kingkimwe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,966
- 2,636
Njoo tabata
Sikushauri kuna wezi wa tv balaa nliibiwa tv Tatu ndani ya mwezi lbd tabata segerea na kinyerezi ila uku barakuda ni balaa
Njoo tabata
Tabata nako sio mbaya, kule ni kwa wala bata kumetulia sana, ila kuamka kwenda kazini ni saa 11 asubuhi
Zipohivi kuna self contained sinza (master room) ya kuanzia laki moja..
Huku akiosha macho jinsi ndege inavyoshuka na kupaa pale JNIAKaribu buza sigara upate upepo mwanana
Kazini wapi?? Buguruni au umekariri kazini lazima pawe posta mpyaTabata nako sio mbaya, kule ni kwa wala bata kumetulia sana, ila kuamka kwenda kazini ni saa 11 asubuhi
Buguruni kwa Mnyamani,Vingunguti,Ukonga Stakisharinipe suggestion yako boss
Kibamba LuguruniToa specifications za nyumba kama vyumba vingapi, kuwe na nini, house rent Tsh kwa mwezi, kama unataka geti, njia ya gari, n.k.
Hao wanaokuambia Goba, Ubungo, na kwingineko bila kutaja Goba ipi ubungo ipi watakuingiza chaka.
Kila Sehemu kuna pazuri na pabaya isipokuwa Masaki na Oyster Bay tu hakuna pabaya ila gharama ndiyo kubwa.
Duka mbili naunga mkonoTemeke hasa mwisho, uwanja wa taifa mpaka chang'ombe maduka mawili/uhindini/unubini.
Goba ni Squatter areakaa GOBA mkuu
Akaishi Ubungo kibangu hamna uswahili
Nipo nawe. Me mwenyewe naishi ubungo kibangu
Nadhani alimaanisha Mbezi ya KimaraKumbe mbezi beach sio gharama sana?
Ukisema kigamboni kwa ujumla utakuwa umedanganya. Huko hata Uber hakuna, ukiita zinatokea posta, wakijua ulipo ni mbali hawaji.Njoo uishi kigamboni nitakupa na sababu. Before mm nilikuwa naishi sinza, maisha ya sinza kwa kijana anaetaka kuwa na Mae ndeleo sio pazuri hata kidogo...kwa sababu kuna vishawishi vya kila aina kuhusu swala zima la starehe.
Pili aina kubwa ya watu utakakutana nao sinza, sio watu wa kukupa mawazo ya kimaendeleo wengi wao wanawaza starehe na kuvaa. Kama ujuavyo Mazingira yananguvu kubwa sana ya kubadilisha maisha ya mtu.
Nije kwenye point kwa nini kigamboni.
1. Ni mji unandelea kukua kwa kasi hivyo nirahisi ukiwa mkazi wa huku kununua eneo lako (Kiwanja) kwa ajili ya kuandaa makazi yako ya kudumu.
2. Huduma zote muhimu zinapatikana kama vile Maji, umeme, Hospitali n.k
3. Aina ya watu waliowengi waishio kigamboni ni watu wa kipato cha kati na juu, hivyo nirahisi kuwa na motisha ya kimaendeleo.
4.Usafiri unapatikana 24hrs , pia ni karibu na mjini hivyo nirahisi kufanya mambo yako kirahisi zaidi.
5. Ni mji wenye mipango mikubwa sana ya maadae, kiufupi ndio itakuwa Miami ya Dar es salaam hivyo ukifanikiwa kujenga makazi ya kudumu kigambonk i swear huwezi kujuta baadae.
6. Mazingira ya maeneo mengi ni ya kuvutia nyumba nyingi zimejengwa kisasa...hivyo hata akija mgeni wako uko proud ukiamini unakaa mazingira mazuri.
7. Ni sehemu yenye usalama, uhalifu huwezi kukosekana sehemu yoyote lakini kuna kuzidiana ukifwatilia matukio ya kiuhalifu kwa mkoa wa Dsm kigamboni utaisikia mara chache sana.
Kwa hayo machache nafikiri unaweza kufanya maamuzi mazuri.
KARIBU SANA KIGAMBONI MKUU.
Kweli kabisahii ndio pointi ya msingi maeneo mengi ya dsm yanafanana fanana, na ni kawaida mji huu kukuta jirani kajenga ghorofa pembeni nyumba ya vyumba viwili, ama huyu anaishi kizungu kabisa halafu jirani anaishi kiswahili kimtaani kabisa, la msingi anagalia umbali wa unapokaa na kazini, ila lifestyle ni maamuzi yako na aina ya nyumba uliyopanga maana hata hiyo manzese yenye tandale kuna watu wamepanga apartment mpya mpya za barabarani na morogoro road , wako karibu na mwendokasi wako karibu na mjini na ubungo haf ni manzese hiyohiyo