Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Uongo mbaya jamaa ameshajichanganya! Aliacha kazi ili afungue kampuni ya upimaji ardhi yenye ofisi masaki halafu anasema yupo mbeya!
-Wewe popoma, acha ushabiki, mimi nilikuwa namzingua tu mr Liverpool,
  • Na sikusema kuwa Niko mbeya nilimtania kuwa Niko Njombe kwenye bar inaitwa Mwechimpya, hiyo bar nimeijua kwa sababu nilisha kwenda Njombe kufanya upimaji ardhi, nilikuwa nakunywa hapo bia jioni
  • Ni kweli nilikuwa Mpima ardhi muandamizi nilikuwa naelekea kuwa principal land surveyor,
  • Nimefungua ofisi iko Masaki kama hutaki basi kaa usubiri makombo ya CCM ambayo hayafiki hata 4m
 
Labda kasafiri
  • mimi nilikuwa namzingua tu Liverpool,
  • mimi taaluma yangu ya upimaji ardhi Ina hela, hata nilipokuwa Manispaa nilikuwa napata hela nyingi (halali) kutokana na kufanya upimaji ardhi kwa watu binafsi, nilikuwa sipigi mayowe tarehe kama hizi kama kina Liverpool
  • wengi mnaopiga mayowe tarehe hii, wengi mmesomea zile taaluma zisizoweza kukuingizia hela
 
Mr. Bilionea, emu tutajie jina la Ofisi yako hapo masaki pamoja na location tuje kufanya Consultation
  • una hela ya kulipia consultation?, huo mshahara unaopata huwezi kunilipa
  • Nafanya consultancy za mashirika mbalimbali, makampuni mbalimbali, na ambapo consultancy 1 si chini ya 5,000,000/- unayo?
 
Nasisi Mtukumbuken basi tayari huku,
H ni 62,400 ongezeko,Kwa mujibu wa mdau alie daraja Hilo.
Slip sALARY NAONA ZIMEGOMA.
 
Wakuu, huu ndo mfano halisi wa kujitia umasikini kupitia Top Up.
Angalia hapa chini mahesabu ya jamaa mmoja alikua na mkopo wa M 29 akataka Top up, ambapo kwa mshahara wake kikomo cha mkopo wake ni M 35.

Sasa aka Top up, kwa kupewa M 5.2 alafu Deni likasoma M 58 kwa miaka 10 yaani deni likaongezeka mara 2 ya lile deni la awali la M 29 tena kwa miaka 10 mbele alafu wewe unapewa M 5.2
Hii ni maajabu ya ukope 5.2m ulipe 29m Duu noma
 
Ninachogundua ni kwamba pamoja na mishahara midogo kwa ndugu zetu wafanyakazi ila bado serikali inawanyanyasa katika kuwawekea limit katika mishahara yao ambayo ni midogo ndo maana watumishi wetu wanaumia na top up maana unamkuta mtumishi hana option nyingine kupitia kiwango chake cha mshahara alichonacho.

Huyu aliependekeza watumishi kukopa moja ya tatu (1/3) ya mshahara ndo mchawi mkubwa wa watumishi.

Zamani mbona huu ujinga ulikua haupo na watumishi walikopa na kuendelea na maisha yao bila shida kupitia taasis za kifedha mbalimbali.

Sasa hii sheria ya moja ya tatu ndo imekua janga kwa watumishi mpaka kwenda kwenye mikopo ya kausha dam.

Mtumishi apewe uhuru ,mshahara kwake ndo chanzo muhim kwake cha mapato, limiti iwe asikope chini ya elfu 50 basi mengine tumwachie mwenyewe ili hali anatimiza majukum yake , hii itawasaidia sana watumishi kuepukana na mikopo ya kausha dam, madam hakuna mtumishi ambae amewahi kwenda kumfuata mwajiri kwamba ameshindwa kujikimu .
 
Back
Top Bottom