Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Ushauri wangu msamehe, muache dogo azae, chukueni mtoto muishi naye, huyo ni mtoto wenu sasa muombe sana Mungu akupe hekima, uvumilivu na upendo kwa ndugu yako na mtoto wenu,
 
Duuh! Pole sana! Hii dunia imearibika total.. Yesu arudi tuuh hamna namna nyingine..! Ndoa ya kanisani pia inavunja kienyeji hivyo?!
 
Habari bibie Leah

I feel sorry for you kwa kile kilichotokea.
Ninafikiri ukikubali kuendelea na huyo mmeo hakutakuwa na ndoa tena, hata kwenye Biblia inaruhusiwa kumwacha mwana ndoa kwa uasherati.

Bahati mbaya sana jipu limeota pabaya, I am very sure Mdogo wako hataolewa na huyo the so called mmeo, umetumia hekima kubwa sana kushirikisha Pande zote mbili.

You've got to think about uamzi wako huo, labda nikwambie kitu kimoja, achana na mume wako, samehe na sahau, ila wakiamua waoane na waoane, asipomuoa usimchukie Mdogo wako, na natakiwa kuwa karibu sana na Mdogo wako ndiye mwenye wakati mgumu kuzidi hata wew na anaweza chukua maamzi ya ajabu sana, msamehe Mdogo wako hata kama kakukosea pakubwa.
 
Ndoa ni makubaliano ya watu wawili, lakini zitokeapo changamoto tunafanya kuwa tena si makubaliano ya watu wawili bali ya jamii.

Naamini ukweli wa nini kimetokea, jinsi mlivyoishi, jinsi mlivyokubaliana kutopata mtoto , na jinsi hisia zenu zilivyo juu ya kila mmoja wenu, hivi vyote wewe na mumeo mnavijua!

Na hii haihitaji ushauri hapa, hii inahitaji kusimama binafsi kutetea unachoamini!

Tunaweza kushauri hapa na usifanye kama tulivyo shauri, lakini ngoja tusiache kushauri ukasema niliwaomba mshauri tukasema uende mwenyewe.

Binafsi nashauri Simamia unachoamini kitakupa faraja na amani, changamoto zipo na usiangalie mwingine anakuonaje as long as huvunji sheria ya Mungu na ya Wanadamu. Nakutakia kila la Kheri na Amini siku zote Ubongo wako unaweza tafuta majibu mazuri kadri unavyouongoza.
 
Nasalute kwamba leo kichwa changu kimegota na kukosa la kukushauri.....yataka moyo wa ziada hapa maana umepondeka na kuumia kuanzia kichwani hadi moyoni....pole
 
Wewe ungeweza kuvumilia iwapo mkeo angezaa Na mdogo wako ama kakako? Anyway kwenu mnautaratibu mzuri hongereni.

Dada yangu, African culture is male dominant! Hujui kuwa "Kuchapiwa ni siri ya ndani"? Kama ninampenda, i'll keep it silent till I die na wataniheshimu kwa hilo. Huyo mtoto atakuwa ni mwanangu na ole wake mtu anyanyue mdomo (That is IF I love her na alinipa sababu za kueleweka ilikuwaje akazaa na ndugu yangu, huenda ni uzembe wangu).
 
Kaa na mumeo kwa Mara nyingine tena muongee na akuombe msamaha naamini kama utamsamehe kwa mara nyingine tena huyo mumeo kwa aibu aliopata atakuwa mume mwema mbele zako
 
Pole dada ,
ulimwengu umeoza huu,hakuna hiyana wala utu kama zamani.ukweli kuishi na huyo mume ni kuishi kinyume na matarajio yako !
Afadhali hata angekuwa mtu baki....
Ushauri huu ni mzuri Ila hao bora walikua tayari Na watoto hivyo hata huyu Leah angekua Na watoto Na huyu jamaa hata Mimi ningemsihi amsamehe kwa ajili ya watoto lakini sasa hivi hana aaah bora asepe zake aisee.
 
Dada leah, mimi naanza kwa kukutupia wewe lawama, pili mumeo na tatu ni dogo lako.
wewe naona ndo ulie_create ili tatizo pasipo kujua, simanish tusikae na ndugu zetu kwenye ndoa la asha, lakin ulijisahau sana. tumezoea kusema wanawake ni dhaifu ila sio kweli, ila wanaume ndo tulio dhaifu sana. dogo pengine aliletewa vishawishi kwa akili yake na mazingira kama yale hasingeweza kuvikwepa mbele ya mumeo.

Lakini zingatia wew ndo uliesababisha mumeo amuone mdogo wako. na wanawake mlioajiriwa ndoa huwa mnashindwa kuzitekeza ipasavyo mwishowe matatzo kama hayo yanatokea, kwa kilichotokea si mdogo wako, hata angelikuwa house_girl, au rafik yako kama unaishi naye ingelitokea, hivo mwenye kosa ni mumeo lakin naye katengenezewa mazingira.

Kosa lingne husingewaita wazaz hapo ulikosea japo walichokushaur ungekitmiza wew pasipo tatizo, wew umefunga ndoa umekula kiapo basi timiza hicho kiapo, kama angelikuwa house girl uamuzi ungelimfukuza bila kujar chochote, japo ni ngumu lakin inawezekana kuish na mumeo vzur tena sana.
 
Mimi naona uachane na huyo mwanaume, kwasababu, hutoweza kuwa na mapenzi ya kweli kwa mtu aliyezaa na mdogo wako(au utaweza?)Afu kizuri zaidi ni kwamba bado hamjapata mtoto wewe na mume wako
 
Dah.
Hapo kuna mambo mawili inabidi yawekwe sawa.
  • Achana na huyo mume, kwa maana ya kuvunja ndoa, ukikubali kuendelea naye utapata majuto maisha yako yote na aibu ya milele mpaka unaenda kaburini, hilo ni donda zito sana katika maisha yako, huwezi kulibeba.
  • Pili hakikisha pia hata mdogo wako haolewi na jamaa, maana pia akiolewa bado itakuwa ni pigo kubwa sana kwako na maumivu yake huwezi kuyabeba pia, kifupi huyo jamaa na mdogo wako inabidi watengane kabisa tena kwa makubaliano maalumu ustawi wa jamii au polisi, mdogo wako kwa kukuingilia ndoa yako inabidi achague moja either aendelee na undugu na wewe kwa kuachana na jamaa au aendelee na jamaa kwa kuendelea na wewe.
Tatizo litakuja kwa mtoto atakayezaliwa, inabidi muweke makubaliano ya namna mtoto atakayezaliwa atalewewa na nani. Kama ni mama pekee baba asithubutu kuja hata kumjulia hali, kama ni baba pekee mama yake amkabidhi kwa baba yake na asahau kabisa kama aliwahi kuzaa.

Kinyume cha hapo hio ni aibu ya familia na audui mkubwa sana baina yenu ninyi wawili, mtu na dada yake
 
Dah.
Hapo kuna mambo mawili inabidi yawekwe sawa.
  • Achana na huyo mume, kwa maana ya kuvunja ndoa, ukikubali kuendelea naye utapata majuto maisha yako yote na aibu ya milele mpaka unaenda kaburini, hilo ni donda zito sana katika maisha yako, huwezi kulibeba.
  • Pili hakikisha pia hata mdogo wako haolewi na jamaa, maana pia akiolewa bado itakuwa ni pigo kubwa sana kwako na maumivu yake huwezi kuyabeba pia, kifupi huyo jamaa na mdogo wako inabidi watengane kabisa tena kwa makubaliano maalumu ustawi wa jamii au polisi, mdogo wako kwa kukuingilia ndoa yako inabidi achague moja either aendelee na undugu na wewe kwa kuachana na jamaa au aendelee na jamaa kwa kuendelea na wewe.
Tatizo litakuja kwa mtoto atakayezaliwa, inabidi muweke makubaliano ya namna mtoto atakayezaliwa atalewewa na nani. Kama ni mama pekee baba asithubutu kuja hata kumjulia hali, kama ni baba pekee mama yake amkabidhi kwa baba yake na asahau kabisa kama aliwahi kuzaa.

Kinyume cha hapo hio ni aibu ya familia na audui mkubwa sana baina yenu ninyi wawili, mtu na dada yake
Asawa kwa ushauri wako..nimekuelewa vizuri
 
Mimi naona uachane na huyo mwanaume, kwasababu, hutoweza kuwa na mapenzi ya kweli kwa mtu aliyezaa na mdogo wako(au utaweza?)Afu kizuri zaidi ni kwamba bado hamjapata mtoto wewe na mume wako
Asante kwa ushauri
 
Nimeelewa kwa nini unajiita leah2, lakini mbona huyo wajina lako pamoja na ndugue waliolewa na mwanamme mmoja!!?

Kama amekiri msamehe mmeo maisha yasonge au tayari umeshapotoshwa na wanaume wa dar!! angalia usije kuwa unaruka majivu then ukaangukia motoni

Elewa kuwa hakuna aliemkamilifu na hilo nijaribu tu, yakupasa ulishinde. Ebu rejea kiapo chenu cha ndoa

Samehe 7 X 70
 
Pole sana kwa maumivu hayo. Kwa chochote utachoamua kulingana na maono yako ni sahihi kwasababu wewe ndiye uliyekosewa. Una haki ya kuadhibu au kusamehe. Lakini pia lazima ujifunze makosa yako. Maamuzi ya kukataa kuzaa mpaka umalize shule hayakupaswa kuwa ya kwako pekee yako. Kama uliamua hivyo bila ridhaa ya dhati ya mumeo inawezekana hili tatizo umelipalilia mwenyewe.
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Once a cheater always a cheater. Hapo umejua uhusiano sababu ya mimba la sivyo ungeendelea kufanywa mjinga ndani ya nyumba yako mwenyewe. Bora kidogo ingekuwa mtu wa mbali lakini kama ni mdogo wako daima itakuwa ni kumbusho la usaliti maana uwezekano wa kukutana nae ni mkubwa. Hawana sababu ya kuwa maishani mwako.

Shukuru mungu hujazaa na huyo mwanaume maana ungezaa nae ingemaanisha daima ungekuwa na muungano nae kupitia mtoto. Inauma lakini muda ndio mganga wa yote. Utasahau na maisha yataendelea. Mungu akutangulie katika kipindi chote hiki.
 
dada leah, mim naanza kwa kukutupia wewe lawama, pili mumeo na tatu ni dogo lako.
wewe naona ndo ulie_create ili tatizo pasipo kujua, simanish tusikae na ndugu zetu kwenye ndoa la asha, lakin ulijisahau sana. tumezoea kusema wanawake ni dhaifu ila sio kweli, ila wanaume ndo tulio dhaifu sana. dogo pengine aliletewa vishawishi kwa akili yake na mazingira kama yale hasingeweza kuvikwepa mbele ya mumeo. lakin zingatia wew ndo uliesababisha mumeo amuone mdogo wako. na wanawake mlioajiriwa ndoa huwa mnashindwa kuzitekeza ipasavyo mwishowe matatzo kama hayo yanatokea, kwa kilichotokea si mdogo wako, hata angelikuwa house_girl, au rafik yako kama unaishi naye ingelitokea, hivo mwenye kosa ni mumeo lakin naye katengenezewa mazingira.
kosa lingne husingewaita wazaz hapo ulikosea japo walichokushaur ungekitmiza wew pasipo tatizo, wew umefunga ndoa umekula kiapo basi timiza hicho kiapo, kama angelikuwa house girl uamuzi ungelimfukuza bila kujar chochote, japo ni ngumu lakin inawezekana kuish na mumeo vzur tena sana
Daaah! Haya ngoja tuone
 
Dada angu, African culture is male dominant! Hujui kuwa "Kuchapiwa ni siri ya ndani"? kama ninampenda, i'll keep it silent till I die na wataniheshimu kwa hilo. Huyo mtoto atakuwa ni mwanangu na ole wake mtu anyanyue mdomo (That is IF I love her na alinipa sababu za kueleweka ilikuwaje akazaa na ndugu yangu, huenda ni uzembe wangu,).
Nakubaliana Na wewe kuchapiwa Na vitu vingine ingekua mimba kapewa binti mwingine uko mtaani ningemwambia avumilie tu lakini mdogo mtu chaaa hii ngumu.
 
Back
Top Bottom