Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

leah2

JF-Expert Member
Nov 15, 2015
584
1,437
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
 
Leah2

Tambua kuwa hapo hakuna ndoa tena. Mme wako ameshavunja misingi ya ndoa kwa:
(1) Kufanya uasherati
(2) Kuzaa mtoto nje ya ndoa.

Ingelikuwa tayari nyie mna watoto, ungelisema ngoja tuendelee kuishi pamoja kwa ajili ya kulea familia/watoto.

Watoto hamna, je unachotaka kukivumilia ni kipi?
 
Pagumu hapo. Pole. Kuna maswali ya kujiuliza.. Je, wakiishi pamoja uko tayari kumuita huyo mumeo shemeji? Mumeo alijuta na kuomba msamaha kwa dhati? Hapo kuna tatizo kubwa sana kwenye mahusiano wewe na mdogo wako.

Chuki yako haitakwisha kwake akiendelea kuishi na Mumeo na ndo aibu itaendelea milele.
Ushauri mumeo akijirudi itakua nafuu na mdogo wako angeondoka angeolewa baadae na mtu mwingine ungepata nafuu kidogo ya chuki. Kwa sasa hata ukija pata mtu mwingine baadae wa kukuoa akisikia hii story anaweza kubadili mawazo.

Ukiweza kapatane na mumeo.
 
Dah pole Leah 2 hakika nayaona maumivu moyoni mwako Mungu akutie nguvu zaidi ktk maamuzi utakayo, uamuzi wowote utakao chukua Mimi nakubaliana na wewe maana am speechless hili zito kama ugaidi vile.
 
How old are you?
Partly kabla ya kuanza kumlaumu mumeo nitakulaumu na wewe.
  1. Kutokuufwatilia kwa karibu uhusiano kati ya mdogo wako na shemeji yake. Mbali na kuwa ni ndugu yako wa damu,utakuwa unajua tabia zake na ni mwanamke kama wanawake wengine.
  2. Hilo la kuchelewa kumzalia mumeo mtoto. Inaweza kuwa lilikuwa jambo lako tuu na namna alivyokubali inaweza kuwa kutokana na sababu zako ila je? mliridhiana pasipo shaka kwamba atakubali wewe umalize kusoma ndio umzalie mtoto?
Wanaume ni wadhaifu being a man I know this, na wanahitaji kufuatiliwa kwa ukaribu sana hasa kwenye mambo kama haya yanayohusisha hisia. Ki mtazamo sijui namna mambo unavyoyaendesha nyumbani kwako ni maoni yangu kuwa unaipa sana kazi yako na masomo as priority kuliko mume wako (sisemi usithamini kazi) to me, family comes first. Na hiyo weakness shetani ndio akapitia hapo hapo.

Bottom line: Fuata ushauri wa wazazi, dogo arudi kijijini ajifungue mtoto, mtoto akiwa mkubwa, aje hapo nyumbani, kaeni kikao cha kifamilia mdogo wako na mumeo waombe msamaha kwa jambo lililotokea na mzungumzie utaratibu wa matunzo ya mtoto. Life goes on. Ukishindwa hilo. File for a divorce ukaolewe na mtu atakayekusubiria umalize shule (tena Masters, unga na PHd kabisa) ndio ukubali kumzalia mtoto.
 
Pole sana Leah..

Swala lililopo hapo ni kuangalia pia kua je mumeo anaonekana kujutia kitendo alichofanya au laa..maana unaweza msamehe lkn bado still akaendelea kua na mahusiano na mdogo wako na lkn pia unaweza kumuacha mumeo ili umpe room mdogo wako Wa kuvinjari lkn pia akaachwa..coz nafsi itaendelea kumuuma kula vya haramu.

Endelea kutafakari zaidi kabla ya kuchukua maamuzi
 
Back
Top Bottom