Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Asante sana nao..kinachoniuma zaidi yeye anaona ni jambo la kawaida sana yaani hasumbuki..tangu nimegundua sijawahi kusikia neno nisamehe kutoka kwake zaidi ya kisema yaishe
Daah Leah hata kama utaamua kumsamehe huyu mmeo jipe muda kuanza kuishi nae kama mme.yaani angekua mwingine neno nisamehe/samahani zisingeisha mdomoni mwake
 
Imeandikwa samehe saba mara sabini, sisi wanaume ni mbwa.
7c0f4e49b9de2044e5d2c26e5ae5a065.jpg
 
Leah ninakusihi,km mwanandoa, hayo mabo yote mwachie, Mungu, kuna leo na kesho, pia husdiriki, kumwambia mdogo wako atoe mimba eti kisa kulinda soni yako na mmeo, mnajua mtakaye mmua angekuwa nani?na ni kwambie mdgo wako akifa wakati anatoa mimba, utajikisiaje? je wewe huspo zaa? na mtt wa mdogo wako yupo itakuaje? hacheni hizo, Leha mrudie mmeo, nendenei kanisani kaomba kumuona padri, nina imani mtashauriwa vizuri, sjui kwa nini naiona ndoa yenu km yakikatoliki lakini nakusihi, mrudie mmeo, huyo ndochaguo lako, ebu rejea ushauri wangu hapo juu, km nilizo zitaja ni weekneszao, work on it mamy!
 
Msamehe mumeo subiri mdogo wako ajifungue mlehe mtoto na mdogo wako akatafute mchumba aolewe ukimwacha mume itakuchukua muda mrefu sana kupata mwingine na visa ktk familia ukimwachia mdogo wako mume hawezi kuishi kwa amani na chuki kati yenu itaendelea mpaka kifo.Ila ukisamehe believe utakuwa umesolve mambo Mengi na umemshinda SHETANI. Pole na kila la kheri.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
mdogo wako alipokuita na kukuambia ukweli kwa kukuomba msamaha ulipaswa kumuelewa na kulifanyia kazi pale ulipowaita wote wawili. Ila kwa kuwaitia wazazi pande zote 2 ni wazi uliamua kuwaaibisha na kuwa vua nguo waziwazi. Ulipaswa kumuelewa mdogo wako kwann aliamua kukuelezea ukweli huku akijuta

Inawezekana sababu ya mumeo kuchepuka ni vile unavyoishi nae coz una mahitaji yote na uwezo ndo maana unampotezea na hata wazo la kupata mtoto baadae ukimaliza masomo inaonekana umempangia ww. Hivyo basi ni dhahiri kuna mengi unampangia zaidi ya hili kwani hata kielimu na kimaisha hakufikii tena ukizingatia nyumba ni yako.

Kwa nafasi ya elimu yako ulikuwa na uwezo wa kulimaliza hili jambo ulipokuwa na watuhumiwa kabla hujalipeleka juu zaidi kwa wazazi. Jitahidi kuwa mvumilivu ndani ya ndoa na kumaliza changamoto na mume wako kabla ya kupeleka nje kwa usuluhishi kwa shida na raha, matatizo na furaha.

Ndoa zina changamoto sana, usiwabebeshe mzigo wazazi wakupe ushauri wa kuachana nae.

Niwapongeze Wazazi wamekusihi sana umsamehe na muendelee na maisha ya ndoa sema HUJISIKII kuendelea kuishi na mwanaume huyo.
Mapenzi ni hisia na kama hujisikii ni bora ukae pembeni utakuja kujuta zaidi ya hivi.

Pole sana
 
Mmh, naona bora umwachie mdogo wako mume Tu, Mungu atakupa mwingine, maana huo uhusiona wao hautovunjika mapema, pili tayar wana mtoto hapo, pia ameonyesha uchafu wake mapema Sana ungali ukiwa hapo, chapa raba bidada
Kuna muda una akili [emoji51] [emoji51] [emoji51]
 
  • Thanks
Reactions: nao
Dada yangu leah2 ningependa ufwatwe ushauri wa mwisho wa Don Mangi na sifi leo... Wamesema na kuchambua vyema sana. Nami nasema USIVUNJE NDOA YAKO. No body is perfect under the sun. Unaweza kimbilia mume mwengine na huyo akaja kuzaa na Dada yako mkubwa (Kama yupo) ama akafanya kituko zaidi ya mumeo wasasa. Uvumilivu ndio ndoa. Hata sisi tupo kwenye hii taasisi. Ni ngumu sana. Mungu ndio hututangulia. Hakuna fundi wa ndoa leah2

Hongera kwa busara zako za kutafuta ukweli wa mambo. Heshimu mawazo na ushauri wa wazazi. Mwisho, hata Kama una mali kiasi gani, umekorofishana na mume kiasi gani, usiweke mipakano ya umiliki. Kwamba nyumba yangu hivyo toka! Gari langu usipande, bafuni peleka maji mwenyewe n.k. Hapana!

Busara ukiuongoze na uone kila kilichopo ndani ni chenu nyote, regardless. Usifukuze mume. Ni indication ya mwanamke jeuri na mwenye majivuno. Kwa maana ya kwamba siku ukimaliza PhD ukarudi home baba kachelewa basi kuna hatari ya yeye kulala nje au sitting room. Ni mbaya sana. Samehe. Piga moyo konde maisha yaendelee.

Goodluck Mshana
 
Mnaoshauri aachane na mumewe kuna mambo mawili kama si matatu:

1. Mumewe being desperate atamuoa huyo mdogo mtu (in which im not sure kama bado hajafanya hivyo) kawafukuza kwake na hajui walipokwenda. Mdogo mtu hana kazi, lazima atamtegemea shemeji mtu. Mume mtu ni mfanyabiashara, vi shilingi vya hapa na pale havimpigi chenga. In her life, she (leah) will never get away with this itakuja kuonekana ni mke alishindwa kumzalia mtoto and mume ended up eloping with her sister. Itakuuma zaidi kuliko kuachana na mumeo

2. Mtoto atakayezaliwa bado atakuwa anakupa uchungu, unless kama utakuwa na control juu ya ukuaji wake na aku acknowledge kama "mama mkubwa" point ambayo ukiachana na huyu mumeo hii heshima haitakuwepo tuu. A second thing you will not get away with it.

3. Undugu una heshima, utakapomrudisha mumeo nyumbani, utaset clear boundaries na ndugu yako kwamba una maamuzi juu ya ndoa yako kama mke wa ndoa,nafasi ambayo yeye hatakuwa nayo.

So uchaguzi bado ni wako, ila kwa upumbavu wangu naona madhara yakuachana ni ya muda mrefu na kidonda chake kitakuuma zaidi kuliko hilo lililotokea.

mkuu umeongea vizur sana! mimi kuna case km hii nimeisikia na kuishuhudia! iko hv......

jamaa alioa, sasa mkewe akapata ujauzito hivyo akaw mtu wa nyumbani! huyo mme yeye alikua anafanya biashara za kupeleka bidhaa dar!

baada ya mkewe kua mjamzito ikabidi sasa mdogo wa huyo mkewe awe anaenda nae dar kwa nia ya kumfundisha biashara! kwa udhaifu wa wanaume ulivo akampa nae mimba! so mtu na mdogo wke wakawa na mimba za mtu mmoja!

kilichotokea,wote wawili wakajifungua, sasa huyu mdogo mtu baada ya mtoto kukua akampeleka kwa dada yake(ambako ndo kwa baba wa mtoto wake)...... walipishana miez 5 tu kuzaliwa!

baadae huyu mdogo mtu alifariki, hvyo watoto wamekua pamoja! ukiwaona km mapacha vile! sasa mpk leo huyu aliezaliwa na mdogo ndo kasoma na ndio anailea familia yote baada ya baba yao kufariki!!......

SASA USHAURI WANGU HUYO DADA AJIFUNZE KWA HUYO MAMA NA MATUNDA YA UVUMILIVU ANAVUNA!.......
 
Ni kosa kubwa kumdhalilisha mumeo Wa ndoa kiasi hicho yeye si wakwanza au Wa mwisho, si bora amezaa na
Mdogo wako jee angezaa na mtu mwingine kabsa unge fanyaje, fumilia kwenye ndoa kuna mengi yako yananafuu, pili ukitaka ndoa idumu ondoka kwako mfuate mwanaume hata kinyume na hapo utakuwa kimada tu.Nafikir mtarudiana ila Mimi siwezi kurudi, mwanaume hapewi taraka
 
Leah ninakusihi,km mwanandoa, hayo mabo yote mwachie, Mungu, kuna leo na kesho, pia husdiriki, kumwambia mdogo wako atoe mimba eti kisa kulinda soni yako na mmeo, mnajua mtakaye mmua angekuwa nani?na ni kwambie mdgo wako akifa wakati anatoa mimba, utajikisiaje? je wewe huspo zaa? na mtt wa mdogo wako yupo itakuaje? hacheni hizo, Leha mrudie mmeo, nendenei kanisani kaomba kumuona padri, nina imani mtashauriwa vizuri, sjui kwa nini naiona ndoa yenu km yakikatoliki lakini nakusihi, mrudie mmeo, huyo ndochaguo lako, ebu rejea ushauri wangu hapo juu, km nilizo zitaja ni weekneszao, work on it mamy!
Arejee nn Andika vizuri
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Pole sana! Maamuzi uliyochukua ni sahihi kwa asilimia 100% hongera sana kwa kutokuwa mkurupukaji.. naamini kuanzisha upya sio ujinga, usijali jamii itakuchukulia vipi maumivu yako haiwahusu hiyo jamii .. keep calm and move on.
Hapo umeongea pointi kabisa, hata mi simshaur arudiane nae
 
Ni kosa kubwa kumdhalilisha mumeo Wa ndoa kiasi hicho yeye si wakwanza au Wa mwisho, si bora amezaa na
Mdogo wako jee angezaa na mtu mwingine kabsa unge fanyaje, fumilia kwenye ndoa kuna mengi yako yananafuu, pili ukitaka ndoa idumu ondoka kwako mfuate mwanaume hata kinyume na hapo utakuwa kimada tu.Nafikir mtarudiana ila Mimi siwezi kurudi, mwanaume hapewi taraka
Aisee nimekutana Matusii mengine sana
 
Nakupongeza Dada kwa uhamzi uliouchukua zaidi Muombe Mungu akupe busara na ujasiri ili uweze kufanya maamzi sahihi. Ambayo hutojutia ningekuwa Mimi mme natupa kule amchukue tu Mdogo wangu.
Pia wadada tujifunze hizi issue za kukaa na wadogo eti oooh anatafuta kazi tuziangalie kwa jicho la Pili......Mungu akupiganie dadangu
 
Back
Top Bottom