Msaada: Maeneo mazuri ya kuishi Dar es Salaam

Msaada: Maeneo mazuri ya kuishi Dar es Salaam

Kama utawekeza Mwenge sehemu Nzuri kupanga

Usizo tumia usafiri
1)Sinza
2)Mwenge
3)Mikocheni..
4Mawasiliano

Utazo tumia usafiri (umbali mfupi)
1)Kijitonyama
2)Ubungo
3)Mawasiliano
4)Mwananyamara

Katika sehemu hizo nashauri upange SINZA kutokea Mlimanicity unaingia ndani kidogo kuna eneo lina sifa zote tajwa.
 
Habari wana JF,

Kwa wale Wana-Ndugu ambao wanaifahamu Dar es Salaam vizuri, ni Maeneo au Mitaa gani ya kuishi (kupanga nyumba/chumba) ambayo yanalandana na sifa zifuatazo?

1. Sio maeneo ya uswazi/uswahilini
2. Sio pakishua sanaa/Expensive estate
3. Hayana matukio makubwa ya wizi na vibaka
4. Hakuna tatizo la maji tiririka
5. Upatikanaji wa karibu wa huduma za kijamii na kiuchumi. (maji, kiosk, etc)
6. Inaweza kuwa nje ya mji ila isiwe mbali sanaa na mjini kivile
7. Haikumbwi na mafuriko wakati wa mvua

Ahsante.
SINZA
 
Kama una usafiri private Tabata kuzuri sana baadhi ya maeneo, usiende Taba ya mbali huko Segerea.
Au shughuli zako kama zipo Ilala-CBD Tabata kupo vizuri tu.
tabata ipi ni nzuri na siyo ya mbali
 
Kaaa Sinza Kwa usalama wako, huko goba utachinjwa mchana kweupeeee, Sinza Hakuna wizi utarud hata saaa tisa usiku utatembea Kwa mguuu kila mahali taa zinawaka hakuna vibaka na sio uswahilini na kuna raha Sana Sinza kuliko eneo lolote la dar kwa wale wenye starehe za Kati na maisha ya Kati
 
ahsante joyce...
 
kaa GOBA mkuu
Goba ni sehem tulivu ila inategemea shughuli zake anafanyia wapi.
Kama shughuli zake anafanyia maeneo ya kawe,mwenge,makumbusho ni sawa haitamcost sana kwenye ya usafiri.
Lakini pia goba kuna wezi wa kuvunja magrill/madirisha halafu wanazama ndani na kuhamisha vitu vyote vya kubebeka kirahisi mfano Flat tv,subwoofer,radio,pesa,na begi za nguo.
wanakuachia vitanda na makochi.
 
Back
Top Bottom