Watu wanapiga kelele kuhusu majiji fulani kutokuwa na hadhi na mengine kunyimwa sifa. Sio suala la kuona mji una ghorofa ngapi ili upewe hadhi ya kuwa jiji. Tanzania tuna kanuni zetu za kuufanya mji kuwa jiji - mbili kuu ni idadi ya watu na pato. Lakini zipo nyingine. Kama hatupendi mji fulani kutofanywa jiji au mji fulani kufanywa jiji inapaswa tuzirudie sifa tulizojiwekea wenyewe na kuzirekebisha.
Bahati mbaya sana ukiacha Mwanza na Arusha, majiji mengine yalipopata hadhi ya kuwa jiji hayakupata pesa za kutengeneza miundo mbinu. Mwanza ilipewa pesa nyingi sana za kujenga miundo mbinu. Kipindi kile ilipata hadhi peke yake baada ya Dar es Salaam.
Nje ya mada, wewe binafsi umefanya nini hapo ulipo hadi uone mji wako ni mzuri au mbaya. Usije ukawa kuchwa nzima wasifia au wachukia kazi za mikono ya wenzako. Kazi yako imeung'arisha mji uliopo?