Ushauri: Tumeachana hataki nimuone mtoto, nifanyeje?

Vivan cappatinho

JF-Expert Member
Mar 25, 2018
269
230
Habari,

Mimi ni kijana wa miaka 28 ambae bado sina mbele wala nyuma kwenye maisha yangu, bado najitafuta ila uhakika wa kipato kiasi ninao. Changamoto yangu ni kwamba nilikuwa naishi na mwanamke kama mume na mke na tulibahatika kupata mtoto mmoja wa kike kwasasa ana mwaka na miezi 6, kwa bahati mbaya nilipoteza kazi sehemu niliokuwa nafanya, hali ya maisha ikawa ngumu akiba yote ikaisha nikabakiza elfu 20000 tu.

Nikawa sina muelekeo nikarudi kuanza kubet ikiwa imebaki kama 8000 tu, nikaweka elfu 3000 kwenye account ya kubet nikaliwa 1300 ikabaki mia 700. Pressure ikawa juu sana, nikabetia hasira Mungu akabariki nikala laki na 9700 kidogo ndani mambo yakawa sawa.

Nikachukua laki nikaanza biashara ya dagaa na mke wangu akaanza kuuza karanga za mboga wote tukiwa kwenye soko moja na meza moja na tukiwa tunaamka saa 10 usiku kwenda kutafuta usafiri tunafika saa 12 kasoro.

Niweke wazi, mke wangu alipata wateja wengi sana kwenye biashara yake sababu alikuwa eneo zuri na peke yake, ila upande wangu nilipitia changamoto kwenye kuuza dagaa maana tulikuwa eneo moja wauza dagaa kama 13, baadae ilibidi nisubiri wenzangu kama wanne wauze wamalize na me ndio niuze.

Siku moja mke wangu alisaga karanga kilo 15 hazikutoka vizuri, msagaji akamshauri aweke maji baada ya hapo zikavunda akawa kapata hasara kubwa, maana kipindi icho karanga kilo ilikuwa 4000 (ulikuwa mwezi wa 3) so nikaamua kuvunja biashara yangu na mtaji wote nimpe mke wangu kwa maana yeye alikuwa na wateja wengi kuliko mimi na hata faida yake ilikuwa mara 3 ya faida yangu.

Mimi nikaenda sehemu moja inaitwa Mwaloni watu wa Mwanza wanapajua, nikaanza kujitafuta na niweke wazi tu nilikuwa sili asubuhi na mchana na jioni, nlikuwa narudi nyumbani na 3000 ama 4000 hapo ukitoa nauli inabaki 2500 ama 3500 na shida ndio zilianzia hapo, maana yeye anaweza pata kwa siku elfu 20 hadi 25 na anadeal kuvaa yeye na mtoto.

Kuanzia hapo maelewano yakawa mabovu, ndani hakuna amani, ilifika kipindi hakuna sex hata week mbili na ikitokea basi yeye ndio kataka na mbaya zaid ndani nilikuwa sina sauti nikawa napangiwa kila kitu na maamuzi nafanyiwa.

Kiukweli nilikuwa naumia sana, mwanamke nampenda sitaki kumuacha na kila nikiongea nae hataki kuelewa. Siku moja alinitukana nikampiga na ndio ikawa safari ya kuvunja mji, maana kwa week tukawa tunaongea mara moja na yenyewe akiwa anataka msaada wa kitu.

Nilijikaza kwa mambo yote haya nikiwa naona aibu nitamwambia nani, badae nikashindwa ikabidi niongee na ndugu zangu wakaongea nae lakini hakuna kitu ilisaidia. Maana alikuwa anawakubalia na kujifanya yameisha ila wakiondoka tu anaendelea alipoishia.

Hii ilinichosha nikaongea na wazazi wake, dakika ya mwisho alinambia anajutia kuzaa na mimi na alifanya kosa na akawa anarudia rudia hili neno mara kwa mara. Mwisho kabisa ni week kadhaa zilizopita niliamua kuondoka kwangu nikamuachia kila kitu, nikabeba nguo tu na alinambia kama nataka kuondoka niwaishe anataka kufunga mlango alale.

Kiukweli kwasasa nina amani na Mungu kabariki kidogo naweza kumudu mahitaji ya kila siku na akiba ikabaki, ila changamoto ni moja tu inayonifanya nishindwe kujielewa, mke wangu nimeambiwa kamuachisha mtoto kumnyonyesha na kampeleka kwa bibi yake.

Roho yangu inauma natamani niwe namuona mtoto wangu kila muda na nipo tayari kuwa napeleka matumizi ya mtoto kwao na mke wangu, lakini mama mkwe wangu hataki kuniona na hataki nimuone mtoto japokuwa wakati nataka kuondoka kwangu niliwajulisha kila kitu ila mama mkwe alikuwa upande wa binti yake na alinijibu vibaya kwa kumtetea mtoto wake mmoja na wapekee.

Mwisho, naomba ushauri kwa wakubwa zangu natakiwa nifanye nini maana ndugu zangu wananishauri vibaya eti niachane na mtoto akikua atanitafuta na mimi nashindwa kuvumilia.
 
img_1_1651152978059.jpg
 
Pambania damu yako mkuu, usimuachie mama amlee pekee yake hawa wadada wa sasa akili zao zimekaa tenge kweenye malezi hasa wakiwa pekee yao.

NB. Kuweka picha yako sikupingi ni uamuzi wako, ila kuweka ya mtoto huku hujatenda kwa hekima. Umemkosea huyo mtoto, wewe umefanya kwa wema ila huku ni baharini kuna kila aina ya watu hadi Mapedo/Pedophiles.
 
Pambania damu yako mkuu, usimuachie mama amlee pekee yake hawa wadada wa sasa akili zao zimekaa tenge kweenye malezi hasa wakiwa pekee yao.

NB. Kuweka picha yako sikupingi ni uamuzi wako, ila kuweka ya mtoto huku hujatenda kwa hekima. Umemkosea huyo mtoto, wewe umefanya kwa wema ila huku ni baharini kuna kila aina ya watu hadi Mapedo/Pedophiles.
Sorry mkuu hata sikujua nitafuta
 
Ni kweli mkuu Mungu aliniokoa na kubeti sio kitu nachofanya ni mara moja moja sanaa tena kwa kufata mkumbo
Achana na mkumbo ukishaanza kubeti kwa maisha uliyonayo utapitia hali ngumu sana kuyaona mafanikio bora hizo senti uwe unatuma redio maria mkuu
 
Habari. Mimi ni kijana wa miaka 28 ambae bado sina mbele wala nyuma kwenye maisha yangu bado najitafuta ila uwakika wa kipato kiasi ninao...
Nakupa ngumu kumeza.
Anza maisha upya, futa picha ya huyo mwanamke na mtoto wake kwenye akili yako na uanze kujijenga kuwa Mwanaume bora zaidi, panga mipango ya kibiashara na uyatimize, weka nyege pembeni kwa muda.

Usijionyeshe uko desperate kumuona mtoto wako, fanya kama umesahau na endelea na maisha yako, itafika kipindi watajileta wenyewe, mpokee mtoto ila usirudiane na mwanamke maana umemuona Kila rangi zake, usifanye kosa la kumrudia, mhesabie kama mzazi mwenzako.

Mungu akikufanikisha , uoe kabisa mwanamke mwingine na tengeneza familia upya.
Kuwa Mwanaume, Lia kidogo na usonge mbele maana vita bado mbichi.
 
Back
Top Bottom