Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Ajali zaondoa uvumilivu wa Kikwete

2009-01-23 10:14:31
Na Mwandishi Wetu
Rais Jakaya Kikwete, amesema serikali haiwezi kuvumilia kutokea kwa ajali za barabarani zinazosababisha vifo na upotevu wa mali, wakati mamlaka zenye kusimamia usalama katika eneo hilo zipo.
_____________________________________________

Kama kweli Serikali haiwezi kuvumilia basi cha kufanya si kuweka sheria kali au kuwatuma askari wa usalama barabarani kuangalia nani na nani wanaendesha magari kwa kasi ,hilo halitasaidia zaidi ya kuzidisha ulaji kwa polisi hao ambao,wanaposimamisha basi au lori huenda nyuma ya gari hilo na kumngojea dereva au konda awakatie chao ili waendelee na safari bila ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,hilo nililiona nilipokuwa nasafiri kutoka Dar kuelekea Tanga ,basi letu lilikamatwa na radar likienda spidi ,polisi alipewa chake nasi tukaendelea kwa kasi mpya.

Ili kuondoa ajali hizi ifahamike siku hizi umilikaji wa magari umeanza kukua katika Tanzania kwa kweli ni maendeleo na nionavyo si muda mrefu kila nyumba itakuwa na kijigari japo kidogo.

Hivyo tukubaliane kuwa kuna wimbi la ongezeko la magari makubwa na madogo yaliyomo mjini na yaendayo mikoani kinachotakiwa ni kuboresha barabara zetu ziwe dual mita nne kwa mita nne nikimaanisha yakuendea na ya kurudia,lakini kwa barabara hizi tulizonazo ambazo ni mita nne one way au kama zijulikanavyo face to face tutaendelea kuvuna ajali mpaka mwisho wa dunia.

Na vile vile bara bara hizi za face2face zimejengwa kihatari sana angalia sehemu zile magari yanapopandisha kilima utaona yamejengwa matuta ambayo yanamfanya hata yule dereva anaepandisha kilima apunguze mwendo na akifanya kosa gari yake itarudi kinyumenyume matuta haya nimeyaona katika barabara hiyo hiyo iendayo Mikoani ikitokeayo Dar na vilevile kama bahati tulilikuta lori la tela ambalo ambalo lilipinduka na kunusurika kuingia bondeni baada ya kushindwa kupanda tuta lilipunguza mwendo kati kati ya mlima wa Daraja la Ruvu likipandisha kuelekea Dar ,dereva alisema alipopunguza kasi kulivuka tuta ndipo alipokutwa na masaibu ya lori lake kupoteza nguvu za kupandishia mlima na kujikuta gari likiserebuka kinyumenyume.
Vipi utaweka matuta katika barabara inayopandisha mlima tena mlima mkali hivi mainjinia wetu hawajui athari za kushindwa kwa gari kupandisha mlima ,yaani kama sehemu hizi wangelijaribu kuweka barabara mbili(Dual) na wakaweka matuta kwa wale wanaoshusha mlima , na pia kuendeleza uwekaji wa njia mbili kutokana na kuzidi kwa magari haiwezekani kuepuka ajali kwa kutumia njia hizi hizi za ulimi wa nyoka,serikali isitafute mbaya na kutaka kubambikizia madereva makosa wakati makosa ni yao ya kushindwa kuboresha njia na kuzifanya ziweze kupitika kwa usalama..nchi inakuwa hivyo barabara ziendane na wakati.
 
Kingine kinacholea ajali za barabarani zinazoua abiria ni abiria!

Unaona kabisa basi lenu haliko upande wenu wa barabara, liko spidi full nondo linashuka kilima cha curve kuelekea kidaraja cha mbao, mbele kule huoni chuma gani kinakuja your way, na wewe umekaa tu unaangalia kama sindimba inachezwa!

Mimi nishamkoromea dereva wa ki-Hiace alipiga overtake ndeeeefu halafu mbele hatuoni nini kinakuja, barabara iko busy kinoma, konda akaniletea complaini kama namna gani niachie ngazi, abiria wenzangu badala wanisapoti wote wananishangaa. Nikajisikia kama dissident mmoja nimetangaza twende msituni vile. Nikasema screw this utulivu utulivu na nidhamu ya ujamaa thing.
 
Matatizo hapa ni uelewa mdogo wa watumia barabara wote. Upande wa abiria wengi wetu hatuna utaalamu wa kuendesha hivyo dereva anapotoa hiyo michezo na mbwembwe tunadhani ndio utaalamu wa kuendesha gari. Kuhusu suala la kinywaji ndiyo kabisa hatuoni kama ni kitu kibaya na hatufikirii kama kinaleteleza dereva kuwa na uamuzi (wa kidereva) potovu. Nimeshawahi kuwa kwenye basi la safari ndefu ambapo dereva alisema kuwa asipokunywa atapata usingizi hivyo alcohol itamsaidia asisinzie ( it was an overnight trip) abiria tumekaa tu hata hatukumkatalia.

Udereva wetu pia hauko makini kwa sisi tunaoendesha, hakuna anayejali ishara za bara bara, niliendeshwa na kijana siku moja tukafika kwenye taa nyekundu akapita, nikamuuliza kulikoni akasema hakuna gari hivyo ni sawa tu kukatisha ( japo taa ni nyekundu). Madereva hatupeani "courtsey" utaona mwenzio anajaribu kuingia baranara kuu anapiga turn signal mpaka inaungua, huwezi kumuachia aingie unatwanga tu.

Tail gating ndiyo usiseme sasa hizo ajali kweli zitapungua? Shoulder driving ndiyo hata haijulikani kama ni kosa.

Kitu kinachotakiwa ni wadau wote wanaohusika na matumizi ya barabara wapewe elimu jinsi ya kutumia barabara. Barabara zitengenezwe vizuri, na kuwe na adhabu kali kwa watu wanaokiuka matumizi salama ya barabara.

Dereva akilewa , tuteremke kwenye bus polisi waitwe halafu yeye atajieleza kwa nini wasafiri waliteremka, apimwe kilevi, mengineyo yatafuata. ( naelewa kuwa hii itasababisha (pengine) kuchelewa katika safari zetu, lakini lazima tujitoe muhanga.) Wamesema waswahili kawia ufike.
 
Kuna habari kuwa kumetokea ajali mbaya hapo Jet, barabara ya Nyerere karibu na Airport. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana sasa hivi, inawezekana ikawa imechukuwa idadi kubwa ya maisha ya watu (VIFO). Mwenye habari kamili atuhabarishe!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu shedafa ni kweli wamekufa watu kumi na moja!!! on spot,,kulikuwa na lori linakata kona ikatokea hiace ya dalala ikiwa imetokea machinjioni pale pugu ndipo roho wa mauti alipowakuta,,ila cha kusikitisha nilifika ajali imetokea tangu saa kumi kasorobo usiku na qwngi wamekufa sababu ya bleeding labda kuna umuhimu wa kuwa na kikosi cha kusaidia ajali sby,,na si kutegemea hawa polisi wetu wa defender walichofanya ni kuja na kushuka na kuangalia watu wakiwa wanakata roho badala ya kuwakimbiza hosp,ni pale kipawa inasikitisha saana.......
 
Ni kweli nimesikia redio uhuru wakitangaza, askari walichelewa kufika walipopata taarifa.

Kwa mara nyingine ndani ya mwezi 1 nguvu kazi ya taifa imepotea, familia zimepoteza wapendwa wao, watoto wamepoteza baba/mama na taifa limepoteza watendaji wake, kampuni zimepoteza wafanyakazi wake, baba ameacha mjane, jamani hivi hizi ajali hazina kinga?

RIP...
 
Kama kawaida Raisi atatuma salamu za rambirambi, hii ni sawa lakini sidhani kama jamii tunatimiza wajibu wetu vizuri, abiria, wamiliki, madereva, makonda, sumatra, vyombo vya habari na wadau wengine JE tunatimiza wajibu wetu vizuri?

Kwa mfano kwa nini dereva anaendesha kwa mwendo kasi na kudharau alama za barabarani na sisi abiria tunakaa kimya? Tukumbuke kuwa ikitokea ajali kwa uzembe basi waathirika si majerui na wafu tu bali kuna familia, serikali na jamii nzima kwa ujumla kwa wengine ni kukaribisha umaskini ndani ya nyumba.

Inatokea ajali unakatwa mikono na miguu unaletewa barua kuwa kibarua ndio basi tena, haya sasa umaskini ndio umepiga hodi, mmiliki hayupo, serikali imekupa pole na wewe una mke na watoto wanaokutegemea, embu tuwe tuna tafakari mambo haya na kutimiza wajibu wetu.

INAWEZEKANA AJALI KUWA NA KINGA TIMIZA WAJIBU WAKO USIMYOOSHE MTU KIDOLE WEWE UMEFANYA NINI?
 
Hii ni ajali ya pili eneo moja ndani ya siku 2.

Jana asubuhi katika eneno hilo hilo kulitokea ajali ya gari dogo likiwa limebeba nyama ya ng'ombe toka Pugu machinjioni na lori.

Leo hii ndio hiyo ajali ya gari 3. kinachosikitisha zaidi ni kuwa gari liloua watu wengi(Hiace) imekuwa involved ktk ajali ambayo ilikuwa imetokea more than 10min baada ya kushindwa kufunga break na kwenda kugonga gari zilizokuwa tayari zimekwisha gongana.

Nadhani kuna haja ya askari wa barabarani kukagua ubora wa magari na si kuangalia bima, leseni na vitu vidogo pekee. Ikiwezekana kuwe na serious check-up za magari ya abiria baada ya muda fulani na yasiofaa yaondolewe barabarani.
 
Msongamano wa abiria ndani ya vi-hiace ndio kunakosababisha maafa na si mgongano, abiria wanajazwa ndani ya gari hizo utazani mananasi na wakikamatwa usalama barabarani anajua kuwa kila abiria aliezidi nauli analipwa yeye na kuacha jamaa aondoke kwa kasi mpya.

inajulikana wazi idadi ya abiria wa haisi hawazidi kumi na mbili lakini inafanywafanywa mpaka inapakia watu 24 na spidi ndio hivyo wengi wamesimama ,sa hapo ikikanyagwa brake ya gafla ,unadhani patatokea nini kama si vifo? Kwa nini gari zinazofanyiwa modifikashon ya viti zisiruhusiwe kupakia na kufanya kazi ya kusafirisha abiria?

Na hawa usalama wa barabarani wawe na usalama wanaowasimamia kuona shuguli zao wanazingatia maadili ya kurekebisha, aidha abiria aliezidi ateremshwe.
 
Nadhani kuna haja ya askari wa barabarani kukagua ubora wa magari na si kuangalia bima, leseni na vitu vidogo pekee. Ikiwezekana kuwe na serious check-up za magari ya abiria baada ya muda fulani na yasiofaa yaondolewe barabarani

Kwa hili tuanze kwanza na kukemea Pepo Wa R ushwa Barabarani ndipo haya yote yataisha...kama askari anauliza license anapewa licence feki na sh 2000 ndani mwisho anarudisha na kumwambia dreva usirudie tena,,,hii ni ngumu hata wazaliwe wakina ""KOMBE"" mia hakuna kitakachofanyika kama hawataacha rushwa barabarani kibaya ama cha kusikitisha wanahongeka kwa pesa ya kijinga bila kujali thamaani za watu ....

Mungu awalaze mahali pema peponi,,imenisikitisha sana wakati nafika ndio wanaingizwa nndani ya defender kama ""ZOMBE""hii ni swali la kujiuliza lini rushwa itaisha barabaranni??
 
ajali imetokea tangu saa kumi kasorobo usiku na qwngi wamekufa sababu ya bleeding labda kuna umuhimu wa kuwa na kikosi cha kusaidia ajali sby,,na si kutegemea hawa polisi wetu wa defender walichofanya ni kuja na kushuka na kuangalia watu wakiwa wanakata roho badala ya kuwakimbiza hosp,ni pale kipawa inasikitisha saana.......

Saa kumi kasorobo "usiku" au "asubuhi"? Madereva walikuwa wanaendesha magari usiku wote au ndio walikuwa tu wameanza siku? Wananza siku mapema hivyo?

(1)Iko haja ya kuwa na taa za barabarani ili magari yaonane.

(2) Lazima madereva wapate muda wa kutosha wa kulala. Walale angalau masaa 8 kwa siku.

(3) First responders (Polisi, Zimamoto, Ambulance Crews) lazima wawe standaby wakati wote. Kila kikundi kiwe na sehemu yake ya kuhusika. Search and Rescue groups save lives.

(4) Ukaguzi wa gari na dereva ufanywe angalau mara moja kwa mwaka. Leseni za udereva na za magari ziwe renewed baada ya kuthibitisha ubora. Nchi nyingine zina utaratibu wa kila gari kukaguliwa na kupata road worthiness licence kila bada ya miezi 6. Wanakagua break, usukani, taa, indicators, etc.

(5) Safety audits za barabara zifanywe, na sehemu zenye mapungufu zishughulikiwe.

Mungu awalaze pema marehemu wote.
 
Mkuu augustino sorry si usiku wala asubuhi ni Alfajiri,ok!!!!??
 
- Again? There must be something wrong with that "JUNCTION"!!

- Pole wafiwa and RIP waliokutwa na umauti
 
RIP walikutwa na mauti
Ila Tanzania kuna mambo mengi yanatokea tunakaa kudanganyana tu
Kila siku ajali zinatokea na watu wanakufa, ukijaribu kufanya utafiti ajali hizo ni uzembe tu, sasa kwanini serikali haiingilii kati na kutafuta suruhisho la kudumu jamani?
Mkuu BabaH hilo gari inasemekana wamegundua lilikuwa haliwaki taa!!hapa alaumiwe nani??matraffick wanaokula rushwa na kushindwa kukagua magari inavyotakiwa ??

First responders (Polisi, Zimamoto, Ambulance Crews) lazima wawe standaby wakati wote. Kila kikundi kiwe na sehemu yake ya kuhusika. Search and Rescue groups save lives.

Mkuu Augustino hivi sasa hivyo vitu imekuwa biashara ndugu yangu! Kuna watu waliwapigia ama Ultimate au kampuni moja ya ulinzi ina ambulance service waliishia kuulizwa watatoa shillingi ngapi! Imagine...

Suala ni serikali kuwa committed na ajali ama mpaka siku ajali itakapolamba familia za viongozi ndipo watajua umuhimu wake! Leo hii hata ukiunguliwa na nyumba unamwambia Mungu akusaidie isiishe yote maaana hata ukiita FAYA wanakuja na kukwambia wapi kuna bomba karibu! Mambo kama haya yanaitishia hata usalama wa nchi means mpaka tuvamiwe ndio tuanze kujiweka sawa kwa mapambano...

MUNGU AWALAZE MAHALA PEMA PEPONI

kama nilivyosema hapo juu huyu "RUSHWA" kama hataisha familia nyingi zitapotea kila siku kwenye ajali!
 
Vifo pale vimesababishwa na ukosefu wa huduma ya kwanza.

Ajali imetokea watu wa huduma ya kwanza wamechelewa kufika.Imefika Defender pale ikiwa imechelewa.wengi wamefariki kwa kupoteza damu.

Hivi tunakitengo cha kushughulika na ajali? kwa maana ya huduma ya kwanza?
 
Mungu awarehemu wale wote waliofikwa na mauti. Mungu awajaze nguvu wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine.

RIP.
 
RIP marehemu wote.
Nchi hii huwa hatuna vitengo vya msaada wakati wa ajali. Ukiuliza utaambiwa hatuna fedha au hatujapata ufadhili.
Basi siku zote tubaki tukiomba Mungu atunusuru na majanga haya.
 
Back
Top Bottom