Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

mkuu, kuna makosa ya KUSAMEHEKA lakini sio hili. hebu jiweke kwenye nafasi ya Leah 2 halafu unambie huo MSAMAHA utaanzia wapi na kuishia wapi.
Watu wanaongea tu yani hilo ni ndoa ningekuwa mie nadai talaka tena hata maandiko yana ruhusu eti usamehe na mtoto wamwona
 
Baada ya kusoma nkakumkumbuka mambo ya yokobo baba Wa Israel,

alafu nikamkumbuka yule jamaa anayewahubiria watu wawatafune ma housegirls wao na wadogo wa wake zao wanaoishi nao majumbani mwao. Nahc mumeo atakuwa muumini wa yule jamaa
 
1. Cjajuia ww dini gani kama ni muslim nafikiri omba talaka then fuata uamuzi uliouchangua.
 
Ndoa za kanisa hakuna kuachana,waendelee tu na maisha na ukae tu na mdogo wako hamna noma.kiroho safi tu leah
 
Dada Leah, pole sana, nimeona huzuni yako ni kubwa, tena ni kubwa. Napenda kukushauri kitu. Iwapo utaishi na mmeo nakuhakikishia hutapata amani maishani mwako....tafuta maisha mengine mwanangu.

Hutaishi kwa amani kwa sababu hizi.....

1. Mdogo wako ataendelea kuishi, mtoto aliyemzaa nae ataishi na utakuwa unawaona, hii itaendelea kukupa kumbukumbu na kutompenda mmeo ikiwa utaendelea na ndoa yako

2. Mmeo atakuwa mzazi mwenzie na mmeo, haitakuondoa wasiwasi kamwe kama mahusiano yao yalikoma, hata kama ataolewa kwingine

3. Mdogo wako hataweza kufika nyumbani kwako kwa uhuru, ni bora mkutane nae ukiwa huna huyo mme au mkutane kwa wazazi wenu kuliko yeye kukutembelea nyumbani kwako ukiwa unaishi na mmeo

4. Mmeo atahitaji kumhudumia mtoto wake, hii itakuwa inakupa flasback (those negative ones) na itaendelea kukuumiza

5. Kama haya yote unaweza ukayamudu, yasikuvuruge katika kipindi chenu cha ndoa, basi endelea na ndoa yako.
Yote hayo nimeyawaza House of Commons, Ninaumia sana sioni njia nyingne ya kujinasua zaidi kuendelea na maisha nje ya hii ndoa, sijutii kutoka kbsa..let him go ahead with his foolishness..
 
Mwenye makosa ni mme wako ambaye kamshawiahi mdogo wako. Mimi naona umechukua maamuzi mazuri nayakistaarabu
 
Umefanya maamuzi ya busara kumpiga chini, kwasasa just stay alone and relax, huhitaji kuanzisha mahusiano mapya kwasasa, give urself some times ili akili ikae sawa
 
Pole sana mtoa mada.......uamuzi wako ni mzuri otherwise hata ungeamua kuishi nae hiyo ndoa isingekua na afya
 
  • Thanks
Reactions: nao
Hayatuhusu. This is your private business. Nendeni mkamalizane kifamilia. Tumechoka kusoma mada zisizo na mantiki.
 
dada leah, mim naanza kwa kukutupia wewe lawama, pili mumeo na tatu ni dogo lako.
wewe naona ndo ulie_create ili tatizo pasipo kujua, simanish tusikae na ndugu zetu kwenye ndoa la asha, lakin ulijisahau sana. tumezoea kusema wanawake ni dhaifu ila sio kweli, ila wanaume ndo tulio dhaifu sana. dogo pengine aliletewa vishawishi kwa akili yake na mazingira kama yale hasingeweza kuvikwepa mbele ya mumeo.

lakin zingatia wew ndo uliesababisha mumeo amuone mdogo wako. na wanawake mlioajiriwa ndoa huwa mnashindwa kuzitekeza ipasavyo mwishowe matatzo kama hayo yanatokea, kwa kilichotokea si mdogo wako, hata angelikuwa house_girl, au rafik yako kama unaishi naye ingelitokea, hivo mwenye kosa ni mumeo lakin naye katengenezewa mazingira.

kosa lingne husingewaita wazaz hapo ulikosea japo walichokushaur ungekitmiza wew pasipo tatizo, wew umefunga ndoa umekula kiapo basi timiza hicho kiapo, kama angelikuwa house girl uamuzi ungelimfukuza bila kujar chochote, japo ni ngumu lakin inawezekana kuish na mumeo vzur tena sana
Unaweza ukanilaum kirahisi lkn siwezi kukuzuia kuwaza hivyo, sina haja ya kujitetea maana haitaondoa kosa lkn ninachotaka kusema ni kwamba mwanaume huyu amenifanya kama mtu asiye nathamani kwake..nimeeleza kifupi sana maana kama ningeelezea kila kitu ingekuwa uzi mrefu na pengine ungechosha kusoma.
Mdogo wangu alieleza mbele zake kuwa alimkatalia Mara kibao lakin hakusikia ,na Mara ya kwanza kusex alimfuata chumbani kwake na kumlazimisha tokea hapo akawa anamwambia Hana haja ya kukataa kwani mbona wameshaanza
 
mkuu Leah 2 naona kuna watu wanachukulia hii skandali lightly. hili suala halisameheki. hebu tupia hapa hiyo AUDIO kati ya dogo & msherati wasikie ufirauni na usaliti uliokufanyiwa. mm naseha hapa hakuna MSAMAHA na wala hakuna NDOA! it's over.
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.

Pole sana.

Hapo huna tatizo kabisa.

1. Uliolewa kwasababu ya mapenzi uliyonayo kwake mumeo. Kama bado UNAMPENDA na yeye ANAKUPENDA kwa dhati + hana mapenzi ya dhati kwa mdogo wako na unaweza kuthibitisha hilo basi endelea naye.

2. Kinyume na hapo anza maisha yako upya. Hii dunia ina wanaume wengi sana wanaokupenda(tunaokupenda) kuliko wewe unayodhani, tatizo lenu mabinti mnakariri sana mambo.
 
Daah Leah hata kama utaamua kumsamehe huyu mmeo jipe muda kuanza kuishi nae kama mme.yaani angekua mwingine neno nisamehe/samahani zisingeisha mdomoni mwake
Binafsi sitaweza kuishi nae tena nilitakupata justifications ya maamuzi yangu ndo maana nikaomba ushauri humu ndani

Watu wanaongea tu kirahisi nisamehe lkn hawajaribu kuvaa uhusika waone ilivyo ngumu
 
Pagumu hapo. Pole. Kuna maswali ya kujiuliza..Je, wakiishi pamoja uko tayari kumuita huyo mumeo shemeji? Mumeo alijuta na kuomba msamaha kwa dhati? Hapo kuna tatizo kubwa sana kwenye mahusiano wewe na mdogo wako. Chuki yako haitakwisha kwake akiendelea kuishi na Mumeo na ndo aibu itaendelea milele.
Ushauri mumeo akijirudi itakua nafuu na mdogo wako angeondoka angeolewa baadae na mtu mwingine ungepata nafuu kidogo ya chuki. Kwa sasa hata ukija pata mtu mwingine baadae wa kukuoa akisikia hii story anaweza kubadili mawazo.
Ukiweza kapatane na mumeo.
Mkuu usimpotoshe hakuna ndoa hapo, huyo mume ni pasua kichwa, katamani shemeji house girl atamuacha? Aanze maisha upya afute kila kitu kuhusu huyo mume, ashukuru Mungu sana hana mtoto naye, atampata mume nzuri na mwema ambaye huyo atakuwa ndiye mwenye ubavu wake, atasahau ujinga wote aliofanyiwa na huyu muacha zipu wazi
 
Pole Dada Leah. Kwanza ninakusifu umahiri wako wa kutokupanic na kutulia siku uliposikia wakiongea pamoja. Kwa maoni yangu wewe ni mke mwenye busara sana kwa jinsi ulivyochukulia mambo. Kwa sasa ulivyofanya ni vizuri. Kwa ushauri wangu chunguza kwanza wamekwenda wapi. Kama wamekwenda kuishi pamoja kwa sasa basi wape uhuru uendelee na maisha yako. Lakini kama mdogo wako amekwenda kukaa na wazazi au anaishi sehemu tofauti basi tafakari na umsamehe mme wako. Kama ulivyosikia wanaume ni wadhaifu na inawezekana mdogo wako ndiye aliyeanza mambo haya ulipokuwa unamwaacha na mumeo. Ninakutakia kila la heri na mungu akusaidie katika kufikia uamuzi wako.
 
Msamehe mumeo subiri mdogo wako ajifungue mlehe mtoto na mdogo wako akatafute mchumba aolewe ukimwacha mume itakuchukua muda mrefu sana kupata mwingine na visa ktk familia ukimwachia mdogo wako mume hawezi kuishi kwa amani na chuki kati yenu itaendelea mpaka kifo.Ila ukisamehe believe utakuwa umesolve mambo Mengi na umemshinda SHETANI. Pole na kila la kheri.
Siyo ktk hili man mvua.
Karibu kuvaa uhusika alafu unishauri tena
 
Back
Top Bottom