Msaada: Mke wangu hataki kusuka wala kununuliwa nguo nzuri

Duh una bahati ya kumpata wife material ambao ni ki kizazi ambacho kinapotea duniani lakini ana bahati mbaya kampata mwanaume ambaye amejaza makamasi kichwani. Watu wanahangaika wapate wapi wa namna hiyo ambao wapo bize na watoto, miradi na tayari walishakana usichana wapo kifamilia zaidi na hata maisha yakidunda mjini mnaweza kwenda kijijini kuanza moja na mkaishi wewe akili yako ipo kwa magumegume ya mjini ambayo yanapenda kujiremba ili kuendelea.......
Yaaan anashangaza kwa kweli huyu mtu
 
Huyo ndio mke acha utoto. Una miaka mingapi?
Wekeza hela kwenye maendeleo, maadam anaoga ,anafua bra na pichu mengine ingiza mzigo site.

Kama ulioa wa matumizi nenda kwa mpalange
 
Wakuu habari.

Nimeoa na nina mwaka na nusu wa ndoa sasa. Nina tatizo ambalo ninahitaji ushauri kwa wazoefu. Binafsi napenda mwanamke anayependeza na kujijali, na napenda awe mke wangu ili nisilazimike kutoka huko nje kuchepuka.

Sasa nina mke wangu hapendi kusuka, yaani kichwani yupo rough, mara chache (mara moja kwa miezi minne hivi) ndio huwa anakubali kwenda saluni kusuka tena kwa ugomvi.

Hela za saluni kila mwezi natenga elfu hamsini hadi sabini hivi (kwa uwezo wangu wa kipato) ila mtihani ni kumshawishi akubali. Mara kadhaa nimejikuta natembea na vibinti vinavyopendeza au vinavyokubali nivipendezeshe nje ila hili linanikwaza sana maana sipendi kumsaliti. Hata kumtoa kwenda kununua nguo nzuri hataki mara nyingi.

Nahitaji ushauri namfanyaje huyu mke wangu ili moyo wangu uweze kutulia.

Asanteni.
Kwa mawazo yako mkuu unaweza hata kumulazimisha ajichumbue

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu habari.

Nimeoa na nina mwaka na nusu wa ndoa sasa. Nina tatizo ambalo ninahitaji ushauri kwa wazoefu. Binafsi napenda mwanamke anayependeza na kujijali, na napenda awe mke wangu ili nisilazimike kutoka huko nje kuchepuka.

Sasa nina mke wangu hapendi kusuka, yaani kichwani yupo rough, mara chache (mara moja kwa miezi minne hivi) ndio huwa anakubali kwenda saluni kusuka tena kwa ugomvi.

Hela za saluni kila mwezi natenga elfu hamsini hadi sabini hivi (kwa uwezo wangu wa kipato) ila mtihani ni kumshawishi akubali. Mara kadhaa nimejikuta natembea na vibinti vinavyopendeza au vinavyokubali nivipendezeshe nje ila hili linanikwaza sana maana sipendi kumsaliti. Hata kumtoa kwenda kununua nguo nzuri hataki mara nyingi.

Nahitaji ushauri namfanyaje huyu mke wangu ili moyo wangu uweze kutulia.

Asanteni.
Sasa wakati mnakutana hadi mkapendana, uchumba mpaka akaja kuwa mkeo haya yote ulikuwa huyaoni??
 
Sasa ilikuaje akawa mkeo? Means hata wakati wa uchumba alikua hivyo.

Kuna watu wana bahati na hawajui kuzitumia.
 
Wakati wa urafiki, uchumba mpaka mnaingia katika ndoa alikuwaje? Je kabadilika tuu ghafla?
 
Umeshajaribu kwenda kupima ujauzito. Kama anao unaweza kuwa chanzo maake unakujaga na mambo kibao
 
Kuna wakati tunafunga mbuzi na kuondoka tukiamin cc co mbuzi kumbe yawezekana cc n mbuzi zaid ya mbuzi ,70k aah !,
 
Back
Top Bottom