Moshi yakataliwa kuwa jiji

Moshi yakataliwa kuwa jiji

Kama Mwanza ni maskini kwanini watu wanazidi kuingia Mwanza na kuufata huo uchuro na umaskini?, ukiona sehemu kuna watu wengi na wanazidi kuongeza ujue wanafata vitu ambavyo sehemu nyingine hakuna, pia wanafata tulizo la mioyo yao, ndio maana population density ndio figure kubwa kwenye uchumi.
Kuingia kutoka wapi? Si wanatoka kwenye mikoa maskini inayowazunguka?

Nani atoke Kusini au Dar aende Mwanza ?
 
Mbona hayo magorofa yana hesabika acha ushamba tembea uone.
Hesabu na hapa 👇

Screenshot_20211017-120649.png


Screenshot_20211017-120150.png


Screenshot_20211017-120207.png


Screenshot_20211017-120338.png
 
SIFA ZA SEHEMU (MAKAZI)KUWA JIJI NI ZIPI?...naomba mjibu hili swali Kwanza,Kama watu hawafahamu sifa hizo basi hawana haki kuseme hii sehemu inafaa iwe jiji au siyo...na Kama hakuna sifa hizo basi Kama ni sababu za kisiasa basi pia zitajwe zijulikane hapa hapa jamvini...
Sifa ni moja tu, population( au wengine husema mzunguko wa hella), insue za majengo hazihusiki, duniani kote wanaangalia population density na si vinginevo
Ni kama Tanga, hamna chochote ni kama imezidiwa ata na ka Musoma kwa majengo ya mitaani na mjini ila Tanga ni jiji Musoma sio
 
Kuna faida gani mahali kuitwa jiji?
Kwa mfano kesho Kigoma ikaitwa jiji itafaidika nini tofauti na leo ambavyo haiitwi jiji?
Faida zipo kisiasa, mapendekezo ya maendeleo kwa jiji ni tofaut na manispaa, kama kuna bajeti ya barabara au hospital, jiji litapewa kipaumbele zaidi
 
Kwa nini tusifanye mikoa yote iwe majijij ile ipate vipaumbele katika barabara na hospitali kwa sababu hivi ni vitu mahali popote?
Faida zipo kisiasa, mapendekezo ya maendeleo kwa jiji ni tofaut na manispaa, kama kuna bajeti ya barabara au hospital, jiji litapewa kipaumbele zaidi
 
Kwa nini tusifanye mikoa yote iwe majijij ile ipate vipaumbele katika barabara na hospitali kwa sababu hivi ni vitu mahali popote?
Adi kuwa na hadhi lazima ufike population flan
 
Tanzania jiji ni moja tu Dar pekee yake. Kwingine kote kujipaka mafuta kwa mhongo wa chupa
 
Watu kiasi gani?
Kama kuna vigezo vya wazi mahali kuwa jiji kwa nini watu wana lobby na kubishana kuhusu eneo fulani kuwa jiji? Si hivyo vigezo viweke wazi ili watu wajue kama wanakidhi au la?
Adi kuwa na hadhi lazima ufike population flan
 
Tanzania majiji tunajipajipa tu ilitakiwa yawe mawili tu DSM na MWZ kwa sasa hayo mengine bado sana
Dar na dom..

Hayo mengine miundombinu hovyo kabisa.

Kama Arusha ndo nashindwa kuelewa kama serikali ilikuwa inautupia macho huu mji.

Jiji la kitalii hovyo kabisa kwa miundo mbinu.

Katika kukuza utalii na kuvutia international offices ziwekwe Tanzania, Arusha inatakiwe ivunjwe saaaanaa.

Acha tuendelee na harakati na mama yetu samia msije mkamhujumu.
 
Miji inayofaa kuwa au kubaki majiji kwa mkakati maalumu ni
1. Dar Es Salaam
2. Mwanza
3. Mbeya
4. Arusha
5. Mtwara
6.Kigoma
7.Dodoma
8.Tanga (iongeze bidii kurejesha miundo mbinu iliyokuwa imejengwa na hayati Mwl Nyerere kama bandari, viwanda na kilimo cha mikonge)

Miji ya Kitalii iwe ni
1. Kilimanjaro
2. Arusha
3. Iringa
4. Kagera
5. Morogoro
6. Pwani
7. Lindi
8. Ruvuma
9. Mara
10.Manyara

Mikoa ya kilimo cha mazao ya chakula
1. Songwe
2. Rukwa
3. Katavi
4. Ruvuma
5. Morogoro
6. Iringa
7. Mbeya
8. Njombe

Mkioa ya kilimo cha mzao biashara
1. Mwanza
2. Simiyu
3.Shinyanga
4. Singida
5. Tanga
6. Mtwara
7. Morogoro

Miji ya viwanda
1. Dar Es Salaam
2. Pwani
3. Morogoro
4. Mtwara
5. Tanga
6. Moshi
7. Arusha
8. Mwanza
9. Kigoma
10. Mbeya
11. Dodoma
12. Iringa
Mkuu Kagera inalisha 60% ndizi kwa nchi nzima na kahawa 45% ila sioni ukiitaja kwenye kilimo ama kwa chakula ama kwa biashara ..hebu tupe haki mkoa huu. Hapo sijataja mazao kama maharage na vanilla, ama ndo wale wale?
 
Tanzania jiji ni moja tu Dar pekee yake. Kwingine kote kujipaka mafuta kwa mhongo wa chupa
Siyo kweli hiyo ni sawa na kusema aliyepata Div.I kwenye mtihani ndiye amefaulu ila aliyepata Div. II au III eti amefeli.
 
Tatizo ukabila umewajaa sana pale yani kama si mchaga wanakuona kama taka tu
Ukabila siyo mkubwa, pale ni kutafuta kwa kwenda mbele, magofu ya zamani ni vile vile jumapili ukienda mji umepoa wote wamejisunda milimani
 
Back
Top Bottom