Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Poleni nyote mliofikwa na kadhia hii. Mungu awape nguvu.
 
Mungu uwape pumziko la milele marehemu na wale walioumia uwajalie kupona haraka....hizi ajali ni madereva, bara bara zetu ama magari mabovu, ama ni machanganyiko wa vyote? Kila kukicha ajali tu ajali....

Nawapa pole sana waliofikwa na mkasa huu.
Tatizo kubwa ni daraja jembamba magari mawili makubwa hayawezi pishana na lipo kwenya kona pande zote mbili. ufumbuzi ni kupanua daraja au kuweka matuta kama ilivyo mto wami, madereva siku zote huwa na haraka kinachotakiwa ni kuwathibiti kwa njia ya namna hiyo maana kama ni askari wa kuthibiti mwendo hawakai masaa 24 bali matuta yatakuwepo mda wote
 
Ripoti za hivi punde zinasema waliopoteza maisha ni 16

Poleni wafiwa wote.

Hili daraja linahistoria ya kutoa maisha. Tatizo ni hili eneo ni sehemu ya mteremko pande zote za daraja halafu kuna kona. Daraja linatosheleza kwa magari mawili makubwa kupisha, na both sides baada ya daraja kuna emegency exits. Lakini naona uzembe wa madereva ni mkubwa.

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi Amina
 
Jamani poleni sana. Eneo hilo nalifahamu vizuri. Liko barabara kuu iendayo Moshi kutokea Arusha. Pana mteremko mkali sana pale. It is about 7 kilometers from AICC. Actually stretch hiyo kutokea Kwangulelo kupitia kwa mrefu hadi Tengeru ni black spot haswa. Wakati Magufuli akiwa waziri wa Ujenzi, sisi wakazi tuliwahi kumuomba iwekwe matuta TANROADS wakakataa kwa kutoa majibu ya kisheria. Lakini barabara hiyo hiyo uingiapo tu mkoa wa Kilimanjaro matuta hadi njia panda ya Himo. Yaani double standards at its best. Sielewi sielewi. It is very sad indeed.
 
Pale hapahitaji matuta, utawekaje matuta kwenye mlima/mteremko mkali, zaidi ya hayo kuna kona na daraja! Basi matuta yakawekwe pia Kitonga, Ngorongoro au hata Sekenke!

Kinachohitajika ni alama za barabarani na madereva waangalifu.

Marehemu wapumzike kwa amani. Poleni majeruhi na wafiwa.
 
Last edited by a moderator:
Na. Mwandishi Wetu

Taarifa kutoka Arusha zinasema kuwa kuna magari kama matano yametumbukia katika mto Nduruma nje kidogo ya mji wa Arusha. Kw amujibu wa vyanzo vyetu ajali hiyo imesababishwa na lori la Coca Cola kugongana na magari mengine madogo na kusababisha magari hayo kutumbukia mtoni na mengine kuning'inia kwenye kingo ya mto huo. Hadi hivi sasa kuna watu kadhaa waliofariki na wengine kujeruhiwa. Tutawaletea taarifa kamili hivi punde.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Bw. Robert Boaz ameiambia KLHN kuwa ajali hiyo imetokea mchana wa leo kwenye barabara ya Arusha Moshi ambalo semi-trailor iligonga basi ambalo nalo likagonga magari mengine madogo. Hadi hivi sasa Bw. Boaz amethibitisha kuwa waliofariki ni watu 16 miongoni mwao ni wanaume 10 na kina mama 6.

Bw. Boaz amesema kuwa walifika eneo la ajali mara moja ambapo waliweza kupata msaada wa wananchi kutoa miili ya marehemu na kuwasaidia majeruhi na kuwakimbiza katika hospitali za Arusha kwa matibabu. "Wananchi wametupatia ushirikiano mkubwa" alisema Bw. Boaz.

Alipoulizwa kuhusu chanzo cha ajali Bw. Boaz alisema kuwa hadi hivi sasa uchunguzi unaendelea ingawa alitoa ushauri kuwa madereva na watumiao vyombo vya usafiri kuwa wanaozinggatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali nyingine ambazo kwa kweli si za lazima.

Hii ni ajali kubwa ya tatu kutokea nchini tangu mwaka huu mpya uanze. Ajali moja kubwa nyingine ilitokea karibu wiki moja na kitu iliyopita ambapo watu 27 walikufa baada ya basi la Tashrif kugonga lori la magogo lililokuwa limeegeshwa pembezoni maeneoo ya Hale kwenye barabara ya kuelekea Tanga (Muheza - Segera).

Ajali hiyo ya basi ilitanguliwa na ajali iliyotokea huko Himo Moshi ambapo watu 11 wa familia moja walipoteza maisha yao Januari 4 wakiwa wanarudi kutoka kwenye sherehe za Ubarikio. Basi dogo la (hiace) nalo liliparamia lori lililokuwa limeegeshwa pembezoni.

Ajali za namna hii zimekuwa zikitokea mara kwa mara huku serikali na vyombo vya usalama vikitupa lawama nyingi kwa madereva na watumia barabara wengine kuwa waangalifu wakiwataka wafuate sheria za usalama barabarani.
 
Watu kadhaa walikufa baada ya magari kugongana (coaster na lori lililobeba coca). Wengine walikufa wakati wakiruka kutoka kwenye basi na kutumbukia mtoni (kama mita 20) hivi, wengi wamevunjika viungo katika harakati za kujiokoa kwa kuruka umbali huo
 
Hospitali ya mkoa wa arusha ina surgeons wa kusaidia majeruhi au ni mpaka kcmc?
 
Ajali za namna hii zimekuwa zikitokea mara kwa mara huku serikali na vyombo vya usalama vikitupa lawama nyingi kwa madereva na watumia barabara wengine kuwa waangalifu wakiwataka wafuate sheria za usalama barabarani.

Mimi nina mtazamo tofauti kwenye vyanzo vya ajali hizi. Sheria zipo sawa na ni lazima zifuatwe ila ajali kama hizi zinaweza epushwa kwa kuboresha barabara. Barabara zetu ni za karne ya 18 yaani "Two way one lane"(barabara moja inatumiwa na magari ya pande zote mbili. Hapa nina maana kama hakuna gari inayokuja mbele dereva anaweza kuendesha upande wa magari yanayokuja. Wao wana sema ni uchumi mbovu. Hivi kweli hatuwezi kujenga "Two way two lane"(Chukua mifano ya Nyerere, kawawa, Mandela na morgoro Road mpaka Mlandizi) Roads?. Jibu ni dogo tunaweza ila hatuna utashi kwa kutawaliwa na Tamaa za kifisadi.

Na kuna Taarifa za kuaminika kuwa hizi ajali zinatumiwa na watunga sera katika kuhalalishia kukinga bakuli la kuomba misaada ama wakisingizia kuzipunguza au la. Kuna wakati nilikuwa nafanya utafiti fulani ambao ulinilazimu kupata details za ajali nilihangaishwa pale traffic makao makuu na mmoja wa askari akaniambia hizi details hutoka kwa kibali maalum.

Sasa tumefika mahali tuangalie zaidi maisha na kutupiana lawama, kama ni uzembe wa barabarani kila sehemu duniani upo ila wenzetu wamechukua tahadhari sana kiasi kwamba uzembe wa dereva isiwe adhabu ya kifo kwa watu wasio na hatia.
 
Dah hizi ajali zitatumaliza jamani,mwezi mmoja tu na haujaisha bado, watu zaidi ya sabini wamepoteza maisha kutokana na ajali hizi.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi
 
Mimi nina mtazamo tofauti kwenye vyanzo vya ajali hizi. Sheria zipo sawa na ni lazima zifuatwe ila ajali kama hizi zinaweza epushwa kwa kuboresha barabara. Barabara zetu ni za karne ya 18 yaani "Two way one lane"(barabara moja inatumiwa na magari ya pande zote mbili. Hapa nina maana kama hakuna gari inayokuja mbele dereva anaweza kuendesha upande wa magari yanayokuja. Wao wana sema ni uchumi mbovu. Hivi kweli hatuwezi kujenga "Two way two lane"(Chukua mifano ya Nyerere, kawawa, Mandela na morgoro Road mpaka Mlandizi) Roads?. Jibu ni dogo tunaweza ila hatuna utashi kwa kutawaliwa na Tamaa za kifisadi.

Na kuna Taarifa za kuaminika kuwa hizi ajali zinatumiwa na watunga sera katika kuhalalishia kukinga bakuli la kuomba misaada ama wakisingizia kuzipunguza au la. Kuna wakati nilikuwa nafanya utafiti fulani ambao ulinilazimu kupata details za ajali nilihangaishwa pale traffic makao makuu na mmoja wa askari akaniambia hizi details hutoka kwa kibali maalum.

Sasa tumefika mahali tuangalie zaidi maisha na kutupiana lawama, kama ni uzembe wa barabarani kila sehemu duniani upo ila wenzetu wamechukua tahadhari sana kiasi kwamba uzembe wa dereva isiwe adhabu ya kifo kwa watu wasio na hatia.

Mkuu,

Tatizo ni sisi watu, madereva wasio na heshima kwa uhai wa mwanadamu. Dual carriage haitasaidia kitu hapo. Pia watanzania huwa hatujifunzi, leo watu wanakufa na kesho tunasahau.

Barabara inajengwa kulingana na matumizi ya magari na uwezo. Unataka barabara kubwa wakati ukitafuta average kwa saa magari yanayopita ni kidogo sana?

Hata uwe na lanes kumi kwa Tanzania tutaendelea kupata hizi ajali kwasababu hatuheshimu maisha na serikali pia haijali kupoteza raia wake.

Hata hawa walioendelea wana barabara kama hizo nyingi tu na zinatumiwa na magari mengi labda mara tano ya TZ na hakuna ajali za ajabu ajabu.

Muhimu hapo ni alama za barabarani na mkondo wa sheria.

Inasikitisha sana, kila mwaka tunaongelea hili jambo hapa JF lakini baadaye watu wengine wanakufa tena.

Pia elimu ya barabarani kwa TZ ni sifuri, kwa mfano gari linapoanguka watu wanaanza kuruka madirishani. Kama hao inasemekana wengine walikuwa wanaruka kutoka kwenye gari linaloning'inia kitu ambacho ni makosa makubwa.

Poleni sana kwa wote.
 
Nimeendesha katika barabara za Tanzania kwa miaka mingi sasa. Nyingi ya barabara hizo hazina usalama kabisa kwa kuwa ni nyembamba mno, hata kupishana tu inakuwa shida. Kama haitawezekana kujenga dual carriageways, basi angalau tupanue barabara hizo. Vile vile ujenzi na uboreshaji wa barabara uzingatie ongezeko la matumizi ya barabara. Nyingi zilitengenezwa wakati magari hayakuwa mengi kama sasa.
 
2.JPG

1.JPG

basi%2Blikiwa%2Blinaning%27inia.JPG

Ajali ya Arusha katika picha (Mroki Mroki)
 
Poleni sana waliofikwa na ajali na Mungu atupe nguvu katika kipindi hiki cha majonzi
 
Mimi nina mtazamo tofauti kwenye vyanzo vya ajali hizi. Sheria zipo sawa na ni lazima zifuatwe ila ajali kama hizi zinaweza epushwa kwa kuboresha barabara. Barabara zetu ni za karne ya 18 yaani "Two way one lane"(barabara moja inatumiwa na magari ya pande zote mbili. Hapa nina maana kama hakuna gari inayokuja mbele dereva anaweza kuendesha upande wa magari yanayokuja. Wao wana sema ni uchumi mbovu. Hivi kweli hatuwezi kujenga "Two way two lane"(Chukua mifano ya Nyerere, kawawa, Mandela na morgoro Road mpaka Mlandizi) Roads?. Jibu ni dogo tunaweza ila hatuna utashi kwa kutawaliwa na Tamaa za kifisadi.

Na kuna Taarifa za kuaminika kuwa hizi ajali zinatumiwa na watunga sera katika kuhalalishia kukinga bakuli la kuomba misaada ama wakisingizia kuzipunguza au la. Kuna wakati nilikuwa nafanya utafiti fulani ambao ulinilazimu kupata details za ajali nilihangaishwa pale traffic makao makuu na mmoja wa askari akaniambia hizi details hutoka kwa kibali maalum.

Sasa tumefika mahali tuangalie zaidi maisha na kutupiana lawama, kama ni uzembe wa barabarani kila sehemu duniani upo ila wenzetu wamechukua tahadhari sana kiasi kwamba uzembe wa dereva isiwe adhabu ya kifo kwa watu wasio na hatia.

Mkuu barabara inaweza kuwa ni tatizo,lakini tatizo kubwa ni uzembe wa watumiaji wa barabara na ubovu wa magari ni tatizo kubwa sana,hii ya Arusha inasemekana breki za lori zilifeli,ya Tashrif tulisikia basi lilitoka Dar likiwa bovu,tusipobadilika tutakwisha kwa hizi ajali.
 
Pale hapahitaji matuta, utawekaje matuta kwenye mlima/mteremko mkali, zaidi ya hayo kuna kona na daraja! Basi matuta yakawekwe pia Kitonga, Ngorongoro au hata Sekenke!

Kinachohitajika ni alama za barabarani na madereva waangalifu.

Marehemu wapumzike kwa amani. Poleni majeruhi na wafiwa.

Mbona mto Wami kuna matuta na ni mlima/mteremko mkali????????????
Kitonga hakuna ajali za mara kwa mara
 
Back
Top Bottom