Msaada: Maeneo mazuri ya kuishi Dar es Salaam

Msaada: Maeneo mazuri ya kuishi Dar es Salaam

Hapo si ndio kwa wandengereko na wamatumbi? Bora usogee kijichi aisee.
Naona unatafutwa kurogwa bila sababu za msingi..

Hapo ukiwa nacho utarogwa,Usipokuwa nacho pia utarogwa.

Achilia mbali wivu,majungu na wizi hapo ndipo nyumbani kwake
 
Goba sio tu wezi, bali unaingiliwa ndani mwako usiku umelala

Inasemwa kwamba wezi wengi wanaokwenda kuiba Goba wanatokea sehemu yaitwa (Kinzugi kama sijakosea) ni kasehemu kamekaa kiswahili hivi, pana maduka na muda mwingi pana giza.

Watu wengi hapo Goba wameweka "electrical wire" juu ya "fence".

Nna rafiki yangu anaishi hapo na mwaka juzi alimtengua mmoja wa hao vijana kwa risasi na tangu siku hiyo wanakwenda sehemu zingine.

Lakini alimsaidia huyo kijana na akamlipia gharama za matibabu na tangu siku hiyo huyo kijana anatufanyia shughuli za hapa na pale yaani tumemwajiri.

Pia, kuna sehemu ina bonde na kalavati ukitokea "Kwa Ulomi" hiyo sehemu vibaka hupora watu liingiapo giza hivyo si sehemu salama kwa kutembea peke yako.

Ila kwa utulivu na hali nzuri ya hewa Goba, Mbezi mwisho na Mbezi Beach ni maeneo salama sana.

Lakini kama una fedha ya kutosha karibu Mbweni pametulia sana.
 
Walikuwa wanavunja dirisha? Au walikuwa wanawapulizia dawa?

Wanatanua nondo kwa jeki na wanapuliza dawa.

Ni vijana wadogo sana na hutumia watoto kuingia ndani kupechua mlango.

Wezi wengi hupata taarifa za mali ya kuiba kutoka kwa mafundi ujenzi ambao hufanya surveys zao wee ukiwa kazini.
 
njoo mbezi ya kimara pako powa kwanza maisha yapo nomo sana suala la wizi sio sana but kwenda touni gali moja tu chap kwa haraka yani hutojutia
Gali moja -Gari moja
Umeongea vzr ila vyote porojo kisa tu ulemavu wa kuharibu lugha daah nyie wakurya mnaboa sana
 
Habari wana JF,

Kwa wale Wana-Ndugu ambao wanaifahamu Dar es Salaam vizuri, ni Maeneo au Mitaa gani ya kuishi (kupanga nyumba/chumba) ambayo yanalandana na sifa zifuatazo?

1. Sio maeneo ya uswazi/uswahilini
2. Sio pakishua sanaa/Expensive estate
3. Hayana matukio makubwa ya wizi na vibaka
4. Hakuna tatizo la maji tiririka
5. Upatikanaji wa karibu wa huduma za kijamii na kiuchumi. (maji, kiosk, etc)
6. Inaweza kuwa nje ya mji ila isiwe mbali sanaa na mjini kivile
7. Haikumbwi na mafuriko wakati wa mvua

Ahsante.
Ukonga Moshi bar
 
Sema tu jina mbagala Ila maeneo Kama chamazi mpk mbande Ni mazuri kuanzia Hali ya hewa (joto utalisikia kwenye radio) Huduma za kijamii, gharama za kimaisha.
Usafiri wa kwenda kariakoo na town Ni shling 600
Wakikamilisha mwendokasi patakua hot cake

NB.
Watu wa mikoani wakisikia mbagala Huwa wamejenga mentality vichwani kwao Ni sehemu ya ajabu ajabu
Kama diamond platnum alivyo imbaga.

Pia ubungo, tabata some how
 
Mkuu we utakuwa jirani yangu mpk mbande unapafahamu?basi tumlete msongola au mvuti
 
Habari wana JF,

Kwa wale Wana-Ndugu ambao wanaifahamu Dar es Salaam vizuri, ni Maeneo au Mitaa gani ya kuishi (kupanga nyumba/chumba) ambayo yanalandana na sifa zifuatazo?

1. Sio maeneo ya uswazi/uswahilini
2. Sio pakishua sanaa/Expensive estate
3. Hayana matukio makubwa ya wizi na vibaka
4. Hakuna tatizo la maji tiririka
5. Upatikanaji wa karibu wa huduma za kijamii na kiuchumi. (maji, kiosk, etc)
6. Inaweza kuwa nje ya mji ila isiwe mbali sanaa na mjini kivile
7. Haikumbwi na mafuriko wakati wa mvua

Ahsante.
Mikocheni B
 
Wakati nipo dar nliishi mbezi beach ni pazuri Sana pia nlikaa kidogo sinza pia pazuri ata usafiri sio washida Kama unaenda kupanga nyumba angalia sehem isiwe mbali na mji wala mbali na barabara pia zingatia usafiri na Kama panafikika kirahisi
sasa hivi uko wap
 
Nafikiri mleta mada mpaka hapa umeshachanganyikiwa uishi wapi, by the way kuna sehemu hamna wizi Tanzania acha Dar!
 
Back
Top Bottom