Ajali zaondoa uvumilivu wa Kikwete
2009-01-23 10:14:31
Na Mwandishi Wetu
Rais Jakaya Kikwete, amesema serikali haiwezi kuvumilia kutokea kwa ajali za barabarani zinazosababisha vifo na upotevu wa mali, wakati mamlaka zenye kusimamia usalama katika eneo hilo zipo.
_____________________________________________
Kama kweli Serikali haiwezi kuvumilia basi cha kufanya si kuweka sheria kali au kuwatuma askari wa usalama barabarani kuangalia nani na nani wanaendesha magari kwa kasi ,hilo halitasaidia zaidi ya kuzidisha ulaji kwa polisi hao ambao,wanaposimamisha basi au lori huenda nyuma ya gari hilo na kumngojea dereva au konda awakatie chao ili waendelee na safari bila ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,hilo nililiona nilipokuwa nasafiri kutoka Dar kuelekea Tanga ,basi letu lilikamatwa na radar likienda spidi ,polisi alipewa chake nasi tukaendelea kwa kasi mpya.
Ili kuondoa ajali hizi ifahamike siku hizi umilikaji wa magari umeanza kukua katika Tanzania kwa kweli ni maendeleo na nionavyo si muda mrefu kila nyumba itakuwa na kijigari japo kidogo.
Hivyo tukubaliane kuwa kuna wimbi la ongezeko la magari makubwa na madogo yaliyomo mjini na yaendayo mikoani kinachotakiwa ni kuboresha barabara zetu ziwe dual mita nne kwa mita nne nikimaanisha yakuendea na ya kurudia,lakini kwa barabara hizi tulizonazo ambazo ni mita nne one way au kama zijulikanavyo face to face tutaendelea kuvuna ajali mpaka mwisho wa dunia.
Na vile vile bara bara hizi za face2face zimejengwa kihatari sana angalia sehemu zile magari yanapopandisha kilima utaona yamejengwa matuta ambayo yanamfanya hata yule dereva anaepandisha kilima apunguze mwendo na akifanya kosa gari yake itarudi kinyumenyume matuta haya nimeyaona katika barabara hiyo hiyo iendayo Mikoani ikitokeayo Dar na vilevile kama bahati tulilikuta lori la tela ambalo ambalo lilipinduka na kunusurika kuingia bondeni baada ya kushindwa kupanda tuta lilipunguza mwendo kati kati ya mlima wa Daraja la Ruvu likipandisha kuelekea Dar ,dereva alisema alipopunguza kasi kulivuka tuta ndipo alipokutwa na masaibu ya lori lake kupoteza nguvu za kupandishia mlima na kujikuta gari likiserebuka kinyumenyume.
Vipi utaweka matuta katika barabara inayopandisha mlima tena mlima mkali hivi mainjinia wetu hawajui athari za kushindwa kwa gari kupandisha mlima ,yaani kama sehemu hizi wangelijaribu kuweka barabara mbili(Dual) na wakaweka matuta kwa wale wanaoshusha mlima , na pia kuendeleza uwekaji wa njia mbili kutokana na kuzidi kwa magari haiwezekani kuepuka ajali kwa kutumia njia hizi hizi za ulimi wa nyoka,serikali isitafute mbaya na kutaka kubambikizia madereva makosa wakati makosa ni yao ya kushindwa kuboresha njia na kuzifanya ziweze kupitika kwa usalama..nchi inakuwa hivyo barabara ziendane na wakati.