kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
3,058
8,726
Rais Mseven wa Uganda amekutana na ujumbe wa serikali ya Tanzania ambao umeongozwa na mtoto wa wa kiume wa Rais Samia.

Uzuri wa taarifa hii imethibitishwa rasmi na ofisi ya Mseveni mwenyewe kupitia akaunti ya raisi.

Swali- mtoto huyu wa rais wetu, ana cheo gani serikalini?

Kama taarifa hii isingetolewa na Mseveni, tungetangaziwa na ofisi gani huku Tanzannia?

Swali la kujiuliza pia,mambo mangapi mtoto huyu amekua ameyafanya kwa kutumia kodi za Taifa na pasi na taarifa kuwekwa wazi kwa umma?!!

Ni wazi kua mtoto huyu anafanya haya kwa ruksa ya Rais Samia ambae ni mzazi wake,je huu sio uvunjaji wa katiba?

NB: Imewahi kuandikwa tetesi kua kijana fulani amefungua ofisi Dubai kwenye kasri mojawapo na kua hata DP WORLD ni moja wapo ya mradi wake/wao na waarabu!!.

Kuhoji haya ni kwa nia njema,kama kijana ana kampuni zake za biashara iwekwe wazi Ila pia na wahusika wapime kama yanayofanywa yanatoa taswira hasi ama kua familia imekaa kibiashara tu?

20230812_140727.jpg
20230812_140753.jpg
Screenshot_20230812-140813.png
 
Back
Top Bottom