Msaada: Maeneo mazuri ya kuishi Dar es Salaam

Msaada: Maeneo mazuri ya kuishi Dar es Salaam

Njoo uishi kigamboni nitakupa na sababu. Before mm nilikuwa naishi sinza, maisha ya sinza kwa kijana anaetaka kuwa na Mae ndeleo sio pazuri hata kidogo...kwa sababu kuna vishawishi vya kila aina kuhusu swala zima la starehe.

Pili aina kubwa ya watu utakakutana nao sinza, sio watu wa kukupa mawazo ya kimaendeleo wengi wao wanawaza starehe na kuvaa. Kama ujuavyo Mazingira yananguvu kubwa sana ya kubadilisha maisha ya mtu.

Nije kwenye point kwa nini kigamboni.

1. Ni mji unandelea kukua kwa kasi hivyo nirahisi ukiwa mkazi wa huku kununua eneo lako (Kiwanja) kwa ajili ya kuandaa makazi yako ya kudumu.

2. Huduma zote muhimu zinapatikana kama vile Maji, umeme, Hospitali n.k

3. Aina ya watu waliowengi waishio kigamboni ni watu wa kipato cha kati na juu, hivyo nirahisi kuwa na motisha ya kimaendeleo.

4.Usafiri unapatikana 24hrs , pia ni karibu na mjini hivyo nirahisi kufanya mambo yako kirahisi zaidi.

5. Ni mji wenye mipango mikubwa sana ya maadae, kiufupi ndio itakuwa Miami ya Dar es salaam hivyo ukifanikiwa kujenga makazi ya kudumu kigambonk i swear huwezi kujuta baadae.

6. Mazingira ya maeneo mengi ni ya kuvutia nyumba nyingi zimejengwa kisasa...hivyo hata akija mgeni wako uko proud ukiamini unakaa mazingira mazuri.

7. Ni sehemu yenye usalama, uhalifu huwezi kukosekana sehemu yoyote lakini kuna kuzidiana ukifwatilia matukio ya kiuhalifu kwa mkoa wa Dsm kigamboni utaisikia mara chache sana.

Kwa hayo machache nafikiri unaweza kufanya maamuzi mazuri.

KARIBU SANA KIGAMBONI MKUU.

Bro naomba bei za viwanja kigamboni.
 
Habari, vipi kuhusu mahali wanaita kwa AZIZ ALLY changamoto zake ni zipi hasa kwa upande wa usafiri, usalama pamoja na huduma muhimu kama umeme na maji?
 
Kweli
1.Sio pa kishua sana pia sio uswazi
2.Hakuna matukio ya wizi na ya ajabu ajabu
3.Hakuna tatizo la maji kabisa
4.Upatikanaji wa huduma za kijamii upo karibu Hasa hicho kiosk/usafiri upo/mandhari nzuri/upepo mwanana tena huku kibangu juu unaona City view yote
5.Hapajawahi kukumbwa na mafuriko hata siku
6.Hakuna uswahili uswahili kila mtu na maisha yake
 
Back
Top Bottom