Msaada: Maeneo mazuri ya kuishi Dar es Salaam

Msaada: Maeneo mazuri ya kuishi Dar es Salaam

Habari wana JF,

Kwa wale Wana-Ndugu ambao wanaifahamu Dar es Salaam vizuri, ni Maeneo au Mitaa gani ya kuishi (kupanga nyumba/chumba) ambayo yanalandana na sifa zifuatazo?

1. Sio maeneo ya uswazi/uswahilini
2. Sio pakishua sanaa/Expensive estate
3. Hayana matukio makubwa ya wizi na vibaka
4. Hakuna tatizo la maji tiririka
5. Upatikanaji wa karibu wa huduma za kijamii na kiuchumi. (maji, kiosk, etc)
6. Inaweza kuwa nje ya mji ila isiwe mbali sanaa na mjini kivile
7. Haikumbwi na mafuriko wakati wa mvua

Ahsante.
Nyumba ya kupanga ukienda Mbali sana Mbezi beach,otherwise tafuta Mikocheni,Kijitonyama,Victoria,Makumbusho,Kinondoni block 41.
 
Habari wana JF,

Kwa wale Wana-Ndugu ambao wanaifahamu Dar es Salaam vizuri, ni Maeneo au Mitaa gani ya kuishi (kupanga nyumba/chumba) ambayo yanalandana na sifa zifuatazo?

1. Sio maeneo ya uswazi/uswahilini
2. Sio pakishua sanaa/Expensive estate
3. Hayana matukio makubwa ya wizi na vibaka
4. Hakuna tatizo la maji tiririka
5. Upatikanaji wa karibu wa huduma za kijamii na kiuchumi. (maji, kiosk, etc)
6. Inaweza kuwa nje ya mji ila isiwe mbali sanaa na mjini kivile
7. Haikumbwi na mafuriko wakati wa mvua

Ahsante.
Kijitonyama!
 
Temeke hasa mwisho, uwanja wa taifa mpaka chang'ombe maduka mawili/uhindini/unubini.
Unubini ipo ya uswahilini ambayo ni Noma io!!!bora useme Chang'ombe mazongela street anyoonyeshe ad uko maduka mawili...ayo maeneo fresh kuishi
 
Njoo uishi kigamboni nitakupa na sababu. Before mm nilikuwa naishi sinza, maisha ya sinza kwa kijana anaetaka kuwa na Mae ndeleo sio pazuri hata kidogo...kwa sababu kuna vishawishi vya kila aina kuhusu swala zima la starehe.

Pili aina kubwa ya watu utakakutana nao sinza, sio watu wa kukupa mawazo ya kimaendeleo wengi wao wanawaza starehe na kuvaa. Kama ujuavyo Mazingira yananguvu kubwa sana ya kubadilisha maisha ya mtu.

Nije kwenye point kwa nini kigamboni.

1. Ni mji unandelea kukua kwa kasi hivyo nirahisi ukiwa mkazi wa huku kununua eneo lako (Kiwanja) kwa ajili ya kuandaa makazi yako ya kudumu.

2. Huduma zote muhimu zinapatikana kama vile Maji, umeme, Hospitali n.k

3. Aina ya watu waliowengi waishio kigamboni ni watu wa kipato cha kati na juu, hivyo nirahisi kuwa na motisha ya kimaendeleo.

4.Usafiri unapatikana 24hrs , pia ni karibu na mjini hivyo nirahisi kufanya mambo yako kirahisi zaidi.

5. Ni mji wenye mipango mikubwa sana ya maadae, kiufupi ndio itakuwa Miami ya Dar es salaam hivyo ukifanikiwa kujenga makazi ya kudumu kigambonk i swear huwezi kujuta baadae.

6. Mazingira ya maeneo mengi ni ya kuvutia nyumba nyingi zimejengwa kisasa...hivyo hata akija mgeni wako uko proud ukiamini unakaa mazingira mazuri.

7. Ni sehemu yenye usalama, uhalifu huwezi kukosekana sehemu yoyote lakini kuna kuzidiana ukifwatilia matukio ya kiuhalifu kwa mkoa wa Dsm kigamboni utaisikia mara chache sana.

Kwa hayo machache nafikiri unaweza kufanya maamuzi mazuri.

KARIBU SANA KIGAMBONI MKUU.
 
Back
Top Bottom