Msaada: Mke wangu hataki kusuka wala kununuliwa nguo nzuri

Woga tupa kulee

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
1,752
1,311
Wakuu habari.

Nimeoa na nina mwaka na nusu wa ndoa sasa. Nina tatizo ambalo ninahitaji ushauri kwa wazoefu. Binafsi napenda mwanamke anayependeza na kujijali, na napenda awe mke wangu ili nisilazimike kutoka huko nje kuchepuka.

Sasa nina mke wangu hapendi kusuka, yaani kichwani yupo rough, mara chache (mara moja kwa miezi minne hivi) ndio huwa anakubali kwenda saluni kusuka tena kwa ugomvi.

Hela za saluni kila mwezi natenga elfu hamsini hadi sabini hivi (kwa uwezo wangu wa kipato) ila mtihani ni kumshawishi akubali. Mara kadhaa nimejikuta natembea na vibinti vinavyopendeza au vinavyokubali nivipendezeshe nje ila hili linanikwaza sana maana sipendi kumsaliti. Hata kumtoa kwenda kununua nguo nzuri hataki mara nyingi.

Nahitaji ushauri namfanyaje huyu mke wangu ili moyo wangu uweze kutulia.

Asanteni.
 
Pole sana...endelea kumshawishi na endelea kumwambia wewe unapendelea Mkeo aweje....na kabla ya kuoana alikuwa hivyo hivyo au kabadirikia ndani ya ndoa baada ya kugundua wewe na yeye ni kufa na kuzikana!?
Kabadilika baada ya ndoa. Ninajaribu kuongea nae ila haambiliki na ukizingatia mimi pia sio muongeaji ki hivyo
 
Wakuu habari. Nimeoa na nina mwaka na nusu wa ndoa sasa. Nina tatizo ambalo ninahitaji ushauri kwa wazoefu. Binafsi napenda mwanamke anaye pendeza na kujijali , na napenda awe mke wangu ili nisilazimike kutoka huko nje kuchepuka. Sasa nina mke wangu hapendi kusuka, yaani kichwani yupo rough, mara chache
Huyo mwanamke ni mzuri sana mkuu mtunze.Anakupunguzia operation cost.

By the way,unaweza nunua nguo nzuri kama surprise akate mwenyewe kuzivaa .

Ila hiyo ya kutoka nje kwa sababu ya mke wako hasuki,haiko solid,wewe ni mchepukaji full stop mwenye tamaa mbaya.Ila umepata good excuse.Mpaka unamuoa inamaana ulishajua kwamba yukoje nini.Nadhani wakati unamuoa maisha yako yalikuwa chini,na ulizipenda hizi tabia zake za kuwa simple.Sasa hivi umepata mihela ghafla na unataka kumbadilisha mwenzio haraka.
 
Back
Top Bottom