Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

source ya ajali nyingi ni kwamba hatujui ku-keep time, so kwenye gari kila mtu anataka kuwahi hapo nani atakayemwambia dereva punguza mwendo?
 
Kwa mtindo huu bado kabisa ajali haziwezi kuisha nenda SUMATRA sasa hivi utakuta vishoka wamejaa pale kibao wanasubiri wateja wa kuwakatia leseni za faster faster, unatoa kitu kidogo unapata vehicle inspection report hapo hapo bila hata gari kukaguliwa. je tutafika? bado wazee wa "TIGO" nayo wakipewa kiasi dereva anaendelea na safari.
Ajali haziwezi isha, tutaishia kusikia hizo ni kafara imani potofu watanzania tuache, abiria raia tushikamane katika hili. MUNGU AWALAZE MAREHEMU PEMA PEPONI.
 
Ni kweli nimesikia redio uhuru wakitangaza, askari walichelewa kufika walipopata taarifa.

Kwa mara nyingine ndani ya mwezi 1 nguvu kazi ya taifa imepotea, familia zimepoteza wapendwa wao, watoto wamepoteza baba/mama na taifa limepoteza watendaji wake, kampuni zimepoteza wafanyakazi wake, baba ameacha mjane, jamani hivi hizi ajali hazina kinga?

RIP...

Wa kulaumiwa ni viongozi wetu ni wepesi mno kupanda majukwaani kutoa hotuba nzuri kuhusiana na askari wa barabarani kufanya kazi za kwa ufanisi ili kupambana na wavunjaji wa sheria barabarani na magari yasiyostahili kuwepo barabarani, lakini ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo ya 'hotuba hizo nzuri' ni ZERO. Katika mwezi huu wa January tumeshapoteza Watanzania wenzetu zaidi ya 50 kwa ajali za barabarani ambazo zinaweza kabisa kuzuilika. Mwenyezi Mungu awalaze marehemu mahali pema peponi~AMEN.
 
Jamani kama taa za Morogoro road haziwashi na ukipita pale usiku ni giza balaa na haya malori huwa yanapaki pembeni ya barabara na ukipita na gari usiku hukioni mpaka ulikaribie kwa kweli hii ni hatari sana! sasa huwa najiuliza hivi manispaa ya Kinondoni wanabana matumizi ya umeme au wanajifanya hawajui kuwa barabara ya morogoro kuanzia ubungo maji mpaka mbezi taa usiku huwa haziwashwi?
 
Poleni wafiwa,

Muda si mrefu JK atatuma salamu na kusema hio ni kazi ya Mungu na pia atasema anawataka Traffic wawe wakali zaidi. Ataibuka Kombe na kusema kuwa kuanzia leo hakuna dala dala kutembea saa 6 mpaka sa 11 asubuhi.

It will take 10years to get where we want but at this point this can be done ila nashangaa akina Kombe matumbo makubwa tu. Fuatilia uniambie how much will cost to have this in place....
- Nimetembelea mikoa yote Tanzania na kuna mabasi yakutisha. Ni tetenus tupu. Magari standard yalioko barabarani ni ushindani wa kibiashara sio according to regulation. Hivi spacing ya kiti na kiti inahitaji mkopo from WB kuenforce? Hiace inabeba watu 20, hii inatoka wapi?
- Utengenezaji wa seat ni balaa, kuna siku nimesafiri kutoka Mpanda kuja Tabora na lile basi ni balaa. Seat imechomewa nyingine imefungwa na nut. Kuna sharp edges za kufa mtu. Hizi si zinasababisha wound panapotokea ajali? Ina maana hili Kombe nae hajui au kwa kuwa hawajui kusema wanabakia tu ajali ni Mapenzi ya Mungu? Ole wenu Wachungaji/maaskofu/wainjilisti na washeik. Hii dhambi ni yenu mana mnadanganya sana watu nyie.
- Mabasi yote hayana mikanda labda yale yanayopitia Kenya. Hivi kuwa na mikanda nayo ni dhambi au kwa kuwa mpo kwenye payroll za hawa wenye umiliki wa mabasi? Hivi ni magari gani ya first aid kits?
- Hivi kila mkoa kuwa na Rescue Team na vifaa vya kisasa ni aghali sana? Hivi kweli tukiomba mkopo kwa hili au msaada kutoka scand countries unafikiri watatunyima?
- Hivi traffic kuongelea sababu za kusimamisha gari ndani ya gari badala ya conductor kumfuata kule inahitaji mtaji wa pesa au dhamira ya dhati kusimamia majukumu yako?
- Hivi traffic hawajui kama kuna magari ambayo hata number mpya hazina na yanafanya biashara bila bima wala nini ndani ya Dar?
 
Magari ni chanzo kizuri cha mapato ya serikali. Kwanza kodi ya Road licensi ni kubwa lakini tunalipa. Mafuta yanakodi kubwa lakini inalipwa kila lita ya mafuta. Kunahaja ya kuongeza mapata kutumia chanzo hiki- Faini ya uendeshaji mbovu na kukiuka taratibu za barabarani. Wote wana "overtake" kushoto na sasa imekuwa kawaida! Watu wanaendesha pembezoni mwa barabara kuongeza mumomonyoka ni kawaida! Honi hospitali na pengine pasipo sitahili kawaida! Kupita taa nyekundu kawaida! Je tutafika kweli.
Pale Jet panatakiwa papate taa za kuongozea magari kwa kweli.
 
Daladala lililohusika lilikuwa limefungiwa tangu 2007. Lilikuwa likifanya kazi usiku tu
 
Daladala lililohusika lilikuwa limefungiwa tangu 2007. Lilikuwa likifanya kazi usiku tu

Sasa hapo ndio watakulupuka kutoa maagizo, kuwa magari yasiyosajiliwa yasifanye kazi kwa kuiba usiku. Wakati ni kawaida, kuanzia 4 usiku mpaka 11 asubuhi Dar gari zifanyazo kazi ni zile hazijasajiliwa na mbovu. Na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa, manake gari nyingi ambazo hazijasajiliwa zina matatizo.
 
Daladala lililohusika lilikuwa limefungiwa tangu 2007. Lilikuwa likifanya kazi usiku tu

Madaladala kama haya yako mengi tu na madereva wasiostahili kuwa barabarani wako wengi tu na magari yasiyo na hadhi ya kuwa barabarani yapo mengi tu. Ni uzembe wa askari wa barabarani wakishashikishwa mshiko basi wanawachia jamaa wapete tu na matokeo yake ndiyo hayo barabara zetu zimekuwa ni machinjioni 🙁
 
Zombe anasema watu tisa wamefariki na 11 wamejeruhiwa

Mpaka wanasiasa watakapoacha ubinafsi na kuanza kujali maisha ya mtanzania.Likiwemo suala la kuwa na first responder team. Mungu apishirie mbali haya majanga...utafikiri tu kama Somalia ambayo haina serikali. Mambo ya msingi kama magari ya huduma ya kwanza. Jaribu kupiga 911 operator wa hiyo line achelewi kukuomba vocha.
 
Mpita Njia Zombe amerudishwa police. Mimi najua yuko mahabusu kwa kosa la mahujaji au......?

Msalime Mtume. Kosa la mahujaji, aliwafanya nini?

Poleni wafiwa, madaladala bubu yamejaa dsm hata bububu lakini serikali yajitia ububu

Asha
 
Bongo bwana hamnazo
Utasikia raisi anatoa rambi rambi.....huyu raisi yeye kazi yake ni kutoa rambi rambi za redioni tu....mimi napata wasi wasi ndio yale yale kafara zinatolewa.....

Yaani Mungu hajapenda kabisa hawa watu wafe.......
 
Msalime Mtume. Kosa la mahujaji, aliwafanya nini?

Poleni wafiwa, madaladala bubu yamejaa dsm hata bububu lakini serikali yajitia ububu

Asha

Asha Abdala, Thanks. it was a typo. I have alreadyremoved that post and replaced with the new one.
 
RIP marehemu wote.
Nchi hii huwa hatuna vitengo vya msaada wakati wa ajali. Ukiuliza utaambiwa hatuna fedha au hatujapata ufadhili.
Basi siku zote tubaki tukiomba Mungu atunusuru na majanga haya.

Tatizo hatuna viongozi tuna wafanyabiashara, kama kitu hakina maslahi kwao si muhimu. Ila ingekuwa kinasaidia washinde uchaguzi kitengo hicho kingekuwepo siku nyingi
 
Nimepokea kwa masikitiko makubwa ajali ya HIACE kuingia chini ya lori kisa ni mwendo wa kasi jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Je hawa madereva wetu wanakuwa na haraka gani hadi kuua watu tisa kwa mpigo. Cha kushangaza ni kitendo cha gari hilo la abiria kuendesha huku leseni yake ikiwa imeisha miaka au niezi kadhaa iliyopita. Je kupita kwa muda wa usajili wa gari hiyo ya abria na kufanya kazi wakati wa usiku ni kosa la nani? Na abiria wana makosa gani? Na je watalipwa fidia kwa walioumia. Kwani nina imani hiyo gari haina bima.
 
15 perish in Dar, Morogoro accidents
DAILY NEWS Reporters
Daily News; Friday,January 30, 2009 @21:15

At least 15 people have died on the spot and 21 others injured in road and train accidents which occurred yesterday in Dar es Salaam and Morogoro regions. Nine people died and eleven others got seriously injured in a car accident that occurred in Dar es Salaam yesterday, the Dar es Salaam Special Zone Police Commander, Mr Suleiman Kova, said.

The accident occurred at around 4am along Nyerere Road at Jet area in Ilala district. According to Mr Kova, the accident involved three vehicles, a Scania with the registration numbers T 452 ACP that was heading towards Tazara from Jet, a Tipper Fuso (T 334 ADH) heading towards Tazara from the airport and a Hiace (T 700 AFT) which was heading towards Tazara from Kipawa butchery.

He said the Hiace, being driven by an unknown driver hit the Tipper Fuso which had earlier collided with the Scania. The nine people who died on the spot were passengers of the Hiace which they had hired. The deceased have been identified as; Ally Issa, Kabla Msambaza, Michael Maujiro, Augustino Yohana, Elly Athumani, Alifonsi Golesh, Maiko Msangila, John Stephen and one man whose name could not be identified immediately.

The RPC said the Scania that had earlier collided with the Fuso at a sharp corner of the main road caused injuries to Kalulu Lykole (35), Philemon Joram (26) and an unidentified lady who were in the Fuso lorry. Mr Kova named other people who were injured during the crash as Saimon Silvester (27), a resident of Gongolamboto, Eva Joseph (28) from Makongo Juu, Karunde Osambi (34) from Mwenge, Zamoyoni Mogella (36) from Mbezi Louis, Joshua Jumanne (29) and Alex Msuya (65) both from Buguruni.

Others are; Ratibu Abdalla (21), a resident of Ukonga, Emilly Stephen (40) from Mbagala and an unidentified man. They were admitted to Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) while the bodies of the deceased were preserved at the Muhimbili National Hospital mortuary. Speaking to ‘Daily News on Saturday' at MOI, Saimon Silvester (victim) said the cause of the accident was due to negligence of Hiace's driver.

He said the driver, suspected to have been drunk, was driving at a high speed. "We really complained about the speed…but the driver could not heed to it," he said adding that the driver had earlier claimed that he should not be directed on what to do since he was a professional driver. The MOI Senor Social Welfare Officer, Dr Mary Ochieng, said most of the injured people admitted to the hospital were in critical conditions and were therefore admitted to the Intensive Care Unit (ICU).

According to Mr Kova, the Hiace was operating illegally as its licence expired since March 13, 2007. Information had it that the bus was operating only during nights. In Morogoro, six people died on the spot and 10 others injured in a train accident which occurred between Mzaganza and Kidete railway station at Kilosa district, Morogoro region. Police Commander of Railway Unit Yessaya Msigwa said the train which was heading to Dar es Salaam from upcountry regions crashed at the area around 1am yesterday.

He said the train overturned at Msaganza village and passengers were coming from an auction. Msigwa named the deceased as Said Pindupindu, Seif Bakar, Nassoro Mohammed, Jonas Lukanda and Abbas Kandoro, all businessmen from Kilosa and one person who could not be identified. He named the casualties as; Hamis Chamwitu, Seleman Mohamed, Sadic Monera, Esther Mbwambo and Asha Hamis, all residents of Morogoro and were admitted to Kilosa District hospital. Others also admitted to Kilosa District hospital are; Edward Athanas, Aziz Seleman, both residents of Dar es Salaam and Hamis Manyeleta, Hamis Selemani and Mecha Jackson, residents of Kilosa.
 
Back
Top Bottom