:
1. Huenda umejifanya msomi na kuanza kuleta mambo ya ajabu ndani.Maana unadai wewe unasomea Masters; na mnapokaa ni kwako. Hakika huyu mwanaume japo hujaweka wazi kila kitu atakuwa na sababu ya msingi kufanya hivi.Huenda unamnyanyasa kisa kwako na elimu. Aende kwa Baba Paroko? Tulia kampata mama paroko

2. Haya mambo ya watu kuleta leta ndugu zenu ni shida.Mtapinga lakini ukweli ndo huo. Mwanaume anadai shemeji ananitaka kimapenzi; mwanamke anadai shemeji kanigegeda.Na mbunye ni kitu kibaya kwa ndugu aise.Af haya ya kike utakuta mother house haupo, anavaa kanga tu! kisa anafua chupi au anaenda kuongea na simu nje. Kwa nini ukiwepo hawezi kufanya hivyo kama siyo uchokozi? Yaani ingekuwa raha sana mkiwa karibu na ndugu.Lakini kwa mambo hayo ya kila leo,una uhakika gani kama hayatakukuta?
 
Unafikiri akiondoka na kubaki ni wapi atakuwa amempa unafuuu mdogo wake
According to yeye, tayari mumewe keshaondoka sivyo, anachokifanya saiv ni kumake decision, ndio maana nasema, asamehe na katika kusamehe means hata Mdogo wake akijifungua usiwe na kinyongo nae maana ni damu yake.
Biblia inasema mwanaume hatamuacha mke wake isipokuwa kwa uasherati (uzinzi), so kwa mantiki hiyo vice versa is true.
But stl she has got room to think about it, kama ataona amrudie na amsamehe its OK. Lkn kwangu mm naona amwachie huyo Mdogo wake a dictate temple, au siyo jamaa yangu.... Maana tayari hawa washaonjana kuachana kwao hadi kifo baba, at least angekuwa mtu baki kaini ndg

Au siyo ndugu wa damu huyu leah2 ?
 
Wanaume wengine bwana,watu tunatafuta wake wenye heshima ,wao wanawachezea,Du dunia hii bwana kama vipi ni PM tuongee zaidi.
 
Teh teh teh shetan wapi wanawake wanamambo ya hovyohovyo sana ukiachana na alichoandika kiuhalisia ukifuatilia 100% utakuta yeye ndo tatizo,wanaume ndoa tunaziheshimu sana,by the way mzee umenitusi kuniambia nikasubri mm nitake radhi.
Hahahahaha sory mkuu munkali wa mada by the way haya mambo siyo mwanume peke yake mwehu aweza kuwa mwanaume au mwanamke.
 
Some men are selfish jamani khaaaa. Hivi ukiolewa ndo huruhusiwi kwenda shule, kwamba ndoa ndo mwisho wa ndoto zako? Mbona wanandoa wengine wanaamua kukaa kwa muda bila kupata mtoto? What if huyu mdada kwa mapenzi tu ya Mungu angechelewa kupata mtoto mumewe angeenda kuzaa nje? Angekuwa anamnyima mumewe haki yake ya ndoa at least tungesema mume alizidiwa (though hakuna justification ya cheating). Afu mbona huyo mume kama alikuwa na shida sana ya kuitwa baba, alimwambia huyo mdogo mtu atoe mimba, shida yake si mtoto au na alikosa wa kuzaa naye hadi mdogo wa mke wake? Shameless man.

Wamekubaliana wasizae kwanza dada amalize shule, kosa liko wapi? Mwanaume hatakiwi kusupport ndoto za mkewe? Kila familia ina maamuzi yake na jinsi wanavyoendesha maisha yao, tusilazimishe watu waishi kama sisi. No wonder wanawake wengi wenye mafanikio ni either
1. Hawajaolewa
2. Waliolewa wakaachika
3. Wamefanikiwa kabla ya kuolewa. (I'll get married though hihihi, Amen)

Bana wewe leah2, cheating is a deal breaker. Ukiweza kusamehe samehe tu kwa moyo mmoja. Ukishindwa pia no one is gonna blame you. Watu wanasema tu humu easy "eti huyo mtoto akikua arudi tu nyumbani umleee" eishhhhhh. Mtu unamkuta tu mwanaume ana mtoto before, but still kumlea kuna kaugumu fulani sembuse huyo wa kuletewa ndani ya Ndoa!!!! BTW are you a nanny or what kwamba mtu akaspread tu his seeds afu wewe unaletewa tu kulea mtcheew. Afu worse enough mumeo haonyeshi kuregret at all na wakati ana makosa kabisa. Haya wewe ndo ukamuombe msamaha umrudishe ndani ya nyumba au? Cha mwisho kama una dream za kusoma tena hapo baadaye kasome tu na PHD my dear na ndoa isiwe mwisho wa ndoto zake.

Hao wa kusema eti ukimuacha huyo unaweza kukosa mume mwingine, then let it be, God knows what's the best for you. Kama ndoa haikupi amani ya moyo just quit it kabla hujapata na depression kabisa au hujadondoka kwa presha. Huna haja ya kuishi na maumivu for the sake of a purposeless union. Kuna mtu kafa mapema kwa sababu hajaolewa/ kaachika ? Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu. It shall be well with you
 
My kaka hata kwetu uku kahama ni tuzi ndo maana nilikua namshangaa huyu mchaga anasema kwao ni kawaida.hata huyu mwenye hii inshu ambaye ni Leah nimeona bora akasonga mbele aibu kwa pande zote za familia amwache tu huyu bwana.
Sahihi kabisa my dada halafu maisha ya ndoa mungu akiwapa uhai ni marefu sana kwanini uishi na kidonda maisha yako yote kumbe upo uwezekano wa kujinasua?
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Kuna mijitu ni zaidi ya shetani sister kimbia hapo hapakufai tena
 
Pole dada ,
ulimwengu umeoza huu,hakuna hiyana wala utu kama zamani.ukweli kuishi na huyo mume ni kuishi kinyume na matarajio yako !
Afadhali hata angekuwa mtu baki....
Lakini tafadhal hem jaribu kuongea tena na moyo wako usifate maamuzi ya ubongo ya ghafla...acha jazba.
Nikupe mfano kidogo ,hii ilitokea kwa watoto wa mjomba wa marehem mama yangu!

Dada aliolewa mjini ,baadae akaona amchukue dogo wake aje kumsaidia kazi ya kuuza duka..mdogo kaja na biashara ikakuwa vyema,miaka miwili mbele mdogo kapata mimba kuulizwa ya nani hasemi!
Kwa huruma ikaamliwa akae na kuzaa pale,haya kamaliza kunyonyesha kabeba tena na tena.!

Dada kaamua amtafutie pake aishi, wanabe wakaanza yao chini chini kuwa watoto ni wa shemeji kula..,lakini dada kapuuza na hakuwahi kuhisi jambo. Sasa siku moja ikaja kesi ,mume wa dada kajeruhi mtu vibaya ,kisa kamfuma ndani na shemejie! Hapo ndo ikaliki..mana ikibidi wabanwe na polisi kutokana na mazingira ya kesi yalivyo..
Majirani na mwenye nyumba kule alikopanga mdogo mtu walikuwa wakimjua yule shemeji ndo mumewe, na siku nyengine akilala vzr tu.

Mwisho walikubali kuwa ni wapenzi na washa zaa watoto watatu tena wanamfanana baba yao,dada mtu alilia kilio cha mbwa! Akajuta majuto ya farao..na akaachana na mume kwa miaka mingi.
Lakini hivi naandika dada alisha msamehe mumewe na wanaishi kama kawa,mdogo karudi kijijini anapelekewa matumizi.

Ukimuuliza dada sababu anajibu ,alijaribu kuishi na watu tofauti lakini hakuna aliyefikia sifa za mumewe wa mwanzo.!
Sasa nawe sikiliza nafsi yako...sema na moyo wako mama !
upate kilicho bora kwako...

Duh! Huyo dada yako kiboko. Ana moyo wa chuma aseee
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Yuko sahihi wapi! Wakati haya wanayatakaga wenyewe! Kuna sehwmu ameandika mdogo wake kabakwa! Hapa kuna badhi ya mambo:
1. Huenda umejifanya msomi na kuanza kuleta mambo ya ajabu ndani.Maana unadai wewe unasomea Masters; na mnapokaa ni kwako. Hakika huyu mwanaume japo hujaweka wazi kila kitu atakuwa na sababu ya msingi kufanya hivi.Huenda unamnyanyasa kisa kwako na elimu. Aende kwa Baba Paroko? Tulia kampata mama paroko

2. Haya mambo ya watu kuleta leta ndugu zenu ni shida.Mtapinga lakini ukweli ndo huo. Mwanaume anadai shemeji ananitaka kimapenzi; mwanamke anadai shemeji kanigegeda.Na mbunye ni kitu kibaya kwa ndugu aise.Af haya ya kike utakuta mother house haupo, anavaa kanga tu! kisa anafua chupi au anaenda kuongea na simu nje. Kwa nini ukiwepo hawezi kufanya hivyo kama siyo uchokozi? Yaani ingekuwa raha sana mkiwa karibu na ndugu.Lakini kwa mambo hayo ya kila leo,una uhakika gani kama hayatakukuta?
aise inawezakana alizidisha sana usomi mpaka kusahau majukumu ya familia kama mke ndiyo maana jamaa uzalendo ukamshinda atatembea na mdogo wake ajifunze cku nyingine ndoa na usomi ni vitu viwili tofauti
 
Pagumu hapo. Pole. Kuna maswali ya kujiuliza..Je, wakiishi pamoja uko tayari kumuita huyo mumeo shemeji? Mumeo alijuta na kuomba msamaha kwa dhati? Hapo kuna tatizo kubwa sana kwenye mahusiano wewe na mdogo wako. Chuki yako haitakwisha kwake akiendelea kuishi na Mumeo na ndo aibu itaendelea milele.
Ushauri mumeo akijirudi itakua nafuu na mdogo wako angeondoka angeolewa baadae na mtu mwingine ungepata nafuu kidogo ya chuki. Kwa sasa hata ukija pata mtu mwingine baadae wa kukuoa akisikia hii story anaweza kubadili mawazo.
Ukiweza kapatane na mumeo.
mkuu KUPATANA kuko wapi hapa? je, kama ikiwa hivyo watoto wake watakuwa wanamuitaje mtoto wa mama mdogo aliyezaliwa na baba yao? acha kabisa hiyo habari mkuu. wewe unadhani hii skandali ni rahisi kihivyo? huyo muasherati hana undugu (mtoto) wowote na huyo muasherati...akachukue taimu zake!
 
According to yeye, tayari mumewe keshaondoka sivyo, anachokifanya saiv ni kumake decision, ndio maana nasema, asamehe na katika kusamehe means hata Mdogo wake akijifungua usiwe na kinyongo nae maana ni damu yake.
Biblia inasema mwanaume hatamuacha mke wake isipokuwa kwa uasherati (uzinzi), so kwa mantiki hiyo vice versa is true.
But stl she has got room to think about it, kama ataona amrudie na amsamehe its OK. Lkn kwangu mm naona amwachie huyo Mdogo wake a dictate temple, au siyo jamaa yangu.... Maana tayari hawa washaonjana kuachana kwao hadi kifo baba, at least angekuwa mtu baki kaini ndg

Au siyo ndugu wa damu huyu leah2 ?
Yesu alisema jambo la kuachna lilisemwa Hivyo kwa sababu ya mioyo yenu kuwa migumi. Lakini tangu Mwanzo Mungu hakuumba kuachna. Kuachna sio option ya Mungu .
2. Kwa mtazamo wangu alimwachia mdogo wake atachukua milele

3.akiondoka atamuumiza milele sababu dogo atajihisi amevunja ndoa ya dada. Kwangu mimi abaki.

Kuondoka home yeye ndiye aliyewaambia wampishe atafakari.
 
Labda mumeo alikuwa anahamu sana na Mtoto ila wewe ukaweka maslahi yako ya kuto kubeba mimba yake mpaka umalize masomo unaweza kuachana nae leo ila elewa kuwa siku zote ukishakuwa ndiwe mwenye maamuzi ndani ya ndoa vitu kama hivyo tena na zaidi ya hivyo hutokea ushauri wangu ni kuwa rudisha moyo wako kwa mumeo najua yeye ni binadamu hatarudia tena huo ujinga mpaka hapo ameshajifunza vya kutosha.
 
dah pole sana mwaya..hawa wanaume sijui sometimes akili wanaweka wapi..yaani of all wanawake outside there ndio atue kwa mdogo wako..mxiuu

Endeleeni kukaa michupi nje! Maziwa mnaanika weeeee! Sawa tu! Mtaishia kuwavunjia ndoa ndugu zenu! Juzitu hapa si kuna mtu alilalmika kamla mamkwe kisa alikuwa anamtega jama uzalendo ukamshinda! Huu utandawizi huu! Huu huu! utawafanya mjute na kuolewa.Kisa mtoto wa kizazi kipya nakuja kwako unampa uhuru kwa kira kitu! Hadi wengine wanawapokea mashemeji zao kwa furaha na tabasamu; na ndo yamekushinda huku na wewe unayaweza! Pili mi naona siku hizi wanaume hawatishiwi ndoa.Ukimpiga chini, faster anapewa relief na care vya kutosha. Dakika tu kashakusahau,na wewe utaendelea kujiproud kwamba keaho au kesho kutwa atarudi! Thubutu! Umeshakuwa spare tire huku ulikuwa mama mwenye nyumba.Sasa subiri mwaka wa pancha atakuja
 
Imeandikwa samehe saba mara sabini, sisi wanaume ni mbwa.
mkuu, kuna makosa ya KUSAMEHEKA lakini sio hili. hebu jiweke kwenye nafasi ya Leah 2 halafu unambie huo MSAMAHA utaanzia wapi na kuishia wapi.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Pole Dada Leah, Kwa ushauri wangu naomba utafute jinsi kuludiana na mmeo kwani hata tukisema umwachie huyo Mdogo wako ndio utakuwa umepanda mbegu ya chuki kila ukiwaona utakuwa unatamani kuwamaliza, vile vile ndoa yao hautakuwa na amani, ila ww kama mmeo akijutia makosa yake na ukamsamehe mtaishi Kwa amani labda ushindwe kutoa msamaha
 
Dada sikupond lkn naongea tu ndoa inapofungwa kinachofuata n watoto haina kusema nimalize masters au kujenga hao n wazinzi kwa muda wa miez mnne kama mdogo wako alivyokuambia mimba tu ndio imewaumbua labda alikuwa anakula hausigal kabla ya dogo kuja piga chn maisha yaende
 
yaani walikuwa wanafanya tena bila condom uamuzi uliouchkua upo sahihi..japo haita free your mind but at least itapunguza kuliko kuendelea naye halafu usikia anakuja ndugu yako wa kike unaanza kupatwa na wasiwasi.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom